DO YOU LOVE ME..... S2 (16)
AM I WRONG?
"Kuna nini...?" Nilimuuliza Rely ambaye alikuwa na hasira sio poa. Akanitazama usoni, macho yetu yalipokutana nilihisi utfauti katika macho yake. Kulikuwa na majimaji ambayo yalianza kudondoka. Ni machozi, nahisi Rely alikuwa na maumivu ambayo yalikuwa yakimuandama ndani ya mwili wake. Kulikuwa na kitu kinachomuumiza. Tukajikuta tunatizamana kwa zaidi ya dakika mbili, akaniuliza.
"Unachokifanya unadhani ni kizuri?”
“Sijaona ubaya” nilimjibu kwa dharau, kilio cha kwikwi kikazaliwa. Rely alianza kulia akisema
“Inamaana unamhangaikia Rola si ndio? Hukumbuki kama alikufukuza kwake? Hakutaka tena mazoea na wewe? Hukumbuki?"
“Yote tisa, hakuna kitu kitatafuta upendo wangu kwake. Ulikuja kwangu kama mbadala wake baada ya ushawishi mkubwa na mkali kutoka kwako na kwa ndugu zako. Hukumbuki?”
“Lilishaisha na tukayaanza maisha yetu. Tukawa hapa pamoja”
"Lakini..... Bado nampenda na huo ndio ukweli. Nani ambaye hajui hilo?"
"Rahim..... Unaongea nini?"
"Umesikia nilichokio...." Sikumaliza kuzungumza, nilipigwa kofi. Jambo ambalo lilinifanya nichukie sana.
Kwanini anipige kofi? Amenichukuliaje hadi ananyanyua mkono wake na kunipiga ikiwa hata yeye ameleta ujauzito wa mwanaume mwingine mle ndani huku wakipanga kabisa mikakati? Nilichukia sana. Nilitaka kumwambia mbona hata hiyo mimba sio yangu lakini nilijiambia ‘Mimi ni mwanaume na uvumilivu huleta mbivu as long as najua ukweli basi sipaswi kurumbana na mtu’ niliondoka nyumbani bila hata kumuaga. Nyuma nilimuacha Rely aliyekuwa akimwaga machozi ya maumivu juu ya kile ambacho kimetokea. Mimi sikujali hilo, niliondoka.
Nilienda pembezoni kabisa mwa bahari na kuzunguka kandokando yake. Niliimani hii ndio ingekuwa njia sahihi ya mimi kuwa sawa kiakili kwani nilikuwa na msongo wa mawazo wenye maswali yasiyoisha. Ni kweli nilikuwa nampenda Rola lakini alipokuwa mzima hakuwa na muda na mimi. Je, niendelee kumpenda na kumnyanyasa Rely kama ambavyo nilikuwa nimepanga? Kama kweli Rely alikuwa ananipenda, kwanini ashawishike na kupata ujauzito wa mwanaume mwingine? Hili ndilo lilikuwa swali lililonipa msongo wa mawazo mno.
Nikiwa huku simu yangu iliita sana, Rely ndio alikuwa anapiga kila wakati lakini sikupokea. Alipoona nimepuuza simu zake, akaanza kutuma meseji akinitaka nirudi nyumbani na nimsamehe. Meseji zilikuwa ni nyingi sana kiasi kwamba hadi nikaona ni kero, niliamua kuzima simu.
Nakumbuka nilikaa sana katika eneo hili hadi pale nilipochoka ndipo niliporudi nyumbani. Ulikuwa ni usiku haswa, ndege wamelala na hata magari yalipungua barabarani. Nikataraji kwamba Rely atakuwa amelala lakini haikuwa hivyo, nilimkuta akiwa bado hajalala. Alikuwa akinitazama kwa jicho la huruma lilojaa huzuni, halikuacha kudondosha machozi. Akaniuliza.
“Unadhani unachokifanya ni kizuri kwangu?”
“Kama ni maamuzi ya maisha yangu je?”
“Ndio uache maumivu kwangu?”
“I’m sorry” nilimjibu na kutaka kujilaza kitandani kwa sababu nilikuwa nimechoka lakini alinizuia huku akinifuata na kuniuliza.
“Kitu kimoja nataka kujua kutoka kwako. Je, upo tayari nikijue?”
“Kikiwa ndani ya uwezo wangu nitakujuza”
“Ok” Rely aliitikia na kukaa kimya, hakuzungumza neno lolote lile kwa zaidi ya dakika tano. Tukatazamana kama kuku waliopigana muda mrefu.
Nikastuka. Kwanini atake kujua kitu na baada ya kumpa sikio hazungumzi tena? Nilimuuliza.
“Kimya?”
“Unajua nini Raheem?”
“Hapana”
“Njia pekee ya kuwa huru ni kusema ukweli”
“Hilo najua”
“Ukweli utakuweka sehemu salama na sahihi ambayo mtu mwingine hawezi kukaa. Niambie ukweli”
“Upi?”
“Unanipenda au unanionea huruma ndio maana bado niko kwako. Huenda huu ujauzito ndio unakufanya u’fake na unioneshe upendo hewa?” Rely aliniuliza huku akionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua ukweli. Shauku ya kupewa jibu lenye hatima ya mwisho..... ITAENDELEA.