Kutoka mliyayoyo hadi msindo mwendo ulikuwa ni mdogo mdogo kulingana na barabara kuwa yenye mashimo mengi na udongo mwekundu ngunja ilichukua kama dakika 20 hivi tukawa tayali tumeingia ardhi ya Msindo ,Dereva alipenda sana maandhali ya Msindo na akawa anauliza hapa ndio mshindo nilitabasamu na kumwambia sio mshindo ni Msindo oooh sawa gari ilikuwa inatembea mwendo mdogo sana na hatimae tukaipita kichangani na kuanza kuipata pacha nne tulienda mwendo mdogo sana huku tukiwaona wa mama wamebeba kuni wengine ndoo kichwani mbele kidogo kulikuwa na watu wengi pembeni nika mwambia dereva pitia njia hii nyumba zile ndo kwenye msiba basi alifuata maelezo yangu hatimae tuka fika na kupaki gari dereva alikuwa mtu wa kwanza kushuka kisha mubaba na mimi nikafuatia na wale mabinti wawili ile kushuka tu shangazi aliniona na kuanza kulia kwa nguvu Adija mwana vangu huuuuuuuuuuu huuuu nenga yooyoooooo .
Zilipita dakika kadhaa za vilio mwisho tulipelekwa kwenye nyumba ya mama mkubwa na wageni wangu Dereva na mubaba walibaki kwenye hema na watu wengine mimi na mabinti wawili tuliingia ndani na kukaa tulipo tandikiwa mkeka huku hudhuni ikawa tayali imenitanda nikikumbuka mambo mengi ya zamani nikawa na lia sana joyce akawa ananibembeleza anti pole pole antii ,πππππππ
Muda kidogo wakaingia watani mnajifanya kulia wakati mnachekelea
πππππ
nyama acheni kulialia Mtani mmoja akanigeukia mimi kwa hiyo wewe unakula ziwa au pajaa akanishika kichwani nakuuliza unakula nini??? maana mnagawana kimyaa kimyaa waliongea mambo yao ya utani yenye kukela sana huku wanandugu wote tukiwa tunalia kwa sauti kubwa,
Muda huo tayali giza lilikuwa linaingia watoto waliogeshwa na watani mimi na ndugu zangu pia tuliogeshwa na watani tukaletewa moto kwani kilikuwa kipindi cha baridi sana na niliko tokea Morogoro ni joto kali sana nilikuwa na tetemeka sana halikadhalika mdogo wake joyce nae alikuwa anatetemeka sana baridi nili muomba mtani mmoja aende kwa wale wageni wangu na kuomba nguo nzito kama kuna makoti ya hawa mabinti
Mtani alileta begi na card kutoka kwa mubaba yenye namba ya simu niliwavalisha mabinti nguo nzito na kuwa sogezea moto karibu pia mtani mmoja alileta chai ya moto nikawapoozea nika mpa joyce na mdogo wake nilikuwa namnywesha mimi mwenyewe, hali ya kutetemeka baridi ikawa imetulia na wakawa wana sinzia kulikuwa na mkeka pembeni na kigodolo kidogo nika mlaza binti mdogo na joyce nae akasogea akalala
Nilichukua namba na kuiweka kwenye simu yangu na kuanza kuwasiliana na mubaba joyce na mdogo wake wamelala ,"mubaba oooh sawa hata hivyo siwezi kuondoka usiku huu hivyo tutashiliki kwanza msiba huu kisha tutaenda mtakanini ", Asante nashukuru sana Shangazi alikuja na kuniuliza wageni wamepata chakula mtani mmoja alimjibu ndio sawa haya shangazi mimi nipo chumba hiki nyinyi mnalala hapo nika mwambia ndio Shangazi.