*CHAGUO SAHIHI* SEHEMU YA....10
Na
Mamuh Mohd
(0716730000)
Tulipoishia........
Manga alifunika kombe mwanaharamu apite basi akatoka nnje kuendelea na shuhuli....
SONGA NAYO.......
Nafsa alimaliza kujiandaa akatoka nnje tayari kwa part kuendelea.
Alikata kila pale na watu wakala na kunywa vizuri sana.
Zawadi alipewa za kutosha na kufikia jioni party ikawa imeisha.
Nafsa aliwashukuru marafiki zake waliokuja pale haswa michael"
"Michael sikujua kumbe utakuwa huku umeshatoka shule?"
"Yah nipo tokea wiki iliyopita"
"Asante sana kwa kuja na pia asante kwa zawadi yako"
"Usijali kuna ujumbe nimekuwekea katika zawadi niliyokupa plzzz uzingatie".
"Sawa asante".
Nafsa kusikia vile si akadhania labda michal kamuambia anampenda.
Binti haraka akakimbia chumbani kwake Ambapo zawadi zake zote ziliwekwa huko.
Akaitafuta zawadi ile aliyopewa na michal kwa nnje kwenye bahasha iliandikwa,
"Muheshimu mama yako Nafsa.
Sio vizuri ulivyomfanyia mbele za watu imeniuma sana sana muombe msamaha".
Nafsa alishangaa lakini alichukia sana.
********
Usiku huo manga alikuwa chumbani ndipo alifika chumbani humo mwanae yule wa kuitwa Nayla.
"Mama onja juice hii nimeitengeneza.....nimemuelekeza dada huyu mgeni wa jikoni kuchanganya matunda kama unavyofanyaga yeye akasaga".
"Mhhh ni tamu sana inamaana kumbe huwa unaniangaliaga navyochanganya matunda?"
"Ndio mama...ngoja nimpelekee na dada Nafsa".
"Haya fanya ivyo mwanangu sawa eeeh".
Nayla aliondoka zake, ni kabinti kadogo lakini kama upendo wa hali ya juu.
Nayla alifika chumbani kwa dada yake akamkuta na hasira zake za ule ujumbe wa michael weeee alimfukuza Nayla.
Wakati Nayla anatoka Joan alikuwa nae mlangoni anaingia chumbani kwa Nafsa.
"Anty kwema? Upo sawa binti yangu?"
"Kuna rafiki yangu eti kaniandikia ujumbe huu angalia".
Joan kutazama akauchana,
"Achana nao wetu kusema ni kawaida yao.
Mhhh vipi lakini umemsamehe mama yako?"
"Ahhh nadhani yameisha kwa sasa"
"Sawa lakini kuwa nae makini sana sana.
Hakikisha nafasi yako ya upendo kwa baba yako hakuna anaekupokonya sawa?"
"Hilo nalijua shangazi kuwa baba yangu ananipenda sana".
"Ongezea hapo na anty yako pia anakupenda sana".
"Sawa shangazi nadhani nahitaji kupumzika sasa"
"Sawa usiku mwema".
Waliagana na Joan akatoka zake.
********
Wiki moja ilipita, siku hiyo Manga alikuwa alimtumua nywele binti yake Nafsa wamekaa eneo la nnje.
"Mama ujue shuleni kule tulikuwa hatuendagi saloon kuosha nywele ndio maana unaona zipo ivi"
"Lakini si nilikufungia shampoo nzuri kuwa uwe unaosha nywele zako mwenyewe? Sema ulikuwa mvivu eeeh.
Ngoja nikuoshe leo kisha nikakukaushe".
"Sawa mama".
Basi wakati wanafanya hayo joan alikuwa akiwatazama kupitia Dirisha la jikoni.
"Mhhh haya ngoja tuone itakuwaje?".
Kisha haraka alikwenda mpaka katika chumba cha Kaka na wifi yake akachukua ile mashine ya kukaushia nywele akabadilisha na ya kwake.
Ya kwake alijua huwa inapiga shoti ivyo alijua Akiitumia Wifi yake huyo manga itampigia tu shoti wala hakujali nani atadhurika.
Sasa manga mwenyewe alikuwa hana hili wala lile na si mjuzi sana wa mambo hayo yeye alikalili zake akiwasha anaseti moto na kukausha nywele.
Basi alifanya hivyo ile anaanza kumkausha nywele Nafsa mala shoti ilipiga moto ukaja mkali bahati aliwahi kuidondosha mashine ile na kuzima katika swich.
Weweeh nafsa aliogopa,
"Mama nini hiki?"
"Hata sijui mwanangu mashine hii naona imepata shoti".
Mala aliingia Joan chumbani huko,
"Wifi kuna nini mbona umepiga kelele sana?"
"Ni shoti hii mashine sijui imekuwaje ilitaka kutuunguza".
"Mhhhh ungeazima ya kwangu si huwa unaazimaga hiyo ya kwako ni mbovu sasa leo ilikuwaje ulitaka kumfanyia kusudi Nafsa ama?"
"Wifi unaongea nini? Lini niliazima ya kwako na wewe ndo huwa unaazima ya kwangu".
"Wifi wacha uwongo huwa unaazimaga ya kwangu tokea Nafsa aende shule unatumiaga kumkaushia nywele mwanao Nayla sasa kwa Nafsa ulitaka imdhuru ama?".
Manga pozi lilimuisha Wifi yake Kaamua kuonesha ubaya wale live kwa kuongea uwongo.
Nafsa ndo alizidi kuunganisha matukio akamuamini shangazi yake.
"Kweli mama wa kambo haujawahi kuwa mama kwangu".
"Nafsa unaongea nini? Unawezaje kuzungumza maneno makubwa kiasi icho?"
"Ndio ukweli nilisamehe mwanzo lakini wewe ni mbaya kwangu unaumia kwa kuwa baba yangu ananipenda kuliko watoto wako Una roho mbaya mwanzo ilikuwa unajifanyisha tu".
Kisha Nafsa akaondoka chumbani huko jumba bovu likamuangukia tena manga.
Joan mtafuta sababu sasa weeeh hapohapo akampigia simu kaka yake.
"Kaka njoo haraka Nafsa amejifungia chumbani kwake anaweza akajifanyia hata vibaya amechukia sana".
Mr jarden kuambiwa ivyo alichanganyikiwa.
Ndani ya dakika 20 tu,alifika nyumbani na kumkuta Nafsa yupo chumbani kwake analia.
"Baba inamaana mama kwa sasa ndio ananichukia kiasi hiki? Yani anajua fika mashine yake inapiga shoti alafu anataka kuitumia kwangu? Kwanini yani Kwanini?".
"Plzzz relax sawa.... niachie mimi hili siwezi kuruhusu mtu yoyote yule alikoseshe raha mwanangu sawa?"
Mr Jaden basi alimfuata Manga ambaye alikuwa akatikisa kichwa tu kuonesha Hapana hajafanya jambo kama hilo.
"Nilikuoa sababu nilikuona unafaa kuwa mke, ulionesha mapenzi makubwa sana kwa binti yangu inamaana yote hayo ulikuwa unaniigizia?"
"Mmewangu naomba niamini sipo ivyo mimi siwezi ".
"Sasa basi nakupa talaka naona umeshindwa kuishi na binti yangu utaenda kukaa Sehemu nyingine na watoto wako.
Sitaki mwanangu ajihisi mnyonge kwa sababu yoyote ile".
Mama Jarden ndipo akajibu,
"Huwezi kufanya ivyo Jarden, namuamini manga hawezi kufanya ivyo hapa kuna kitu hakipo sawa sio bule ebu wacha kumnyima raha mkewako".
"Mama huwezi kuelewa maumivu yaliyopo moyoni mwangu.
Kila wakati ambao nafsa anachukia basi huwa nakumbuka machungu yale ya zamani kwanini?".
"Nakuelewa mwanangu lakini jaribu nawe kumuelewa mkewako sawa? Wacha kumfukuza kama unaniheshimu mimi mama yako".
Jaden aliamua Kuondoka tena pasina kusema chochote..
Mama Jaden ndio akawa salama kwa Manga kupewa talaka.
Joan alimkuta mama yake akiwa anambembeleza manga ndipo akamuambia,
"Mama wakati mwingine ebu acha kutetea ujinga jamani".
"Nyamaza barazuli wewe.
Unazeeka ukiwa nyumbani hapa kazi kujaribu kwa mwenzio kwanini umemgeuka?"
"Kwaiyo mama unanitukana na hali yangu hii? Kisa natembea kwa kuchenjegua hakuna mwanaume anaenitaka ni kama unanizalilisha si ndio?"
"Sikuzalilishi mwanangu lakini unakosea sana.
Huwenda hata ndio sababu haujapata hayo yote sababu una roho ya namna hiyo acha mwanangu".
Joan aliamua kuondoka zake maana maneno hayo ya mama yake ni kama yalikuwa yanamgusa moyoni mwake.
Maisha ya kujishusha ndio aliyokuwa akiyaishi Manga kwa ajili ya kutafuta amani ya familia.
Alivumilia kusingiziwa, matusi wakati mwingine na vipigo kutoka kwa mume wake.
Suala yeye kuwa mfanyakazi wa zamani ndio ilimtesa sana ilifika mahali ikawa ni fimbo kwake.
ilifika mahali hadi Jarden akawa mtu wa wanawake wengi kuponda raha.
Yaaaani alimuonesha manga dharau za waziwazi.
Mfanyakazi aliekuwepo pale alifukuzwa na jarden mwenyewe.
Jambo ambalo lilimshangaza manga Ndipo alimuuliza mumewe,
"Mmewangu umemuambia dada wa kazi aondoke gafla kwani pana shida gani?"
"Si wewe upo? Mbona una kipaji cha kuwa mfanyakazi au unaikana kazi yako? Umeshindwa kuwa mama bora kwa binti yangu Nafsa basi endelea na kazi yako kama zamani".
Ndio jibu alilopewa manga ndoa kwake ilikuwa chungu.
Alilazimika kuanza kufanya kazi zote za ndani japo haikumuwia vigumu kwa kuwa alikuwa hodari.
Wakati mwingine mwanae Nayla alikuwa akimsaidia hata kuosha viombo.
Manga kutwa alikuwa ni mtu wa kulia tu.
Chumba alibadilishwa sasa akawa analala na watoto wake tu.
Majira ya usiku saa 7 manga aliamka na kwenda chumbani kwa mume wake.
Alifika akafungua mlango na kuingia ndani.
Jarden alikuwa amelala lakini akashtuka taa imewaka.
"Wewe umefuata nini chumbani kwangu manga?"
"Sina mwingine wa kumfuata zaidi yako wewe Mmewangu.
Nakukumbuka mmewangu tafadhali naomba nisamehe kama nimekukosea".
"Kwanini ulijenga chuki ya gafla kwa Nafsa yani umebadilika aisee umenifanya nijute kukuoa kwa kweli.
Sina haja ya mapenzi mimi yameshanitenda.
Zaidi namuangalia binti yangu Nafsa na hao wengine ulionizalia kama zawadi nashukuru ila basi".
"Mmewangu tafadhali nakupenda naomba walau kidogo tu sitamwambia mtu kuwa tupo pamoja tena...sina wa kumlilia hamu zangu zaidi yako"".
Alikuwa akiongea huku analia manga hadi Jaden akaamua kuinuka na kumsogeza kitandani.....
Full 1000.
Whatsapp no 0716730000.
Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya 11
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni