CAPTAIN MAVERICK NA MISSION YA MAPENZI ๐๐ SEHEMU : 6
" Bro muache huyo demu aishi hapo kwa huo mwezi mmoja najua hupendi ku share nyumba na watu wengine lakini mvumilie kidogo anamatatizo nyumbani kwao "
" Hizo ni shida zake sio zangu "
aliongea maverick huku anamuangalia Gabriella , Gabriella aliweka sura ya huruma
"afu kumbuka ni mtoto wa kike huyo hapo kwako Nina uhakika atakuwa salama kuliko akienda kwingine ni mwezi mmoja tu kaka "
bakari alijaribu kuendelea kumshawishi maverick
Maverick alimuangalia Gabriella ni kama aliingiwa na roho ya huruma
" Poa nitamuacha aishi hapa ila ni kwa mwezi mmoja tu na sio zaidi " maverick alikata simu
" Jina lako ?"
Aliuliza maverick
" Jina langu ni Gabriella " alijibu Gabriella kwa adabu
" nitakuacha uishi hapa lakini sitaki karaha zako ,sipendi uchafu na ukiwa nyumbani sitaki ulete mwanaume wako hapa ,ukinunua mwanaume nenda hotelini malizana nae huko huko tumeelewana Gabzilla"
" Ndiyo tumeelewana.. ,what umeniutaje ?"
Gabriella alimuuliza maverick
Maverick hakumsikiliza Gabriella aliingia chumbani kwake
" Jina langu zuri Gabriella , cute Gabby , Gabby babe , Geebee yeye anaanzaje kuniita Gabzilla sijui hata Ina maana gani itakuwa tu Ina maana mbaya " Gabriella aliburuza begi lake akaiingiza chumbani Mchana Gabriella akiwa chumbani kwake alianza kuhisi njaa alielekea jikoni alifungua hotpot alipakua chakula na kuanza kula
" Mmmh mkaka anapika chakula kitamu kama Cha hotelini "
Gabriella alijikuta anakula tu aliongeza na kuongeza tena mpaka chakula kiliisha chote
Maverick alirudi kutoka matembezini aliingia bafuni alioga na baada ya hapo alitenga mahotport mezani Alifungua Cha ajabu alikuta hotpot limejazwa maji na hakuna chakula
" Huyu binti anataka kuvuka mipaka yake sasa "
maverick alimfuata Gabriella chumbani aliingia bila kugonga mlango
" Vipi wewe unaingia bila hodi ungenikuta Sina nguo je "
Gabriella aliongea huku amekunja sura
" Binti nimekubali uishi humu ndani kwa huruma zangu tu na Sasa naona unataka kuupima uvumilivu wangu kama unataka kula pika wewe si mwanamke katika vitu sipendi ni mtu kula msosi wangu Leo iwe mwisho ....na kingine Hata nikukute kama ulivyozaliwa siwezi kukutamini hauna kipya " maverick aliondoka
" Uchoyo tu lione afu anadharau mbwa huyu wenzie wananililia yeye anajifanya kauzu enzi zangu chuoni nimewatesa sana wenzio nyau wewe " Gabriella aliendelea kuangalia vedio za tick tock Usiku Gabriella akiwa anaperuzi mtandaoni alikutana na picha aliyo post Tristan akiwa na Silvia alijikuta anaumia sana
" Utalipia hili Tristan nilikupenda kweli lakini wewe uliamua kuniumiza lazima siku moja na wewe uje utoe machozi kama sio mimi nitakaye kuuliza basi utalizwa na uliyempenda na hato Iona thamani yako "
Gabriella alifuta machozi alizima data akaweka simu pembeni akaiwasha redio sauti mpaka mwisho alianza kuimba na kucheza Maverick alikuwa akijaza report zake kwenye laptop yake alikunja sura baada ya kusikia mziki uliotokea chumbani kwa Gabriella
" Gabzilla zima huo mziki "
aliongea maverick kwa sauti lakini Gabriella hakusikia aliendelea kuimba na kucheza
" Huyu mwanamke ni kichaa kama isingekuwa huruma zangu ningemtinua usiku huu huu "
maverick alienda kufungua mlango wa chumba Cha Gabriella alienda moja kwa moja kuzima redio
" Ahhhhh nani kazima tena Yani palikiwa panaenda kukolea " Gabriella aligeuka akakutana USO kwa USO na maverick
" Sitaki kelele nyumbani kwangu unataka mziki nenda club hii ni mara ya mwisho Gabzilla sitoongea tena " maverick aliondoka
" Huyu nae ana boa , hii ni mara ya mwisho sitoongea tena " Gabriella alimuiga maverick anavyoongea kwa sauti yake ya besi
Kesho yake asubuhi Gabriella alienda kupika chai yake alikaanga na mayai alitenga mezani alikula na baada ya hapo vyombo aliweka kwenye sinki bila kuosha
"Gabzilla vile vyombo ulivyotumia umemuachia nani aje akuoshee ?"
Maverick alimuuliza Gabriella
" Kwani hauna mfanyakazi mimi siwezi kuosha vyombo kwanza sijawahi kuosha vyombo kwenye maisha yangu " Gabriella aliongea huku anaangalia kucha zake zilizopambwa vizuri
" Hii ni nyumba yangu na Sheria zangu hakuna Cha mfanyakazi Wala nini ukitumia jiko kupika sharti uoshe vyomba baada ya kutumia na usafishe jiko ,kile ni nini ulichokifanya jikoni chai tu na mayai umechafua jiko zima na vyombo nusu ya kabati nataka nikitoka kuoga nikute jiko safi "
maverick alielekea chumbani kwake
" Watu wengine wana shida gani jamini mimi Gabriella mimi nikaoshe vyombo kweli Tristan hakuwa ananifanyia hivi nilikuwa na wafanyakazi kila Kona na nyumbani kwetu pia Kuna wafanyakazi hapa nimekuja kuteseka tu " Gabriella alilalamika alitamani asifanye lakini akikumbuka Hana pesa na account zake zimefungiwa aliishiwa pozi
Zilipita dakika kumi maverick alitoka chumbani alielekea jikoni alibaki mdomo wazi Gabriella alikuwa amevunja sahani na vikombe
" Una Fanya upuuzi gani ?"
Aliuliza maverick kwa kufoka
" Mimi si nilikwambia mimi siwezi kufanya kazi vyombo vyako vyenyewe vinatereza kama nini "
aliongea Gabriella huku analia Maverick alimuonea huruma
" Sio kosa lako ni kosa la waliokulea , likizo yangu imekuwa mbaya sana " alijiongelea maverick
"Ondoka nitafanya mwenyewe "
maverick alichukua fagio na kuanza kusafisha Gabriella aliondoka huku anatabasamu
Maverick alianza kuandaa chakula cha mchana Gabriella alienda
" Naweza kusaidia chochote ?"
Aliuliza Gabriella
" Kata vitunguu " maverick alimsogezea Gabriella chopping board na vitunguu majiGabriella alianza kukata vitunguu hakuwa anajua kukata alikata vipande vikubwa kitunguu kimoja alikata mara nne tu tena alikata huku amefumba macho
" Achaa acha sogea pembeni nitaandaa mwenyewe "
maverick alikata vitunguu vizuri Gabriella alimuangalia akamzomea
" Ingekuwa sio hii njaa hata usingeiona hii sura yangu zuri huku jikoni kwako "
alijiongelea Gabriella Baada ya kula ilibaki kazi kwa Gabriella
" Gabzilla natoka kidogo safisha hivyo vyombo pamoja na jiko ,sitaki kukuta umevunja chombo chochote " maverick aliongea kwa msisitizo
" Sawa nitafanya lakini usiongee na mimi kama unanipa amri za kijeshi " aliongea Gabriella Maverick alimuangalia akaondoka bila kusema chochote
" Mijitu mingine bhana ndo aninyanyase kisa hicho chakula chake ana bahati Sina pesa hata nisinge hangaika nae ningekuka zangu hotelini "
Gabriella aliondoka mezani hakutoa hata kijiko alienda kujilaza kwenye kochi alipeluzi mtandaoni
" Wow hili gauni ni zuri sana tena lio hapa hapa mjini ngoja niulize bei" Gabriella aliuliza alitajiwa laki tatu na nusu
" Usiliuze hili gauni kesho nakuja kulinunua " Gabriella aliingia makubaliano na muuzaji
" Oh mungu wangu kumbe Sina hata mia kwenye pochi yangu ..Sasa nitafanya nini na hili gauni nimelipenda sana na nimemuahidi nitaenda jamani "
Gabriella alikuna kichwa Kuna wazo lilimjia
:" yes ngoja nitapata tu hiyo pesa tena kirahisi sana "
Gabriella alienda kutoa vyombo mezani siku hiyo alijitahidi kuosha vyombo kwa uangalifu na kuvipamga vizuri alitumia masaa mawili kuosha vyombo na kusafisha jiko
" Kiuno changu ....mgongoo" Gabriella alilalamika alienda kujilaza kwenye kochi alipitiwa na usingizi bila kutarajia kutokana na kuchoka....
FULL 1000
whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi






Maoni