MIMBA YA DHARURA* *_____________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*
Nadia alibaki amekaa kwenye kiti chake, akili yake ikimzunguka kama upepo mkali. Kila jambo lililokuwa likitokea maishani mwake lilionekana kama sinema ya ajabu.
“Jayden anataka kuwa baba wa mtoto wangu?” alijiuliza taratibu huku akijiegemeza nyuma ya kiti.
Machozi yalijaa machoni kwake sio kwa sababu ya huzuni , bali kwa mshangao na mchanganyiko wa hisia.
Hakuwahi ameota ndoto kwamba siku moja mwanaume mwingine angejitokeza kwa ujasiri kiasi hicho, akitamani kumchukua yeye na mtoto wake kama sehemu ya maisha yake.
Lakini bado kaburi la maumivu ya Kabir na kumbukumbu za usaliti wa Jawad halikuwa limefukiwa.
Usiku Nadia alikaa kitandani akimwangalia Tawakal aliyekuwa amelala usingizi mnono. Uso wa malaika yule mdogo ulimpa tumaini jipya, lakini maswali yalimsonga:
"Nitakubali upendo wa Jayden? Nitakuwa na ujasiri wa kuanza upya?"
Amina aliingia chumba kwa Nadia.
" Vipi mbona leo upo chumbani mapema hivi?
" Sina hamu ya kukaa na kuangalia TV kichwa changu linasonga na mawazo mengi sana.
" Kama kawaida yako na yote itakuwa ni kabir.
" Hapana yameibuka mapya kabisa.
Amina alimuangalia huku akiwa anakaa vizuri.
" Niambie hayo mapya.
" Jayden amenishsngaza sana siku ya leo .
" Acha kukatisha maneno sema ilivyokuwa.
" Anataka nimpe nafasi kwenye maisha yetu , anataka kuwa baba wa Tawakal.
" Unasemaje?
" Ndio hivyo unajua kanishangaza sana.
“Wewe kweli una bahati Nadia. Mungu anaweza kuwa amekufungulia ukurasa mpya kupitia Jayden. Huyo siyo mwanaume wa kawaida, amekusoma vizuri kazini, amekuona ukiwa dhaifu na bado anakutaka. Wengine wangeikimbia hiyo hali yako ila yeye kajitokeza kifua mbele .
Nadia aliguna.
“Lakini Amina, moyo wangu bado una alama za Kabir. Na Jayden anajua kuwa bado kuna mwanaume mwingine ambaye ndiye baba wa mtoto wangu.
Amina akacheka kidogo “Ndio maana nakwambia mpe nafasi, usiogope. Wakati mwingine mwanamke anaweza kujikuta ameanguka mara mbili au tatu lakini bado akasimama na kupata furaha.”
" Yani wewe unazidi kunichanganya kabisa.
" Yani Nadia una bahati wewe, sijui kwanini mimi sipati hizo bahati?
" Amina hebu fanya kwenda kwanza nataka kumpumzisha hiki kichwa maana ninapozidi kuongea na wewe ndio akili Angu inazidi kuchoka.
Kesho yake kazini
Jayden hakumsemesha Nadia kwa lolote la kimapenzi, aliheshimu ahadi yake ya kumpa muda.
Alikaa mbali kidogo, lakini macho yake yalikuwa yakimfuata Nadia kila wakati.
Kila mara alipoona Nadia akitabasamu, moyo wake ulikuwa na faraja.
Baada ya kazi Nadia alipotoka ofisini, Jayden alimsubiri nje.
“Nadia…” aliita kwa sauti ya upole.
Nadia alisimama, akashusha pumzi ndefu.
“Jayden, sina jibu kwa sasa. Lakini nataka ujue, maneno yako yameingia moyoni mwangu. Hata hivyo, naomba tuende taratibu.
" Sawa na kuelewa sana Nadia na bado nimekupa muda. Nilikuwa naomba nikupeleke nyumbani pia nilikuwa nataka kumuona Tawakal.
Nadia hakuwa na neno alikubali.
Walielekea parking wanapanda kwenye gari la Jayden wakaelekea mitaa ya njiro.
Walifika kwenye nyumba anayoishi Nadia walimkuta dada wa kazi anamnywesha maziwa Tawakal.
Nadia akisalimiana na dada wa kazi na kutaka kujua wanaendelea je . Alimkagza mtoto wake na kumuona yupo sawa.
" Mr J karibu sana jisikie upo nyumbani.
" Asante sana.
" Naweza kumbeba Tawakal?
" Bila shaka.
Jayden walimchukua Tawakal akamuangalia .
" Hongera una mtoto mzuri sana.
" Asante.
" Huyu mtoto baba yake ni Mmanga au kwenu mna asili ya ushombeshombe?
Nadia alicheka
" Hapana labda niseme baba yake ni shombeshombe.
" Umepata mbegu mzuri sana.
" Mmmh utakunywa kinywaji gani?
" Maji yanatosha sana.
" Maji tu?
" Ndio.
" Hapana kuna juice , nitakupasua juice na maji.
Nadia alienda kuchukua juice na kipande cha keki akarudi sebleni alimkuta jayden akimrusha rusha Tawakal na kufanya mtoto kucheka kwa sauti.
Kile kitendo lilimpeleka Nadia mbali kimawazo alitamani kabir ndio afanye lile tukio kwa mwanae.......
Full 1000
Whatsp 0784478229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni