JAMANI NIPE CHANCE KIDOGO Chapter 3 Siku zilizidi kwenda huku Abisal akiwa amepania kumbadilisha Leyna
kwa kujificha ficha. Alikuwa akitoka na marafiki alizima simu yake na kuiacha nyumbani.
Kesho yake Abisai alipouliza sababu za kutokuwa hewani Leyna alimwambia alizima hakuwa anataka kusumbuliwa.
"Leyna unataka kuniambia huwa kuna watu wanajisumbua sana nyakati za usiku?na hao watu ni wakina nani?
"Sijamaanisha hivyo.
"Kumbe ilimaanisha nini?
Leyna alitafuta jibu la kujitetea lakini hakupata.
Leyna michezo inayochezwa ipo siku. itakughalimu, taratibu na moyo wangu sitaki majereha ya moyo, sihitaji kuumizwa. Alafu
sitaki kutumiwa simu usiku kama simu yako itakuwa na tatizo basi nitanunua nyingine ilimradi tubnikupate.
"Unajua kila siku najiuliza unataka nini hasara lakini sikupatii jibu.
Nataka utulie, sitaki mambo yako ya kutoka usiku kwenda sehemu za anasa na ushawishi kama vile club, bar na sehemu za ajabu ajabu ambazo sio salama kwako mtoto wa kike. Na lingine nguo zako za kuacha maungo nje huwa zinanikera sana.
Oooh nimeshskusoma wewe unataka niwe kama binti wa kilokole yani sketi za kinda box, magazini ya solo, nafsini ya vitenge ya kivita malinda. Sasa mimi hizo swagga siziwezi maana hata hivyo bikira vyenyewe kuvaa mtihani.
"Kuna nguo nyingine nyingi tofauti na hizo na ni nzuri tu. Nia yangu sio kufuja bali ni uvae nguo
za heshima zenye kupendeza nipo tayari kununua hata nguo za bei ghari ili mwanamke wangu upendeze.
"Sawa baba wivu
Maneno waliyokuwa wanaongea yalikuwa yanaingilia sikio la kulia yanatokea sikio la kushoto.
Siku moja usiku Leyna alikuwa amekaa kitandani kwake akapigwa simu na rafiki yake. "Wewe upo wapi? "Nipo home.
"Acha ujinga wewe huku mambo ni moto leo Erick amefanya kufuru huku yani watu wanakunywa mpaka wanaoga. Yani watu wengine kwa mara ya kwanza tumekaa VIP. Wacha wewe hiyo sio ya kuikosa baada ya
muda nitakuwa hapo.
Leyna alikata simu akaenda kabatini kwake
akatoa nguo za kuvaa na kuweka kitandani. Alisimama kidogo akawa anafikiria kitu | alihofia kukutana na Abisai maana amekuwa akimuonea. sana kwenye mitoko yake.
Aliwaza kiiti na kumwambia pacha wake. "Leyla unaonaje leo tukaenda club maana leo ni furu raha Erick yupo huko.
"Erick yule boyfriend wako?
"Alikuwa zamani, kumbuka tukiachana tukawa marafiki tu.
"Hapana kwakweli hekaheka za usiku siziwezi. "Aaaah sasa hekaheka gani na watu tunaenda kurulia VIP
Starehe hizo zenye fujo siziwezi alafu
kuongozana na wewe ni kujisabanishia matatizo tu. "Mmmm ushamba tu.
Leyna kumwambia Leyla waende pamoja alikuwa ana akili yake Alijua ikitokea kakutana na Abisal ampambanishe nae mpaka anakuja
kujua sio Leyna yeye atakuwa kashaondoka sehemu ya tukio.
Una bahati kama ungekubali basi ninge.
kupambanisha na Abisai huenda mngeendana. Hata hivyo nitafanya hivyo tu ili nitoe kwenye haya mateso
Leyna alisema mwenyewe.
Aliamua kujiandaa alivaa nguo zake sketi ya jeans fupi na top nyeupe kisha akatoka.
Alichukua usafiri na kuelekea club.
Alipofika aliingia club huku akiwa anaangalia
nacho maeneo ya VIP, aliwaona wenzake wakifurahia ile anataka kwenda akashituka ameshika mkono alipo geuka kumuangalia mtu. alimshika moyo wake ulipasuka kwa mshituko alikuwa ni Abisal. Waliangaliana kwa hasira huku akijisemea.
"Hivi huyu mwanaume ni jini, amejuaje kama. nipo hapa
"Vipi? Abisai alimuuliza
"Safi.
"Kwanini upo hapa?
"Nimekuja kufurahi na marafiki.
Ulimwambia nani unakuja hapa?
Nilikwambiajebkufika maeneo kama haya? Abisal utanichunga mpaka lini, hivi unafikiri
utaniweza? Leyna aliongea kwa hasira Abisal hakutaka kuharibu starehe za watu alimvuta nje mpaka alipoacha gari yake, alifungua mlango wakapanda kwenye gari
na kuondoka
Leyna kwanini hupendi kunielewa kile
ninachokiongea kila siku? Kukuelewa nakuelewa sana ila ni ngumu kutekeleza sababu mimi na wewe tumekutana kwenye haya mazingira.
Kwangu hizi sio sehemu zangu nilikuja tu kupunguza stress na bahati nzuri nikakupata
wewe na kuanzia siku ile wewe ndio umekuwa furaha kwangu na kupoozwa cha mawazo yangu kwahiyo kama hautaweza kubadilika kwa kukwambia kistaarabu basi utabadilika kwa lazima.
"Kwani wewe umekuwa mzazi wangu, au mume
wangu?
"Ukitaka kujua jibu la swali lako basi pingana na mimi.
Wewe mwanaume wa ajabu sana, sijawahi kupata mtu wa kunichangacna kunifuatilia hivi, yani unanibana hunipi chance.
hata kidogo?
"Nitahakikisha banana mpaka penati. "Tutaona, itakata tamaa mwenyewe.
"Bahati mbaya kwako msichana sijawahi kukata tamaa kirahisi. Leyna alimuangalia kwa hasira
Kama itashindikana mbona rahisi tu si tunaacha kwani mimi na wewe hatuna mkataba wala cheti cha ndoa.
"Ni kweli hatuna hivyo vyote lakini kuachana mimi na wewe Itakuwa ngumu sana yani sikuachi ngo.
"Mimi ndio nitakae kuacha. Jana uliwahi kuwaacha ni hao wa zamani ila. kwangu mimi siachwi.
Abisai alijibu huku akiwa anajiamini na kufanya Leyna kushikwa na hasira hakuwa tu na uwezo wa kumpiga.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni