WEWE NI WANGU SEHEMU YA 19
SONGA NAYO......
Muda ulienda na sikupata wasaa wa kuzungumza na mama maana alikuwa hataki kusikia chochote kutoka kwangu, so niliona nimsubiri dada yeye ndie anaweza kuwa msaaada wangu
Hatiame muda wa dada kurudi nyumbani ulifika, nilimsubiri kwa hamu sana baada ya muda kweli dada aliweza kurudi huku akiwa amechua na dawa za mama
Dada baada ya kufika alishangaa sana kuniona namna nilivyobadilika usoni
"Yani nilitegea kukuona ukirudi ukiwa handsome, lakini nashangaa unarudi na makovu, usiniambie ulifumaniwa na mke wa mtu ...??"
Dada aliniuliza
"Aah dada ni misunderstand tu imetokea kwa bahati mbaya kule kazini kwangu ndio ikapelekea kuwa hivi, lakini ukweli hizo tabia nilishaacha..."
Nilijieleza
"Mh, sawa sawa na huyu ndio wifi...??"
Dah dada alinifanya nitabasamu walah π₯° ewaaa hivi ndio vitu navitaka kusikia kutoka kwa ndugu zangu
"Dada wewe umejuaje...??"
Nilimuuliza
"Anaonekana tu maana ni mama kijacho tayari tujiandae kuitwa aunt..."
"Dada kumbe unajua kutazama wewe yan dah..."
"Kwa hii kazi nishindwe kujua tu, kwanza nilipoingia tu nikajua hapa tayari Henry kashafanya yake.."
Nyiee nilifurahi balaa
"Dada naomba ukazungumze na mama, mama hataki kabisa kunielewa anasema nimrudishe binti wa watu lakini dada ukweli me nataka mtoto na unavyotuona hapa tumetoroka ili kuokoa maisha ya mtoto wetu maana kaka yake alikuwa ameshinikiza atoe ujauzito..."
Nilijieleza huku nikiwa nimejitilisha uso wa huruma kabisa πππΎ acheni tu ndugu zangu.
"Kwahiyo huyu ni mwanafunzi wako..??"
"Ndio dada lakini naweza kusema kuwa haikuwa dhamira yangu kabisa naapia kwa mungu sikudhamilia kumuingilia kwa nguvu ni vile tu yani dah...."
Nilikuwa nashindwa hata nielezeeje jamani maana kama maji yamenizidi kimo walah πππππΎ
"Henry sio rahisi kabisa mama kukubali ukiangalia huyu ni mwanafunzi na tena yupo form four kweli, si ungesubiri akamalizia hilo darasa ndio mkafanya sasa ety we binti kwanini ulikubali kumpanunlia huyu ...??"
Dada alimuuliza Lizy huku akinichoma choma na kidole kichwani, nilikubali kupokea lawama zote maana makosa ni yangu
Lizy wa watu yeye alikuwa kimya tu anawaza yake.
"Basi subiri naenda kuongea na mama kama atakubali.."
Nikamjibu tu sawa huku nikiwa nimejikatia tamaa kabisa, baada ya dada kuondoka Lizy nae akapandisha mashetani yake sasa πππΎ
"Usiniambie kwamba haya yote ninayoyasikia ni kweli ulikuwa hutulii enhee...??"
Aliniuliza, eeeh aisee yani natoka hili linaingia hili walah nachoka
"Liz...."
"Usinishike yani bora ningekubali tu kubaki kule na kutoa ujauzito kuliko kubaki na mwanaume kama wewe ambaye huwezi kabisa kutulia..."
SEHEMU YA 20
Maneno yake yalikuwa makali sana kuna namna nilikuwa naona. Kabisa nimekosea kweli na kujutia kabisa kutotulia na mwanamke mmoja
"Lizy mke wangu, nisikilize.."
Nilisema huku nikimshika nikasukumwa hukoπ
"Nimsema niache we vipi..?"
