Jina langu ni Sasha. Nimeamua kuandika simulizi hii si kwa ajili ya huruma, bali kwa ajili ya wale waliopitia maumivu kama yangu na hawajawahi kupata nafasi ya kusimulia. Nimekuwa nikihukumiwa, nikitengwa, na kuonekana kama mhalifu… lakini watu hawajui ni nini kilinifanya kuwa hivi.
Nilizaliwa mkoani Morogoro, katika familia ya watoto wanne. Mimi ni wa pili. Tulikuwa familia ya kawaida, si tajiri, si maskini sana, lakini maisha yalikuwa ya furaha. Tulikuwa karibu kama familia au ndivyo nilivyodhani.
Dada yangu mkubwa aliitwa Cynthia. Alikuwa mrembo, mwenye mvuto wa ajabu na akili nyingi. Alikuwa mfano wa kuigwa, kila mtu akimtaja kama fahari ya familia. Mimi nilimpenda sana… sana kupita kiasi. Nilimwangalia kama malaika, mtu asiye na doa, asiye na kosa.
Lakini kuna jambo ambalo watu hawajui kuhusu Cynthia.
Siku moja jioni nilikuwa na miaka 13, nilikuwa nimelala sebuleni baada ya kutoka shule. Mama na baba walikuwa hawapo—walikwenda msibani kijijini. Cynthia alirudi nyumbani mapema kutoka shule ya sekondari. Nilifurahi kumuona kama kawaida. Alikuja akanikumbatia, akanichezea nywele zangu… nikadhani ni mapenzi ya dada kwa mdogo wake.
Lakini siku hiyo, kulikuwa na kitu tofauti. Macho yake yalikuwa na kitu… kitu kisicho cha kawaida. Nilihisi msisimko usio wa kawaida, lakini nilikuwa bado mdogo kuelewa.
Alinikumbatia kwa nguvu, akaniambia,
“Usiogope, Sasha. Hili ni siri yetu.”tulichokifanya daaah naogopa mpaka kusema ...
Siku hiyo maisha yangu yalibadilika. Sikuelewa kilichotokea mwanzoni, lakini nilijua tu moyo wangu ulivunjika vipande vipande. Cynthia alinigeuza kutoka mtoto mwenye ndoto kuwa mtu mwenye hofu, mwenye mkanganyiko wa kimwili na kiakili.
Kilichotokea usiku ule kilinirarua rohoni. Na kilikuwa mwanzo wa mlolongo wa mateso kimya kimya kwa miaka miwili, hadi alipomaliza shule na kuondoka kwenda chuo. Hakuna mtu aliyewahi kujua. Hakuna aliyeweza hata kuhisi kilichokuwa kinaendelea.
Miaka ilivyopita, nilianza kujiuliza maswali. Kwa nini sipendi wavulana? Kwa nini ninamkumbuka Cynthia kwa namna ya ajabu? Kwa nini moyo wangu huvutwa kwa wasichana waliokuwa na sura kama yake?
Mpaka nilipokuwa na miaka 19 ndipo nilikubali:
Nilikuwa msagaji.
Lakini si kwa sababu nilizaliwa hivyo…
Bali kwa sababu nilijeruhiwa na mtu niliyempenda zaidi…
Dada yangu.
Lakini hiyo ni sehemu ya mwanzo tu…
SEHEMU YA PILI inakuja hivi karibuni….