MMMM DADDY NIKIKUPA UTANIOWA KWELI?* *___________* *SEHEMU YA 01...02* Jamani maisha haya sometimes yanatufanya tufanye kila jambo ilimradi tu tuzipate hizo sasampaππ
Mwenzenu mimi nilitamani sana nisome ili nije kuyabadirisha maisha ya kwetu maana maisha yetu yalikuwa ni magumu kupita kiasi..
Nilifanikiwa kumaliza primary nikajiunga na secondary kiukweli wala sijui nilifaulu vipi maana hata hizo akili my wenu sikujaaliwa kuwa nazoπ
Nilivofika secondary hali ilizidi kuwa mbaya kichwani nikazidi kuwa empty yani nilikuwa naenda tu shule kumridhisha mama maana alikuwa anapiga vibarua nisome ili kesho nimsaidie..
Nilipambana mwaka wa kwanza secondary ukapita ukaingia mwaka wa pili udada ukanikolea nikaanza usumbufu wa hapa na pale πukafika mtihani wa 4m2 nikafeli na huo ndo ukawa mwisho wa masomo yangu ..
Baada ya ndoto za shule kuishia njiani nikaanza kuwaza namna ya kupata maisha mazuri kwa urahisi... niliwaza kuolewa na mwanaume tajiri hiyo ndo njia pekee itakayonitoa kimaisha..
Kwa pale kijijini kwetu walikuwa wananifuata watu wa hali ya chini sana maboda boda wakulima na wafugaji hata hivo wala sikutaka kuwa na mtu wa pale kijijini ndoto yangu ni kuishi mjini..
Sasa mjini nitaendaje?? Nilianza kuumiza akili namna ya kufika mjini na nitafikia wapi?? Siku zilizidi kusonga namimi nikazidi kuipambania ndoto yangu ya kwenda mjini..
Namshukuru Mungu ndoto yangu ya kwenda mjini ilijibiwa baada ya kupata kazi katika familia moja hivi tajiri sana..
Nakumbuka that day aliniita jirani yetu akaniambia kuna mtu anatafuta mdada wa kazi anaishi huko mjini kama ikiwezekana niende mimi..
My wenu nilivosikia kuhusu mjini nikasema yes mambo si ndo haya sasa... yani haijalishi nini kinanipeleka kikubwa nifike mjini mengine yatajulikana mbele kwa mbeleπ
Tulimpigia Boss anaehitaji mdada tukaongea nae tukakubaliana akaniambia ye atakuwa ananilipa vizuri sana na nitaishi vizuri sana kikubwa niwe mwelewa tu..
Basi nilielezewa machache kuhusu familia mpya nayoenda kuishi nayo huko mjini nikaambiwa pia niwashirikishe wazazi wangu nikikubaliwa nitatumiwa nauli ya kwenda..
Nilikwenda kumwelezea mama kuhusu mimi kupata kazi mjini lakini mama alinikatalia akaniambia mjini nitaenda kuharibikiwa...
Kwetu mimi ndo mkubwa mama aliniambia nikiharibikiwa mimi na wadogo zangu watadumbukia humohumo...
Niliambiwa kama shule imenishinda basi ni vyema tu niolewe niondoke nyumbani nikiwa nimeolewa na si hayo mambo mengine ya hΕvyoππ yani huyu mama nae..
Nilichukia baada ya mama kunikatalia ombi langu nikajisemea bora nitoroke tu nikifika mjini nikifanikiwa atanisamehe tuππ
Yani mimi niliamini huko mjini lazima nikafanikiweee kama ni urembo mashallah nimetimia kila idaraππ
niliingia ndani nikaanza kupanga nguo zangu kwa ajili ya kutoroka hatuwezi kuwa masikini kila siku acha nitoke nikatafute maisha huko mbali..
Mama yangu kanilea kwa shida sana mimi na wadogo zanguππyeye ni single maza na kwetu kila mtoto na baba yake...
Wnme wote alozaa nao mama hakuna hata mmoja anaemsaidia kwa chochoteπ₯Ήπ₯Ήndo maana mama anataka niolewe haraka kabla sijaharibikiwa kama yeye alivyoharibikiwa..
Wakati napanga nguo zangu mama alinikuta akaniambia mwanangu usije ukaondoka hapa nyumbani bila ruhusa yangu fuata kile nilichokwambia mwanangu kabla Dunia haijakuhadaa..
Ilibidi nimpigie mama magoti nikamwambia mama please ndoto yangu ni kuyabadirisha maisha yako kutoka kwenye hizi shidaπ₯Ή..
niruhusu mama niende mjini nikatafute maisha nakuahidi mama huko nitapata mume tajiri wa kuniowa na atayabadirisha maisha yetu..
Nilimbembeleza sana mama mwisho akakubali kishingo upandeπ
Baada ya mama kukubali nilimpigia yule Boss anaehitaji mdada akaongea na mama aliahidi atakuwa ananilipa vizuri pesa ya kutosha ili niwe napata chochote kitu cha kutuma nyumbaniπ
Mama alikubaliana naye lakini akamsisitiza nisiende kuteseka... nilifurahi sana jamani niliona ndoto yangu tyr ishatiki bado kufika tu huko mjini..nilitumiwa nauli yangu na pesa ya kula njiani..
Nilijiandaa fresh nikakata tkt huyoooooo nikaianza safari yangu kuelekea mujiniπ₯°π₯°
Njia nzima nilikuwa nayafikiria maisha yangu ya mjini jinsi yatakavokuwaπ₯°π₯°I can't wait ππ
Safari ilitia nanga katika stand kubwa za mabasi nikapokelewa na Boss wangu vizuri akanipakiza kwenye gari lake safari kuelekea nyumbani ikaanza..
Wakati tuko njiani yule Boss alianza kunipigisha story akaniambia nyumbani kwake wanaishi maisha mazuri sana ila kuna changamoto moja kubwa ambayo hiyo ndo ilomfanya atafute mdada wa kumsaidia..
Nilishtuka kidogo nikamuuliza ni changamoto gani?? Akaniambia usijali twende tu utaiona lakini kabla ya yote nataka uniahidi kitu kimoja..
Kitu gani??
Niahidi ya kwamba utavumilia kila kitu na hautonikimbia...kheee niliogopa..yule Boss aliniambia wasichana kadhaa wamekuwa wakimkimbia ndo maana akataka niweke ahadi kabisaaaa mapema kabla hatujafikaπ₯Ί..
Itaendeleaaaaaaa
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni