Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

CAPTAIN MAVERICK NA MISSION YA MAPENZI😍 SEHEMU : 15

22nd Aug, 2025 Views 62



"Umekuja kufanya nini chumbani kwangu ?"

" Nataka kuongea na wewe nataka kukuomba msamaha mke wangu "

" Tristan sikutaki nenda kaendelee na maisha yako siwezi kurudiana na wewe Kuna vikwazo vingi mbele yetu toka nje " Gabriella alifungua mlango ili Tristan aondoka

" Vikwazo vipi kama huyo mtoto uliyembeba tumboni mwako au Kuna kingine "
Gabriella alishtuka sana alifunga mlango haraka

" Umejuaje kama mimi ni mjamzito ?"

" Hilo halina umuhimu nataka tu kukwambia nitalea huyo mtoto kama mtoto wangu na umsahau baba wa huyo mtoto "
aliongea Tristan bila aibu

" Naona umechanganyikiwa Tristan bado tu kubeba makopo Yani hicho ndo kilichobaki "

" Gabriella namaanisha ninachokisema na hakuna mtu yoyote atakayejua kuwa mtoto sio wa kwangu najutia sana kukupoteza mama angu "
Tristan alipiga magoti

"Tristan Hilo haliwezekani nyanyuka tu uondoke unapoteza muda wako Bure Gabriella wasasa sio kama yule wa zamani Gabriella wa Sasa anampenda sana mwanaume mwingine na nimembeba mtoto wetu kama ishra ya upendo wetu , ondoka tu Tristan "

" Sitokata tamaa Gabriella nitapambana hadi mwisho ili nikurudishe kwangu " Tristan aliondoka kwa hasira Gabriella alifunga mlango akaanza kulia

" Uko wapi maverick wewe mwanaume mbona unanitesa hivi " Kwa upande wa kambi ya Ndundu askali waliokuwa kwenye mafunzo walirudi kambini wakiongozana na captain maverick

" Naona unatabasamu tu niambie huyo mwanamke unampenda sana ee ?"
Captain Raymond alimuuliza maverick

" Umejuaje kama ni mwanamke anayenifanya nitabasamu hivi ?"

"Sio hapo tu najua hadi jina lake Gabriella si ndio"
aliongea Raymond huku anatabasamu

" Hahaha umejuaje wewe boya"

" Kila siku ulikuwa unaweweseka ukitaka jina lake Fanya haraka usije ukatufia hapa " Maverick alitabasamu akaondoka alienda moja kwa moja nyumbani kwake alikuta nyumba imefungwa nafunguo ipo kwa jirani

" Gabriella nisameheni najua nilikukwaza sana kuondoka bila kukuaga " maverick alijiongelea mwenyewe Simu ya maverick ilimshtua kutoka kwenye mawazo yake alikuwa ni baba yaler flanklin

" Baba .."
aliita maverick

" Nimepata taalifa toka kwa general kuwa umerudi "

" Ndiyo nimerudi baba "
" Leo usiku kutakuwa Kuna sherehe nyumbani kwa baba yako mkubwa hutakiwi kukosa ni sherehe ya uzinduzi wa kampuni yake mpya " alisema Mr flanklin

" Sawa baba nitafika kwenye sherehe bila kukosa "
maverick alikata simu

Kwa upande wa nyumbani kwa Mr Alphonse , Gabriella alijifungia chumbani kwake

" Wewe Gabriella nataka ufungue huo mlango Leo jioni utaenda kwenye sherehe utake usitake " bi Carina aligonga mlango kwa nguvu

" Usimlazimishe unatakuwa kuongea nae taratibu "
alisema Mr Alphonse

" Gabriella binti yangu mimi kama baba yako nakuomba Leo jioni twende kwenye sherehe kwa heshima yangu tafadhali "
mr Alphonse alimuomba Gabriella

" Sawa Dady nitaenda kwaajili yako "
Jioni ilifika nyumbani kwa Mr Edward kulikuwa kumepambwa vizuri na lilikuwa ni jumba la kifahari wageni waalikwa walikuwa wengi sana

Gabriella hakufurahia kabisa kuwa pale aliamua kwenda kukaa nje hakutaka kusumbuliwa na Tristan Alishtukia amekumbatiwa kwa nyuma alishtuka sana mwanzo alidhani ni Tristan

" Tristan naomba uniache Sina mood ya kuzozana na w..." Gabriella hakumalizia sentence yake alibaki amezubaa..

" Maverick .."
aliita Gabriella huku machozi yanamtoka alimuhisi maverick hata bila kugeuka na kuiona sura yake Gabriella aligeuka akamkumbatia maverick kwa nguvu alianza kulia

"Usilie mrembo wangu Niko hapa Sasa nisamehe niliondoka bila kukuaga "
maverick alimbembeleza Gabriella , Gabriella alijitoa kifuani kwa maverick

" Unadhani nitakusamehe sikupendi nakuchukia "
Gabriella alitaka kuondoka maverick alimvuta akamkumbatia

" Nisamehe Gabriella nakupenda sana nitakuelezea kila kitu hata ambavyo hukuwahi kuhisi vinaweza kutokea "
Gabriella alimuangalia maverick usoni

" Kama vipi ?"
Maverick alitaka kumuelezea Gabriella lakini Kuna mtu alimuita kwa mbali

" Maverick umekuja kwenye sherehe na hutaki kumsalimia baba yako mkubwa " aliyesema hivyo hakuwa mwingine alikuwa ni Mr Edward
Mr Edward hakuwa amemuona Gabriella

" Nakuja uncle "
alijibu maverick Gabriella alisukuma mikono ya maverick akaondoka Maverick alitaka kumfuata ila aliona aende akaongee na Mr Edward kwanza

" Gabriella unaota utakuwa unaota Yani imekuwaje maverick anamuita Mr Edward uncle "
Gabriella aliendesha gari huku anaongea mwenyewe kama mtu aliyechanganyikiwa

Maverick aliingia ndani alikutana na Mr Edward akiwa na Tristan

" Hongera sana uncle hii ni hatua kubwa sana uliuyopiga "
alisema maverick , Tristan alimuangalia maverick kwa jicho Kali alikumbuka alimuona akiwa na Gabriella kwenye sherehe ya Jonas lakini hakujua kama ni ndugu yake ila
kwa upande wa maverick yeye alimfahamu Tristan kama ndugu yake

" Asante sana ,ngoja niwatambulishe naona mtakuwa hamkumbukani ni muda mrefu sana umepita hasahasa Tristan kwasababu hakuwepo Tanzania kwa muda mrefu ,maverick huyu ni mtoto wangu Tristan kama unamkumbuka , Tristan huyu ni maverick mtoto wa baba yako mdogo flanklin "

" What ? Dad hiki ni nini huyu mwanaharamu anawezaje kuwa ndugu yangu "
Tristan alipaniki alitaka kumvaa maverick alikuja Mr flanklin

" Kwani Kuna shida gani mbona kama mnagombana?
" Aliuliza Mr flanklin

" Mimi sijui chochote baba labda mumuulize yeye ?"
Maverick aliongea huku anamuangalia Tristan kwa hasira

" Unasemaje wewe eti hujui kwanini nipo hivi ,unajua vizuri sana ulichokifanya na kamwe sitokusamehe "
Tristan aliondoka

" Huyu kijana ana mawenge sana siku hizi ngoja niongee nae " Mr Edward alitaka kumfuata Tristan,maverick akamzuia

" Uncle acha mimi nikaongee nae " maverick alimfuata Tristan

" Simama hapo wewe boya "
maverick alienda kumzuia Tristan asipande kwenye gari lake..
" Unataka nini ? Pisha nipite "

" Hasira zako haziwezi kusaidia kitu Tristan ukweli utabaki pale pale ulimuacha Gabriella kipindi alipokuwa anakuhitaji sana na ulikuwa na mwanamke mwingine unajua ni Kiasi gani ulimuumiza ?,Sasa nakwambia hivi Kaa mbali na Gabriella sitaki kumuona anahuzuni tena kwasababu yako " alisema maverick

" Nini ? Unakisikia unachokiongea maverick,wewe ndo unatakiwa kukaa mbali na Gabriella kwasababu ni mke wa ndugu yako "

" Umesahau kwamba ulipoteza hiyo haki ya kuwa mume kwake? ,sitaki kuongea sana Tristan nakuonya tena hii ni mara ya mwisho Kaa mbali na Gabriella la sivyo nitasahau kama wewe ni ndugu yangu, "
maverick alipanda kwenye gari akaondoka....... Itaendelea

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

CAPTAIN MAVERICK NA MISSION YA MAPENZI😍 SEHEMU : 15  >>> https://gonga94.com/semajambo/captain-maverick-na-mission-ya-mapenzi-sehemu-15

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest