Miaka ya 1930s wakati Urusi ikipigwa na lile janga la njaa kali kuwahi ikumba nchi hiyo. Inasemekana kuna baadhi ya watu walianza tabia za kula nyama za watu. Wapo walioenda mbali sana na kusema kaka yake Chikatilo alikua moja ya watu waliochinjwa enzi hizo na kuliwa nyama. Hii inatosha kutuambia Chikatilo alitokea katika maisha gani. Lakini…
Wakati wa ujana wake alikua mtu safi tu. Akiwa kijana alihitimu shahada ya ualimu katika chuo cha Rostov. Baadae aliajiriwa kama mwalimu kabla ya kufukuzwa kutokana na matukio yake ya ukatili wa kijinsia. Na kuhusu mauaji yake…
Bado haijulikani kwanini alikua akiua zaidi watoto na wanawake. Taarifa zinasema alikua akitumia vitu vidogovidogo kuwatamanisha wahanga wake. Na kila walipojaa kwenye mfumo… aliwaua vibaya kwa kuwatia vitu vyenye cha kali kwenye miili. Baadhi ya maiti alizibaka huku nyingine zikiwa na ishara za kukeketwa..