DAKTARI WA JESHI SI UNGENIOMBA TUU* *SEHEMU YA KUMI NA TANO*
Siku moja nimekaa zangu nje napunga upepo, kwa sababu kulikuwa na joto kali sana ndani, nikashangaa mama mkwe wangu huyo anakuja na mwanae...
Nikamsalimia mama mkwe kwa heshima sana, kwa maana hata kama amekuja kishari hakubadilishi yeye kuwa mama mkwe wangu, nib ado atakuwa mkwe wangu hata iweje....
shika na wewe kama rahisi, akajibu mama mkwe kwa sauti ya kebehi..
"karibuni, ikabidi niwakaribishe ndani, sikuwa najua kuwa wamekuja kuangalia kamka kuna kitu cha kichawi ambacho nimeweka labda kwa Solomon mpaka akawa ananipenda hivi,, wakzunguka weee, nikawa nyuma yao nisije kutegeshewa kitu, walipohakikisha wamekagua. nyumba nzima wakanirudia...
" embu nambie tukupe shilling ngapi ili uachane na Solomon kwa sababu tunajua kabisa umefata pesa zake, na umemroga, hatujawah kuona mwanaume ambae anapokea mwanamke akiwa na mimba tena mimba ya mtu mwingine, akawa anasema mama mkwe, na Yule binti akadakia na kusema " sema tukulipe shilling ngapiuachane na kaka yangu...
Nikaona sasa huyu nammudu kabisa, siwez kuendelea kukaa kimya, nikamsogelea kisha kwa sauti ya kujiamin nikasema najua mnahamu sana ya kunilipa ili jiachane na mume wangu, labda niwaambie yu, mkitaka niondoke hakikisha mnanilipa kwa mahaba na upendo wake kwangu, mnanilipa utamu anaonipatia na alivyo anaweza kulisakata hakikishen mnamzidi, na mnanipa mahela, kwa sababu mume wangu ni zaidi ya mume kwangu....
naona umeamua kututukana, akaendelea
kusema wifi yangu wa mchongo.. "uzuri siyajui hayo matusi yana rangi gani, wifi naomba sana yakipita njoo nioneshe, nikajibu kwa kujiamin kisha nikaanza kuelekea chumban kwangu, maana niliona kama wanataka kunitibua tu hawana lingine lolote lile....
"unaenda wapi? Wifi kisebengo akauliza tena, ni kama alitaka nimjibu vibaya aendelee kulalamika kuwa nawatukana, nikajifanya sijasikia, nikawa naendelea na safari yangu...
nakuuliza wewe unaenda wapi, yaan hata adabu huna kwa mama wa mumeo.. naenda moyoni kuchimba madini, kama una umaskin wa akili twende na wewe, nikamjibu maana niliona kama anazidi kunizoea sasa kisha nikaenda zangu chumban nikawaacha wapambane wenyewe kwa wenyewe, maana ni kama hawana kazi za kufanya mpaka kuja kufuatilia maisha yetu, ambayo hayawahusu hata kidogo............
Basi walikaa ukumbini sijui hata ni kwa muda gani, nakuja kutoka jion nashangaa sikuti mtu, nikabidi kuuliza kwa Yule msaidizi wangu, kuwa wameondoka saa ngapi, akanambia muda mrefu kuanzia nilipoenda chumban, ila kuna kitu wamechukua chumban nimewaona, na wakawa wanatoka kwa kunyata, sijui hata wanakipeleka wapi na sijui wamebeba nini...
Basi siku hio ilipitya na kesho yake mume wangu alirudi nikamsimulia kuhusu kitu ambacho mama yake pamoja na mdogo wake walifanya, akaniambia niwapuuze maana anajua namna ya kushughulika nao...
Basi kama tunavyojua siku hazijawah kusimama hata mara moja, basi miezi tisa ikafika, chupa ilianza kusimama na mume wangu ndio alinipima njia kisha akanambia "mamaa tunaenda hospital kuwa jasiri ili ujifungue...
Sikubisha, maana maumivu ambayo nilikuwa nayapata hayakuwa ya mchezo, nikaenda hospital na sikukawia sana nikajifungua mtoto wa kiume, na mama yangu alikuwa ameshafika, sijui ni nani ambae alimpa taarifa, nakuja kumuona mwanangu amefanana kila kitu na mume wangu solomoni, nilishangaa, na mama alishangaa pia, ila Solomon yeye alikuwa ana futaha isiyo kifani kitu ambacho kikatushangaza mimi na mama yangu...........
Inakuwaje mtoto afanane na Solomon na wakati nilikuwa nina uhakika yeye sio mwanaume alienipa mimba ?..
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi