Simulizi za john
0789 824 178 ,
1000
Nilikosa pozi, nikashindwa kujibu. Lakini nikawaza, “Namuogopa nini? Mumewe natembea naye, na hawezi mrudia.” Nikasema, “Nilitaka kujua kama wapo.” Akasonya, akarudi jikoni. Nikapanda chumbani, nikampigia Neema, nikamweleza. Akasema, “Amerudi? Mwambie Scott amtimue!” Nikasema, “Powa.” Nikampigia Scott, akapokea, akasema, “Nambie, bby.” Nikasema, “Bby, nimetoka kununua nguo, narudi, nimemkuta Mama Zawadi yupo.” Akasema, “Amerudi kwa ajili ya watoto.” Nikasema, “Mbona hujaniambia?” Akasema, “Huoni watoto wanalia, wanamtaka?” Nikasema, “Nimeona, lakini kuna ubaya?” Akasema, “Hapana, hakuna ubaya. Nina kazi, nitakucheki baadaye.” Akakata.
Nilishangaa—majibu gani haya? Ananipenda kweli? Nikampigia Neema, nikamwambia. Akasema, “Mambo ya wazazi hayaeleweki, angalia atalala wapi.” Nikasema, “Sawa.” Nikaoga, nikavaa, nikawaza, “Yeye yupo jikoni, naendaje?” Nikajikaza, nikaingia jikoni. Alikuwa anawapa watoto chakula, amepika. Aliniangalia, akasema, “Osha vyombo. Unavaa kimalaya ili iweje? Ulidhani unamiliki ghorofa hii? Nimerudi sasa!” Nikasema, “Sawa,” nikaelekea vyombo. Akasema, “Vaa kanga, unavaa visuruali kwa nini?” Nilitaka kumjibu, lakini nikajizuia. Niliosha vyombo huku akinisema mbele ya watoto. Nikamaliza, nikadeki. Nikaona shanga zangu nilipoinama, akasema, “Umepaka nini kiunoni?” Nikasimama, sikumjibu. Akasema, “Mbona hujibu?” Nikasema, “Mama Zawadi, naomba niache, mbona unanisema sana?”
Akakasirika, akasema, “Unanijibu hivi? Kiruuu, umekuwa nani? Tunalingana?” Nikasema, “Utajua wewe, sitaki kuongea, niache nipige deki!” Akasema, “Umepata wapi ujasiri wa kunijibu?” Akanisogelea, nikadeki, nikasema, “Unataka kunipiga? Gusa uone, safari hii mume wako hataweza kunifumba mdomo, nitakushtaki, utaozea jela!” Alistuka, hakuamini najibu hivyo. Nikamaliza deki, nikarudi jikoni, nikamenya, nikapika chips na mayai, nikachukua nyama aliokaanga, nikaandaa sahani yangu, nikapanda chumbani, nikajifungia.
Nikamweleza Neema, akasema, “Safi, umemkomesha!” Nikiwa naongea, simu ikaingiliwa, nikaangalia—Keanu. Nikamwambia Neema akate, akakata, nikapokea. Keanu alinisalimia, akauliza kama nimefika. Nikasema, “Ndiyo.” Akasema, “Lini utakuja tena, Zawadi?” Nikasema, “Sijui.” Akasema, “Panga siku, uje unisalimie, nimekuandalia zawadi nzuri.” Nikasema, “Keanu, hujaoa? Nisije nikapigwa!” Akasema, “Sijaoa, wala sina mchumba. Ukitaka, nikupeleke kwangu uone.” Nikasema, “Unidanganye, nitapigwa!” Akasema, “Hakuna wa kukupiga, niamini.” Nikasema, “Sawa, nitaangalia ratiba.” Akasema, “Sawa.”
Nikakata, mlango ukagongwa. Nikafungua—Scott. Akasema, “Umeshindaje?” Nikasema, “Salama, pole na kazi.” Akasema, “Asante.” Nilitaka kumudu tai kama kawaida, lakini alinizuia, akasogea nyuma, akasema, “Zawadi, naomba unisikilize. Mama Zawadi ni mama wa watoto wangu, amekuja kwa ajili yao. Tambua hilo na umudu kwa heshima. Wewe ni mdogo, hupaswi kushindana naye.” Nikamuangalia, nikacheka—ananichukuliaje? Akasema, “Umenielewa?” Nikasema, “Amekuambia simuheshimu?” Akasema, “Umemjibu vibaya leo, mpaka anahisi kuna kitu kati yako na mimi.” Nikasema, “Ahaa, kumbe ndiyo wasiwasi wako, asijue?”
Akanisogelea, akasema kwa sauti ya chini, “Zawadi, tunajua jinsi tulivyo, ninakupenda sana. Niko mbioni kumpa talaka, lakini sitaki ionekane namuacha nikiwa na mwanamke mwingine, itaninyima haki. Acha ionekane namuacha kwa tabia zake. Nakuomba uelewe, niko wako.” Akanikumbatia, akanipa busu zito, nikajisikia raha, nikamuelewa. Akasema, “Kipindi hiki akiwa hapa, jifanye unamuheshimu, watoto wakienda shule, anaondoka.” Nikasema, “Sawa, nimekuelewa.” Akasema, “Ndiyo maana nakupenda, wewe ni mskivu.” Nikatabasamu, akatoka.
Nikaangalia saa, muda wa kupika ulifika. Nikachukua kitenge, nikavaa, nikashuka. Nikamkuta Mama Zawadi anapika. Aliponiona, akaniangalia juu hadi chini, akasema, “Kapumzike, naipikia familia yangu leo.” Nikasema, “Sawa.” Nikatoka nje kwa Masai. Aliponiona, akasema, “Umemuona kisirani?” Nikasema, “Yupo anapika.” Akasema, “Mambo ya ndoa yanakwenda, si unaona amerudi?” Nikasema, “Wamerudiana, au amekuja kwa watoto?” Akasema, “Watoto ndiyo hurejesha wazazi, wewe ni mdogo, unajua nini? Wamerudiana, utaona usiku atalala chumba gani.” Nikasema, “Atalala na watoto.” Akasema, “Tuweke dau, shilingi elfu kumi.” Nikasema, “Sawa.”
Tulipiga story, nikarudi ndani. Chakula kilikuwa mezani, mumewe akikaa sebuleni. Alimudu chakula, lakini sikusogea. Lulu akaniita, “Zawadi, mwanangu, njoo tule!” Nilishangaa, lakini nikakaa, kwani niliambiwa nimpe heshima. Tulikula, Mama Zawadi akimpa story mumewe, wakaongea, wakacheka. Nilishangaa—hii ni zaidi ya kuja kuwaona watoto? Lulu akasema, “Baba, mlisha mama chakula kama ulivyonifanyia.” Scott akacheka, akamlisha mkewe, naye akamlisha, watoto wakafurahi. Moyo wangu uliuma, nikaangalia chini. Nilikula kidogo, nikaacha, nikatoa sahani yangu, nikakaa jikoni, maumivu moyoni.
Wao walimaliza, wakaenda juu na watoto. Niliosha vyombo, nikapiga deki, kwani sikuwa napenda jiko chafu. Nikaenda chumbani, nikawasikia wakiwaimbia watoto, waliwalaza chumba kimoja. Kisha nikaskia Mama Zawadi akisema, “Haya, bby, muda wetu sasa.” Scott akasema, “Yes, my wife, twende chumbani kwetu.” Nilistuka—huyu ni nani? Nikasimama mlangoni, nikawasikia wanaongea, mlango wa chumba cha Scott ukafunguliwa na kufungwa. Nikisubiri dakika tano, nikiwa na hofu, nikatoka nikinyata hadi mlangoni mwa chumba chao. Walikuwa wanafanya yao, Mama Zawadi akilia kimahaba, Scott akisema, “Nilikumiss, mke wangu.” Mama Zawadi akasema, “Nataka nikuzalie mtoto wa tatu, nakupenda sana.” Hasira zilinipanda—huyu mbwa ananichezea? Haiwezekani! Nilijiweka sawa… Itaendelea.