Amekomeshwa sasa chezea shemu wangu. Stewart anakupenda sana. Sikia mdogo wangu. Simamia mahusiano yako usiogope chochote yapiganie.โ
Nikavuta pumzi na kusema โndiyo dada, tujiweke naye mbali sio mtu mzuri.โ
Dada alisikitika sana, na mara simu yake ikaita. Nilishtuka maana pia ilikuwa mpya. Akaongea alipomaliza nikamuuliza ndiyo naye akanielezea kuhusu furaha yake na Mr Fabian.
Aliniambia pia watoto wanampenda na Mungu akipenda amekubali kuolewa na huyo baba. Mimi nani niache kumbariki dada yangu na kitu kizuri kama hicho.
Nilifurahi sana dada pia ana furaha sasa, hana kizazi ila kapata watoto watatu kwa mara moja na atakuwa mama. Alifurahi hakika.
Ulikuwa wakati wa furaha sana. Nakumbuka Martha alipiga simu yangu. Nilishangaa sana. Nikamuonesha dada. Dada alisema โpokea tumsikie.โ
Nami nikafanya hivyo, Martha alisema โnipo mbele ya nyumba yenu. Nina maongezi na wewe.โ
Dada alisema โhuendi peke yako. Twende wote.โ
Nikamtazama tu, na kisha tukatoka. Alipotuona alishtuka. Dada alimsogelea na kusema โumenitia aibu sana. Najua nina dada kumbe huna akili. Kwanini umfanyie hivyo mdogo wangu ambaye na wewe ulisema unampenda.โ
Nakumbuka Martha alisema โnaomba kuongea na Ndeana wewe tutaongea siku nyingine.โ
Dada alitaka kujibu, nikamwambia dada kwa upole โdada nisubiri pale. Usijali.โ
Dada alitii na kusogea pembeni.
Nakumbuka Martha aliniambia โNdeana, kaa mbali na Stewart. Ni mwanaume wangu, ninampenda sana. Wakati wewe unaenda sikujua kama itakuwa hivi, nilijua ni kama anavyowafanyia wengine. Sijui umemfanya nini kakuganda ila nataka utambue ni wangu. Hakuna mwanamke atakuwa naye, nipo tayari kwa lolote ila sio kuwa mbali na Stewart. Yule ni mwanaume wangu tu.โ
Nikajikuta nacheka nikisema โkwahiyo ulitaka kuharibu maisha yangu. Sasa kama ni mwanaume wako upo hapa kufanya nini. Kila mtu atumie nafasi yake vizuri. Wewe ni wako haya tamba naye na mimi ni wangu nitatamba naye.
Mwanaume mwenyewe yule utakulaje peke yako dada. Hata hivyo mlipokuwa mnafanya mapenzi sikuwepo, na sasa ni muda wangu. Kama unampenda sana. Kamwambie akae mbali na mimi.
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 142
Ila kwa ushauri kwako wifi yangu kipenzi. Ni bora wakati kama huu mimi nipo nyumbani, wewe kafurahi naye, maana akija kwangu hatorudi kwako. Likaka kama lile nakuachia vipi ufaidi peke yako eti wizouh.โ
Alinitazama kwa hasira midomo ikitetemeka na nikamwambia โnikupe pesa yako ya mafuta maana umetoka mbali, karibu ndani basi upate hata maji.โ
Aliniambia โsasa cheka utalia Ndeana, utalia sana.โ
Nikacheka na simu yangu ikaita. Nikamuonesha anayepiga hapo nimesave โMy sweet person. โ
Nikapokea na kusema โHello chautamu wangu.โ
Akacheka akisema โtotoo, niko tayari. Hapa nilivyo na hamu na wewe nikikukamata.โ
Nikacheka nikisema โhata mimi nipo tayari my love, lakini dada yako kipenzi Martha yupo hapa ananisumbua sana.โ
Alibadilisha sauti na kusema โhivi huyo malaya ananitafuta nini lakini, kwanini anakusumbua, nakuja hapo sasa hivi mke wangu, nakuja please usinune nakuomba sana.โ
Nikadeka nikisema โnaanzaje kununa dady wakati tunamtoko wetu leo. Nakusubiri.โ
Aliniambia โI love you my Sweet person, Nakupenda.โ
Nami nikajibu โNakupenda my sweet person, ninakusubiri kwa hamu.โ
Stewart akashuka pumzi na kusema tena โNakupenda.โ
Kisha nikakata simu.
Martha alichanganyikiwa huku akisema โmalaya mimi, malaya, mimi malaya kweli Stewart. Utaona, utaona Ndeana. โ
Alikuwa anajikuna nywele zake na kuingia kwa gari. Mimi na dada tulitazama na kuanza kucheka huku dada akisema โsaafi sana, umekua mdogo wangu safi.โ
Nikacheka na kushikana mikono na dada yangu kuingia ndani huku dada yangu akiuliza โalikuwa anasemaje?โ
Nilimsimulia basi tulicheka sana huku dada akisema โdada mnafiki yule, marafiki wengine wanafiki sana na nafutilia mbali namba yake simtaki tena. Mtu mzima hana akili kabisa. Roho ya kwanini mbaya sana.โ
Ingawa uso wa dada yangu hauna ile nuru kama zamani unajua tena anayopitia ila najitahidi sana kumfanya afurahi na nashukuru Mr Fabian kaweka mambo sawa walau dada hata maumivu ya kusalitiwa yanapungua na hata ya kukosa mtoto walau ana watoto wa Mr fabian wanamchangamsha hivyohivyo maisha yanasonga
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 143
Baada ya kufika ndani nilionelea ni vyema nikaoge kwa maana My baby kaniambia anakuja na hivyo nimemvuruga na Martha basi najua atafika sio muda. Nilibadili nguo zangu na kutoka kwenda bafuni. Basi nikiwa bafuni yeye alifika nyumbani na alipokelewa na dada yangu. Mimi nilipofika sebuleni tu, tukagongana macho tukishangaana. Kisha nikasalimia, aliniitikia kwa kusubirisha sana. Ilinibidi nipite niwaache kwanza pale mimi nikavae haraka haraka.
Nimefika tu chumbani, nimekutana na meseji yake. Ameniandikia โUnafanya nini sasa totoo, unataka niumbuke mbele ya dada huku unaniamsha na hiyo kanga yako. Ndeana hivi unajua wewe ni mzuri sana. Wewe ni mzuri aiseee!!, nimechanganyikiwa. Nakupenda sana, Nakupenda kama nikukamate huko chumbani kwako ila ndiyo siwezi sasa.โ
Nikacheka na kusema โNjoo, unamtania baba Vee wewe. Atakupiga ufe. Nakupenda baby wangu mzuri mzuri, navaa haraka tuondoke.โ
Basi alikaa kimya nadhani alikuwa anaongea na dada yangu.
Mimi nikajindaa vizuri, nikapendeza. Nikabeba na ile pochi yangu mpya.Hakika nilipendeza sana. Hata mimi mwenyewe nilijua nimependeza sana.
Basi taratibu mtoto mzuri nikatoka. Waliponiona, Big Boss akasimama. Taratibu alinifuata tena karibu yangu na kusema โumependeza sana. Umependeza.โ
Dada pia alisema โSanaa mdogo wangu, umependeza mno.โ
Nilitabasamu nikisema โinatosha basi mnanifanya najisikia vibaya sana.โ
My boss akatabasamu, kisha akanikumbatia akisema โNakupenda sana Ndeana, nakupenda sana. Nisamehe kwa yote yanayotokea. Sijui niseme nini kwasasa, Sijui nimfanye nini Martha. Kwasababu sitaki mtu yeyote akusumbue. Ila yote kwa yote nisamehe mimi.โ
Dada yangu aliinuka na kusema โShem, acheni kumpa shetani. Mnakaa mnamzungumzia mtu ambaye lengo lake ni kuwaharibia furaha yenu. Msimpe shetani nafasi. Ni kitu kibaya sana kwenye mahusiano kuongelea mambo ambayo yamepita na yanawaumiza. Zaidi nawatakia mapumziko mema. Shemeji yangu Happy birthaday.โ
Stewart wangu alitabasamu tu na kisha alisema โnashukuru sana shemeji yangu. Nafurahi sana kusikia maneno haya kutoka kwako. Asante sana.โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 144
Yaani Nilikuwa nasikia raha sana, nilikuwa nasikia raha mno, nilisahau kabisa kama tuna dereva mule ndani. Hivi jamani, huwa mnapenda kukiss kama mimi na mnapata raha kama nnayopata mimi au mnakiss ili mradi tu.
Nilikuwa na utalivu nafurahia busu kama sipo duniani vile. Hakika nilifurahia sana. Barabara yote sisi tunaambiana kwa kunongโona โI love you baby!!โ
โ I love you baby!!โ
โNakupenda.!!โ
โNakupenda.!!โ
Huku vimidomo kama tunakula ndimu tu โmwaaaah!!, mwaaaahh!!, mwaaah!!โ
Mimi moyoni najisema โmwanaume huyu sitosheki, sitosheki hata kidogo asiache kunibusu. Anikiss tu na hata sijui wapi tunaenda.
Nimekuja kushtuka gari imefika uwanja wa ndege. Ndiyo Dereva anasema โTumefika.โ
Nikamtazama Baby wangu. Hapo dereva alishuka tukabaki wawili.
Basi Boss wangu aliniambia โnatamani nikukamatie nisikuachie. Yaani siwezi hata kutembea baby, una nini lakini, kwanini wewe mtamu hivi baby?, niambie unapakaga nini totoo, maana utakuja kuniua ujue.โ
Nikatabasamu nikisema โunachopakaga ndiyo na mimi napaka.โ
Akacheka akisema โIna maana na mimi ni mtamu kumbe.โ
Nikacheka nikisema โmapenzi matamu nikiwa na wewe.โ
Akaniuliza akitabasamu โwanaosemaga mapenzi mabaya kwani huwa wanafanya nini baby wangu. Mapenzi yamepatwa na sisi yaani tumeyapata.โ
Nikacheka nikisema โsasa baby, tunaenda wapi mbona sikuelewi.โ
Akatabasamu na kusema โumewahi kwenda Zanzibar baby?โ
Nikatikisha kichwa changu kukataa tena huku natoa macho yangu.
Alitabasamu na kusema โbasi ndiyo tunaenda hivyo, hotel kubwa sana ukaone wenzetu wanavyofanya. Nakuamini najua utatoka na kitu. Si ndiyo mpenzi?โ
Nikamuuliza kwa kushangaa โYaani mimi napanda ndege?โ
Akatabasamu akisema โacha kunichekesha ndiyo uongee na vitendo baby.โ
Nikacheka nikisema โSijawahi kupanda ndege hata siku moja. Naogopa sana unajua hili. Naogopa mwenzako.โ
Akasema โusijali, upo na mimi, upo na mimi kipenzi changu. Nataka ufurahi kama hutokuja kufurahi tena.โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 145
Nikatabasamu ila ndiyo naogopa. Huo uwanja wa ndege wenyewe sijawahi fika. Basi nikapata ma muda wa kumpigia baba yangu na hatimaye tuliingia ndani sasa huku Stewart akisema โyaani na ushamba wako nakuchukua video mpaka uchanganyikiwe.โ
Mimi nikawa tu mnyonge tu maana naogopa mno nilikosa raha. Nikamuuliza tu โsasa kwanini mimi sina nguo?โ
Akasema โwewe achana na mimi, twende nikakucheke.โ
Nikacheka tu nikisema โwewe haya tu.โ
Basi akafanya utaratibu wote muhimu, kisha sasa tukaelekea kwenye ndege sasa. Tulipigana picha wenyewe. Kisha alinishika kwa kunikumbatia sisi hao tukaingia ndani ya ndege.
Sitaki hata kuelezea palivyo na raha yake. Ni pazuri sana. Mimi nikakalishwa sehemu yangu maana sijui hata wapi natakiwa kukaa. Akakaaa pembeni yangu, akanifunga mkanda. Basi muda wa ndege kuondoka ulipofika.
Mkiniona nilivyomshikiria, mngecheka. Nilimkumbatia kwa nguvu hata ilipokuwa sawa kabisa ndiyo nikafumbua macho yangu. Stewart sasa mkimuona anavyonicheka, anacheka hana mbavu, mimi nami nikaanza kucheka. Tulicheka ila mwisho wa siku yakaisha, atafanyaje sasa na mwanamke ndiyo mimi mtoto wa uswahilini.
Basi mwenzenu nilitamani safari isiishe ila sasa ni safari fupi sana. Tulifika mji mzuri sana. Pale pia tulichukuliwa na usafiri maalumu wa ile Hotel. Basi kufika kwenye ile Hotel. Ni nzuri sana, nilimtazama na kutabasamu nikisema โbaby ni pazuri sana, ni pazuri sana hapa. Kwanini umenileta sehemu nzuri hivi.โ
Akatabasamu akisema โumefurahia?โ
Nikasema โbaby Hotel ni nzuri sana unajua, nzuri mno.โ
Akatabasamu tena akisema โI told you, tuingie ndani sasa.โ
Nikawa nachekacheka tu. Basi sasa tukaingia ndani yaani pazuri. Mimi natabasamu tu. Tulipokelewa mpaka kupelekwa kwenye chumba chetu maalumu. Nyie!!!, nyie!!, jamani mnaonaga zile video mtandao wamepamba maua kuanzia mlangoni mpaka kitandani halafu taa fulani hivi. Ndiyo!!, hizo hizo najua umewahi kuona. Sasa mimi, mimi Ndeana baby wangu aliandalia chumba cha hivyo.
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 146
Nilijikuta naanza kulia, naanza kulia kwa furaha. Wale wahudumu walimuimbia tena Happy birthaday, nilijikuta namkumbatia nalia kwa furaha kwa vyote ambavyo amewahi kunifanyia.
Nililia huku na yeye tena akilia kwa uchungu akiniambia โNdeana wangu Nakupenda. Asante kwa kubadilisha maisha yangu.โ
Nilisema kwa hisia nikimtazama huku machozi yananitoka machozi ya furaha โNakupenda Stewart. Nakupenda baby.โ
Akanibusu tena kwa hisia akisema โYou Know what totoo(unajua nini totoo?โ
Nikasema kwa kulia huku nadeka โsijui baby, sijui kwanini unanipenda hivi, kwanini?โ
Akatabasamu huku akiwa na hali ya kulia akisema โNdeana, I am not getting enough of you(sitosheki na wewe) Sikuchoki kabisa. Wewe ni mwanamke mzuri sana. Sijawahi kukutana na mtu mzuri kama wewe kwenye maisha yangu. Najua kuna mapungufu na mazuri. Nivumilie sana, usinichoke.โ
Nikasema kwa kulia โi will baby, mimi pia niambie utanivumilia?โ
Alitabasamu akisema huku ameshikilia kiuno changu โNdeana, nataka nikuambie kitu. Promise me utakubali?โ
Nikajibu haraka โunataka kuniambia kitu gani baby, Please tell me!!โ
Akanitazama akisema โNiambie utabaki na mimi hata baada ya kukuambia?โ
Nikamtazama nikasema kwa upendo na kusema โhakuna kitu cha kunitenga mimi na wewe, hakuna Stewart tell me.โ
Akashusha pumzi yake ndefu sana, Akafumba macho yake na kusema kwa hisia sana huku machozi yakitaka kumtoka (Ndeana, nisamehe sana... Ndeana mimi.. โ
Mimi nikamtazama nikisema โTell me, tell me Stewart!!โ
Akanibusu kwa hisia sana na kusema ......๐คฃ๐คฃ๐คฃnyie sijui hata nachekacheka nini๐๐๐๐๐๐
NAAAAAAAAAM
Offer inaanza rasmi leo
Malizia SEASON FOUR na FIVE zote kwa offer ya sh 1000
Kumbuka mwisho wa story ni season five.
Na hapa facebook tutaishia season FOUR tu five itapatikana WhatsApp pekee
Kwa hiyo mdau, njoo umalizie leo vipande vyote vya season four na five kwa offer ya sh 1000
๐ต๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐ฝ๐๐
๐๐๐๐ ๐ด ๐๐๐๐ 0743433005 ๐๐๐๐ ๐จ๐ฎ๐ถ๐บ๐ป๐ฐ๐ต๐ถ
๐ผ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐พ๐๐๐๐๐จ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ +255743433005 ๐๐๐๐๐๐๐
๐๐๐๐
KUMBUSHO, Hapa Facebook story hii itaishia season four pekee, season five italipiwa
LET'S GOOOO.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments