ELIE MPANZU KIBISAWALA alisaini Simba mkataba wa miaka 2 wenye kipengele Cha kuongeza mwaka mmoja mwingine Hadi sasa kwenye mkataba huo Mpanzu ameshautumikia miezi 4 tu maana ameanza kucheza kwenye dirisha dogo la usajili la January.
NIMEPIGWA simu nyingi sana na mashabiki wa Simba kutosha sehemu mbalimbali wengine wakinitumia sms lukuki wakiniuliza juu ya swala la MPANZU kwenda Yanga kama ni taarifa za ukweli? Maana Kuna mchambuzi Wa YANGA aliwalisha matango pori kuwa Mpanzu anakwenda Yanga jibu la SWALI hili ni BIG NO MPANZU HAENDI YANGA NG'OO.
Kuna offer tatu ambazo zimekuja kwenye uongozi wa mchezaji na offer moja imekwenda moja kwa moja kwenye uongozi wa Klabu ya Simba za kutaka kumnunua Mpanzu na mkataba wake moja kwa moja akitokea Simba Sc
1.AL AHYL ya nchini Misri wametuma offer moja kwa moja kwa Simba ya kutaka kumnunua ELIE MPANZU yenye thamani ya Bilioni 3 na milioni 200 yaani 3,200,000,000/= na mshahara wa milioni 75 kwa mwezi maana yake ni kununua Pamoja na mkataba wake ili msimu ujao akawatumikie katika Klabu Yao.
2.Yanga Wanaongea na menejiment ya mchezaji kuona uwezekano wa Dirisha kubwa la Kiangazi Kama wanaweza kumsaini mchezaji kwa kupitia timu nyingine yaani aende kwanza kwenye timu nyingine Kisha wao wamsajili kutokea timu hiyo maana Simba hawawezi kamwe kuwauzia Yanga ELIE MPANZU.
3.Wydad Casablanca pia wamewasiliana na uongozi wa mchezaji kuona uwezakano wa kumsajili msimu ujao.
Hadi Sasa wenye maamuzi ya mwisho ya ELIE MPANZU KIBISAWALA abakie Simba au aondoke kwa kuuzwa ni uongozi wa club ya Simba.
Mashabiki wenzangu wa Simba tuishi humu HAYA sasa kuanzia sasa nimeufunga huu mjadala sitaki tena kuulizwa hili SWALI.
Sasa tujikite na maandalizi ya Fainali ya Kombe la shirikisho Barani Africa dhidi ya RS Berkane.