Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
21 Dec 2025
364 views
VYOTE NDANI GONGA94
*DAKTARI WA JESHI SI UNGENIOMBA TUU* *SEHEMU YA KUMI NA SITA*
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Mume wangu alikuwa na furaha kubwa sana, sikuamin maana nimefika nyumban nashangaa ananizawadia kumsababisha aitwe baba, ikabidi baadae. gari kwa kunishukuru nilipotulia nimuulize, " ni wewe siku ile kwenye hoteli?..
"unauliza maswali gani bana, si tulikubaliana kuwa mwanao ni mwanangu, kama nimekupenda wewe ni sawa sawa nikimpenda na mwanao, na umepitia mambo mengi sana ulipokuwa na huu ujauzito, acha kufikiria sana, na ufurahie maisha, maana nimeshamkubali mtoto kwa moyo wangu wote na kila mtu kwenye hii dunia atajua kuwa wewe ni mwanamke wangu na mtoto tuliozaa ni mtoto wetu, akaongea mume wangu kwa kujiamin..
Nilijisikia vizur sana, maana angalau na mimi ni mtu katika watu, angalau na mimi mungu kanikumbuka baada ya mapito yote ambayo amenipitisha, ila familia ya mume wangu hawakukubali kabisa namna ambavyo Solomon alimkubali mtoto wangu, wakataka kunmiangaza bila kujua kuwa mungu ananipigania na dua za wazaz wangu zilikuwa na mimi kila siku....
Sijui hata walifanya nini, wakaenda kupima vinasaba vya mwanangu pamoja na mume wangu bila sisi kujua, majibu yaliwashangaza wakaja nayo nyumban na matusi juu, kuwa haiwezekani kila mahali ni wewe tu, najua wewe ni mchawi ila sikuwah kujua kuwa ni mchawi kiasi hiki, yaan umeenda hadi kuloga ili vinasaba vya huyo gaidi wako vifanane na vya mwanangu, akawa anasema mama mkwe wangu huku akiwa amesbikilia nyaraka flani hivi...
Nikaenda kuangalia, nikashangaa kukuta kuwa mwanangu simon ana uhusiano wa vinasaba na mume wangu kipenzi Solomon kwa asilimia tisin na tisa na alama tisa, nilihisi kuishiwa nguvu, nilichukua vile vinasaba na kwenda navyo chumban, hapo sasa ndio nilielewa kuwa Solomon alinichezea mchezo, na kama alinichezea mchezo kwanini sasa ameniacha mpaka nimeteswa na ulimwengu kwa kiasi chote kile ndio maana alikuwa anajifanya ananijali sana na anampenda sana mwanangu, kumbe anajua kabisa ni mwanae...
Wakati anarudi kazini nikamuacha akala na mara baada ya kumaliza kula, nikampa zile nyaraka kisha nikawa namuangalia usoni, akazisoma ila ni kama alishajipanga, alijua ni lazima kuna siku nitakuja kujua ukweli, akanigeukia kisha akasema " umeshangaa au unataka na mimi nishangae, haya ndio majibu sahihi, mimba uliyobeba ni yangu na nashkuru sana kwa kunizalia jembe langu, embu nambie unataka maelezo gani mengine, maana najua wasiwasi wako wote umeshaondoka...
" ilikuwaje mpaka ukaniingilia kimwili bila ridhaa yangu, kwanini ulinifanyia vile Solomon..
sidhan kama hilo swala ni la kujadili hapa, nimekubali makosa yangu yote, sasa shida kwani ipo wapi na nilikuwa nakupenda, akasema kana kwamba hajali kabisa kilichotokea...
Nilimuangalia kwa hasira, nikaenda kuchukua mtoto wangu kisha nikawa nataka niondoke...
ITAENDELEA........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
MY WANGU❤️ sehemu ya 69 na 70
Basi nilipata kafuraha mno. Nikachukua pesa yangu .nikarudi darasani kuendelea na ratiba zangu. Uwiiiiii nilifurahi sana...
*DAKTARI WA JESHI SI UNGENIOMBA TUU* *SEHEMU YA KUMI NA SITA*
Mume wangu alikuwa na furaha kubwa sana, sikuamin maana nimefika nyumban nashangaa ananizawadia kumsababisha aitwe baba, ikabidi baadae. gari kwa kunishukuru nilipotulia nimuulize, " ni wewe siku ile kwenye hoteli?..
"unauliza maswali gani bana, si tulikubaliana kuwa mwanao ni mwanangu, kama nimekupenda wewe ni sawa sawa nikimpenda na mwanao, na umepitia mambo mengi sana ulipokuwa na huu ujauzito, acha kufikiria sana, na ufurahie maisha, maana nimeshamkubali mtoto kwa moyo wangu wote na kila mtu kwenye hii dunia atajua kuwa wewe ni mwanamke wangu na mtoto tuliozaa ni mtoto wetu, akaongea mume wangu kwa kujiamin..
Nilijisikia vizur sana, maana angalau na mimi ni...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/daktari-wa-jeshi-si-ungeniomba-tuu-sehemu-ya-kumi-na-sita