JAMANI NIPE CHANCE KIDOGO. Chapter 10 Kesho yake mapema Abisai alifika nyumbani kwa kina Leyna na kumkabidhi Leyla simu yake mpya tena haikuwa kama ile ya bei rahisi ilikuwa ni simu ya gharama mno, simu ambayo Leyla
hakuwahi kuimiliki.
"Umesema hii ni simu yangu mimi?
"Ndio
"Asante sana, barikiwa sana shemeji......
"Simu usijifanye ukamwaga sifa na kutoa vyeo ambavyo havipo. Alafu sema Leyna kisha akamshika mkono Abisai wakaondoka.
Siku zilisigea mbele Abisai akawa anafika nyumbani kwakina leyna mara kwa mara na walikuwa wanaongea sana na Leyla kuhusu mwenendo wa Leyna.
Kwakuwa Leyla nae alikuwa anatamani ndugu
yake abadilike basi alikuwa bega kwa bega na Abisai, Leyna alipokuwa anafanya mambo yake
ya ajabu alimwambia Abisai. Abisai alikuwa alinyoosha. Hatimae
hali ilianza kubadilika leyna alibadilika, aliacha
mambo yake ya kutoka ovyo pia alipungiza.
marafiki waliokuwa wakimpotosha.
Siku moja Abisal na Leyna walitoka na kwenda kukaa kwenye bustani moja huku walioulizwa na
upepo mwanana, "Leyna kuna jambo nataka kukueleza.
"Jambo gani?
"Sasa umefika muda wa mimi na wewe kufunga ndoa.
Leyna alishituka na kumuangalia usoni.
"Abisai unaniomba au unanipa taarifa?
"Sio ombi nakupa taarifa sababu siwezi kuwa
imepoteza muda wangu kuwa na wewe alafu mwisho wa siku unaenda kuolewa na
mwanaume mwingine.
Leyna alimuangalia kwa muda kama vile anasoma kitu kisha akasema.
"Abisai hiyo ndoa tunayotaka kufunga itakuwa ndoa au ndio unataka kuniweka gerezani?
Sijawahi kutajacuhusi hivyo ila mambo yako ya zamani ndio sababu ya mimi kuwa vile.
"Kwahiyo utapunguza wivu wako?
"Itategemea na na wewe utakavyokuwa. Walitulia kwa muda huku Leyna akiwa
anatafakari. Baada ya muda flani Leyna alitoa jibu.
"Sawa nitaolewa na wewe.
Abisai alifurahi na kumkumbatia kwa furaha. "Asante mpenzi wangu kwa kukubali ombi langu
nilijua itakuwa ngumu kukubali.
"Nimeshakuzoea haina budi kukubali.
"Kumbe ni mazoea na sio mapenzi.
"Vyote kwa pamoja kama ilivyo kwako mapenzi na wivu.
Wakiendelea kuongea huku wakieleza utani ilimradi wafurahie tu.
Usiku Leyna alikuwa ameoaa kitandani kwake na
Leyla alikuwa anajiandaa kulala. "Leyla unataka kulala?
"Ndio. Alijibu Leyla na Leyna alikuwa kimnya.
"Kuna tatizo? "Hapana.
"Lakini inaonekana una jambo.
"Ni kweli, Leyla mwenzio nimekubali kuolewa na Abisal
Leyla aliachia tabasamu na kusitishwa kulala akajikuta anakaa"
"Hilo ni jambo zuri sana hata mama akisikia atafurahi sana "Kwakuwa kanichoka si ndio?
"Hakuna mzazi akae mchika mwanae, licha ya kufanya mauzauza yako lakini mama bado
alisimama na wewe na hata kukutetea. Alikuwa anataka uolewe na Abisai sababu ni mwanaume
aliyeweza kunyoosha kidogo umetulia na mtaani kumepoa mpaka watu wanajiuliza umepatwa na nini.
"Na bado wakisikia naolewa na ndio watabaki midomo wazi maana wengi wao waliniona laana
na kunisemea vibaya kuwa sitakaa kuonja ndoa. Hayo yalikuwa yao na Mungu ameshaanza
yake. Sawa lakini nina wasiwasi nitaweza kwenda kudumu kwenye ndoa na Abisai?
"Kwanini usiweze?
"Yule mwanaume ni mkoloni wewe hujui tu.
"Naamini mpaka kufikia hapo mtakuwa mmesha zoeana na mkifunga ndoa mtazoeana zaidi.
Leyla alizidi kumpa moyo na kufanikiwa kumtoa hofu pacha wake.
Hatimae mwezi mmoja ulipita baada ya kukubaliana kufunga ndoa. Abisai akaanza
utaratibu wa posa na kutoa mahari Familia ya
Leyna ilipanga ndoa baada ya miezi miwili ili wajipange lakini Abisai alipopewa hiyo taarifa na
Washenga aliipinga Wazee wangu ni mingi sana, kinaweza
kukatokea kitu cha kuvuruga uchumba wangu naombeni mkaombe ndoa ifungwe mwezi ujao.
Kila kitu nitasimamia Alijibu Abisai kwa
Kijana unajua mambo ya sherehe yanahitaji kujipanga, hapo pesa unatakiwa.
kujiamini. "Sawa tutajaribu.
Mshenga alirudi kuomba huku abusai alimbembeleza Leyna ndoa yao ifungwe mapema.
Ombi la Abisai Iilikubaliwa.
Wiki iliyofuata abusai akitoa hela ya nguo za bibi harusi, huku wazazi wake wakishuhudia na
maandalizi ya harusi kwakuwa walikuwa ni watu
wenye uwezo haikuwa shida kwao mambo
yakienda kama yalivyo pangwa. Siku Leyna alipokuwa anataka kwenda kupima
nguo ya harusi alimpigia simu Abisal.
"Baby nataka kwenda kwa fundi kupima nguo. "Unakwenda na nani?
"Leyla
"Hivi fundi ni mwanaume au mwanamke?
"Pale wapi mchanganyiko lakini mafundi wakuu wapo wawili na mwanaume.
Sasa sikiliza msiende wenyewe nakuja kuwachukua niwapeleke.
"Lakini upo ofisini.
"Sina kazi nyingi, nisubilini hapo nakuja. Abisai
alikata simu. Leyna alimgeukia Leyla. Amesikia mafundi wanaume sasa anataka twende wote.
Leyla alicheka mwenzie kisha akasema.
"Umepata kiboko yako"
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni