Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

MUME WA RAFIKI YETU Episode 2

30th Nov, -0001 Views 164

MUME WA RAFIKI YETU

Episode 2
Basi mambo yalipita ,na tukawa tumeelekea sebuleni kwa ajilo ya chakula cha usiku ...tulikula chakula lakini nilizidi kumtazama Erick kweli ananivutia jamani ...

Baada ya chakula, tulikaa sebule tukiongea mambo ya maisha ya mjini. Erick alikuwa amekaa pembeni kidogo, akiwa kimya llakini nilikuwa namgusa gusa na mgui wangu.....Naye alitulia alikuwa hana shida wala kushtuka ....

Nilimwangalia kwa jicho la kuibaiba. Mikono yake ilikuwa bado imetuna, iliyoonyesha alichotoka kukifanya uwanjani. Hakuwa na shati, bali fulana ya madoa ya jasho, ambayo kwa njia isiyo ya kawaida, iliongeza tu mvuto wake.

Aggy naye alionekana kimya isivyotarajiwa kwake. Kawaida alikuwa muongeaji sana. Lakini usiku huo, alikuwa akigusa simu yake kila baada ya sekunde kadhaa, kisha anamtupia Erick jicho dogo, haraka na la aibu. Nilimjua. Nilimwelewa. Hakusema, lakini nilijua.

“Nawaachia wageni wangu,” Sandra alisema kwa furaha baada ya muda. “Ninaenda kumalizia kazi . Shemeji Erick atasindikiza wageni hadi vyumbani, si ndiyo mume wangu?”

Erick alitabasamu. “Lazima kabisa,” alijibu kwa sauti yake nzito yenye ukarimu. “Msijali, najua wageni wa mke wangu ni wageni wangu pia.”

Sijui kama Sandra alitambua kuwa nafaai ile nilikuwa naitafuta sana na yeye kanipa nafasi ya wazi kwanink nitegee sasa jamani niligurahi sio siri...

Tulisimama wote watatu mimi, Aggy na Erick kuelekea kwenye korido ya vyumba. Aggy alikuwa mbele, nikafuatia, na Erick nyuma yetu. Tulifika mbele ya chumba cha Aggy, akasimama na kufungua mlango wake.

“Nahisi nitapata usingizi wa mapema,” alisema Aggy kwa sauti ya chini.

“Lala salama, mrembo,” Erick alimjibu kwa sauti ya kutuliza.

Macho ya Aggy yalicheza cheza, kisha akaingia ndani na kufunga mlango wake kwa upole.

Sasa tulibaki wawili tu – mimi na Erick.

“Na wewe je?” aliniuliza kwa utulivu.

“Nipo sawa. Nashukuru kwa ukaribisho. Kweli hapa ni paradiso,” nilijibu kwa tabasamu la kujizuia.

“Tuliamua kuhama mjini kwa ajili ya utulivu huu. Huku maisha ni rahisi, ya kweli.”

Alisogea kidogo karibu na mimi. Mwanga wa taa ya ukutani ulimuonyesha vivuli vya misuli yake vikicheza kifuani na shingoni mwake. Macho yake yalikuwa yamejawa na maswali yasiyo na sauti.

Nilifikia mlango wa chumba changu. Alinifungulia, kisha akashikilia mlango kwa mkono mmoja. Nilipogeuka kumuaga, macho yetu yalikutana. Na wakati huo, kulikuwa na ukimya uliosikika. Ukimya uliojaa hisia. Ukimya ulioandika maandishi

“Usiku mwema Chautamu,” alisema taratibu.

“Usiku mwema Erick…”

Alisubiri sekunde moja zaidi, kisha akarudi nyuma taratibu na kutoweka kwenye kivuli cha korido. Nilipoingia chumbani, moyo wangu ulipiga kwa kasi ya ajabu. Nilifunga mlango na kukaa kitandani bila hata kuvua viatu.

‘Mume wa rafiki yangu…’ nilijikumbusha.
Lakini sauti nyingine ndani yangu ilijibu, ‘Lakini mbona macho yake yamesema mengine?’

Nilinyanyuka taratibu na kufungua pazia. Dirisha lilionyesha sehemu ya uani. Nilijaribu kuona kama Erick alikuwa huko, lakini hapakuwepo. Lakini hisia zake zilikuwa bado karibu, kama harufu ya manukato mazito yaliyobaki hewani.

Nikiwa pale dirishani, mlango wa chumba cha Aggy ukafunguliwa polepole. Nilimwona akitoka na kujifanya kama anakwenda chooni, lakini alipotoka kwenye kivuli, alikuwa kavaa kanga moja ...... Anaelekea alikoelekea Erick .
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MUME WA RAFIKI YETU Episode 2  >>> https://www.gonga94.com/semajambo/mume-wa-rafiki-yetu-episode-2



#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #war

#love #photooftheday #fashion #beautiful #happy #tbt #followme #picoftheday #art #nature #travel #fitness #motivation #life #fun #instagram #friends #smile #food


 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in


Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi mume-wa-rafiki-yetu-episode
‎MUME WA RAFIKI YETU  ‎Episode 3
‎MUME WA RAFIKI YETU ‎Episode 3
MUME WA RAFIKI YETU  Episode 1
MUME WA RAFIKI YETU Episode 1
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
You're not logged in



Warning: Cannot modify header information - headers already sent by (output started at /home/u428456227/domains/gonga94.com/app/pages/includes/header.php:83) in /home/u428456227/domains/gonga94.com/app/core/function.php on line 258