JAMANI NIPE CHANCE KIDOGO EP 04 Abisai alimrudisha mpaka nyumbani kwao
*Hakikisha umeingia ndani maana ukitoa tu mguu wako nitajua mtandao wangu ni mkubwa
kuliko unavyofikiria. Leyna alishuka kwenye gari kwa hasira na
kubamiza mlango. "Uwe na usiku mwema kipenzi changu. Alisema
Abisai huku akimuangalia. Leyna alienda kwenye dirisha la chumba chako na kugonga.
"Leyla nifungulie mlango.
"Wewe nae ni msumbufu siungelala hukohuko. Wewe usiendelee kuichanganya akili yangu
hapa nilipo nimesha changanyikiwa vya kutosha.
Leyla alinyanyuka na kwenda kufungua mlango. Leyna alimpiga kikumbo na kuingia ndani.
*Wewe vipi mbona unanipamia, Leyna hakujibu aliendelea kutembea kwenda.
chumbani kwake. Alijikaza kitandani huku akiwa
anafyonza fyonza.
"Wewe una shida gani?
Leyna alinyanyuka akakaa.
*Yani nimepata mwanaume kichefuchefu yanΔ± mpaka najuta kumfahamu.
Leyla akitabasamu
Kwahiyo unataka kuniambia umepata kiboko yako?
Aaaah wapi hawezi kujiendesha hivi yani nitahakikisha namnyoosha, Hanijui vizuri.. Kwani huyo mwanaume ni nani na umemtoa
wapi? "Si tuliokotaba huko club tukaanza kupendana,
mapenzi motomoto dada ananipa kila kitu na ukimuona ni bonge la bwana, ana sifa zote za kuitwa mwanaume lakini ana wivu hatari kila
ninapoenda nae yupo yani utafikiri shetani kila
muda Anisa nipo wapi? Lakini ulikuwa unataka mwanaume.
mwenye pesa na sasa imempata ndugu sasa. vumilia hayo mambo madogo.
Unaongea nini wewe, siwezi kuvumilia ujinga amenikuta na mambo yangu ataniacga na mambo yangu.
Baada ya wiki moja majira ya saa mbili usiku mama Leyna na Leyla wakiwa kijiweni wakiuza samaki na Leyna alikuwa mtaani na mashoga
zake huku wakiwa wamekaa na wanaume.
Ilikuwa ni kitendo cha ghafla sana Abisai alishuka na kumkuta Leyna akiwa na kikosi cha
sigara mdomoni.
Alimsogelea na kumpiga kibao cha shavu mpaka ile sigara ikaanguka chini.
Wale wenzake walitaka kuingilia,
"Wewe vipi inawania na kuanza kupiga watu. Tafadhali kaeni mbali na hili atakaesogea kibao kitamgeukia. yoyote
Jamani huyu ni mpenzi wake mambo ya
wapendanao hatuingilii. Walisomea nyuma na kumuacha Leyna. akipambana na mwanaume wake.
"Ukanipigia kama nani? "Shhhh unapoongea na mimi jaribu kushusha sauti yako.
Wewe ni nani mpaka niongee na wewe kwa heshima, mama yangu mwenyewe simnyenyekel iweje uwe wewe?
Maneno ya Leyna yalimaanisha hasira Abisai Alimshika mkono na kuondoka nae. Alienda kumkabidhi kwa vijana wawili waliokuwa
wameshiba kwa mazoezi. "Hashim, Yusuph huyu ni shemeji yenu, mpenzi
wangu mimi mke wangu mtarajiwa. Sasa bro mbona shem amekasirika hivyo na
hana viatu? Tulia Yusuph bado sijamaliza utambulisho..
Abisai alimgeukia Leyna Mpenzi, lazizi wangu, mama wa wanangu.
Leyna aliweka midomo yake pembeni, Abisai akaendelea kutambulisha.
"Hawa ni wadogo zangu. Ni wanajeshi wamemaliza mafunzo yao jeshini na sasa ni
waajiriwa Sasa mimi unanisaidia nini? Alijibu Leyna kwa
dharau.
Yusuph, Hashim naombeni mumfunze adabu shemeji yenu ili ajue jinsi ya kuniheshimu..
*Aaaah bro...
Mmegoma nifanye mwenyewe?
Hapana tutafanya.
"Haya kazi kwenu
Usiku ule ule Leyna akaamuliwa akimbie kuzunguka eneo la uwanja wa nyumba.
Siwezi kukimbia na sifanyi adhabu yoyo.....
Kabla hajamaliza kuongea kibao kizito kilishuka
shavuni kwake mpaka akahisi wenge. "Nyanyuka haraka na uanze kukimbia.
Leyna hakuwa na chagua alianza kukimbia akarushwa kichura, kupiga pushapu na
kurukaruka. Leyna alikuwa amechoka sana.
Jamani nisameheni sirudii tena.
Mbona ndio kwanza tunaanza bado kidogo shemeji maliza kupiga pushapu 20.
Siwezi
"Wewe usitutanie.
Leyna alipiga push up huku akiwa analia jasho na machozi vilichanganyikana. Alipomaliza
alilala hapohapo chini.
Shemeji kipenzi bado kidogo nyanyuka. umalizie kukaa hewani. "Sasa nakaaje hewani.
"Hashim muenyeshe shemeji yetu kipenzi. Hashim alimuonyeshea mfano alipanda hewani kama vile amekaa kwenye kiti.
Leyna alifanya mara moja na kuanguka wakimuamuru arudie tena lakini baada ya muda miguu ilitetemeka na kuanguka chini.
"Nyanyuka haraka...
*Basi inatosha kwa leo.
Alisema Abisai huku akinyanyuka kwenye kiti na kwenda kumnyanyua. Alimbeba juu na kuingia naye ndani.
Wakati huo taarifa zilifikia mama Leyna na Leyla. Yani kapigwa kibao na kusombwa kama
mtuhumiwa.
Jamani sasa huyo mwanaume ni nani na kumpeleka wapi? Mama Leyna alionekana kuwa na hofu.
Mama huyo ni mwanaume wake acha kujipandisha presha.
"Huyo mwanaume unamjua?
*Hapana
Daaaah huyu mtoto atakuja kunisabanishia kifo cha ghafla. "Mama tulia atarudi.
Japokuwa Leyna alikuwa akimsimbua mama.
yake lakini alikuwa na wasiwasi juu ya usalama wake sababu mzazi ni mzazi tu
Abisai alipompelekea ndani akamjalisha. kitandani
"Pole kwa mazoezi mke wangu. Aliyoambiwa hivyo Leyna alikuwa kwa hasira.
"Basi mpenzi wangu.
Toka hapa nakuchukia Abisal.
Mimi nakupenda mpenzi wangu sasa ngoja
nikupeleke bafuni ukaoge ilinipate nguvu. Alimchukua tena na kumpeleka bafuni, Leyna
alioga alipomaliza akatoka na kukuta Abisai akiwa anamuangalia abaya zuri tena la bei ghari. Utavaa hii mpenzi alafu utakuja tupate chakula.
pamoja.
Leyna hakuwa mbishi alivaa nguo akiyoandaliwa. na kujitanua vizuri kisha taratibu akitembea huku miguu yake ikiwa inakosa nguvu.
Alifika sebleni akamkuta Abisai akiwa na ndugu
zake wanakula. Shemeji njoo tuungane pamoja, njoo tule. shemeji
Hashim na Yusuph walimchangamkia na. kumuonyesha kumjali wakati huo yeye aliwaona kama mashetani wawili wenye mapembe.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni