Gilbert alishtuka kidogo kwa ukali wa maneno ya Leon.
" Mbona umekuwa mkali kiasi hicho Leon ilikuwa ni kwaajili ya chakula tu.
" Ndio Leon mpe nafasi secretary wako akutane na watu wengine ili kubadilisha mawazo. Leyna aliongea .
" Kwani kuja ajenda gani inayoendelea hapa?
Nimesema hapana hapana , hatukuja hapa kubadilishana mawazo bali ni kwenye mkutano wa kibiashara kama mkutano umeisha sioni haja ya mambo mengine.
" Sawa leon nimekuelewa. Jasmine nitakutana na wewe kwa wakati mwingine ukiwa nje ya kazi. Pia karibu sana kwenye kampuni yangu ya G&G ....
Kabla hajamaliza kuongea Jasmine alisema
" Sawa, sawa nitakuja.
" Ok kwaheri.
" Mr Girbet wakati mwingine naomba ikumbukwe kuwa jasmini hayupo hapa kama bidhaa ya kuchaguliwa na mtu anayetaka bali yupo kazini na ni mali ya kampuni.
Girbet alitabasamu alafu akasema
" Hongera sana Jasmine boss wako ana kujali sana
Girbet aliaga alafu akaondoka
Leyna akakunja midomo kana kwamba hajapendezwa na kile alichosema Leon. Akamgeukia Leon, kwa sauti ya kike yenye kejeli akasema.
“Kwa nini uwe mkali hivyo? Ni chakula cha mchana tu, sio harusi. Au kuna kitu kingine unachoficha?”
Maneno yale yalimgusa Jasmine moja kwa moja moyoni. Alimgeukia Leon taratibu, macho yake yakiwa na furaha ya siri, lakini moyoni mwake alihisi ameshinda hatua kubwa.
Leon hakutoa jibu kwa Leyna alinyanyuka na kusema. Jasmine beba mkoba wangu tangulia kwenye gari. Jasmine alibeba haraka mkoba kisha akaondoka kwa mwendo wa Madaha.
"Leyna huwa sipendi kupangiwa kwenye mambo yangu kumbuka kila mtu ana utaratibu wake kwenye haya maisha.
" Ila umeonyesha picha mbaya sana , watu watajua unatembea na secretary wako.
" Sijali chochote kuhusu watu wanafikiria nini juu yangu. Nafuata kile ninachokiamini na ninachotaka mimi.
" Yani wewe ni kijeuri kupitiliza huwezi hata kubadilika.
" Labda ndivyo nilivyo. Kwa heri.
Leon aliondoka akamuacha Leyna akimuangalia.
Leon alifika miaka parking lakini hakumkuta Jasmine.
" Huyu nilimwambia aje hapa kaenda wapi tena.
Aliangaza macho lakini hakuona dalili ya kumuona . Ilibidi arudi tena kumuangalia .
Akiwa anatoka maeneo ya parking alimuona Jasmine kwa mbali akiwa kasimama na kijana mmoja alisimama na kuwaangalia huku akiwa kakunja uso.
" Huyu msichana ni kichaa hivi anataka nipige kelele na kila mtu hapa?
Alitoa simu yake ya mkononi na kumpigia.
" Boss......
" Unafanya nini hapo?
" Hili eneo ni kubwa na mimi ni mgeni hivyo nilikuwa nimepotea..... Kabla hajamaliza kuongea akamkatisha
" Acha usumbufu wa kijinga angalia kushoto kwako na uje haraka sana.
Jasmine aligeuka kushoto akamuona Leon kasimama. Alikata simu na kumfuata aliko.
" Wewe una mambo ya ajabu sana sijui kwanini unaleta mambo ya Uswahili huku.
" Kuongea na watu ni mambo ya Uswahili?
" Unaongea nao una wajua, ni kaka zako au baba zako wale?
" Basi punguza hasira mr arrogant usije ukapasuka.
Walienda kupanda kwenye gari na kuanza safari muda wote kulikuwa kimnya . Mara ghafla Jasmine akaanza kucheka.
Leon alimuangalia
' unacheka nini?
“Boss hebu sema ukweli umenizuia kuungana na mr Girbet kwa sababu ya kazi… au kwa sababu ya moyo wako?
“Usijaribu kufasiri vibaya, Jasmine. Hii ni kazi, na hutakiwi kujiweka karibu na watu wasiohusiana na kazi. Umeelewa?”
“Sawa Boss,” Jasmine akajibu kwa utulivu, lakini tabasamu dogo la ushindi likabaki likicheza mdomoni mwake. Leon alimuangali kwa siri jinsi alivyokuwa anatabasamu .
Mara ghafla Leon akafunga breki kali kando ya barabara yenye miti mirefu, kisha akamgeukia kwa hasira na ukali:
" Jasmine nitahudhukia vikao vingi nikiwa na wewe mambo ya kucheka cheka na kujitajirisha mbele za watu sitaki yajirudie wewe ni binti mkubwa hutakiwi kujirahisisha hivyo.
" Boss jamani unajua mimi ni binti sina mwanaume wala sijaelewa sasa kujifanya mgumu ni kukikosesha bahati huenda kwenye ule mkutano ningejiopolea mume wa maisha yangu.
Leon akashusha pumzi kwa nguvu, akijishika nywele zake kwa mkono mmoja.
“Huu mchezo wako Jasmine unanipeleka pabaya.
Jasmine akasogelea karibu na kusema
"kama nitakupeleke pabaya kwenye moyo wangu Utakubali… au utaendelea kujificha nyuma ya kisingizio cha kazi?
" Unamaanisha nini , unataka niseme nini?
" Sema tu kuwa unanipenda.
Leon alimuangalia usoni na Jasmine nae alimkazia macho bila kupepesa .
" Huwezi kunifanya kunguru muoga ngoja nikuonyeshe kuwa siogopi chochote. Alijisemea Leon kisha ghafla alimvamia Jasmine na kuitandika mabusu matata.
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments
*SEHEMU YA KUMI NA MOJA*