Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

🔞 Tahadhari: Hadithi hii ina maudhui ya watu wazima na siyo rafiki kwa walio chini ya miaka 18. Hadithi ya Watu Wazima: Zawadi Sehemu ya 5

27th Jul, 2025 Views 34



Mama Zawadi akasema, “Mimi ndiye bosi wako, nitakaye kukupea mshahara, nakuambia ufanye kitu, unabisha?” Nikasema, “Samahani, mama, sikuwa nimeelewa, mama yangu.” Akasema, “Nataka nikuone mwili wako kama huna mambo ya kishirikina kama chale au hirizi.” Nikasema, “Sawa, mama, lakini sina vitu hivyo.” Akasema, “Vua nguo sasa.” Nikatoa nguo, nikabaki uchi kabisa, kwani hata chupi sikuwa nayo. Akanitazama, akasema, “Geuka.” Nikageuka, akaangalia, kisha akasema, “Vaa nguo zako.” Nikavaa. Akasema, “Na chupi je?” Nikasema, “Sina, mama, nyumbani hawajawahi kuninunulia.” Akasema, “Umevunja ungo?” Nikasema, “Hapana, mama.” Akasema, “Umemaliza shule lini?” Nikasema, “Mwezi wa kumi mwaka jana.” (Muda huo ulikuwa mwezi wa kwanza mwaka mwingine.) Akasema, “Unaitwa nani?” Nikasema, “Zawadi.” Akasema, “Sawa. Nitakupa nguo na vitenge, na utavaa nguo bila vitenge kila wakati, sawa?” Nikasema, “Sawa, asante sana, mama.”
Akasema, “Nifate jikoni, muda wa kupika umefika.” Nikasema, “Sawa.” Nilienda jikoni, kila kitu kilikuwa kigeni kwangu. Alinifundisha kuwasha jiko la gesi, kufungua friji, akanionyesha vyombo vilipo na makopo ya chumvi yaliyokuwa kwenye makabati ya juu na chini. Alinifundisha kusaga juisi na kutumia mashine ya kupikia wali. Alinionesha mambo mengi hadi nikahisi kuchanganyikiwa. Akasema, “Unajua kupika?” Nikasema, “Ndiyo.” Akasema, “Sawa, kama ni hivyo, itakuwa vizuri. Pika wali, nyama imeshapikwa.” Alinipa maelezo ya haraka kuhusu jiko.
Nilichukua nyanya, vitunguu, karoti, na pilipili hoho kama alivyoniagiza. Alikuwa na makopo ya mchuzi na viungo vingi. Nilijaribu kupika wali, lakini nikaboronga—ulikuwa kama boko boko. Mama alikuja kuangalia kabla chakula hakijaenda mezani. Alipouona, alinizaba kibao, akasema, “Mshenzi, unachezea chakula? Hii ni nini umepika? Huu ni ugali au wali? Kwenu mnapika hivi?” Nikasema, “Hapana, mama, samahani, sikuweza kuelewa jiko la wali.” Akasema, “Mpumbavu sana! Kwa nini usiulize? Sasa utakula hiki chakula wiki nzima. Mchele ni bei ghali, naunua kwa pesa, sio mawe! Hamisha wali huu, nioshee kisufuria cha rice cooker haraka!”
Nikahamishia wali kwenye bakuli, nikaosha kisufuria. Yeye akapika wali upya na mboga mpya, kwani sikuweza kuipika vizuri. Aliniambia niandae meza, nikaandaa kama alivyoniagiza. Alipomaliza, akasema, “Chakula chako ni hicho ulichopika, na mboga subiria tule tukimaliza, ikibaki utakula. Nyama ni ghali mjini.” Nikasema, “Sawa, mama, asante.”
Tukiwa tunaongea, tulisikia honi. Akasema, “Mume wangu anakuja, kumbuka nilichokuambia.” Nikasema, “Sawa, mama.” Nilibaki jikoni, yeye akaenda sebuleni. Baada ya muda, nikaskia mlango wa sebule ukifunguliwa. Nikasikia, “Wow, mume wangu, pole na kazi.” Baba akasema, “Asante sana, nimechoka sana, mke wangu. Niandalie maji ya kuoga.” Mama akasema, “Sawa, usijali, bby wangu.” Mara nikaskia, “Zawadi! Zawadi!” Aliniita. Nilikimbia sebuleni, nikapiga magoti huku nimeinamisha kichwa chini. Mama akasema, “Mume wangu, huyu ndiye mfanyakazi niliekuambia.” Baba akasema, “Hujambo?” Nikasema, “Sijambo,” huku bado niko chini, hata sura yake sikuiona. Akasema, “Mbona unaangalia chini? Nitakujuaje sura?” Sikujibu, bado niko chini. Akasema, “Haya, nenda.” Nikanyanyuka, nikarudi kinyumenyume jikoni.
Maisha yalianza hivyo. Siku hiyo, watoto wao hawakurudi, walikuwa wametembelewa na ndugu, lakini kesho yake walirudi. Nilikuwa kama nafanya kazi kwa bidii kama muhindi, nikipelekeshwa hata na watoto wadogo kuliko mimi. Nilivumilia, kwani sikuwa na pa kwenda. Nilizoea mazingira, nikachanganya na ujuzi wa unyago, nikawa nafanya kazi vizuri sana. Mama alipotoka na kurudi na wageni, alikuta nyumba safi, chakula safi, wakanisifu kuwa ana binti anayejitambua.
Nikiendelea kuishi hapo, nilikua huku nikivaa magauni makubwa aliyonipa mama, akiniambia ni marufuku kumudu mume wake usoni. Miezi sita ilipita, bila msaada wala kutoka popote isipokuwa duka la jirani. Mama Zawadi alikuwa akininyanyasa sana. Siku moja, kulikuwa na sherehe nyumbani. Aliniambia, “Utakaa chumbani, sitaki utoke hata dakika moja, utakula wageni wakiondoka, sawa?” Nikasema, “Sawa, mama.” Nilifanya kazi zangu, nikapanga kama alivyoelekeza, kisha nikajikalia chumbani, nikapumzika.
Sherehe iliendelea, nikaskia muziki. Nikichungulia, nikaona watu wanakula, wanakunywa, shangwe tupu. Mabinti waliokuwepo walionekana kama familia bora, nikatamani kuwa kati yao. Nikiendelea kuchungulia, mlango ukafunguliwa. Mama akaingia, akasema, “Mshenzi, unachungulia nini? Sikuambiaje? Unataka watu wanionaje? Njoo hapa!” Alinikamata, akaanza kunipiga. Akaona haitoshi, akachukua skarf (kiatu kirefu), akanipiga magotini na miguuni. Nilipiga kelele, “Mama, nisamehe, sio tena!” Akasema, “Unataka kuniaibisha, si ndiyo? Mshenzi, una tabia mbovu!” Nikasema, “Hapana, mama, nisamehe!” Nililia, damu ikivuja usoni, nikiwa na mialama ya vipigo.
Akasema, “Nikuone unatumbua macho yako makubwa kama mbwa kasoro mkia! Umekuja kufanya kazi, sio kuchungulia wageni!” Aliniacha, akatoka. Magotini navuja damu, bila mshahara, nguo za mtumba zimechakaa. Nilijuta kuzaliwa, nikawakumbuka mama na bibi yangu, bila njia ya kuwaona. Nililia hadi nikapitiwa na usingizi. Nikiamshwa kwa kumwagiwa maji baridi ya friji, akasema, “Amka, usafi hautojifanya! Unalala kwenu kuna godoro kama hiki? Amka!” Nilijikaza, magoti yakiwauma, akanisukuma, “Fanya haraka!”
Nilitoka nje, kulikuwa chafu—vyakula vimewagika, chupa za vinywaji. Nilianza kufanya usafi huku nalia. Maumivu yalizidi, nikakaa chini nikajifunua magoti, nikaanza kuangalia huku nalia. Niliimba wimbo wa huzuni, sikujua nilipata wapi. Mara nikaskia sauti nyuma, “Zawadi, umefanya nini miguu hiyo?” Nikastuka, nikageuka—alikuwa baba wa nyumba. Nilimuangalia, ingawa niliambiwa nisimudu usoni. Nilitaka kunyanyuka, lakini nikadondoka kwa maumivu. Baba alinidaka, akasema, “Taratibu, umefanya nini? Umeshapata dawa?” Alinikokota hadi kwenye kiti kilichobaki nje. Nikasema, “Naweza kutembea, baba, usijali.” Akasema, “Unaweza wapi? Nakuuliza umefanya nini?” Nikasema, “Nilianguka kwenye kokoto.” Akasema, “Kokoto wapi? Ndani hakuna kokoto!” Nikilia, machozi yananitoka. Mara mama akaja, akasema, “Heee! Kiruuu! Nini kinaendelea? Zawadi, unafanya nini na mume wangu? Yesu na Maria leo!” Itaendelea
Sehemu ya 6
Baba akasema, “Umeona huyu mtoto alivyoumia, au unaongea tu?” Mama Zawadi akasema, “Ameumia nini? Nani amemudu?” Akasema, “Mimi ndiyo nimemudu, si ndiyo?” Baba akasema, “Nimesema yeye kaniambia? Mbona unajistukia? Au wewe ndiye umemfanyia hivi?” Nikasema, “Ndiyo, alinituma nje, nikagongwa na pikipiki, nikaanguka.” Baba akasema, “Unaona sasa, Mama Zawadi? Mtoto wa watu ameumia, anaweza kuwa na vidonda vingi. Twende naye hospitali!” Mama akasema, “Haina haja ya hospitali, kuna dawa ndani, nitampaka na kumudu kama ana vidonda vingine.” Nikasema, “Sina, mama, asante.” Baba akasema, “Nenda kalete dawa haraka tumpake.”
Mama aliniangalia kwa macho makali, kama anasema, “Ama zako, ama zangu,” akaondoka. Alileta dawa—sijui ni ya nini. Baba akasema, “Mpake vidondani.” Alinisugua vidonda, dawa ikiwauma sana, nikajikaza nisipige kelele, kwani alinikata macho makali. Baba akasema, “Mbona unamsugua sana, Mama Zawadi? Magoti ni ya binadamu, na dawa hiyo inauma! Kama huwezi, niache nimpake.” Mama akasema, “Una nini na huyu msichana? Mbona unamudu sana? Sikuelewi!” Baba akasema, “Una maanisha nini? Unaongea na nani kwa sauti hiyo? Unataka kusema nini?” Mama akasema, “Nimetoka, nimekukuta unamkumbatia, unataka kumpaka dawa, una nini naye?”
Baba akasema, “Nitakupiga, mwanamke! Unanichukuliaje? Una wivu hata kwa dagaa kama hawa? Kichwa chako kimejaa ujinga!” Akasema, “Ulitaka nimuache mtoto anayetutunzia nyumba, anatupikia, anafua? Wewe ulishindwa hata kuosha vyombo kwa uchukuzi wako na mikucha bandia! Masai ndiye anafanya usafi hapa. Unajua huyu akitaka tufe, tunakufa sekunde moja? Watoto wakirudi boarding, akitaka, tunakufa wote! Kumudu imekuwa kesi?” Alifoka, akaondoka. Mama akamfata, akisema, “Samahani, mume wangu, sikuwa na maana hiyo.” Baba akasema, “Una roho mbaya, kichwa chako kimejaa ujinga! Sitaki kukaa nawe, acha nikalewe huko. Na huyu mtoto sitaki afanye kazi hadi apone.”
Akaita, “Masai!” Masai akaitika, akasema, “Fungua geti, hakikisha uwanja ni safi.” Masai akasema, “Sawa, mseee.” Akakimbia kufungua geti. Mama alibaki amesimama. Nilijikaza, nikaokota uchafu. Mama akanishika mabega, akasema, “Wewe, litoto, unanifanyia nini?” Nikasema, “Amenikuta nimekaa, sikuwa nimemwambia.” Akasema, “Njoo hapa!” Akanivuta kwa nguvu ndani, akanipiga upya, akining’ata mgongoni. Nililia, nikiomba msamaha. Mara tukaskia honi nje ya geti. Alistuka, akasema, “Kelele, mshenzi! Jifunike, ulale, usiseme kitu!” Alitoka chumbani.
Nililia sana, nikawaza, “Hapa sio pa kuishi, ataniua! Bora nitoroke, siwezi kukaa hapa.” Nilikaa chumbani, sikujua nini kinaendelea. Mlango ukagongwa, Masai akaingia. Akanikuta nimejifunika, nalia. Akasema, “Zawadi, pole, usilie, mama. Huyu mama ni mnyanyasaji sana na ana wivu!” Nikasema, “Asante, Masai. Naomba unisaidie, sina pa kwenda.” Akasema, “Usiondoke, mjini ni magumu. Ukienda, utaishia mikononi mibaya. Hapa nitakusaidia—kula, kila kitu. Anakulipa mshahara?” Nikasema, “Hajawahi.” Akasema, “Nitaongea na mseee, ananilipa kila kitu, hana shida. Si unaona ni kijana tu?” Nikasema, “Usimwambie, leo nimepigwa na kung’atwa kwa sababu ya baba. Nisaidie wewe tu, sawa?” Akasema, “Usijali, Zawadi.”
Akasema, “Na mbona una damu kwenye nguo?” Nikasema, “Alinikata, ndiyo maana.” Akasema, “Mama muuaji huyu! Ipo siku nitampiga hadi mseee amsahau!” Akasema, “Nakuja, naenda kukutafutia dawa. Siku nne, vidonda vitapona.” (Aliongea kwa Kimasai.) Nikasema, “Asante, Masai.” Akasema, “Usiogope, nipo na wewe.” Nikasema, “Asante sana.”
Baada ya dakika kumi, alirudi na majani. Akasema, “Nitakupaka siku nne, vidonda vitapona.” Akaponda majani, akanipaka magotini. Nikaenda bafuni, nikatoa gauni, nikaja na kitenge. Akanipaka mgongoni kwenye vidonda vya kung’atwa, akasema, “Zawadi, unajua uko mzuri sana, na shepu kama wacheza muvi wale wa matako makubwa.” Nikacheka, nikasema, “Acha bana!” Akasema, “Napenda watoto weupe, na wewe ni mweupe. Kwenu wapi?” Nikasema, “Mtwara, lakini wewe ni mkubwa kwangu, unaweza kuwa baba yangu!” Akasema, “Kweli, nina watoto kama wewe, mwingine mkubwa kuliko wewe, wako Longido.” Nikasema, “Unaona sasa?” Akasema, “Nimekusifia tu, uko mzuri sana kuliko Mama Zawadi, ndiyo maana anakupiga. Na macho yako makubwa yanaremba!” Nikasema, “Umekaa hapa, mama yuko wapi?” Akasema, “Ametoka na rafiki, usijali. Ngoja nikakuletee chakula.”
Alirudi na sahani ya tambi, kuku, viazi vya kukaanga, soseji, na mishkaki, pamoja na soda baridi. Akasema, “Hii ndiyo walikula shereheni, kula, mwanangu.” Nikasema, “Asante sana, Masai.” Akasema, “Usijali, nitakujali.” Nikala haraka, kwani njaa ilikuwa inauma—siku hiyo sikuwa nimekula. Masai aliniuliza mengi, nikamsimulia. Akasema, “Huyu mama ni shetani, lakini yana mwisho.” Nikasema, “Asante.” Alisema, “Nikuache ulale, naenda getini.” Nikasema, “Sawa.”
Asubuhi, nilipoboreka, nikaamka mapema. Maumivu yalipungua, nikaweza kutembea vizuri. Nilienda kwa Masai, aliyewa anawahi kuamka, akanipaka dawa tena. Nikarudi kufanya kazi. Mama aliamka, akakuta kila kitu safi, chai ikiwa tayari. Akasema, “Pika tambi na soseji.” Nikapika, nikaandaa. Nikiwa mezani, baba alikuja. Nikamsalimia, akaitika, kisha akasema, “Sikuambia usifanye kazi hadi upone?” Nikasema, “Najisikia vizuri, baba.” Huku naangalia chini, akasema, “Sogea hapa.” Nilisita, akanifata, akanifunua gauni kuangalia vidonda magotini. Aliona vyeusi kwa dawa ya Masai. Akasema, “Mbona vyeusi hivi?” Nikasema, “Ndiyo vinapona.” Alipokuwa amenigusa, mama akatokea, akasema, “Baba Zawadi, hii ni nini?” Baba hakujibu, akasema, “Endelea kupaka dawa, sawa?” Nikasema, “Sawa.”
Akasema, “Unaweza kwenda.” Nikaondoka, mama alinikata jicho. Nikasema, “Nimekosea hapa.” Baba alikunywa chai, akaondoka kazini. Nikabaki na mama. Aliniita, akasema, “Zawadi, njoo! Nambie, una agenda gani na mume wangu? Nataka kusikia, kisha ondoka kwangu. Unaleta matatizo kwenye ndoa yangu, mshenzi! Toka, sitaki kukuona hapa!” Itaendelea.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

🔞 Tahadhari: Hadithi hii ina maudhui ya watu wazima na siyo rafiki kwa walio chini ya miaka 18. Hadithi ya Watu Wazima: Zawadi Sehemu ya 5  >>> https://gonga94.com/semajambo/tahadhari-hadithi-hii-ina-maudhui-ya-watu-wazima-na-siyo-rafiki-kwa-walio-chini-ya-miaka-18-hadithi-
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest