Baada ya hapo sasa ndiyo tulienda kuoga pamoja, Yaani kama mtoto ananipigisha mswaki, ananisugua kwa upendo, na tena ananiambia scrub kasema ujisugue sana, na yeye ndiyo ananisugua na ile dodoki kaniletea. Mpaka nacheka. Ngozi inateleza tu nasikia raha sana, uso unateleza mpaka noana maajabu tu na ndiyo naanza safari. Kiisha tulitoka, tukavaa wenyewe tena tulivaa nguo zinazotaka kufanana hivi. Na aliniambia namna nimependeza na kuonekana mzuri zaidi. Kisha alinishika mkono akiniambia sasa tukanywe chai.
Tulipendeza sana, ni umaskini tu ila nakuambia kama una pesa Zanzibar ni sehemu ya kuja kutembea pia. Yaani ni Hotel nzuri pia namna wanahudumia mpaka raha.Mwanaume wangu anapenda kunipiga sana picha. Kila sehemu nzuri atanipga picha na kunisifia. Basi tulikuwa tunakula na akaniuliza “vipi umepapenda huku?”
Nikamwambia “sana baby asante sana.”
Akaniuliza “vipi turudi tena?”
Nikasema “hata kila siku ni vile tu gharama.”
Akacheka akisema “kwako sioni hatari kutumia kila kitu ili mradi tu ufurahi.”
Nikatabasamu.
Basi hii siku sehemu zote unazoona watu wanaenda kutembea wakifika Zanzibar mji wa utalii wenye vitu vizuri vya historia ya nchi yetu mimi nilienda. Kama utalii nilifanya haswa. Nilinunuliwa mavazi ya watu wa huku pia, mitandanio viatu na zaidi. Yaani nilisikia raha sana. Tulienda forodhani, tukala tukacheka tukafurahi maana kuna mengi sana sana. Alinipitisha sehemu wanasimulia kidogo historia basi kwakweli nilitosheka sana. Hapa najaribu tu kuwaambia raha kwa kifupi ili tuendelee na simulizi hii tamu sana.
Tulirudi Hotel tukiwa na furaha sana. Yaani hii sehemu tulifurahia sana, sana, sana , sana. Nikisema simchoki ni kweli simchoki. Mtu nipo naye ila ninamkumbuka kuwa naye mwilini kila muda. Mimi Ndeana ninampenda sana Stewart. Ninampenda kutoka ndani ya moyo wangu. Yeye ni mwanaume wangu mzuri sana. Hakuna kama yeye katika maisha yangu.
Tulipanga kuwa siku inayofuata mchana wake ndiyo tunaondoka. Na nakumbuka aliniambia “raha ya huku totoo, upande na boti pia. Ndege ushapanda ila nakuahidi utapanda ndege tena na tena.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 155
Nataka upande na boti.”
Nikatabasamu. Akawasiliana na watu wa Hotel. Wao ndiyo wanashughulia mambo yote. Tulikunywa chai vizuri na kisha aliniambia “mafuta yamekupenda, siku ya tatu leo ni kama naanza kuona unazidi kunivuruga.”
Nikacheka. Kisha nikamuuliza “uso wako unaonekana kama hauna furaha. Kuna tatizo gani?”
Akanitazama kwa hisia na kisha aliniambia “njoo ukae karibu yangu Ndeana.”
Nikasogea. Akanitazama na akaniuliza “unakumbuka nilikuambia nataka ufurahi hopa kama hutokuja kufurahi tena?”
Nikaitikia kwa kichwa huku moyo ni paaah!!, paaah!!, paaah!!
Aliniambia kwa huruma “nilitamani nikuambie kuanzia siku ya kwanza kwasababu ni kitu kinanisumbua sana. Ila sina ujasiri.”
Nikamuuliza “ni kitu gani?, niambie basi.”
Akanitazama na kusema “unajua kitu pekee naogopa ni kukupoteza wewe Ndeana.”
Nikazidi kuogopa nikisema “usinifanyie hivyo, si uniambie baby lakini!!”
Akatabasamu akisema “ikitokea, sina pesa za kukununulia mafuta, siwezi kukutunza kama hivi, kukupeleka sehemu nzuri, kukunulia simu, kukulipia saluni na mahitaji mengine. Utanivumilia?”
Nikavuta pumzi nikisema “Stewart unaongea nini?, wewe ni mwanaume wangu. Tangu umenifahamu umenipenda na kunijali sasa ni kwanini nishindwe. Niambie una maanisha nini?”
Nilimuona akidondosha chozi katika maumivu, nilimuonea huruma, nikaogopa sana. Nikajikuta namkumbatia na yeye alianza kulia kwa uchungu. Nikamwambia “Please!!, sipendi kukuona hivi niambie una tatizo gani, niambie tafadhali.”
Nikiwa nimemshika mikono aliniambia akiwa anatokwa machozi amefumba macho. Alisema akilia “Ndeana, ninaweza kupoteza kila kitu, hisa katika hoteli yetu niliyoipambania sana, ninahofia kupoteza hisa zote kwa hotel. Na sio hicho na kila ninachomiliki. Ndeana, mimi na familia yangu ndiyo tunahisa kubwa ssna kwa ile hotel.
Ila miaka ya nyuma kidogo kuna matatizo yalitokea. Tulianza kuazima pesa kutoka kwenye akaunti ya hotel. Pesa nyingi mno Ndeana. Nilianza kuhangaika huku na huku kumuhangaikia mama yangu aliyekuwa anaumwa sana.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 156
Kumpeleka nje ya nchi na mambo kama hayo. Bodi ya hotel ilitupa muda.Nami nikajiamini. Ila unajua maisha yalivyo, yakatokea tena matatizo yanahitaji pesa zaidi. Ilinibidia tena nichukue pesa kutoka Hotel.
Ndeana na siku zilipita sana. Leo hii natakiwa nisafiri tena kikao tutafanyia Arusha. Ndeana hiki kikao ndiyo kitaleta maamuzi kama nibaki kwenye nafasi yangu huku nikiendelea kukatwa kila kitu, au niache kila kitu na wao waendelee na maisha yao nami yangu.
Naumia kwasababu nimewaangusha wazazi wangu, waliipambania sana ile Hotel. Mimi mwenyewe nitaishi vipi sasa nianze tafuta kazi.
Ndeana wewe hapo utaishi vipi, Ndeana ninadaiwa pesa nyingi sana na wazee hawanielewi kabisa. Nitafanya nini mimi, nitafanya nini sasa. Ndeana, Ndeana wangu, utabaki na mimi kweli hata kwenye umaskini, Ndeana utanijali, utakuwa na heshima hivihivi au itakuaje?, nakuomba Ndeana ubaki na mimi tafadhali nakuomba sana.”
Nami nikajikuta nalia sana. Nikamkumbatia nikisema “Sikuwa na wewe kwasababu ni Boss. Nipo na wewe kwasababu Nakupenda. Stewart mimi nakupenda sana, mimi nakupenda kwasababu wewe ni mwanaume mzuri sana kwangu.
Usilie Stewart nataka nikutie moyo kuwa utalipa na nafasi yako itabaki tu. Na hata isipotokea wewe bado ni mwanaume wangu. Umefanya mengi kwangu, umefanya mengi kwa familia yangu.
Baba yangu sasa ana afya nzuri kwasababu wewe unahudumia na kuhakikisha anapata kila kitu kwa wakati. Umempa tabasamu dada yangu. Tazama mimi, ni kwasababu yako. Ninakuambia tu kuwa, nipo na wewe, kuanzia mwanzo, mwanzo mpaka mwisho nitakuwa na wewe.
Nakupenda sana, Nakupenda Stewart. Usilie kabisa, Watu wengi kwenye maisha wanapitia changamoto na wanazishinda. Kwanini wewe uogope na upo na mimi. Nitabaki na wewe, nitabaki na wewe mwanzo mpaka mwisho.
Kwasababu ninakupenda kuliko kitu chochote. Wewe ni mpenzi wangu. Mpenzi wangu wa maisha. Nakupenda. Wewe nenda mimi nitakuwa nakuombea na kwa lolote litakalo tokea huko mimi nipo pamoja na wewe. Kwasababu hakuna Ndeana bila Stewart.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 157
Stewart alinikumbatia kwa nguvu sana. Tulilia pamoja. Nakumbuka namna alivyokuwa ananitazama na aliniambia “walau nina wewe. Maneno yako yamenipa nguvu ya kutabasamu. Nilikuwa naogopa kuhudhuria kikao cha bodi. Ila sasa nitaenda na sitaogopa chochote kwasababu hata wakisema nivuke mito na milima nitavuka na wewe. Wakisema niumie nitaumia na wewe na kushinda nitashinda nikiwa pamoja na wewe. Nashukuru sana Ndeana wangu.”
Unajua moyo wangu bado unamuonea huruma sana. Amejitoa kwaajili yangu kumbe ndiyo anaona kwa mara ya mwisho. Kafanya kila kitu kwaajili yangu. Ndani ya moyo wangu nilijikuta nasema “Mungu namuweka huyu mwanaume mikononi mwako. Mimi siwezi kufanya lolote wala chochote. Ila wewe Mungu unaweza. Wewe ni Mungu wa watu wote. Msaidie mwanaume wangu huyu.Msaidie hata kama sio kwaajili yangu basi kwaajili ya familia yake, baba yangu na wale wafanyakazi wengine wanamtegemea maana hata sisi tupo hatiani Boss mpya kama akija anaweza kutufukuza. Tutaishi vipi sisi.”
Alinitazama akisema huku anatabasamu japo sasa najua ananiigizia “Unawaza nini?”
Nilisema “Nakuwaza wewe kipenzi.”
Simu yangu ikaita. Nikapokea na nilipopokea tu Henry naye kunikera tu eti “mpenzi umeamua kuniblock usifanye hivyo. Naomba nielewe.”
Nikajikuta nasonya nikisema “nitablock na hii mpumbavu wewe.”
Nikakata simu, Stewart aliniangalia na hakuuliza kitu. Badala yake aliniambia “Nakupenda sana my sweet person.”
Nikamtazama na kusema “Nakupenda sana Mr Handsome.”
Alitabasamu na kuniambia tujiandae maana yeye anatakiwa kuwahi. Basi hivyo ndiyo ilikuwa wala hakuniuliza kuhusu Henry yaani ni yeye na mimi hana ugomvi kabisa.
Tuliondoka Hotel, ingawa yeye alikuwa anajitahidi kuigiza yupo sawa ila mimi nilikuwa namuonea huruma mpaka naumia. Nakumbuka aliniambia “usijali kipenzi umenitia moyo, siogopi tena naamini kila kitu kitakuwa sawa.”
Tulifika kwenye boti, alinipiga picha ila sikuwa na furaha yaani. Safari hata haikunoga. Nakumbuka tulipofika alifuatwa na yule kaka aliyetusindikiza mara ya kwanza.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 158
Tulianza kuagana na nakumbuka nilimuambia “Will miss you my own favourite Person.. Go safe Dady and come back to me safe, thank you for everything my baby.. Thank you for being the reason behind my happiness. Your love, kindness and support means everything to me and I feel incredibly lucky to have you in my life.. Nakupenda sana Stewart please stay in my life forever babe.
( Nitakukumbuka sana mtu wangu ninayekupenda sana. Nenda salama dadi na urudi salama kwangu. Asante kwa kuwa sababu nyuma ya tabasamu langu. Upendo, ukarimu na kunishika mkono kunamaanisha kila kitu kwangu na najisikia kuwa na bahati sana kuwa na wewe kwenye maisha yangu. nakupenda Stewart tafadhali baki kwenye maisha yangu daima.)
Alitabasamu sana, alinikumbatia na kusema “Till death do us Apart my sweet person. Nakupenda sana. Asante kwa kila kitu nimefurahi sana ni kama sina mzigo moyoni. I wili figth na kufanya kila kitu sawa. Ndeana wangu , Thank you darling... Stay well blessed.. and keep being a nice person.. I love you.”
Nikatabasamu na kusema kama nataka kulia vile “Nakupenda sana Stewart.”
Akacheka kisha akajibu “Ndeana hili ni tatizo la Kitaifa kwa maana mimi nakupenda mno, nakupenda wewe katoto. And i will miss you My sweet person.”
Nilimkumbatia nikilia huku nikisema “I will miss you more baby.”
Basi akatoa pesa ila siku hii nilikataa. Nilisema “hapana, lolote likitokea huko utajua pakuanzia. Tunza mpenzi wangu.”
Alinitazama na kuumia sana. Kisha alinibusu na kuingia ndani ya gari nami nikabaki napunga mkono kumuaga. Ni ngumu sana kumuaga mtu unayempenda.Nikawa tu najisemea “Will miss you Darling, will miss you.”
Sijafika hata mbali, nimeingia tu kwa bajaji alinitumia ujumbe, hata nikacheka “Hivi babe nimeondoka lini? Mbona naona ni muda mrefu sasa, sijafika hata uwanja wa ndiyo kwanza kama sijakuona siku nyingi sana.”
Nikatabasamu na kumjibu “Miss you Loads bby wangu.”
Na yeye akanijibu “Ndeana, I love you. Sitakuangusha.”
Nikatabasamu tu kinyonge na kumjibu kimoyomoyo kuwa sitamuangusha pia.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 159
Nikiwa ndani ya bajaji, huu sasa upepo wa china jumlisha upepo wetu wa Mungu basi napepewa na nilivyo na mawazo hadi lile lipo mlangoni kama pazia, linanifunika mpaka usoni. Nitafanyaje sasa ndiyo baby wangu ana stress. Basi nikawa nakumbuka zile nyakati nzuri na tamu ambazo tulikuwa nazo pamoja Zanzibar. Kuzurula pamoja, mara nibebwe, mara nipigwe busu. Nilikuwa namkumbuka sana Mwanaume wangu mzuri na mkarimu sana.
Unajua kupendwa ni raha, mimi nimeanza kupendeza, nimenawiri vizuri, yaani ninaonekana ni mtu kati ya watu. Moyo ukiwa na furaha na mwili unakuja vizuri sana. Mimi niliongezeka. Nilipendeza na yote haya ni kwaajili ya mpenzi wangu mzuri sana Stewart ambaye kwasasa anapitia matatizo. Ninatamani niwe mtu mwenye pesa nimsaidie ila ninawezaje sasa. Siwezi yaani.
Basi nikafika nyumbani nikiwa mnyonge sana. Nilikuta baba amekaa sebuleni, na mimi ndiyo nilikuwa na begi ambalo tulisafiria. Basi baba alinikaribisha kwa furaha sana akiniambia “karibu sana mwanangu karibu.”
Nami nikamsalimia, wakati nafanya hivyo na dada yangu alitoka. Aliponiona alisema “mdogo wangu, mbona umependeza sana. Kwani umepaka nini huko maana unawaka.”
Nilitabasamu kivivu sana, nikajikuta nashindwa kujizuia kuonesha huzuni yangu. Dada na baba walitazamana na kisha dada yangu aliuliza “Upo sawa kipenzi?, umegombana na shemu?”
Nilikaa chini na kuanza kulia nikisema “sijui hata inakuaje baba. Stewart anapitia wakati mgumu sana. Ameniambia kuwa alipitia wakati mgumu kuuguza mama yake. Hakuwa na pesa, akatumia pesa nyingi za Hotel.
Aliamini anaweza rudisha. Ila imekuwa muda mwingi sana, Hotel inapitia wakati mgumu pesa hajarudisha na anaweza kupoteza kila kitu ili tu kufidia pesa anazodaiwa. Baba anaumia sana, analia. Namuonea huruma itakuaje sijui.”
Baba alikuja karibu yangu, alisema “mwanangu, mwanangu Ndeana. Siku zote nimekuwa nikiamini Mungu kwenye maisha yangu. Mwanangu, Ndeana katika maisha kuna nyakati, nyakati za kupanda, nyakati za kushuka na misukosuko ya kila aina. Unapopitia nyakati zote hizi, iwe furaha au huzuni ni Mungu. Wewe ndiye mwanamke wake.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 160
Mwanamke wewe umeumbwa kumtia moyo, kumfariji, kumpa nguvu na kumuombea wewe ndiyo kibali chake. Ndiyo maana maneno ya Mungu yanasema apataye mke amepata kibali. Ni wewe ulisema unampenda sana yule kijana. Na yeye anakupenda kwa macho tumeona na tumesikia juu ya pendo lake. Wewe hata iwe nini, kuwa karibu na mwenzio.
Na maandiko yanasema Furahini wakati wote, ombeni pasipo kukoma, shukuruni katika kila hali; kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajiliyenu mkiwa ndani ya Kristo Yesu.Naam, hamjui Mungu anataka nini kwenu, nami namuombea heri na pengine hii ni njia ya kuwafikisha kwenye ndoa yenu.
Mwanangu, asiwepo wa kukurubuni, fanya kazi, panapo msaada msaidiane na muwe mfano. Unazijua shida najua utamvumilia na binafsi nina imani na Stewart atashinda, na hata akishindwa sisi tupo pamoja na yeye. Ni kijana wangu katusaidia sana m, tazama sasa nipo imara ni kwaajili ya pesa zake. Mungu atamsaidia.
Mungu anasema “Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini. Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani: wao hawapandi wala kuvuna wala kuweka cho chote ghalani. Lakini Baba yenu wa mbinguni anawali sha. Je ninyi, si wa thamani zaidi kuliko ndege? Ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi kwenye maisha yake?. Mwanangu mtegemeeni Mungu. Funga moyo wako, ziba masikio yako msikilize mwenzio tu. Sisi tupo pamoja na wewe.”
Maneno ya baba yaliniingia moyoni sana, nilijilaza na dada yangu alivuta pumzi na kusema “baba upo sahihi sana. Nimefurahi sana baba kusikia maneno yako. Baba yangu ulichoongea ndiyo na hata mimi ninamuambia mdogo wangu, asitetereke, awe na imani na mwenzie.
Ndeana, mimi sisemi sana baba kasema kila kitu. Ila sijui kwenye Mithali kuna mstari unasema “Moyo wenye furaha ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.”
Ndeana hakikisha hili halikosekani kwenu bila kujali nini kinatokea. Tupo pamoja na wewe.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 161
Nilijikuta nasema “nawashukuru sana, nawashukuru mno, maneno yenu yamenipa faraja sana. Nitahakikisha hilo kwa mwenzangu pia. Asanteni sana.”
Wote walinikumbatia kwa furaha na baba aliniambia nikapumzike kwa maana nilionekana kuchoka sana. Ni kweli nilichoka sana akili yangu kwa kumuhurumia Stewart wangu.
Basi niliingia chumbani, nikajitupa tu kitandani. Nilichoka sana yaani. Nikalala tu. Nililala kwa muda sana. Mpaka mida ya saa tatu hivi ndiyo niliamka.
Nilipoamka nilikutana na ujumbe kutoka kwa mpenzi wangu. Alikuwa ameniandikia “Ndeana wangu, my totoo mimi nimefika salama. Nimejilaza hapa kitandani kama nikuvute uje hapa nikukumbatie kwa nguvu.”
Nilisoma nikitabasamu tu, nikamjibu “Unajua nakumiss sana mjinga wewe”
Yeye alinijibu “nakumiss ovyo mtoto mzuri. ni kama nina mwaka huku ujue.”
Nikacheka, akaniambia “nikuambie kitu ambacho namiss sana.”
Nikamuuliza kwa tabasamu “eeh baby kitu gani hiko?”
Akaniambia kwa viemoji “namiss sana vile ukinikalia usoni😫😫, yaani harufu yako 😋😋si unanielewa baby, harufu yako ya sehemu eenh umeelewa?🙆🙆”
Nikacheka nikisema “🤣🤣🤣Sehemu, sehemu gani sasa baby wangu?”
Akacheka “😂😂😂 totoo bwana we jua tu sehemu, unanukia vizuri, mpaka uso wangu wote unanukia sehemu, hapa nawaza kukuvuta tu.”
Nikacheka nikisema “nakupenda sana baby, unanichekesha sana, huna akili kabisa.”
Akacheka, kisha aliniambia “Mke wangu, nimechoka sana. Naomba ruhusa yako nipumzike.”
Nikamwambia kwa upole nikiwa nimesindikiza na ujumbe mzuri sana “Have a restful night Stewart wangu, dream of us honey pot❣️ sending hugs, cuddles, love and kisses to warm up your night.. I love you more each day than the previous day, I love you too much, I pray for you.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 162
Kila kitu kitakuwa sawa. Ndeana anakupenda Stewart, sana sana yaani sana. Anakupenda mno. Nakupenda sana Stewart wangu❣️. Be happy and strong kwaajili yangu. Una mimi usisahau hilo?”
Nilishika simu yangu nikisubiri jibu la Stewart. Na kweli alinijibu haraka sana. Nakumbuka aliniandikia maneno haya “My sweet Person❣️.. go to sleep knowing that there is a man far .. thinking of you so dearly and tender.. looking forward seeing you so soon... Thanks for your prayers, Najua upo na mimi na Nakupenda sana❣️ (Mtamu wangu, lala ukijua kuwa kuna mwanaume mbali na wewe, anakuwaza sana na anatarajia kukuona hivi karibuni. Nashukuru kwa maombi yako. Najua upo na mimi na Nakupenda sana❣️)
Nilisoma na kutabasamu nikajikuta najibu tena “I can't wait for you to come back and cuddle with me as I go to sleep honey...May your dreams be as soft as your kisses.. Mwaaaah!!❣️❣️, mwaaah!! ❣️❣️❣️.”
Alitabasamu na kunijibu “😋😋, i don’t regret knowing you Ndeana. Sijuti kabisa. Usiku mwema bega langu la kuegemea. Nakupenda, Kesho nitakupa majibu kuwa na amani. Nitashinda.”
Sikujibu hii, nilibaki tu nasema “umeshinda kipenzi, umeshinda.”
Kwa maneno ya baba na dada yangu, hata nilianza kutafuta biblia ilipo nipate neno la faraja. Basi nikatafuta nikaipata kabati la sebuleni. Nikaingia nayo chumbani. Sijui hata kufungua biblia.
Nikafumba macho na kufumbua nikakutana na neno hili “Msiwe na wasiwasi juu ya kitu chochote, ila kwa kila hali, mwombeni Mungu katika sala juu ya mahitaji yenu, kwa shukrani. Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.”
Niliyatafakari sana haya maneno, nikajikuta namuombea heri tu mambo yawe safi.
Siku iliyofuata asubuhi ya kwanza naamka bila ujumbe wa mpenzi wangu. Hii ilinisumbua sana. Nilituma ujumbe lakini hakujibu. Nilipiga namba haikupatikana.
Nilihangaika sana, nilihangaika siku nzima bila mafanikio. Hata dada yangu aliona hilo. Aliniambia “ mdogo wangu tulia, huwezi kujua anapitia nini. Atakuambia kila kitu. Mpe muda wa kuwa mwenyewe.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 163
Nilisema kwa upole “lakini dada, mimi ndiyo mpenzi wake, angeniambia ili nijue namna ya kumfanya afurahi.”
Dada alisema “mdogo wangu wanaume wana namna yao ya kupunguza maumivu. Nakuomba sana uwe mtulivu. Nakuomba mdogo wangu.”
Niliitikia tu na kubaki chumbani. Nalala wala sipati usingizi, nageukia upande huu na huu. Mpaka usiku kimya. Nyie usiombe Mpenzi wako unampenda halafu humpati siku nzima. Moyo unahangaika sana. Moyo unateseka raha unakosa.
Watu wanaosemaga siwezi kula sio waongo. Unakiona chakula hiki hapa hata ukila husikii utamu. ipo namna unajisikia yaani hata huelewi kwanini. Mungu pekee anajua nilifika vipi asubuhi, Mungu anajua ila ilikuwa ni siku ya mahangaiko mno.
Nilisalimiana na dada na nilimwambia naenda kazini. Nilifika kazini, kama utani, kama masihara. Niliwakuta wenzangu wapo kwenye chumba kidogo cha mikutano. Na baada ya muda mkutano ulianza na rasmi, rasmi kwa maumivu makali tulitambulishwa boss mpya kiumri ni sawa tu na mpenzi wangu. Nilijikuta nafumba macho yangu, machozi yalinidondoka. Na sasa naelewa kwanini Stewart hajanitafuta. Ameshindwa yaani, ana maumivu sana.
Ninatamani ungeona wafanyakazi wanavyotazama nilipokaa, wenye kunicheka wananicheka. Joan ndiyo alinishika mkono wangu. Sikufumbua macho mpaka bosi mpya kajitambulisha na kuondoka. Meneja aliruhusu watu watawanyike na yeye alitoka. Ndugu zangu, natamani mngeona nilivyochekwa kwa dharau. Tena nikisikia wakisema “alijiona yeye ndiyo yeye. Yana muda basi, hana lolote, kaishiwa kafulia. Na sasa tupo sawasawa. Boss Boss, tena saafi kabisa aende akafie mbele. Alikuwa anajisikia sana yule kaka. Alikuwa anajisikia mno. Halafu wanacheka.”
Ndeana mimi nimeinamisha kichwa tu, tena wanakuja wananiambia “pole shoga, karibu kudanga wala sio dhambi. Kila siku uwe wewe tu. Haya Mrs Boss karibu. Utaona na sasa akipiga magoti bila pesa kama utasikia raha.”. Wanaongea hivyo Kisha wanacheka na kugonga.
Nilijikuta siwezi kuvumilia, nilijikuta siwezi kabisa, nilijikuta ninaumia sana. Nilienda nyuma ya lile jengo. Nilichuchumaa na kulia kwa uchungu nikisema “Stewart wangu, Stewart naomba nipigie mpenzi wangu. Nakuomba.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 164
Nililia na Joan alinifuata kunimbeleza akinikumbatia huku akisema “Pole rafiki yangu. Usikate tamaa. Stewart umembadilisha. Anakupenda sana na yule ni mpambanaji atapambana tu kwaajili yako.”
Nilikumbatia huku moyoni nikiwa nimejua kuwa kumbe sio wote wanacheka na wewe wanakupenda na kukuombea heri. Wengine wanasubiri anguko lako moja tu, moja tu wakucheke. Nitafanya nini mimi, kazi naiona chungu.
Joan aliniambia, “rafiki yangu, mpigie tena. Mpigie.”
Nikafuta machozi haraka haraka na kutoa simu kwenye mfuko wa Skirt yangu niliyokuwa nimevaa. Nilitoa simu nikapiga. Simu iliita , nikawa nasema kwa uchungu “pokea simu kipenzi nakuomba.”Nilisema kwa kurudia rudia.
Kisha nikasikia sauti ya uchungu sana, uchungu mkubwa sana. Alikuwa analia, aliniita kwa jina langu “Ndeana, Ndeana wangu, nimekwisha mimi. Wamechukua kila kitu changu. Nimepoteza kila kitu. Ndeana naanza upya mimi. Nitaishi vipi, nitaishi vipi sasa, nitakutunza vipi Ndeana, nimeisha!!, nimeisha!!, Moyo wangu Ndeana ni kama vile yai, moyo umepasuka. Naona aibu, siwezi hata kukutazama. Nitaishi vipi sasa, mali zangu zote Ndeana wangu, bila huruma.”
Hata Joan alianza kulia akinikumbatia na mimi nilikuwa nalia tu. Nililia nikisema “Stewart acha kulia, bado hujapoteza vyote, mimi nipo na wewe. Nakupenda bado. Nakupenda sana. Naomba usilie mpenzi. Nakupenda sana.”
Huku analia kwa uchungu alilia akisema “Ndeana Nakupenda.”
Nami nililia nikijibu “Stewart Nakupenda. Niambie upo wapi, nataka kukuona.”
Stewart alilia sana, alilia kwa uchungu akisema “nitapambana kwaajili yako, nitaanza tena kwaajili yako, nitaishi kwaajili yako, nakupenda Ndeana. Umenipa nguvu sana. Sitaacha kupambana. Naomba na wewe pambana. znitajitahidi nikutunze uwe na furaha. Ndeana nipo kwa rafiki yangu, nataka nikuone, nikukumbatie, utakuja mpenzi, naomba uje, nakuomba nakutaka wewe tu.”
Nilimjibu kwa machozi “Nitakuja baby wangu, usilie nyamaza kipenzi. Unajua kulia ni haramu?”
Alicheka akilia, Alinijibu “Ni haramu Ndeana, dini hairuhusu. Sitalia tena ila nataka nikukumbatie peke yako, kwa nguvu kama vile sijawahi kukumbatia.”
🙆🙆watabiri tumebaki tunashanga.......
Offeeeeeer maliza season four na five kwa offer ya sh 1000
Kumbuka, Season four ndio ya mwisho kupostiwa hapa Facebook, season Five itapatikana kwa 1000 whatsapp Tu
Njoo leo whatsapp umalizie yote kwa sh 1000
Na namba ya WhatsApp 0743433005.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞: 154