BUNAIZA:01
Eti ufike kijijini kwetu, halafu usikutane na Sifa za msichana mzuri kijiji chote, msichana mwenye mvuto wa pekee, msichana mwenye kupendwa na watu kwasababu ya uchangamfu, ucheshi na umaarufu wake pale kijijini kwasababu ya kucheza ngoma vizuri sanaaaaa. Msichana mwenye kila aina ya sifa.
Wanaume wa kijijini hapo wanachanganyikiwa kwa sifa na uzuri wa msichana huyo. Utasikia sio ngoma tu Bunaiza, mpaka kitandani unazicheza haswaaa. Haya maneno ni kila mwanaume ambaye nimewahi kumpa mwili wangu ba?? utamsikia akisema.
Wanaume wanapigana, mimi nishagombaniwa sanaa, mimi nishapiganiwa mno lakini ndiyo nipo
kijijini, sijawahi toka nje ya kijiji hiki.
Maisha yangu kijijini sio mabaya kwa hapa kijijini lakini ninazo ndoto za kutoka nje ya kijiji hiki, ninazo ndoto za kwenda mjini kupambana na kubadilisha maisha yangu na bibi yangu ambaye mimi ndiyo naishi naye baada ya wazazi wangu kufariki. Ninampenda sana bibi yangu, ninampenda sana.
Sitaki kuelezea mengi kuhusu maisha yangu ya kijijini baada ya sifa zote hizo, uzuri, ucheshi, kupendwa na watu kwasababu ya kucheza kwangu ngoma vizuri tena sio kijiji hiki tu na hata vijiji jirani sifa zangu zimeenea.
Ninakumbuka sana, siku moja jioni tulipokea ugeni nyumbani. Na huyu alikuwa ni Rahma, mtoto wa shangazi yangu ambaye pia bibi yangu ni bibi yake. Nilipomuona nilifurahi sana, na hata yeye alifurahi sana. Nilimkumbatia nikisema “karibu sana dada Rahma, jitazame umependeza sana nimefurahi sana kukuona.”
BUNAIZA:02
Alifurahi sana akiuliza “bibi yupo wapi nimemkumbuka sana yupo wapi?”
Basi bibi na yeye alitoka, wakakumbatina kwa furaha sana na tukaingia ndani. Na taa yetu ya chemli ikiwaka. Bibi alisema “Rahma mwanangu, Ina maana hutaki hata kuja kuniona bibi yako miaka yote hiyo?. Ni maisha gani haya mjukuu wangu?”
Rahma alimtazama bibi akisema “upo sahihi bibi, nisamehe sana. Nilikukumbuka sana wewe na mdogo wangu ndiyo maana leo nipo hapa.”
Bibi alimtazama na kumuuliza “kwahiyo mjini unaishi na Nani sasa?”
Alitabasamu na kusema “nipo mwenyewe tu bibi, eenh na wewe Bunaiza, vipi unafanya nini sasa?, vipi shule?”
Nilimtazama na kusema “dada Shule?, hapana sisomi hata dada yangu, nipo tu mimi. Ila nacheza ngoma hatari, hapa kijijini pote wananifahamu. Mimi ndiyo Bunaiza.”
Akacheka na kusema “usiniambie, na huo uzuri wote umechagua kucheza ngoma mdogo wangu. Hata hivyo ninatamani sana kuona.”
Nilimtazama na tabasamu nikisema “usijali, subiri kesho tu utaona maandalizi maana kesho kutwa kuna nashindano.”
Bibi akamaliza kwa kilugha lakini alimaanisha “na lazima ushinde.”
Nikacheka nikisema “Bunaiza, Bunaiza, Bunaizaaaaaaaaa.”
Basi dada Rahma alicheka akisema “ooh jamani familia yangu. Nawapenda sana.”
Tulikumbatiana pale, mimi nikawaacha na kwenda andaa chakula.
Ninakumbuka k?la kitu nilifanya kwa furaha sana. Tulikula kWa upendo na nilimuandalia dada yangu maji ya kuoga. Sasa wakati amerudi ndiyo anajipaka vipidozi vyake mpaka nashangaa. Nashika hiki naacha nashika kile namtazama usoni huku namuuliza “Rahma, hivi vyote unajipaka mwili mmoja?”
BUNAIZA:03
Alinitazama na kutabasamu akisema “tena hivi vichache mdogo wangu. Huko mjini watu wana ngozi nzuri sana. Tena wewe na huo uzuri wako sitaki kusema sana.”
Nilimtazama na kumuuliza “Unataka kusema mimi ni mzuri si ndiyo?”
Akanitazama na kusema “wewe Bunaiza ni mzuri mno, ni mzuri kupita kiasi.”
Nilitabasamu tu na kujilaza, nikawa nawaza uzuri una mama gani na nipo kijijini. Mimi pia nataka vitu vizuri na natamani haya maisha mazuri.
Tuliongea mengi na dada Rahima usiku huo, dada yangu ni mtu wa safi kabisa anavaa mavazi kwa heshima sana. Nilimsifia kwa kuwa msichana mzuri, kujitunza na kubaki na maadili yake. Anacheka na kutabasamu tu dada yangu. Nina neno basi namshangaa tu namna alivyo.
Tulipata nafasi tulipumzika, na kesho yake baada ya kuamka tulifanya kazi kwa kusaidiana. Na hata mida ya saa kumi bibi akawa ananitania akisema “kichwa juu juu hapo unawaza ngoma tu mjukuu wangu.”
Nikacheka na kusema “bibi na wewe, unajua napenda kucheza na leo ndiyo mazoezi. Rahima dada yangu vipi unaenda?”
Bibi alimtazama Rahma na kisha alisema “ushauri wangu hapana, leo nenda mwenyewe na Rahma tutakuja wote kesho. Unajua kwanini?, nataka apate uhondo wote vizuri.”
Nilimtazama na kumuuliza bibi yangu “ina maana na wewe utakuja.”
Bibi alicheka akisema “mjukuu wangu mcheza ngoma maarufu katika kijiji hiki(huku akitamba na kutaja jina la kijiji) inakuaje nisije kumuona sio kweli. Lazima nije mjukuu wangu.”
Nilijikuta moyoni ninapata ile hamasa haswa ya kumfanya bibi yangu na dada yangu huyu ndugu aliyefika nyumbani, nilifurahi sana na nilielewa bibi anataka muda wa kuzungumza na mjukuu wake maana tangu binti mdogo mdogo alipomaliza shule ya msingi alichukuliwa na ndugu zake upande wa mama wenye uwezo huko mjini na ndiyo wamemsomesha hivyo nafahamu wana mengi ya kuzungumza.
BUNAIZA:04
Hivyo sikuwa na tatizo kwenye hilo nilijiandaa zangu na kuondoka zangu. Kucheza, kucheza ngoma ndiyo kitu napenda sana kwenye maisha yangu, ninasikia raha. Naishi ngoma, nakula, nalala, natabasamu, nacheka ngoma. Ngoma ni maisha yangu yote. Nikifanya ninapata furaha kutoka ndani ya uvungu wa chini kabisa wa moyo wangu.
Ninakuambia, huku nikiwa na furaha hata kuna mahali nikifika najikuta natazama huku natazama kule nacheza kidogo halafu nacheka. Ninafanya kitu yaani nisipofanya sijisikii. Nakutana na watu wananisalimia kwa furaha wananikumbatia na wakinitakia kila la heri siku inayofuata. Sijui nikuambie kitu gani, sijui niseme nini, ila mimi ni msichana ambaye kunichukia utake wewe, uwe umeamua wewe. Mchangamfu na mwenye upendo sana sana sana.
Nilifika kwa mazoezi, lilikuwa shindano kubwa sana kesho yake. Na viongozi wa serikali, na dau kubwa lilitangaza. Kushinda kwangu mimi ni lazima na kila siku nina hii nguvu ndani yangu ya kujiamini na kujitamkia mazuri.
Ninajiambia kabisa mimi ni namba moja kila ninapoenda kwenye kila ninachofanya. Wengine wanatakiwa kufanya baada yangu au kufuata baada yangu. Jina langu litasikika na halitasahaulika kwenye moyo wa kila atakayenifahamu.
Nami nitakuwa mzuri kwao na nitawafanyia ukarimu. Watanipenda na kuniheshimu kama wanavyofanya kwa pesa. Hii nguvu na roho ya kujiamini ndiyo imenifikisha hapa, daima, kamwe sijawahi jiona mdogo kwenye chochote kile.
Basi nilifanya mazoezi na wenzangu vizuri. Unajua tena haya mambo ya vijijini eenh mganga wa kijiji pale akaja tukaenda kukutana na yeye. Akatufanyia mila zake na mambo yake huku ana furaha tu. Haswa mimi hapa maana mimi ndiyo mchezo wenyewe. Huyu baba alituambia tutashinda na huwa hatujawahi poteza sisi. Tupo vizuri sana kwahiyo kupoteza ni ndoto.
Ninakumbuka baada ya kila kitu kila kitu, nilifika nyumbani kwa kuchelewa lakini walinisubiri kula. Waliponiona walifurahi huku bibi akisema “ilikuwaje mjukuu wangu.”
Nami nikamsimulia, akanitazama usoni na kutabasamu akisema “nakutakia ushindi mkubwa sana binti.”
BUNAIZA:05
Nilitabasamu na kisha Rahma alisema “kiukweli nina hamu sana ya kujua namna una fanya. Nimesikia leo sifa zako nilipoenda na bibi kisimani. Umefanya mpaka bibi yetu ana heshimika hapa. Nina hamu ya kujua mdogo wangu anafanya nini hapa.”
Nilicheka na kusema “ooh dada Rahma ulienda kisimani, ni lazima wamekushangaa huko
Maana nina dada kama mzungu.”
Akacheka na kusema “sana lakini unajua nini Bunaiza hata wewe ni mweupe, ila kuna vitu tu huna na nina hakika utapata kila kitu utakuwa hata zaidi yangu nafahamu hili.”
Nilitabasamu na bibi akatutazama na kusema “mkishaanza sasa, muda wa kulala naomba tule wanangu.”
Tulitazamana na kutabasamu.
Baada ya kumaliza pale nilikuwa nimechoka, nilimsaidia dada Rahma kusafisha kisha nikaenda zangu kuoga na baada ya hapo nikarudi chumbani nimejifunga lubega kimtandaio kifupi.
Halafu nikawa natamani kucheza pale, si nikaanza kucheza. Ile nacheza ngoma, ile nacheza kwa madaha nikasikia mtu ananipigia makofi. Nikashtuka na kuacha.
Dada yangu Rahma akasema “sasa nakubali, mdogo wangu kipenzi, mdogo wangu Rahma, kumbe unajua hivi kucheza Mungu wangu. Umejifunza wapi nashindwa hata kuelewa. Please usiache kucheza mpaka nimetamani ebu nifundishe.”
Nikatabasamu na kumuuliza “unataka kucheza kweli?”
Alitabasamu, basi nikamvuta na kuanza kucheza naye anifuatishe. Basi anacheza lakini sio kama mimi, yupo tu kawaida. Tukajikuta tunacheka na kukumbatiana na kusema “nina hamu sana ya kukuona ukicheza, nina hamu kesho ifike nikashuhudie.”
Nikamuuliza kwa kushangaa “una sema kweli?”
Akanijibu kwa kizungu “What a sisy For Bunaiza?, hii ndiyo kazi ya dada kipenzi. Sikia sisi ni familia. Baba yangu na mama yako walizaliwa tumbo moja. Walipendana sana na bibi na babu waliwalea pamoja si unakumbuka?. Hivyo na sisi tunatakiwa kushikamana kama wao wewe ni ndugu yangu tena damu kabisa.”
BUNAIZA:06
Nilimtazama na kumkumbatia. Alitabasamu na kusema “tulale, ili kesho ifike haraka.”
Nilitabasamu tena, tukalala.
Siku iliyofuata sasa, wenzangu wameamka mpaka saa nne bado hata bibi akaniambia “mjukuu wangu, unajua unachelewa hivyo, unaenda saa ngapi kwenye maandalizi. Fanya uamke sasa.”
Nilijikuta naongea kwa taabu “bibi sijui nini kinanitokea. Mwenzako kichwa kinanigonga mpaka naona kizunguzungu.”
Bibi alisema “hapana haiwezekani, ina maana hutocheza leo mjukuu wangu?”
Machozi yalinitoka, kuamka siwezi, kichwa kizito. Bibi alikuja na dada Rahma. Ile waliponiona bibi mwenyewe alichoka maana ni machozi. Nalia kichwa kinauma.
Dada yangu Rahma akawa ananiambia “usifanye hivyo mdogo wangu, unapolia unazidi kuumia tulia unywe dawa na unywe maji upumzike hata lisaa unaweza kuamka na nguvu.”
Bibi hapo tayari ametoka ameenda kunitafutia majani, huku dada yangu kachukua dawa kwa pochi yake ya maumivu na yeye kanipatia. Basi bibi ile kaja kunipaka dawa ni dawa juu ya dawa ili tu niwe sawa nikacheze.
Nikawa nakunywa na maji kama dada Rahma alivyosema.
Ngoma zinaanza saa nane, mpaka saa tano mimi bado sioni dalili. Ninavyopenda na ile kujua kuwa nakosa ndiyo roho inazidi kuniuma. Niliomba tena dawa hata dada Rahma alisema “mdogo wangu acha dawa zifanye kazi. Zinafanya taratibu taratibu.”
Nikasema kwa maumivu ya kuukosa huu mpambano wa leo “Rahma dada, naomba tafadhali kidogo tu, kidogo nisaidie mdogo wako. Sitaki kukosa leo. Naomba hata kidonge kimoja ili kusudi zifanye kazi haraka. Sitaki kufa nataka kupona.”
BUNAIZA:07
Ukimuona bibi yangu anasikitika mpaka unajua kabisa anaumia. Nilikuwa namtazama nauliza “bibi si nitacheza lakini si ndiyo?”
Bibi alinitazama hadi anataka kulia akatoka chumbani na Rahma pia alitoka.
Hali yangu bado iliendelea kuwa hivyo, mpaka saa saba kasoro kiongozi wangu na mchezaji mwenzangu wanakuja pale wananikuta vile kwanza wakachoka na kujikuta wananiuliza “ina maana hauchezi leo, tumeisha.”
Niliwatazama huku nalia, kiongozi akasema “nilijua tu unahitaji kinga zaidi, hili shindano ni kubwa sana washakupiga wapumbavu. Sasa tutafanyaje.”
Mimi kuzungumza naona kero machozi tu ndiyo yanatoka. Ila mwisho niliwaambia “hata bila mimi mnaweza, mnaweza kufanya zaidi yangu. Moyo wangu upo na ninyi.”
Yule mchezaji mwingine akasema “unaongea nini Bunaiza. Sisi wote tunajua kama wewe ndiyo ngao yetu ya ushindi. Sisi tutafanya nini bila wewe. Nachanganyikiwa kwanini iwe leo, kwanini uwe wewe si bora hata mimi ndiyo ningeumwa.”
Nilimtazama na kusema “usiseme hivyo kushinda ni lazima. Muda umeenda sana fanyeni muende mimi nitawaombea leo mshinde.”
