Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

TAMU YA HOUSEGIRL SEHEMU YA 01

15th Jun, 2025 Views 183

TAMU YA HOUSEGIRL

SEHEMU YA 01

ONYO???


Stori hii ina Maudhui ya Kimapenz** na ya buza kwa Mpalange'

****

Mwanadada au mwanamama Yunisi kulipokucha mapema asubuhi alikuwa bado amelala kitandani licha ya mumewe kuamka kwa ajili ya kujiandaa kwenda kazini, mwanamke huyo kama kawaida yake yeye ni kulala mpaka ahakikishe ameumaliza usingizi wote ndipo aamke, haijalishi iwe saa mbili asubuhi, saa nne au hata saa sita, mumewe Benson alimaliza kuvaa suti yake ya kazini na kumsogelea mkewe kitandani ambae ndiyo kwanza alikuwa anajigeuza kitandani akiendelea kuuchapa usingizi

"Naenda kazini, tutaonana baadae"
"Sawa kazi njema" mkewe alimjibu huku akijinyoosha kitandani, mumewe akatikisa kichwa kujisikitikia mwenyewe kwa jinsi ambavyo mwanamke huyo asivyojali kuhusu maandalizi yake ya kwenda kazini, akabeba begi lake la ofisini na kuanza kutoka taratibu kuelekea nje kwenye maegesho (parking) ili aingie kwenye gari lake na ndipo aliposikia geti dogo likigongwa na mlinzi akiwa amekaa kwenye kiti chake anauchapa usingizi

"Mboya!" alimwita kwa ukali, mlinzi huyo akakurupuka kwenye kiti hicho chenye mguu mmoja ambacho alikitegesha tu, akajikuta anaanguka nacho mzima mzima chali baada ya kukurupuka

"Naam bosi" aliinuka haraka haraka huku akikiokota kiti hicho na kukiweka vizuri kisha akamkimbilia bosi wake huyo badala ya kwenda getini ambapo kulikuwa kunagongwa geti

"Sasa unanifuata mimi tena badala ya kulifuata geti linalogongwa, wewe vipi?"
"Oooh samahani bosi" mlinzi alijibu na kugeuka mbio mbio kurudi getini

"Hapa nina mlinzi kweli au nina mtu tu ninayemsaidia maisha na jinsi ya kuishi?" Benson alitikisa kichwa kwa masikitiko akiwa amesimama pembeni mwa gari lake dogo, kisha akaufungua mlango ili aingie

"Kaka!" aliitwa akageuka na kukutana na dada wa kazi (housegirl) aitwae Mwaneke

"Unasemaje Mwane?"
"Tai yako haijakaa vizuri kaka ndo nilikuwa nakuja kukukumbusha tu"
"Oooh sawa asante" Benson, alijibu na kuifunga vizuri tai yake hiyo shingoni kisha akamtazama Mwaneke, msichana mweusi wa rangi na mwenye upara kichwani, mnene kiasi ambae kanyimwa sura tu ila nyuma mashalaah amebebelea kifurushi

"Kazi njema" alimpungia mkono mwanaume huyo aliyetabasamu tu na kuliondoa gari taratibu huku Mwaneke akilitazama kwa kulisindikiza kwa macho, akiwa amevalia gauni refu na pana la mtumba lililofika mpaka chini miguuni, likiziba hata kifurushi chake nyuma alichojazia kisionekane na yote ikiwa ni amri ya mama mwenye nyumba, Yunisi, gari la Benson lilipita getini kukiwa kumefunguliwa na mlinzi tayari, Mwaneke akibaki anatabasamu tu

"Yule alikuwa anaongea nini na mume wangu?" Yunisi alijiuliza huku akiwa amesimama dirishani chumbani kwake anachungulia kinachoendelea nje, Mwaneke aligeuka taratibu kurejea ndani kwenye nyumba kubwa

"Mwaneke, Mwane" aliitwa na mlinzi akasimama na kugeuka kumtazama, mlinzi huyo akimfuata huku akicheka cheka

"Sema shida yako"
"Sasa vipi lile ombi langu nilililokwambia Mwane eeh?"
"Ombi gani?"
"Aah Mwane unajifanya umesahau, twende basi tukaongelee chumbani kwangu"
"Nani aende kwenye chumba chako, tuongelee hapa hapa, nikumbushe"
"Aaah Mwane usinifanyie hivyo, ni kweli hukumbuki au unanifanyia makusudi tu?"
"Naona unazunguka zunguka sana, nina kazi ndani" alitaka kuondoka, mlinzi huyo akamshika mkono kumzuia
"Sikia, basi tufanye yameisha, mimi nakupenda na nilishakwambia mbona?"
"Siwezi kuwa na wewe, siyo hadhi yangu, nilishakujibu mbona?"
"Mimi siyo hadhi yako, we unachekesha kweli, una hadhi gani ya maana zaidi ya uhousigeli humu ndani?"
"Bora mimi housegirl nalala ndani kuliko wewe mlinzi unalala nje"
"Kwenda huko sura yenyewe huna, kichwani upara kama dume"
"Nipishe, mbona umenitongoza, hukuiona hii sura nyooo?" Mwaneke alimsonya akiondoka kuelekea ndani kwenye nyumba kubwa akimuacha mlinzi anaendelea kumtolea maneno ya kashfa, alipopandisha ngazi kuingia ndani akakutana uso kwa uso na Yunisi, mama mwenye nyumba

"Ulikuwa unamwambia nini mume wangu kwenye gari?" aliulizwa na bosi wake huyo aliyejishika mikono kiunoni akisubiri jibu...

#Comment
#Like.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

TAMU YA HOUSEGIRL SEHEMU YA 01 https://gonga94.com/semajambo/tamu-ya-housegirl-sehemu-ya-01 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu ya 10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu ya 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA sehemu ya 37

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA sehemu ya 36

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

Obi's Pain Chapter 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 02.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DEAR DOCTOR 01

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MPANGAJI ... 01

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 15

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 01

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

Obi's Pain Chapter 1

mjukuu rewards 100 Comments 1
 

MSHANGAZI EPISODE 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MSHANGAZI EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

YAMENIKUTA

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 9

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINSI YA KUTUNZA UKE

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

PART 5 MY HEART

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest