MIMBA YA DHARURA* *SEHEMU YA SITA*
Chumba cha hospitali kilijaa ukimya mzito baada ya daktari kutoa taarifa. Maneno yale “Nadia ni mjamzito wa mwezi mmoja na wiki kadhaa” yalibaki yakining’inia hewani kama radi iliyopiga katikati ya anga.
Mama yake Nadia alishika kifua chake kwa mshangao.
“Eeeh Mungu wangu… Nadia, hivi ni kweli hiki nilichokisijia?
Nadia alimuangalia mama yake huku machozi yakitiririsha.
Baba yake alisimama akitetemeka kwa hasira
“Hii aibu umetuletea kutoka wapi? Wewe ni binti wa heshima, uliyekuwa ukitazamwa na jamii nzima. Umekuwaje? Na hii mimba ni ya nani?
Nadia alishindwa kujibu maswali ya baba yake alijikuta machozi yakimtoka bila kukoma. Alitamani ardhi ipasuke imfunike pale pale.
“Baba… mimi… mimi…” alijikuta akishindwa kuendelea kuongea sauti ilikwama.
Kwa upande wa pili, Jawad alikuwa amekaa kwenye kiti alipata habari za ujauzito wa Nadia alienda wodini haraka huku uso wake umebadilika ghafla. Macho yake yalikosa mwangaza, moyo wake ulipasuka vipande vipande.
“Nadia… hivi mimi ni wakilipwa haya? nilikupenda kwa dhati, nikakungoja kwa miaka yote hii. Halafu leo siku ya harusi yetu ndio ninasikia mambo kama haya?” aliuliza kwa sauti ya maumivu.
Nadia nilijua unajitunza kwaajili yangu kumbe ulikuwa unanizinguka na kuniona mjinga.
" Niambie Nadia hiyo mimba niya nani?
Nadia alishindwa kabisa kuongea alikuwa analia tu.
Jawad alitamani kumkunja na kumlazimisha aongee lakini aliona sio sawa alinyanyuka kwa ghadhabu, akatoka nje ya chumba, alisimama nje na kupiga ngumi ukutani kwa hasira. Rafiki zake walimshika lakini machozi yalikuwa yanamtoka mwanaume mzima.
Mama yake Jawad naye ambaye alikuwa ameambatana nao hospitalini, alitikisa kichwa kwa uchungu.
“Hatuwezi tena kuwa sehemu ya aibu hii. Hii si familia tuliyokuwa tunaiheshimu. Mtoto wangu hatamwoa binti wa aina hii.”
Alimshika mkono kijana wake wakaondoka.
Baba yake Nadia alimuangalia bila kummaliza alafu akasema.
" Asante mwanangu kwa kunivua nguo, nashukuru sana mama. Baada ya kuongea kwa uchungu aliondoka na kumuacha Nadia na mama yake.
Baada ya kelele zote, usiku uliwadia Nadia alibaki hospitali akiwa amekaa kitandani, macho yake yakiwa yamevimba kwa kulia. Mama yake alikaa pembeni, akimnyooshea glasi ya maji.
" Kunywa maji alafu uniambie hii mimba umeokotwa wapi?
Nadia alipokea grass ya maji akanywa kidogo. Mama yake alichukua grass na kuweka juu ya kabati dogo.
" Niambie na usinifiche kitu.
Nadia alimuelezea mama yake kila kilichotokea mpaka kupelekea kubeba ule ujauzito.
“Mwanangu, kwa nini ulinificha? Kwa nini hukuniambia mapema?”
Nadia aligeuka na kuanza kulia kwa sauti ya chini.
“Mama… sikuweza. Sikuweza kueleza. Yote yalinitokea ghafla, na nilijuta kila siku. Sijui nifanye nini sasa.”
Mama yake naye machozi yakamtoka.
“Sasa kila kitu kipo hadharani Kila mtu anajua. Baba yako hayuko sawa kabisa. Hata Jawa, sijui kama atakuangalia tena kwa macho yale yale ya upendo.
" Nisamehe mama.
" Kama mama siwezi kuacha kusamehe binti yangu . Unenyea kiganja sitaweza kuukata mkono nitauosha maisha yataendelea.
Nadia hakuamini akimkumbatia mama yake kwa mapenzi makubwa sana.
" Asante mama, nakupenda.
" Nakupenda pia mwanangu, kuwa na amani kwenye hali hiyo hutakiwi kuwa na mawazo.
" Sawa mama, vipi kuhusu baba nae atanisamehe?
" Nitaongea nae.
Siku iliyofuata asubuhi, daktari alirudi kuangalia hali ya Nadia.
“Kwa sasa mama na mtoto wako wako salama. Lakini unahitaji kupumzika, kupunguza msongo wa mawazo. Mnatakiwa kusahau kila kilichotokea.
Baba yake hakutaka hata kumuangalia.
“Nadia, mimi sina maneno. Umekosea, umetuangusha. Na sasa utakabiliana na matokeo yako mwenyewe. Umeniharibia heshima.
" Mume wangu usimuhukumu mtoto bila kujua chanzo ni nini.
" Alafu wewe ndio chanzo cha haya yote kuendekeza sana huyu mtoto .
Muda ule waliruhusiwa wakarudi nyumbani , Nadia alikuwa kapumzike chumbani kwake na wazazi wake walikuwa chumbani kwao .
" Baba Nadia mtoto alipata matatizo alipokuwa vacation.
" Matatizo gani?
Mama Nadia alimuelezea mume wake kama alivyoelekezwa na Nadia.
" Sasa mbona hakusema?
" Huenda alikuwa na uwoga na hata angesema tungefanya je? Huenda haikupangwa aolewe na Jawad.
" Sasa huyo mwanaume yuko wapi?
" Hata nae hajui huyo mwanaume anapatikana wapi.
" Mmmmmmm huu ni mtihani mke wangu.
" Ndio imeshatutokea tukabiriane nao.
Wazazi wa Nadia waliamua kumsamehe binti yao na kuamua kulea mimba.
Baadaye mchana Amina rafiki yake wa karibu alienda nyumbani kwao kumtembelea. Alimkuta Nadia akiwa kajipumzisha
“Hei rafiki yangu kipenzi unaendeleaje?
" Nashukuru naendelea vizuri.
Pole sana kwa kilichotokea.
" Bado sijapoa Amina , nitaweka wapi sura yangu ,nitafanya nini kuhusu hili mimba?
maisha yangu yamekwisha. Sasa kila mtu ataniona kama msaliti. Jawad hatanivumilia. Baba yangu hawezi kusamehe. Na Kabir… sijui kama nitaona nae tena.
“Hapana Nadia, maisha yako hayajaisha. Kumbuka, mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Wazazi wanaweza kuumia, Jawad anaweza kuondoka, lakini bado kuna maisha mbele yako. Na kuhusu Kabir… hujui Mungu ana mipango gani.”
Nadia akajifuta machozi, akitazama dirishani. Moyoni mwake swali moja likawa linamtesa:
“Kabir uko wapi? Je, utawahi kujua kuwa mimi nimebeba mtoto wako?”
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni