VYOTE NDANI GONGA94
CHUMBA CHA MPANGAJI SEHEMU YA 13 & 14
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
????CHUMBA CHA MPANGAJI
ILIPOISHIA.....
Aliongea Nasra na kumfanya Saidi akae kwanza vizuri kwenye Kochi na kuanza kumtazama Mpenzi wake..
Saidi aliogopa sana hadi alikuwa anaaza kutetemeka kwa hofu..
"" "" Huyu binti kaifungia kamera nyumba yngu au.. Alijiuliza Saidi huku anatazamana na Nasra
"" "" Hapana Saidi hata usije kuhisi kama mimi nimefunga kamera kwako.. Sijafunga chochote lakini nakuomba tu utambue uwezo wangu....
Aliongea Nasra..
Saidi alishtuka zaidi na kubaki anatumbua tu macho..
"" " Au ni jini huyu dem.. Aliendekea kuwaza Saidi..
Saidi akiwa bado haelewi nini cha kufanya.. Alishangaa amesogelewa zaidi na Nasra kisha akashikwa kichwa na kukutanisha Ndimi zao..
" "" Najua unafanya yote kwasababu unanipenda na unapima usahihi wangu kwako..
Jiamini Mwanaume, mimi nikipenda huwa napenda haswaa. Hata usiwe na Shaka...
Lakini Mchezo wako nimeuelewa sana kipenzi... Unafaa sana kwenye kazi kama zetu...
"" "" Mmmhhhh.. Nafaa vipi sasa wakati mimi sijasoma jamani.?? Elimu yangu ya Msingi tu.. Aliongea Saidi na kujisahau kama alikuwa Kichaa ????????????"" ""
"" "" Kumbe siyo kichaa kweli. Maana mimi mwenyewe nilikuwa nabahatisha tu hapa. Ungeendelea na Uchizi wako wala hata nisinge jua..
Siunaona hiyo bahasha hapo mezani.. Nilikopa pesa benk ili nikakutibu..
Afadhali umeiokoa pesa hii... Basi uichukue ukaongezee kwenye biashara zako mpenzi...
Deni nitaendelea kulilipa tu mimi mwenyewe watanikata mshahara wangu...
"" " Saidi, naomba utambue pia kuwa nakupenda na nimekuridhia jinsi ulivyo.. Nimekupokea kwa kila namna.. Sina pingamizi na wewe.. Nimekupa pesa hizo kukudhihirishia kuwa sihitaji pesa zako...
Mimi napokea Mishahara miwili kila Mwezi tena mikubwa tu..
Usijali kuwa na amani.. Lakini ukiwa na mimi utambue tu majukum yako ya kuisimamia familia kama Mwanaume, kwasababu ni majukumu yenu.
Ikitokea umekwama basi niambie hata usiwe na wasiwasi..
ALIONGEA Nasra na kuinuka kuingia chumbani..
Saidi pia aliinuka na kumfuata mpenzi wake kwa nyuma..
Aliingia pia chumbani na kumkuta mpenzi wake anavua nguo ili ajilaze kitandani....
"" "" " Nimechoka baby.. Naomba kupumzika.... Aliongea Nasra....
Saidi aliitika kwa kutikisa kichwa huku anavua pia nguo na kujilaza karibu kabisa na mpenzi wake..
Wote walikuwa wamelala chali wanaangalia Gipsum board juu...
" "" " Saidi.. Umeshanijuana hilo ndilo tatizo.. Hupasi kuwa raia tena kwasababu utaiongea hii siri..
Unapaswa kuwa kama mimi..
Aliongea Nasra..
" "" " Nakuwa vipi kama wewe jamani.. Kazi zenu ngumu, mnaishi na silaha mda wote mimi nitaweza.??
Aliongea Saidi n kugeuka upande aliolala mpenzi wake.....
" "" " Si lazima uwe na Silaha..
Hii kazi ni akili tu, na si akili ya darasani bali akili ya kucheza na mazingira...
Nimeona Movie uliyo nichezea nikatambua kuwa wewe unaweza sana..
Hata kuwa mbea tu au Shushushu wa kukusanya taarifa unafaa sana..
Hutohitaji nguvu.. Hutohitaji elimu ya darasani.. Bali utaongezewa ujuzi wetu kidogo tu na kazi utaianza.
Tunza Siri ya hii kazi yangu.
Ukiivujisha ujue umeisha..
ALIONGEA NASRA..
"" "" UUUUUUHHHHH... Saidi alishusha pumzi na kujilaza vizuri huku anatafakari mengi sana akilini mwake..
Muda pia ulikuwa umeenda sana, ilikuwa ni saa 12 na Madakika Jioni..
Nasra aliinuka na kuanza kuanda chakula cha usiku...
"" " Alafu Baby.. Kesho Asubuhi tutoe huu mtungi na haya majiko tupeleke jikoni..
Hii habari ya kupikia chumbani mwisho leo.. Mimi siyo Mpangaji tena, mimi ni Mother House..
Aliongea Nasra na Wote walicheka..
***×***
" "" " Alafu Baby.
Naweza kukuagiza Mahali.????
Aliendelea kuongea Nasra..
" "" " Wapi tena mpenzi wangu.?? Aliuliza Saidi..
Saidi alikuwa yupo sawa kabisa utadhani siyo yule kichaa aliekuwa anavuruga mashuka na kugaragara chini muda mfupi uliopita...
*******
" "" " Kuna barua yangu ya Bima kanichukulie Pale kwenye Jengo la NSSF.. ukifika wewe Piga honi ufunguliwe geti kisha nenda kaipaki Pikipiki yako sehemu nzuuri na uingie Moja kwa moja hadi Chumba namba 25...
Ukifika utamkuta mbaba Fulani..
Mwambie nimeagizwa na PTIS-041, kisha huyo mzee atakupa kibahasha changu cha bima uniletee..
Aliongea Nasra...
"" "" Poa nipe basi hiyo buku ya bodaboda. Siunajua mimi dereva Boda. Kwahiyo kila napoenda nafunga mahesabu..
Aliongea Saidi na kucheka kisha kuinuka...
"" "" " Saidi.. Hembu vaa suruali ya Jeans na Koti ambalo wenzio hawajalizoea sana ili wasikujue.. Lakini hakuna shida sana muda huu ni usiku hawawezi kukutumbua...
Wasije wakaanza kukimbia kumuona kichaa anaendesha boda ????
Aliongea Nasra na wote walicheka...
*SEHEMU YA 14*
Saidi aliingia Chumbani kwake na kuvaa suruali ya kadet na shati pamoja na koti lake fulani la Suti ambalo havaagi mara kwa mara..
Saidi alitoka na kuwasha pikipiki kisha kuelekea alipoagizwa...
Aliteremka taratibu hadi akafika mjini.. Muda ulikuwa umeenda kidogo. ilikuwa imefika saa moja na madakika Usiku...
Saidi alifika kwenya Jengo lile kubwa la Duara lanye Ghorofa nyingi sana na kupiga honi..
Alifunguliwa na kuingia..
Alipaki Pikipiki sehemu nzuri kisha kuanza kuitafuta Ofice namba 25...
Alizunguka na baadae alielekezwa..
Ofisi ilikuwepo kwenye majengo ya chini tu wala siyo juu Gorofani...
Saidi alipiga hatu za taratibu akiwa na Raba zake za All-star nyeusi yenye Mistari meupe..
Saidi alifika na kutaka kugonga Mlango..
Lakini kabla ya kugonga.. Mlango ulijifungua Wenyewe na kusikia sauti ya mzee ikimwambia.. "" " Ingia ndani..." "
Saidi aliingia ndani na kusimama mbele ya Meza ya mzee yule..
" "" Shkamoo. Nimetumwa..
Aliongea Saidi lakini yule mzee hakujibu kitu. Alikuwa akimtazama tu...
"" " Nimetumwa na PTIS-041.
Aliongea Saidi..
" "" " Unajua PTIS ni nini.?? Aliuliza yule mzee...
" "" Hapana baba... Saidi alijibu kwa upole..
"" "" Karibu sana mgeni wetu.. Utajua tu sawa... Aliongea yule mzee..
Muda huo Saidi alikuwa haelewi nini kinaendelea...
Alitulia kimya akimtazama tu yule mzee..
Ghafla Saidi akiwa bado haelewi..
Alisikia kama kishindo na chumba kilitikisika Ghafla na kutitia chini....
Saidi alirudi nyuma kwa hofu lakini alihisi kizunguzungu baada ya kuona kama chumba kinashuka chini..
Saidi Aliendelea kumshangaa yule mzee.. Lakini mzee hakuwa na Dalili za kushtuka hata kidogo...
Baada ya Chumba kutulia.. Mzee aliinuka na kwenda hadi mlangoni..
Alivuta mlango na kumwambia Saidi... "" " Njoo nifuate ninapoenda..." ""
Saidi alitoka njee na kukuta Mazingira ni tofauti kabisa na yale ya Mwanzo.. Hakukuwa na watu na Taa zilikuwa zinawaka kila Mahali..
"" " Kijana tembea upesi nifuate.. Aliongea yule mzee na Saidi alijikuta anaanza kukimbia taratibu ili awe sawa na mzee.. Mwendo wa mzee ulikuwa wa hatua kubwa kubwa na waharaka ambao saidi asingeweza kuutembea..
Walifika mahali kuna kama kiuwanja kidogo na kuna Nyasi mingi...
Kulikuwa kuna watu kama Sita wamelala chini kati kati ya Uwanja ule.
Walikuwa wamevalia Suruali za Jeshi na T-Shirt za Kijani iliyoivva sana..
Saidi alibaki kupigwa na Butwaa tu, hakujua ni mzigo wa namna gani anaenda kuufuata kwaajili ya mpenzi wake...
Walifika katikati walipokuwa wamelala watu wale sita na Ghafla wote waliinuka baada ya kusikia wameitwa na Mzee kwa jina la PTIS.
Saidi alishika kiuno kwanza huku anawaza kuwa huenda kaingizwa choo cha kike na mpenzi wake..
"" "" Mumpike huyo ajue maana ya jina hilo.. Anatamani aitwe PTIS pia.
Aliongea mzee na kugeuka kuanza kurudi walipotoka mwanzo yeye na Saidi...
Saidi aligeuka pia kwa hofu ili amfuate mzee, lakini Ghafla alishangaa Ameshikwa na wanajeshi wale Sita kisha kuanza kupigwa mangumi ya mgongoni...
"" " Dogo.. Hembu kaa chini hapo.. Huku utakuja kama ulivyokuja ila utaondoka kama tulivyo Sisi...
Aliongea kaka mmoja huku anaendelea kumpiga Saidi mangumi mgongoni..
" "" " Dogo. Mayai sana wewe.. Hembu lala chini tembea kama Kambare hadi mwisho wa uwanja na urudi hapa...
Aliendelea kuongea yule mwanajeshi..
" "" Lakini Broo mimi sikuja kwaajili hii...
Aliongea Saidi huku anawatazama wale majamaa..
Wale wanajeshi wote walimsogelea na mmoja alimpiga Mtama Saidi..
Saidi alidondoka kama Gunia la Chumvi...
Wakati anataka kuinuka.. Alikutana na Buti zito mgongoni...
"" " Tembea kama Kambare mbwa wewe. Aliongea mmoja wa wale wanajeshi...
Saidi alianza kugaa gaa chini kama kambare huku analia kama mtoto kwa maumivu aliyokuwa anayahisi...
Mmoja wa wale wanajeshi alienda kuchukua ndoo ya maji na kuanza kumwagia Saidi mgongoni..
"" " Piga mbizi kamanda..
Kwanza unaitwa nani.??? Aliuliza yule mwanajeshi..
" "" Naitwa Saidi Juma... Alijibu Saidi huku analia...
"" "" Dogo bado hujaiva... Unatakiwa hadi usahau hilo jina na ujiite PTIS kama ulivyotaka..
Aliongea Yule Mwanajeshi huku anamfuata Saidi kwa Nyuma.
*********
"" " Mnisaheme jamani nimechoka.. Kwani mimi nimekosea nini jamani wakati nilitumwa tu.???
Aliuliza Saidi huku analia..
" "" " Sawa tumekusamehe.. Twende basi ukale mdogo wetu.. Huu muda wa kula ukichelewa utakuta wenzio wamekumalizia..
Aliongea yule Mwanajeshi na Saidi aliinuka kuwafuata...
Waliingia kwenye chumba fulani na kukuta watu wengine watatu wenye rika kama la Saidi wamekaa tu wakiwa wamechoka sana wanasubiri chakula..
Mmoja alikuwa wakike na wawili walikuwa wakiume...
"" " Umeona Wenzio hao.. Wamebakiza wiki mbili wamalize kazi ngumu waanze masomo ya Darasaani..
Aliongea Mwanajeshi mmoja..
" "" Wewe Mazoezi ya njee tu bado Wiki 12. Ukizimaliza utasoma ya Darasani kwa wiki mbili kisha utaanza kazi chini ya msimamizi.....
**************
*************
**************
Huko nyumbani Nasra alikuwa ametulia tu anaangalia TV.. Alikuwa anajua kabisa kuwa ni kitu gani kinaenda kumtokea mpenzi wake..
Njia anazo pitia Saidi ni njia alizopitia Nasra. Kila kitu alikuwa anajua Nasra..
***
Usiku huo wakati Nasra anatafakari Magumu na maumivu anayo pitia Saidi.. Alijuta anaanza kumuwaza na Dalali Sele..
"" "" ki rahisi hivyo niliwe na huyu mpuuzi mimi..
Alikumbuka Nasra...
"" "" Ngoja uumie kidogo Dalali sele.. Karib hom..
Aliongea Mwenyewe Nasra...
Nasra alishika Sim yake na kumtumia Dalali Sele ujumbe...
"" "" "" Njoo my lala huku basi... Saidi yupo kwa mganga anauguliwa.. Mimi naogopa kulala mwenyewe,
Nasra aliandika ule ujumbe na kuutuma kwa Dalali Sele...
Full 1000
Whatsp 0784468229
SHUKRANI – Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
Wimbo wenye ubunifu imechanga kiarabu kiswahili na amapiano wimbo wa kushukuru kwa maisha na upendo Sasa sikiliza na ku download hapa gonga94.com
Sikiliza Wimbo Kamili
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi chumba-cha-mpangaji-sehemu-ya

