Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  SIRI YA HUBA ( Official song 1, Audio by Doyy )

⚠️ ONYO: Hadithi hii inafaa kwa watu wazima tu. Zawadi Sehemu ya 1

27th Jul, 2025 Views 58





Kwa majina naitwa Zawadi juma, mzaliwa wa Mkoani Pwani, Mtwara. Mama yangu alinizaa akiwa ameolewa na baba, lakini walitengana nilipokuwa darasa la nne. Baba alioa mwanamke mwingine na kuanza naye familia. Mama alipokuwa darasa la sita, naye akaolewa tena. Baada ya mama kuolewa, mumewe alisema hataki niishi nao, akidai kwamba ikiwa nitaishi nao, baba yangu mzazi na mama wataendelea kuwasiliana kwa kujifanya wananihusu. Hivyo, nikaenda kuishi na bibi yangu, mama wa mama, katika kijiji cha Mwagusi.
Mama alikuwa anajitahidi sana kunihusisha, lakini hakuwa na kazi ya kudumu, alifanya biashara ndogo ndogo ambazo zilimudu tu pesa kidogo, ambazo hazikutosha mahitaji yangu yote. Maisha kwa bibi yalikuwa magumu sana—kilimo cha mtindo mmoja na chakula cha aina moja, lakini niliridhika. Baba yangu hakuwa na muda nami kabisa; hakuwahi kunijali wala kunijulia hali, alikuwa busy na mambo yake. Mama alipata watoto wengine wawili, na hivyo nikawa na wadogo wawili upande wa mama na watatu upande wa baba. Baba yangu alikuwa fundi wa ujenzi, akajitahidi kuwalea wanawe waliokuwa wanaishi naye, lakini sio mimi.
Siku moja, nilifukuzwa shuleni kwa kukosa ada ya dawati na viatu. Nikaenda kwa mama, akasema, “Mwanangu, sina hata mia. Nenda kwa babako, muombe akupe hata kidogo.” Nilimudu kumudu mama yangu kwa sababu alikuwa akinipa pesa za matumizi madogo madogo, na akipokosa, alikuwa amekosa kweli. Nilitoka hadi kwa baba, ambaye alikuwa anaishi kijiji cha pili, Mwang’ombe, toka kwa bibi yangu. Nilipofika, nilimkuta baba akichinja ng’ombe kwa ajili ya kuuza, kwani alikuwa akifuga na kuuza nyama. Kulikuwa na wateja wakisubiri. Aliponiona, akasema, “Wewe umefata nini hapa?” Nikasema, “Shikamoo, baba.” Akasema, “Nakuuliza umefata nini?” Nikasema, “Baba, samahani, nimefukuzwa shuleni kwa kukosa mahitaji.” Akasema, “Leo ndiyo umejua mimi ni baba yako? Nenda, toka hapa! Najua mama yako amekutuma uniroge, ndiyo maana umekuja, si ndiyo? Toka haraka!” Wanawe waliokuwa hapo wakanifukuza. Nilijisikia vibaya sana, nikaondoka nikilia.
Nilipofika kwa bibi, aliniona nikiwa na huzuni, akasema, “Zawadi, kuna nini, mbona uko kama umetoka msibani?” Nikasema, “Bibi, yule mzee Mwajuma ni baba yangu kweli?” Bibi akasema, “Kwa nini unauliza?” Nikasema, “Amenifukuza nilipoenda kuomba pesa ya viatu na mchango.” Bibi akasema, “Mjukuu wangu, msamehe, yeye amechanganyikiwa na mambo yake ya maisha, ndiyo maana anafanya hivyo. Sawa?” Nikasema, “Sawa, bibi.” Akasema, “Chukua hiyo mbaazi, peleka kwa Mzee Rashidi, mkewe alitaka niwauzie. Akikupa pesa, utapeleka mchango shuleni.” Nikasema, “Asante sana, bibi. Nichukue kiasi gani?” Akasema, “Chukua gunia moja, mjukuu wangu.”
Nilipima mbaazi, nikaenda kwa Mzee Rashidi. Nilimkuta mkewe, Bi Halima, pale. Akanikaribisha, nikamwambia, “Bibi amenituma na mbaazi.” Akasema, “Nilishawiana naye, ziweke jikoni huko.” (Mzee Rashidi alikuwa mtu wa uwezo kijijini.) Nilipelekwa jikoni, nikaweka mbaazi chini, nikashangaa na jiko lilivyokuwa kubwa, kubwa kuliko hata chumba changu au sebule ya bibi yangu ya udongo. Kulikuwa na vyombo vichafu sana jikoni. Nikiwa nashangaa, Bi Halima akaja, akasema, “Unaitwa nani?” Nikasema, “Zawadi.” Akasema, “Zawadi, unajua kuosha vyombo?” Nikasema, “Ndiyo, najua.” Akasema, “Unaweza kunisaidia kuosha? Msichana wangu wa kazi ameondoka, na mimi nina kazi nyingi.” Nikasema, “Sawa.” Niliosha vyombo vizuri, nikayang’arisha masufuria, nikafanya usafi wa jikoni, kisha nikamwambia yuko sebuleni. Alikuja, akaangalia, akafurahi sana. Alikwenda chumbani, akaleta pesa, akasema, “Hizi ni za mbaazi, na hii nunua viatu vya shule.” Nilishukuru sana. Aliniona nimevaa kiatu kilichochakaa, vidole vikakanyaga chini. Akasema, “Zawadi, ukiwa unakuja kunisaidia kazi, nitakusaidia matumizi yako.” Nikasema, “Nitakuja.” Akasema, “Nitafurahi.”
Nilirudi nyumbani, nikamwambia bibi kile Bi Halima alichosema. Bibi akasema, “Sawa, mjukuu wangu, jitahidi ili akusaidie.” Nikaanza kwenda kwa Bi Halima kila nikitoka shuleni, naye akawa ananisaidia nguo za shule na vitenge vya bibi. Nilifika darasa la saba, bado nafanya kazi kwa Bi Halima kila nikitoka shuleni. Siku moja, Jumamosi, nilikuwa nafua nguo kwa Bi Halima, mara nikaskia geti lik Rowlingstone ikagongwa kwa fujo. Bi Halima alikuwa ndani, akatoka, akasema, “Nenda kafungue!” Nikasema, “Sawa.” Nilikafungua, nikakutana na baba akiwa na panga mkononi. Akanisukuma, akasema, “Yupo wapi huyo anayeajiri watoto wadogo kufanya kazi? Ni mimi nizae yeye, akufanye msichana wa kazi?” Akanoa panga chini... Itaendelea

Sehemu ya 2
Nikasema, “Baba, mbona umekuja na panga?” Alinikimbilia, akasema kwa kelele, akanizaba kibao. Bi Halima alikuwa nje, lakini alipomuona baba, alikimbilia ndani. Baba alitukana, “Toka nje, mpumbavu! Mnajifanya matajiri, unaajiri mtoto mdogo bila aibu? Toka nikuoneshe uchungu wa mwanangu! Mnawapa watoto kazi za misukule ili muwe matajiri, si ndiyo? Washenzi!” Akanoa panga uwanjani, akasema, “Wewe, nenda nyumbani haraka!” Nikaanza kuondoka, naye akaniandama.
Tulifika kwa bibi, akasema, “Ingia ndani, chukua nguo zako, unaenda kukaa kwa nyanya yangu kwa sababu huyu bibi ameshindwa kukulea.” Sikutaka kwenda, lakini baba alikazania, “Nitakukata miguu, mpumbavu!” Bibi akasema, “Kwa nini unafanya hivyo? Nimemlea mtoto huyu tangu mdogo, leo unanitusi?” Akasema, “Ungejua kulea, ungempeleka afanye kazi kwa watu akiwa na umri huu? Mimi ni babake, nina haki naye. Beba vitu, twende haraka!” Bibi akasema, “Mjukuu wangu, mtii baba yako, chukua nguo zako.”
Nilikwenda kuchukua nguo, nikaweka kwenye gunia la zamani. Nililia, nikamuaga bibi, akasema, “Nenda salama, mjukuu wangu.” Baba akasema, “Sitaki ukarudi hapa tena, utakufa!” Sikumjibu. Tuliondoka hadi kwa nyanya, mama wa baba, huko Msumbiji. Baba akasema kwamba nateseka na kufanyishwa kazi kwa pesa, na mama yangu ameshindwa, ndiyo maana amenileta kwa nyanya. Nyanya akasema, “Hee, ile familia ni ya ajabu sana. Bora uliachana nayo.” Nilijisikia vibaya wakisema hivyo kuhusu ndugu zangu waliyonilea kwa upendo, lakini nilikaa kimya.
Nilipelekwa chumbani, nikaoneshwa kitanda cha ngozi. Nilipolala, kitanda kikadumbukia, nikawa kama nimeingia mfukoni. Nilishangaa—bora kwa bibi mzaa mama kulikuwa na kitanda cha chaga, japo godoro limechoka. Huku ilikuwa maajabu. Nilishindwa kulala, nikaamka nikakaa pembeni. Nikaanza kuona vitu vinaning’ata—viroboto! Nyanya akaja, akasema, “Fanya usafi hapa, walikuwa wanalala kuku, kuna viroboto.” Niliamka haraka, nikaenda jikoni kutaka kuwasha moto wa kuni. Nyanya akasema, “Kaokote kuni kwanza, usiguse chochote!” Nilitoka nje, kwani nyanya aliishi karibu na msitu. Nikaokota kuni, nikachota maji mara nne, kisha nikawasha moto na kuinjika maji.
Nilikwenda kufagia chumba cha vumbi, kilichokuwa na makolokolo mengi. Nikatoa kitanda na nguo zangu nje, nikamwagia maji chumbani kila kona. Chumba kikawa tope, nikatoka nikachukua udongo, nikalisiliba vizuri hadi kikapendeza. Ilipofika saa sita mchana, nyanya akasema, “Pika mboga ya majani ya maboga na ugali.” Nikaingia jikoni, nikapika, nikamaliza, nikamwita nyanya. Tulikula jikoni. Akasema, “Kumbe unajua kupika?” Nikasema, “Ndiyo.” Akasema, “Vizuri, sasa kila kazi ni yako hapa, mimi sitofanya chochote.” Nikasema, “Sawa, nyanya.”
Hakudanganya—nilifanya usafi kabla ya kwenda shuleni, naosha vyombo, nafagia nyumba na uwanja mkubwa, hadi nachelewa shuleni, wakanichapa. Nikirudi, napika na kuchota maji, kwani nyanya hakugusa kitu. Bibi mzaa mama alikuwa anafanya kazi nyingi, lakini huyu nyanya alikuwa tofauti. Alinitukana sana, akimtukana mama yangu na bibi yangu. Siku moja, nilipokuwa naosha vyombo, nikateleza, nikavunja chungu. Nyanya alinipiga sana, akasema, “Utalipa chungu langu! Fanya vibarua, lipa wiki moja!” Nikasema, “Sawa, nyanya.”
Nikaanza kufanya kazi za kulima na kuuza kuni, hadi nikakosa kwenda shuleni. Baada ya siku tano, nilipata shilingi elfu kumi na tano. Nikamwambia nyanya, akasema, “Ilete, mjinga!” Nikampa, akasema, “Usivunje tena!” Nilijisikia vibaya sana. Siku moja, shangazi kutoka kijiji cha Nyerere aliniona nikichota maji, akasema, “Wewe ndiye Zawadi? Una miaka mingapi?” Nikasema, “Kumi na tatu.” Akasema, “Hee, umekua! Ngoja niongee na babako.” Aliondoka.
Baadaye, wabibi wawili walinichukua, wakaniamuru nitoe nguo. Nikasita, wakanilazimisha. Wakanisafisha mwili mzima, kisha wakanipa kitenge cha kujifunga kama lubega. Sikuelewa nini kinaendelea. Tulianza mafunzo ya kulea mwanaume, kuwa mtiifu, msafi, kukata mauno, kupika, na kujiosha. Tulifundishwa mambo mengi kwa miezi mitatu, ikiwa ni pamoja na kupakwa mafuta ya kipekee na kuvutwa visimi kila siku mbili. Nilipata rafiki aitwaye Neema, tukashirikiana sana. Wabibi walitangaza kuwa tunakaribia tukio la mwisho la kumudu mila za kiwao ili tuwe wake wazuri na watiifu. Sikuelewa, lakini Neema akasema, “Nina hisia mbaya kuhusu hili.” Nikasema, “Tutuone.”
Siku iliyofuata, tulipikiwa chakula na vinywaji vya asili, tukacheza ngoma za kitamaduni. Siku iliyofuata, saa tisa usiku, tuliamshwa na kupelekwa uwanjani tukiwa na kanga tu. Mioto iliwashwa, ikatoa mwanga wa kutosha. Tulipangwa kwenye foleni mbele ya wabibi. Sikujua nini kinaendelea. Mara mtoto mmoja akaanza kulia kwa nguvu. Nikamuangalia, nikakuta anakatwa kisimi. Nilitetemeka, nikamwambia Neema, “Hii ni nini?” Akasema, “Tunakatwa.” Nilishtuka, kwani tulikuwa tumejifunza kuhusu ukeketaji shuleni. Watoto watatu waliokatwa, nikawa wa nne… Itaendelea.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

⚠️ ONYO: Hadithi hii inafaa kwa watu wazima tu. Zawadi Sehemu ya 1  >>> https://gonga94.com/semajambo/onyo-hadithi-hii-inafaa-kwa-watu-wazima-tu-zawadi-sehemu-ya-1
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIRI YA HUBA ( Official song 1, Audio by Doyy )
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest