Na
Mamuh Mohd
(0716730000)
Tulipoishia......
Nafaa alishtuka hakuamini kile alichokiona.
Huku Joan alikuwa akicheka sana.....
SONGA NAYO....
"Anty nini kinaendelea? Mbona upo na Joel?"
"Mhhh kama unavyotuona kupitia hela zako tunakwenda kuishi wenyewe.
Joel amenichagua mimi.
Kifupi hakukupenda na nilikuwa natembea nae.
Nashukuru nami nimepata mwanaume na soon nakublock".
Kisha Joan alikata simu na nafsa macho yalimtoka.
Binti palepale alidondoka chini na kupoteza fahamu.
ilikuwa ni usiku alikuwa chumbani kwake ivyo hakuna mtu aliyejua mpaka asubuhi.
Asubuhi hiyo pia hakuna aliejua kwa haraka kwa kuwa nafsa analala chumba cha peke yake na hana anaeelewana nae sana mule Ndani.
Mpaka usiku alizinduka Ndipo binti akashika simu na kumpigia baba yake.
"Baba njoo chumbani kwangu baba naumwa baba...babaaaaa".
Mr jarden haraka kwa upesi akiwa amevaa boxer tu na kaush akafunga na taulo kwa juu akaelekea chumbani kwa binti yake.
Alimkuta amejilaza chini binti nafsa.
"Mwanangu nini tatizo? Kinakusumbua nini binti yangu?"
Nafsa alibaki akilia tu.
"Ok ngoja tuende hospital sasaivi sawa"
"Usijali baba haina haja ya kwenda hospital baba ila ukae na mimi sipo sawa".
Mr jarden akamuinua binti yake na kumuweka juu kitandani na kukaa pembeni yake.
Palikwenda mpaka asubuhi.
Mr jarden alishtuka Na kuona nafsa amelala Ndipo nae akarudi chumbani kwake.
Kufika mlangoni akapishana na manga akiwa anatoka nae katika chumba cha Mr Jarden.
"Nilikuwa nimekuletea chai unywe upate kumeza dawa nikakuta haupo".
"Ndio nililala kwa nafsa"
"Vipi ? Pana shida?"
"Amenipigia simu usiku wa manane nikaenda hajaniambia anaumwa nini".
"Ungeniamsha mimi basi kama mama vipi kama ungemkuta katika mazingira mabaya ya kike binti yako".
Mr jarden alikosa cha kujibu akaingia chumbani.
Basi manga akaelekea chumbani kwa Nafsa na kumkuta amelala.
Lakini punde nafsa aliamka na kumuona bi manga amesimama mlangoni.
"Umefuata nini chumbani kwangu? Mbona unaniangalia?"
"Nimeambiwa na baba yako kwamba haupo sawa nikaja kukuangalia sio kwa ubaya ".
Nafsa wacha aanze kuangua kilio sasa, yaaani kile alichoambiwa na shangazi yake ndo kilijirudia.
"Niache nasema tokaaaa niachee"
Alipiga kelele Nafsa kumfukuza manga basi ikabidi mwanamama huyo aondoke zake.
Nafsa hakuwa wakula wala kunywa alishinda akilia tu.
Halii kusalitiwa tu, bali mpaka hasara ambayo ameiweka ya pesa katika kampuni.
Mr jarden alimfuata binti yake huyo usiku akiwa amebeba vyakula..
Aliingia pia na binti Nayla .
"Baba naomba nizungumze nae mimi kitabibu nadhani itakuwa rahisi".
Nafsa akajibu kwa ukali,
"Tokaaaa huna hadhi ya kuzungumza na mimi eti kitabibu tokaaaa".
Nayla alitoka na kumkuta mama yake amesimama mlangoni kwa maana alikuwa akisikia kinachoendelea.
Nayla akaamua kwenda kuendelea na shuhuli zake.
"Nafsa binti yangu....unajua fika naumwa je unataka kuniongezea maradhi? Usiponiambia mimi utanmuambia nani? Eeeh nafsa wangu.
Nani amekukera? Tafadhali niambie".
"Baba sijui kama utanisamehe baba yangu ahhhh ".
"Haujawahi kunikosoa mpaka umefika umri huo uliopo.
Je unahisi utanikosea sasa? Niambie".
"Baba nilikuwa na boy friend mzungu na tulikuwa tunaenda vizuri nikijua atakuwa mumewangu.
Lakini shangazi Joan kaingilia mapenzi yangu isitoshe wakapanga na yule mwanaume kunitapeli pesa.
Nilijua nawekeza katika biashara kumbe wamenitapeli na wamekimbia Marekani.
Milioni 800 baba milioni 800 uwiiiiii".
Aliangua kilio Nafsa hata Mr jarden pozi lilimuisha.
Alikosa cha kuzungumza aliweka chakula kile mezani na kutoka chumbani kule.
Mr jarden mtu mzima alishindwa kujizuia ,alifika chumbani na kuangua kilio.
Mwanamama manga hakuwa mbali akamfuata,
"Pole kwa hili Ni mtoto bahati mbaya kwa alichokifanya".
"Siumii hata kwa sababu ya pesa.
Naumia kwa binti yangu kusalitiwa maumivu ya mapenzi yanauma sana".
"Mhhh sawa basi mnastahili kupewa pole".
Manga huyooo akaondoka zake chumbani humo.
Lakini ukweli jarden alilia kwani anajua kinachokwenda kutokea katika kazi yake hiyo.
Ukweli anaujua yeye kuwa mmiliki wa kampuni alimuamini Mr jarden kiasi mpaka alihamia na familia yake south Africa akaiacha kampuni mikononi kwa Mr jarden.
Lakini ilikuwa ni siri ya Mr jarden hakuwahi kumueleza hilo Binti yake.
Aliacha mwanae aamini kwamba kampuni ile ni ya kwake.
Mr jarden alipiga moyo konde na kumfuata tena binti yake majira ya jioni hayo.
"Hilo limeshatokea mwanangu naomba kuanzia sasa uwe na furaha yako kama kawaida.
Pesa sio kitu mbele ya Furaha yako".
Nafsa alijikuta anapata afuheni akamkumbatia baba yake.
Mr jarden alitoka na binti yake mpaka mezani wakala wote nia kumfariji japo moyoni anaumia kwelikweli.
Baada ya chakula nafsa alikwenda chumbani kupumzika huku bibie nayla akiwa zake jikoni anamalizia usafi.
Mala alisikia akiitwa na baba yake,
Nayla haraka akamsogelea baba yake kumsikiliza,
"Abeee baba".
"Nayla umuangalie kwa ukaribu dada yako wewe ni daktari unajua mambo mengi".
"Sawa baba nitajitahidi ila hata wewe haupaswi kuwa na mawazo sana kwa ajili ya afya yako pia".
Licha ya yote yaliyotokea lakini Mr Jaden alishangaa kuona nayla bado anamuheshumu na kumjali.
Basi Mr jarden alijikuta anapata amani sana kitendo tu kile cha kuzunguka na binti yake huyo na kuonesha anamjali.
"Asante sana mwanangu".
Nayla pia alifurahi kuona siku hiyo baba yake amezungumza nae vizuri.
*******
Basi palikwenda mpaka asubuhi nayla alikwenda katika chumba cha dada yake.
Aligonga mlango ndipo Nafsa akamjibu
"Nani wewe na unataka nini?"
"Mimi nayla nataka tuzungumze nijue unaendeleaje kisaikolojia".
"Wewe mwehu kweli umeniona mimi ni katibiwa? Kwanza aliekuwambia naumwa nani? Kwendaaa".
Nayla yakuwa na la nyongeza ikabidi aondoke zake.
Binti alikuwa akifanya kazi katika hospital kubwa, baada ya field kufaulu vizuri alipata nafasi ya kuwepo katika hospital ile.
Majira ya mchana Nafsa alikwenda kuonana na rafiki yake Aliyeitwa Dina.
Alikuwa ameshamuelezea kila kitu kwenye simu.
"Ahhh pole nafsa huyo shangazi yako ni mbaya sana jamani khaaa '.
"Sina hamu dina.
Yani nashukuru baba yangu ananipenda na ana pesa za kutosha ndio maana hajataka iwe kesi kubwa".
"Aiseee pole rafiki yangu ila nikwambie kitu umemuona michael?"
"Michael? Michael huyu huyu?"
"Huyu huyu aliekwendaga masomo kumbe amerudi bonge la daktari hospital kubwa pale.
Nilikwenda majuzi kati hapa hospital nilikuwa nimempeleka bibi yangu jamani nikakutana nae".
"Wewe dina mbona haujaniambia mapema?"
"Mhh ile siku nataka nikwambie ndio ukaniwahi kunukuliwa yaliyokutokea".
"Michael mbona hajaniambia kama amerudi napaswa kuonana nae twende nipeleke".
"Heeeee shooga wewe tukifika tunasemaje?"
"Wewe twende Dina ujue habari hizi zimenipa nafuu yaaani siamini".
"Sawa twende ".
Dina kukubali basi wakaelekea katika gari la bibie nafsa kwenda huko hospital.....
full 1000.
Whatsapp no 0716730000.
Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya 16.