Walinitazama mpaka wanalia ile tu kujua kuwa mimi sitakuwepo kwenye mashindano inawaumiza.Wanaumia kukukosa, wanaona kabisa watashindwa, hawatafanikiwa kuna kitu kitaondoka kwao.
Hivi ndiyo wewe unatakiwa kuwa kwenye maisha yako, unatakiwa kuwa chumvi ya kuongeza ladha ya chakula. Kupambana kwako, kupigania hicho unachokipenda watu wanatakiwa kuona wewe ndiyo namba moja.
Pambania mpaka waone bila wewe hawawezi kitu chochote. Pambania mpaka waone wewe ndiyo muongozaji wa mambo yao mengine. Mimi Bunaiza, sio kwasbabu tu najua kucheza ndiyo nimekaa tu.
BUNAIZA:08
Bado nina bidii, bado ninajituma, bado napenda ninachokifanya na ndiyo
Maana nahangaika kifungue njia siku niagane na haya maisha ya kijijini nihamie mjini nikapambane na maisha mengine yaendelee. Ninapambania mno, na ndiyo maana kwenye maisha napenda kusema hivi.
Chochote unachofanya, vyovyote unavyofanya hakikisha unafanya vizuri zaidi ya jana. Unaweza uone kama vile hufiki popote, huendi popote wala huna watu wanaotazama hicho unachofanya.
Nisikilize, endelea kufanya tena kila unapofanya kiwe kizuri zaidi ya ulivyofanya siku ya jana. Kuna watu wapo wanakutazama, hawasemi, hawafanyi chochote wala lolote wapo kimya wanafuatilia hatua zako.
Ili uendelee kufuatiliwa ni lazima ufanye vizuri sana. Usifuate upepo unaoona yaani huuzi, hauonekani. Hakuna hicho kitu watu wanaona na Mungu anaona. Ukianza kukata tamaa unapoteza hawa wanaokufuatilia kwa siri.
Niamini ipo siku yako, siku isiyo na jina, siku haina jina kabisa utabaki unashangaa. Utajiuliza maswali na maswali ila hutokuwa na jibu maana utakuwa umefurahi sana na hiyo ndiyo siku yako wale wanaofuatilia kwa siri watajitokeza na kukupigia makofi ya ushindi. Endelea kufanya, hakuna kukata tamaa.
Wale watu waliondoka na maumivu, familia yangu ikawa na maumivu. Ila nilisema “dada Rahma na bibi nendeni, mimi naomba nipumzike kidogo nakuja.”
Dada Rahma alimtazama bibi kisha mimi na kusema “ni wewe tu ambaye nilikuwa nataka kukuona. Sasa naenda nikamtazame nani?”
Nilimtazama bibi na tabasamu la kuchoka sana. Kisha nilisema kwa upole “bibi, mimi hapa na wewe tunajua kuwa kucheza ngoma ni sehemu ya maisha yangu. Naomba tafadhali niamini. Tangulia nakuja.”
Bibi alinitazama na kusema “lakini kama upo hivi siku kubwa kama leo basi unaumwa. Najua hakuna kitu cha kukuzuia kucheza mjukuu wangu. Tukae tu hapa.”
BUNAIZA:09
Nilimtazama na kusema “niamini bibi, mkibaki hapa hamtaona nikicheza kwasababu hamtaweza kukimbizana na mimi. Tangulieni na muwe na imani na mimi.”
Bibi kwa kutokutaka alimtazama Rahma. Wakapeana ishara, nikaona Rahma anavaa vizuri, bibi naye akaenda kujiandaa na waliniaga na kuondoka zao kwasababu mimi nilitaka.
Ni kweli kuwa sikuwa vizuri na sikuwa nataka kukosa nafasi hii. Ila ningefanya nini, nilijikuta nakunywa maji kwenye jagi pembeni yangu kwa kasi.
Kisha nilikaa nikisema “najua hii siku kubwa kwenye maisha yangu. Mama najua upo unanitazama na unapenda nifanikiwe. Bibi ananiombea ila maombi yako mama ni muhimu zaidi mbele za Mungu kwaajili yangu hapa duniani kama binti yako.
Na wewe umewahi kuondoka na ukaniacha bila wa kuniombea kama wewe ulivyofanya. Tafadhali mama kama upo mahali na unanisikia mimi binti yako, nafsi yako najua inatembea na mimi, na najua nafasi ya mama mbele ya Mungu. Niombee niamke hapa na nikakufurahishe.”
Nikafumba macho na kujiuliza “nafanya nini, kitu kitokee niwe sawa kitu kitokee.”
Ninakumbuka sana hii siku ya mashindano, ninaikumbuka sana kwasababu niliipania, nilijiandaa sana kwaajili ya mashabiki na familia na ilikuwa mashindano makubwa sana mpaka viongozi wakubwa wa nchi halafu mimi baada ya yote naumwa.
Ndani naumia naona kuliko hata ugonjwa wangu, ni sawa na mtu amekuahidi kitu halafu siku ya kukupa hicho kitu ameumwa au ameghairi au sababu yoyote ya kutokukupa imetokea.
Inaumiza moyo hii ndiyo mimi sasa. Ninaumia haswa kukosa mchezo huu. Nililala, usingizi mzito hapo nishakunywa maji jagi limebakiwa na maji kiasi kidogo.
BUNAIZA:10
Nilikuja kuamshwa na mkojo, mkojo umenibana nashindwa kuendelea kulala. Nikajikaza na kukaa kitandani. Kichwa sasa nikishika walau sio kama awali hata sasa niliweza kwenda chooni.
Huko nikanawa uso wangu, nikaona bora nijimwagie maji nipate nguvu. Lakini nikiwa nafanya hivyo ndiyo nashtuka nikisema “leo kuna ngoma mbona kama muda umeenda sana.”
Nikatoka haraka bafuni, kufika chumbani naangalia saa yangu ya kimulimuli ni saa kumi na nusu. Mungu wangu sijui kikundi changu tayari au bado au ndiyo washamaliza wanasubiri kutajwa kwa mshindi mpaka sielewi.
Hata mafuta sikumbuki kama nilipaka, ninachokumbuka nilijiandaa kwaajili ya ngoma namna tunavaa na vitu kama hivyo kisha nilitoka pale nakimbia hata kichwa tena sikujali. Nilitoka mbio.
Nikafika sehemu nikakutana na mtu wa pale kijijini na baiskeli nikaomba msaada. Alifika sehemu akaniacha maana alikuwa anaenda sehemu nyingine. Ile nafika pale uwanjani nipo hoi, nasikia kundi letu linaitwa halafu wanaenda pale, watu hata hawana furaha kwasababu hawajaniona.
Nilitabasamu na kuvuta pumzi. Ile wanajipanga sasa, binti Bunaiza nikasimama, nikatabasamu na kuanza kuingia. Ile naingia watu walioniona huzuni iliisha walianza kuita “Bunaizaaaaaaa, Bunaizaaaaaaaa, Bunaizaaaaaaaaaaaaaa amekujaaaaaaaa eeeneeeeh, saaafiiii safi sana.”
Kila mtu akawa anaongea lake, wachezaji wenzangu wakageuka kunitazama na mimi hapo natazama sura ya bibi yangu ilipo. Mara naona bibi na Rahma, Rahma amemkumbatia bibi yangu haamini hata kama nimefika pale.
Mimi natabasamu tu, natabasamu tabasamu ambalo ni la ushindi. Hata viongozi meza kuu, wanashangaa mimi nami hata nina shangiliwa hivyo. Nilifika pale kwa kundi wakawa wanacheka kwa furaha.
Huu ni mwanzo tu, mtanipa maua yangu mbona
Njoo WhatsApp na sh 1000 upate muendelezo
Namba ya WhatsApp ni +255743433005.