TAMU YA HOUSEGIRL
SEHEMU YA 02
"Dada shikamoo" Mwaneke alimsalimia bosi wake huyo badala ya kujibu swali aliloulizwa
"Shikamoo inaniongezea nini mimi Mwane, nataka jibu la swali langu na siyo unanitazama kama ndumi la kuwili hapa?"
"Mimi kaka aliniita tu kunipa maagizo wala sikumwambia kitu chochote, mbona hakuna tulichoongea mimi na yeye dada?"
"Una uhakika?"
"Ndiyo dada"
"Mwane, ujitazame, humu ndani umeingia kwa huruma tu, wadada wenzio hawakaagi humu siku mbili tu wanaondoka kwa sababu huwa sipendagi ujinga na sijuagi kucheka cheka na mjinga hata siku moja"
"Nakuelewa dada"
"Potea, kuna nguo zinakusubiri na kazi zote humu ndani zifanyike sasa hivi, mimi naenda zangu saluni saa hizi"
"Sawa dada" Mwaneke alimuitikia bosi wake huyo akimpita huku akisonywa, Yunisi akarudi chumbani kwake taratibu huku Mwaneke akielekea chumbani kwake na alipofika alikutana na simu yake ndogo 'kiswaswadu' ikiita kitandani akaichukua na kutazama namba ni ya Benson, baba mwenye nyumba, mke wa Yunisi, kabla hajaipokea akaweka koo lake vizuri kwanza akirekebisha sauti kisha akaipokea na kuweka sikioni bila kuzungumza chochote
"Mwane"
"Abee kaka?" aliongea kwa sauti ya kubana, ya kudeka
"Vipi salama, upo nyumbani?"
"Nipo nyumbani kaka"
"Oooh huyo mwanamke yupo?"
"Mwanamke gani kaka?"
"Mke wangu"
"Yupo ila atatoka anataka kwenda saluni nadhani, kwani namba yangu umeipata wapi kaka mbona sijawahi kukupa?"
"Kwani vibaya mimi kuwa na namba yako Mwane?"
"Hamna nimeuliza tu siyo kwa ubaya"
"Nimeipata kwa huyo mwanamke nimeichukua kwenye simu yake"
"Oooh sawa"
"Sasa na wewe mbona namba yangu umeniitikia tu haraka haraka ikionekana kabisa umeisevu, umeipata wapi, kwani nilikupa namba yangu?"
"Aaaamh hamna mimi nimee...nimee.." Mwaneke alishindwa kujibu akijiuma uma maneno tu, akitafuta cha kusema
"Oky tuyaache hao, atarudi saa ngapi huyo aliyeenda saluni?"
"Mh sijajua saa ngapi ila akiendaga saluni mfano saa hizi asubuhi basi kurudi ni saa kumi na mbili jioni au saa moja moja hivi, harudigi mapema kivile"
"Sawa asante" Benson alijibu na kukata simu
"Mh mbona maswali mengi leo huyu mwanaume kulikoni?" Mwaneke aliguna huku akiitazama simu,
"Wewe mjinga mjinga" alikaripiwa akashtuka kutazama mlangoni alimwona Yunisi mke wa Benson akiwa amesimama anamtazama
"Abee dada?"
"Yaani nimekwambia ufanye kazi wewe unaongea na simu na mabebi zako?"
"Hamna ni kaka yangu tu huyu"
"Na hiyo simu ipo siku yake nitaitupa chooni, nguo zinakusubiri nje, haraka sana"
"Sawa dada" Mwaneke alijibu kwa hofu na kutoka haraka haraka akimpita bosi wake huyo mlangoni huku akisonywa, alipotoka nje akakutana na mlima mkubwa wa nguo za mwanamke huyo na mumewe, zikimsubiri, akatoa macho kwa mshangao, zilikuwa nyingi, za kawaida mpaka za ndani...
Benson baada ya kukata simu ya Mwaneke akatabasamu na kuirudisha mezani
"Mbona unafurahi mwenyewe Ben umepata mchepuko nini?" mfanyakazi mwenzake aitwae Kassim alimwuliza
"Hamna, dada wa kazi tu"
"Ndo kakuambiaje tena mpaka ufurahi, umemuelewa nini?"
"Hamna, ila naenda nyumbani saa hizi kuna dharura kidogo"
"Dharura wapi wakati nimekusikia unaongea na simu sijui mkeo anatoka nyumbani hayupo, naona kabaki housegirl peke yake mzee unaenda kujilia vyako"
"Hamna siyo kweli"
"Siyo kweli wapi, wewe nenda kale bwana, kapige vyako, mke akijisahau wewe kung'uta dada wa kazi usirembe bob, ningekuwa mimi nishamla zamani sana, anaonekana kakuelewa huyo" Kassim aliongea kwa msisitizo akimwacha mwenzake huyo anajikuna kichwa akiwa anatafakari cha kufanya
"Sijawahi kuchepuka na kuwaza ujinga kama huu lakini safari hii itabidi tu" aliongea akifunga laptop yake na kuinuka akichukua ufunguo wa gari, safari tayari kuelekea nyumbani....