muda huo nataka nimtoe askari wake mara ghafla sauti ya king' ora ilisikika ikionyesha kuna mfungwa katoroka hivyo ilibidi askari wote watoke nje na kwenda kumtafuta . Hivyo hata mimi kwa kuwa licha ya kuwa nesi pia ni mwanajeshi niliambiwa niongozane nao naweza nikabaki wakaniba.... Lakini wasijuwe kuwa kwa sasa ni michezo yangu hiyo na hata haichaguwi viwanja .....
Tulitoka pale nje na tochi zetu nilisimama na kutazama ukuta ambao mfungwa karoka mmmh niliogopa sana na kusema kam katoroka hapa huyu ni jambazi maana ukuta ni mrefu sana na kuna walinzi lakini hawakumuona ....
Nilitoka na kamanda denis muda huo bado nakamzuka ka ule mchezo lakini kutokana na hali yenyewe ilibidi nijikaze nikamilishe kwanza kazi ya watu. Basi safari ilianza ilibidi tuingie msituni kumtafuta huyo aliyekimbia na jina lake anaitwa DICKSON au kwa pale jela walimwita " MCHUMIA JUANI".
Mmmmh matukio yake tu yanavyoonyesha ni kwamba huyu jamaa kajaribu kutoroka sana na aliapa akitoroka sahizi hatutaweza kumdhishika kabisa . Na sasa katoroka kweli .daaah nilikuwa naogopa ...
Nilikuwa natembea nawaza ukuta yule jamaa katukaje maana ni mrefu sana hakuna anayeweza kufanya vile ikiwa kuna walinzi lakini kila nikiwaambia askari wafikilie mara mbili mtu anawezaje kuruka pale hawataki kuelewa.......
Tulizidi kutafuta bila mafanikio kufika mbele Denis bila kutazama nyuma aliniamuru mimi na askari mmoja tupite upande mwingine na yeye na askari mwingine wapite upande mwingine .Nilikubali japo kwa woga tukapita upande mwingine...
Nilikuwa namsemesha kuhusu tukio hlo kwamba mtu hawezi kuruka pale lakini hakuwa ananijibu hata neno moja.zaidi ya kupiga hatua kwenda mbele .Lakini nilianza kushangaa mbona huyu kamanda haongei kabisa na kazi ni kusaidiana?
Nilipiga hatua mbele kidogo baada ya kuhisi mchakacho wa majani yeye alikuwa yupo nyuma nilifunua majani lakini sikuona kitu yule askari akawa anakuja nyuma yangu .
" una akili sana kuliko hawa askari wote, ungekuwa kamanda mkuu ungenikamata kwa kuwa wewe ni kibaraka huwezi kusikilizwa".
" kumbe alikuwa ni mchumia juani???
Niliogopa maana tayari bunduki ipo mgongoni mwangu na haja inaweza kutoka maaana ..,.....
Itaendelea .......
.
Maoni