Eeh mungu, kama umeruhusu nipitie haya basi naomba niasmehe maana naumia mno, kweli ndio najua umalaya sio mzuri kabisa maana nashidwa kuaminiwa na kuthamiwa
Nisamehe sana nahaaidi baada ya hapa nitajirejebisha kabisa yani naahidi sitafanya uzinzi wa aina yoyote ile
"Lizy..."
Nilimuita baada ya kumuona anaondoka, nikamuwahi na kumshika mkono na muda huo huo mama na dada wakawa wamefika sebleni
"Lizy nisamehe sana ukweli ni kwamba nilikuwa na hao wakati sijakutana na wewe nakuhaidi upo peke yako, wewe ni wangu kuanzia sasa, wewe ndie ambaye unatembea na moyo wangu tafadhali mama yangu usiondoke
Tambua bila wewe siwezi kuishi, siwezi kabisa Lizy wangu nakuomba mke wangu kubali ubaki tulee mtoto wetu..."
Nilikuwa naongea huku machozi yananitoka kamasi ndio kabisa kama zote, mwanaume nilikuwa sina ujanja, pamoja na kupangilia maneno matamu matamu ila wapi binti hakunielewa kabisa
"Mama, dada niombeeni msamaha kwa mke wangu hata na nyie si mashahidi kabisa ilikiwa zamani ndio nilikuwa situlii mama si unajua kabisa eèhh.??"
Nilimuuliza mama walau anaiitete
"Hizo sio shida zangu..."
Eeh mama ne khaa, πππΎ kwahiyo hata kunitetea tu hamna, kwa kweli ndio nimeamini kila mtu apambane na msalaba wake..
"Lakin mama...."
"Binti unaitwa nani...??"
Mama alimuuliza Lizy
"Naitwa Lizy.."
"Lizy vitunguu au dagaaa...??"
Eeeh huu msemo mama amesababisha kuniambukiza mpaka mimi, na huu msemo umemkaa sana kinywani
"Naitwa Elizabeth Nestory.."
"Mh ndio maana mmeamua kupeana na mimba kabisa.."
Nikadakia
"Aaah mama Lakin..."
"Lakini nini mimi nimewaruhusu tu mkae hapa, ila yakikutokea tusijuane kabisa.."
Mama alizungumza kisha akaondoka mahali pale nikabaki mimi dada na Lizy
"Karibu sana wifi, jisikie upo nyumbani..."
Da Helen alimkaribisha Lizy upande wangu nikatabasamu mpaka jino la mwisho, yani nilikuwa nafuraha sana...
Basi rasmi maisha yakaanza tukiwa nyumbani, namshukuru mungu nilipona kabisa yale makovu yote na uso wangu ukawa na nuru ile mbaya pia ule uhandsome ote ukarudi upya π₯°
Nyie nilikuwa natamba mtaani kwangu, kwani mke wangu alikuwa mzuri na ile mimba yake sasa wee alinawiri sana, basi maisha yaliendelea na nilikuwa nikifanya kazi ndogo ndogo za kusukuma maisha mbele
Nilifanikiwa kununua vifaa vya kujifungulia kwa mke wangu, basi miezi nayo ilikatika, ni usiku wa manane siku hii nilikuwa nimemkumbatia mke wangu na tulikuwa tumelala mara gafla uchungu ukaanza kumuuma
Na siku hii dada alikuwepo nyumbani so kwake hayo mambo yalikuwa mepesi, alihakikisha anammzalisha mke wangu vizuri kabisa, eeh acheni nimuite mke wangu kwa sababu ndie ambaye yupo kwenye mpiango yangu yote ya kuwa mke
Japokuwa umri wake ni mdogo hiyo sio shida yangu bwana, kifupi kwa huyu mimetulia kabisa sina papara na wanawake wengine π₯°....
ITAENDELEA......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni