JAMANI NIPE CHANCE KIDOGO Chapter 8 Leyna alishika njia na kuelekea stendi ya daladala, Abisal alimfuata nyuma
Leyna, Leyna... Abisai alimuita Leyna aligeuka akamuangalia kisha akakata mwendo.
Abisal alikazana kutembea mpaka akamfukia. "Nilikwambia twende kwenye gari huku unaenda wapi?
Sitaki, sihitaji chochote kutoka kwako niache na maisha yangu Abisal.
Hiyo itakuwa ngumu na usitake tujaze watu hapa naomba twende tukaongee tukiwa kwenye
gari.
Leyna alijikuta akimuangalia kwa hasira huku machozi yakimtoka.
Katika siku zote leo umenidhalilisha kupita kiasi, Abisai kama upendo wako kwangu upo hivi basi mimi siwezi.
Kwa mara ya kwanza Abisai alijihisi mwenye hatia, aliona maumivu ya Leyna.
Tafadhali mamy twende tukaongee. Akiongea kwa upole Leyna akajikuta anakubali kumfuata wakaenda alipoacha gari, walipanda na kuondoka.
Leyna alikuwa amenyakua kimnya lakini Abisai alikuwa alimbembeleza huku akisisitiza kuwa anampenda sana na moyo wake huwa hautulii pindi anapomuona akiwa na mwanaume au
akiwa anafanya mambo ambayo yanaweza
kuwapa vishawishi wanaume.
Hayo ni mapenzi gani ya kuniumiza na
kunidhalilisha?
*Lakini leo kosa lilikuwa lako Leyna, kwanini unagawa namba yako ya simu kama karanga? Na ile hali unajua wewe ni mwanamke wa mtu?
Kwahiyo hutaki hata niongee na watu niliosoma nao?
*Wanini, wanajisaidia nini, mlijiana kipindi hicho na sio sasa. Alafu yule kijana muhuni hajawahi
kufahamiana nimekutana tu pale dukani. Nilianza kukufuatilia tangia ulipokuwa unaingia pale dukani.
Leyna hakuwa na la kuongea alitulia kimya. Siku zilienda lakini Abisai hakuweza kabisa
kuacha kumfuatilia Leyna. Siku moja majira ya saa kumi na mbili jioni
Abisai alitoka kazini na kwenda kumfanyia shopping Leyna. Siku hiyo alitaka kumfanyia surprise Alienda mtaani kwakina Leyna, alipofika sehemu alimuona Leyna alikuwa amesimama akluza samani tena alikuwa alimuhudumia mteja wa kiume.
Abisai alipungiza mwendo kisha akaegesha gari pembeni akawa anaangaoia kila kilichokuwa kinaendelea.
Kumbe yule aliekuwa anauza samaki hakuwa
Leyna alikuwa ni Leyla.
Abisai hakujua kama Leyna alikuwa na pacha wake tena wanafanana sana.
Kuna muda yule mwanaume alichukua simu ya Leyla na kuandika namba zake.
Leyla naomba usiache kunitafuta alafu ukiwa
na samaki kubwa kubwa uwe unaniambia. "Usijali kuhusu hilo Ommy.
"Hunipi hata mdogo wa kuonja? Maana hapa mate yamejaa mdomoni.
Leyla akicheka kisha akasimama na kuchagua
samaki mdogo mdogo na kumpatia. "Asante sana, ubarikiwe mrembo, upate mume
mwenye sifa unazotaka.
Leyla alijikuta alifurahishwa na maneno ya Ommy akawa anacheka tu..
Huku abusai alikuwa anapika kwa hasira. *Jamani huyu mwanamke sijui anataka niongee vipi, nimueleze vipi ndio ajue kuwa sitaki?
Alishuka kwenye gari akawa anaelekea alipo Leyla na wakati huo Ommy alikuwa anaondoka.
Abisal alienda akasimama mbele ya Leyla na kumuangalia kwa hasira. Leyla alikuwa anashangaa.
"Nikusaisie nini juu kaka?
Abisai aliguna kisha akatoa tabasamu kulibeba dharau.
Leyla akawa hamuelewi. *Kaka kuna tatizo?
"Wewe acha kujifanyia maigizo yako tangia lini mimi nikawa kaka yako? Hebu nipe huyo simu
yako. Aliongea Abisai kwa ukali. * Kheeee simu yangu ya nini? Yani unataka kumuibia kibabe?
Abisai hakutaka kubishana aliuchukua simu kwa nguvu,
"Wewe nipe simu yangu. Nimesema tulia hapo. Abisai alibonyeza
akakutana na password. Alibonyeza namba kutoa lakini iligoma, alimuangalia Leyla usoni "Unajua Madudu iliyofanya sasa umebadilisha
password.
Unajua unanichanganya sikujui lakini unanisumbua, mimi sio huyo unaemzania. Leyla alihisi huenda Abisai kumfananisha na pacha
wake Leyna
Acha kujiletea ujanja ujanja wako Leyna naomba utoe password. "Wewe kaka mimi sio Leyna......
Abisai alihisi kama anajichanganya aliipigiza chini ile simu na kupasuka pasaka kioo.
Leyla alimtolea macho ya mshangao "Wewe kaka una kichaa? Kwanini unipasulie
simu yangu? Leyla alimsogelea karibu na kumkunja.
Abisai alimuangalia huku akitoa tabasamu la kejeli.
"Unataka kunipiga.
"Nipe simu yangu, nataka simu yangu. Kama hii simu nilinunua mimi huna haki ya
kunidai nenda kwa yule mwanaume wako ulienda namba yako akakununulie.
Ugomvi ulikuwa mkubwa, watu walikusanyika wakishuhudia. Hakuna aliekuwa amuelewe huo ugomvi, Leyla alikuwa akilia na kudai simu yake.
Taarifa zilifikia mama Leyna na Leyna. Wakafika sehemu ya tukio bila kuchelewa. Leyna
Abisai.... Leyna aliita kwa mshangao, Abisai aligeuka alipomuona Leyna alibaki kaduwaa.
alijipenyeza mpaka akafika na kumkuta Leyla akiwa anarumbana na Abisai.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni