Basi baada ya kutaka kuingia ndani nilikutaka na kelvin siyo kulutana naye tu nilikutana naye kanitolea macho kama fundi saa aliyepoteza nati muda huo tayari nimeshajilia vya kujilia sasa mwepesi kama karatasi ...
" ulikuwa wapi lucy?
" nilikuwa nje kwani vipi?
" nilikwamhia nini?
" kuhusu nini tena mbona kama unaniendesha hivo?
" nachojali ni maisha yako shemeji"
" hebi we kaa kimya maisha gani ? Kuhusu nini? Shemeji kwanani? Kwa marehemu au ? Aliyekufa kafa ....
Nilikuwa nimeshaanza kuona kama anaanza kunichoreshea maisha sasa ngoja kidogo ajuwe kuwa mimi ni chizi mi kila siku namuomnba hataki katokea mtu ambaye matawi anayotua na mimi natua kwanini Nisiruke naye ?
" unamjua kaka yule uliyefanya naye hako kamchezo?
," hapana simjuwi kasema anakaaa nyumba ya jirani hapa
" hapa! Mmmmh hapana hapa anayekaa yupo nje ya nchi na ni mzungu sasa huyu sio wa hapa "
NIlishtuka sana na akanambia niingie ndani huyu jamaa ni mpelezi.niliogopa mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio nikajua tayari nimeyakanyaga rasmi na sasa hakuna jinsi zaidi ya kukubali kuwa ujinga wangu ndio umeniponza....
Nilitulia ndani yeye akiwa anatoka nje kwenye kutazama tazma mazingira kama yako sawa nilitulia tuli huku natetemeka sana.Uoga umenishika mpaka kucha zinatetemeka mmmmmh yaani sio powa ........
Mara ghafla zikasikika sauti ya vin'gora vya polisi eneo ambalo tulilokuwa tunaishi zilionekana gari nyingi sana eneo la tukio nilijawa na mawazo sana nikajua kutokana na uzembe wangu sasa naenda jela kuja kuchungulia dirisha la pili yule jamaa ambaye alijifanya anafanya kazi za maua ....kumbe ni askari mpelelezi na mission yake ilikuwa ni kunitafuta mimi na sasa kanipata na kajua napo ishi .....
Basi waliizunguka nyumba haraka lakini nilishtuka baada ya kuona kelvin hayupo na nyumbani kanisusia . Kumbe lelvin baada ya kuona kwamba siwezi kuwa msaada kwake kwa tabia yangu ya umalaya sasa hakuwa na muda tena na mimi aliamua achore yaani akimbie alijuwa wote tutaenda jela
Mimi kwa kosa la kuwatorosha wafungwa wawili na yeye kunitorosha mimi na kunihifadhi kwa makusudi.pia kwa kuua askari wengi sana kutokana na kutaka kunikomboa mimi aliacha barua chini ya meza
" pambana ujiokoe lucy mimi nimeshindwa kutokana na tabia zako nenda kaoze jela byeeee"
Nilianza kulia huko nje polisi wanataka nitoke nje mwenyewe niliona sasa hakuna namna hakuna mtu wa kunisaidia nilipiga hatua mikono ipo kichwani kwangu sina namna nishajikatia tamaa na sina uamuzi mwingine . Kweli nilikamatwa na kupelekwa mahakamani
Huko nikahukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa makosa ya uhaini mpaka navoongia hivi niko jela naomba wanawake wenzangu muyaache haya mtaishi vizuri mwenye masikio amesikia mwenye macho ameona .jifunze vitu hivi
1. UREMBO WAKO HAUPASWI KUWA TIKETI YA KUTUMIKA
Wanawake wengi huamini kuwa urembo ni silaha ya kupata mapenzi au hata pesa pia , lakini kwa baadhi ya wanaume hususani matajiri na wenye mali nyingi huwa tumia wanawake kama chombo cha starehe na wanawake tumekubali hilo ndio maana tuko tayari kufanya chochote ilimradi tu tupata tunachotaka mwisho wa siku tunaishia kudhalilika hamuoni connection mitandao au mambo mengine ambayo wanawake wanayafanya na kujidhalilisha wenyewe tuishi kwenye misimamo , urembo si fursa ya kujidhalilisha tubadilike ......
2. Pesa kwa sasa ndio fimbo inayotumika kwa wanaume wengi kutuadhibu .....
Mimi ni lucy lakini kuna lucy wengi sana nchi hii ambao tunawaona mitandaoni mara oh sijuwi nauza nini sijuwi nafanya nini .wengine wanaanika picha zao za utupu mitandao yaani kukaa uchi kwao ni ajila thamani ya mwanamke sasa haipo yaani tunaonekana ni wadhaifu sana hususani linapokuja suala la pesa tuko tayari kufanya chochote kile tuzipate nipo jela ila nimeyashuhudia mengi mwisho wa umalaya ni aibu,magonjwa na hata kifo na kupotezea wale watu muhimu kwenye maisha yetu
3. USIKUBALI MAPENZI KWA KUHURUMIWA AU KUSAIDIWA
Mwanaume akikutendea jambo zuri au kukusaidia, haitakiwi iwe sababu ya kumlipa kwa mapenzi. Wanawake wengi huingia kwenye uhusiano kwa kulazimishwa na hisia za shukrani. Hilo ni kosa kubwa – usitoe moyo wako kama zawadi kwa mtu aliyekupa msaada wa muda. Na hiki huwakuta wengi penda kujiheshimu na kutunza utu wako sio kila mtu lazima uweke nguo zako za ndani pembeni jiheshimu
KWAKO WEWE MWANAUME ...🥺🥺🥺
4. Siyo Mwanamke Kila Anayekuja Maishani Mwako Anakupenda Wengi Wanakutumia
Wanaume wengi huingia kwenye mahusiano wakiamini wanapendwa, lakini ukweli ni kwamba baadhi ya wanawake huingia kwenye maisha yako kwa sababu una pesa, umaarufu, au vitu vya thamani. Wanajifanya kukujali, lakini wanatazama fursa wanayoweza kupata. Ukikosa hizo "fursa", wanageuka ghafla na kukuacha.Na kibaya zaidi wanaume wengi wamejikuta wakinasa kwenye huo mtego wa wanawake na kutumia pesa nyingi na mwanamke ambaye mwenyeqe ukimuona hana future yoyote na wewe unashindwa hata kusaidia familia yako na hata wadogo zako
👉 Jiulize kila wakati: kama singekuwa navyo, huyu angekuwepo kweli?
5 Usimwonyeshe Mwanamke Kila Kitu Ulichonacho –Mwanamke Anapaswa Kuaminiwa Kwa Majaribio, Siyo Mapenzi ya Ghafula
Wanaume wengi wanapopata mwanamke mrembo, hujisahau na kufungua kila milango ya mali zao, faragha, hata mipango yao ya mbele. Hii ni hatari, kwani mwanamke ambaye hajathibitishwa kwa vitendo, hawezi kuaminiwa kwa maneno matamu tu.Na huwa kuta watu wengi sana hujikuta wanaangukia pua na kujikuta kila kitu hakiendi wakahisi wamelogwa kumbe ni aina ya watu wanaowashirikisha mambo yao ni sawa na wewe kupanga tofali za msingi wa nyumba mwingine anaondoa j hapo nyumba haiwezi kukamilika ......
👉 Mwanamke mwenye nia njema atakupenda hata kama hujamwonyesha kila kitu ila mwenye tamaa ataanza kuhesabu unavyomiliki.
6. Usiwahi Kuwekeza Hisia Kubwa Kwa Mtu Ambaye Hajawekeza Japo Chembe Ya Ukweli Kwako
Mapenzi ya upande mmoja ni chanzo cha maumivu makubwa kwa wanaume wengi. Unampenda, unamjali, unamtumikia lakini yeye hayuko tayari hata kubeba nusu ya uzito wa mapenzi hayo. na kingine wanaume kuwa na wanawake wengi sio sifa au umaarufu zaidi zaidi ni mzigo au mateso tu leo huku kesho kule mnajizolea magonjwa yasiyo na maana kitanda sio maisha maisha nikupambana unakuta mvuvi anakesha siku nzima baharini au ziwani lakini hela zote anahonga mchimba madini ,daktari,mwalimu nk maisha sio kitanda tu usikubali kuwa dhaifu kwa kiumbe anayeitwa mwanaume wakunielewa kanielewa
"Asante sana mwandishi kelvin mlowe kwa kuiandika hadithi yangu na kuwapa hadhira natumaini kuna vingi wamejifunza, nakuombea kwa mungu akusimamie kwenye kazi yako ya uandishi unajitoa sana "
Haya yalikuwa ni maneno ya mwisho ya lucy kabla muda wetu wa mazungumzo haujaisha na sasa karudi tena mahabusu na hapa ndio mwisho wa hadithi hii nzuri natumai wengi mmejifunza asante kwa muda wenu kwa upendo wenu na kwa kila kitu hasa hasa support yenu
Naitwa kelvin mlowe ........
Hili ni onyo:
👉 Kama mwanamke haonyeshi juhudi wala kujali, usijilazimishe kumpenda. Mapenzi ni usawa sio mzigo upande mmoja.
XXXXXXXXX MWISHO XXXXXXXXXXXXXXXXX
.