Walipofika mlango wa kuingilia ukumbi, mlango mkubwa wa kioo ulifunguliwa kwa heshima.
Ndani kulikuwa kumepambwa kwa mapambo meupe na ya dhahabu, maua, taa za kung'aa, na meza zilizopangwa kwa umaridadi wa hali ya Juu.
Prisca alihisi miguu ikitetemeka. Aliinama.
kidogo kuangalia pete iliyokuwa kidoleni mwake.
"Ni kweli haya yananitokea mimi? Alijisemea.
Jimmy alimsogeza karibu na kumnong'oneza,
"Leo ni siku ya furaha Wewe ndiye malkia wa usiku huu naomba usiniangushe.
Wakaingia ukumbini Watu walishangilia, wengine wakapiga makofi, na wengine waliwaangalia kwa mshangao. Kamera ziliwaka kila kona.
Prisca kijasho kilimtoka alikuwa akitetemeka kwa hofu lile jambo lilikuwa kubwa kuliko alivyokuwa amejichukulia. Alimwangalia Jimmy na kuuliza kwa sauti ya chini
"Mbona kila mtu anatuangalia?
"Leo ni usiku wa wetu nataka ulimwengu ujue kuwa wewe ni sehemu ya mafanikio yangu. sitaki mtu afutilie mashaka.
Jimmy alitabasamu kisha akajibu,
Prisca alibaki mdomo wazi.
"Jimmy sijui hata kama naweza kuvumilia.
watu "Shhh... Umeshafika hapa ona wanavyokuangalia, Wewe ndiye staa leo.
Walienda kukaa kwenye viti walivyoandaliwa na mtangazaji wa shughuli hiyo alitangaza kupitia kipaza sauti.
"Kwa mara ya kwanza tunawatambulisha rasmi JIMMY & PRISCA AU MR AND MRS JIMMY.
wanando wapya. Ukumbi mzima ukalipuka kwa shangwe..
Prisca alihisi mapigo yake ya moyo yakienda mbio, Alichanganyikiwa. Jimmy alitambua kuwa
hayupo sawa alimsogelea na kumnongoneza. "Ondoa hofu Kuwa kawaida tafadhali.
Prisca alijikaza akaanza kutabasamu.
Sherehe iliendelea kufana jimmy alisimama
kwenye nafasi yake kama bwana harusi kweli
alikuwa alimshika Prisca kwa kuiachia na hasa
kumpiga mabusu bila kuogopa.
Ukifika muda wa walitakiwa kwenda kucheza.
Walinyanyuka na kusogea mbele, jimmy alisogea na kumshika kiuno wakaanza kucheza taratibu
huku waliangaliana usoni. Prisca alikuwa anaona aibu.
"Usione aibu haya ni maigizo tu.
Prisca alijikaza mpaka sherehe ilipokuwa kuisha Ilikuwa Mida ya saa sita usiku. Walitoka ukumbini na kwenda kupanda kwenye gari ya
Jimmy.
"Inaelekea wapi?
"Kwa sasa siwezi kwenda nyumbani nimpeleke hoteli.
"Sawa.
Walienda mpaka kwenye hotel ya knigh hotel..
Hoteli yenye hadhi.
Jimmy alichukua chumba kisha akamsindikiza mpaka chumbani.
Jimmy alitoa bahasha na kumpatia.
"Malipo yako ni haya.
Prisca alipokea ile bahasha na kushukuru. "Tutaonana kama imepangwa tuonane tena. Alisema jimmy kisha akaondoka
Usiku ule Prisca alilala pake hotelini Kesho yake asubuhi aliamka na kujiandaa kisha akarudi nyumbani kwao.
Alipoingia tu ndani akakutana na sura ngumu ya kaka yake Deo pamoja na mama yake. Prisca alijua hakuna usalama alisimama mlangoni huku akiwa kamshikilia mlango.
"Kilichikugandisha hapo ni kipi? Mama yake aliuliza kwa sauti ya ukali?
Prisca aliachia mlango na kupiga hatua ndogo ndogo alisogea alipo mama yake.
"Hivi umelala wapi? Deo aliuliza
"Nilimuacha mama nilienda kusoma
"Una uhakika na hicho unachokisema?
"Ndio, siwezi mama si. Nilikuaga? "Hukunian Ila kuwa unaenda kuolewa. Prisca alivyosikia hivyo alishituka.
"Unashika nini?
"Hamna mimi sijaolewa. Prisca alikataa lakini kwa bahati mbaya pete ya ndoa aliyovalshwa na
Jimmy bado ilikuwa kwenye kidole chake.
"Hilo bati laki ni kuthibitishia cha kwanza pia kuna picha nyingine hapa.
Deo alitoa simu na kumuonyesha picha zote za ukumbini. Prisca hakuweza kubisha lakini alijiuliza kaka yake ametzipataje pataje zile picha.
"Wewe mimi siwezi kuishi na mke wa mtu hapa. ndani nenda kachukue kila kitu chako uende kwa mume wako.
"Jamani mama...
We hakuna cha mama hapa unatakiwa. kuondoka.
"Lakini yule sio mwanaume wangu ilikuwa ni dili tu.
"Sisi hatujui hilo twende kwa huyo mwanaume. wako.
"Mimi sijui anaishi wapi.
"Leo itajulikana.
Jamani kaka Deo.....
"Prisca usitake nikuvute na mapanga naomba usimame tuondoke...
Prisca hakubisha alikuwa anamjua vizuri sana kaka yake.
"Usisahau begi lako.
"Mama hilo achana nalo litamfuata nyuma.
Prisca aliondoka vile vile wakaenda kupanda kwenye pikipiki na hakujua wanaelekea wapi maana yeye mwenyewe alikuwa hajui wapi kwa kumpata Jimmy..
JE NINI KITAENDELEAAA!! "
OFAAAA KUPATA YOTE NI 1000 TU UNAPATA MPK MWISHO KABISA
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments