Chombezo……………..KIJIJI CHA WAGENI!
Mtunzi…………………..Jack Mambo
Whatsapp………………0715919396
Umri…………….……….18+
KUMBUKA GROUP ZINAPOTEA ILA PAGE ZINAISHI,ILI USIKOSE UHONDO WA HADITHI ZANGU INGIA HAPA LIKE PAGE YANGU,HAPO UTAKUWA NA UHAKIKA WA KUSOMA STORY ZANGU KILA SIKU ----???????????? Story za Mambo
Sehemu ya 01
Leo nataka niwape story ya kijiji chetu,kuna story nyingi sana kuhusu kijiji chetu,hadithi nyingi sana zenye kusisimua!Mmmh!Ila kijiji chetu!Acha nigune tu maana mmh!
Jambo kubwa zaidi kwenye kijiji chetu bwana ni wageni,aiseeh!Kijiji chetu kinapendwa san asana na wageni,na siyo wageni tu kutoka Dar huko au hapa nchini,kijiji chetu kinapokea wageni kutoka ulaya,eeh!eeeh!Yaani hapa naongelea wazungu sasa,kutoka Marekani huko,Ufaransa,Denmark yaaani daaaah!
Eeh bwana eeh itoshe kusema kijiji chetu kinapendwa sana na wageni,najua unajiuliza kwanini kijiji cha TEGAMOYO kinapendwa hivi!Kama lilivyo jina lake,ukiingia kijijini kwetu bwana moyo wako uwe umeuacha huko kwenu!Najua hunielewi,ila sasa nakusanua,ukija na moyo wako uko wazi wazi lazima uondoke na mke au ubaki kuwa mwanakijiji wa Tegamoyo maisha yako yote!
Ndiyo,acha ubishi sasa mimi ndo nakusimulia ivyo,mpaka sasa huko kijijini kuna wanakijiji wazungu kibao,tena wanakipiga Kiswahili kama wamezaliwa huku huku!Tunakula nao ugali na tembele,dagaa mchele,kachumbari na mchuzi wa pweza!
Walikuja kama wageni ila mwisho wa siku wakajikuta wamekuwa wenyeji,mabinti wakaolewa na vijana wa Tegamoyo,lakini wanaume nao wakazama kwenye huba na mabinti zetu!Kwahiyo machotara Tegamoyo utakutana nao wengi mno!
Lakini siyo ivyo tu,huko ulaya kuna mabinti zetu wengi sana na vijana wetu!Wazungu wamekuja hapa wamewapenda wamewabeba wameondoka nao!Kwahiyo ndugu yangu tuna mbegu nyingi sana huko duniani,hahahaha!Oooh Tegamoyo,kijiji chetu kimebarikiwa bwana!Weee Tegamoyo weeeeh!
Tegamoyo,kijiji cha pwani,bahari ileeeee waiona,samaki wa kutosha,hatuna shida na mboga sisi,MUNGU anavyokipenda kijiji chetu,ukifika tu ufukweni we tupa ndoano,sema namtaka Kolekole,kibua,nguru,jodari!Aaaah MUNGU atupe nini wana Tegamoyo!?
Ardhi yenye rutuba haswa,hata ukisema unapanda mawe yanaota Tegamoyo,ardhi ya kijani,miti yenye kivuli tulizo la nafsi,Tegamoyo tunafuga nyama tunazo,kiufupi tulichokosa labda madini tu,lakini nayo tukiyatafuta vizuri tunayaona mbona!
Tunawapenda sana wageni,sababu wamebadilisha maisha ya kijiji chetu kwa kiasi kikubwa sana,japo hawajaharibu tamaduni zetu!
Wageni wametuletea nyumba za bati,wametuletea mitumbwi ya kisasa kwa shughuli zetu za uvuvi,lakini pia wametuchanganyia mbegu bwana,nisisahau mashule na vituo vya afya,ni hawa hawa wageni wetu wametufanyia wema huu!
Najua unajiuliza kwanini wazungu wanamiminika kuja kijijini kwetu,sasa mimi nakupa hii siri leo,bwana kijiji chetu kina wanawake warembo mno,maumbo yao,sura zao mama yangu weeeh!Sijawahi kumuona mwanamke mbaya Tegamoyo,na sidhani kama atakuja kuzaliwa!Hao vijana sasa ukiwaona walivyopanda hewani,humkuti mfupi hata mmoja wa dawa,ukiambiwa utafute mwasnaume mfupi Tegamoyo,hata wa dawa aaaah!tunakuzika mchana kweupeeeee!Mimi nakuambia ukiugua hapa kijijini kwetu,halafu mganga akuambie eti nenda kamletwe mwanaume mfupi ndiyo unapona,basi mi nakuambia ndugu yangu unakufa huku tunakuona!Hakuna binadamu mfupi hapa,labda wageni,na hata hao wageni wakijaga Tegamoyo ukiwa mfupi hakuna anayekubabaikia!Hutopata binti wala kijana wa kusuuza naye moyo!
Tegamoyo tunapenda sana wageni,na wao wanatupenda sana tu!Tunapokea wageni wote,ila sisi tunawapenda sana wazungu,sababu ya dola zao,ukimkaribisha mzungu kwako ujue umekaribisha pesa,umekaribisha dola za kigeni nyumbani kwako!
Wote wanaokaribisha wageni,mwisho wa mwezi huwa kuna bus la kwenda mjini,unakuta wamebeba dola zao wanaenda kubadilisha kuwa pesa za Mwalimu Nyerere!Wakirudi wanarudi wamejaa tele,wamenunua kama ni nguo,vyombo na kadhalika!
Kwa ajili ya wageni sasa kuna umeme wa Sola na REA,kuna TV za kisasa,kuna redio,na vingine vingi mno ambavyo hatukuwa navyo kabla!
Sasa nataka nikupe kwanza historia ya Tegamoyo,ndugu yangu vuta kiti ukae,maana hapa sijaenda bado kwenye visa vilee vya kusisimua!Baado sijakusimulia mambo mambo ya Tegamoyo,weeh!Kuna mambo humu,acha tu hawa wageni wana balaa wewe kijana wewe!
Basi bwana,hapo mwanzo tulikuwa sisi kama sisi,yaani hakuna wageni wala hakuna machotara,ilikuwa siku moja tu ndiyo ilibadilisha maisha ya kijiji chetu!
Siku hiyo binti mmoja alikuwa anaenda zake baharini kuogelea,basi binti yule wa kuitwa Moza,akafika ufukweni na kuvua nguo zake akaanza kuoga!Sehemu hiyo ni maalumu kwa wanawake tu kuoga!Basi wakati anaoga kumbe kuna mzungu mmoja mtembezi,namuita mtembezi sababu aliamua yeye na familia yake kuizunguka dunia na meli yao ya kifahari!Sasa katika pitapita zao ndiyo wakauona ufukwe wa Tegamoyo!Mandhari yake yakawavutia na kuamua kusimama hapo walau kidogo!
Mr Franklin akaamuru wakae hapo kwanza kabla hawajaendelea na safari yao,alikuwa na mkewe Rosa,pamoja na binti yao mrembo Blenda!
Sasa wakati ule wa jua kali,ni mara chache sana kumkuta mtu ufukweni,na hapa nikuambie tu,wanakijiji wa Tegamoyo hatupendi tabu sana,kwahiyo jua kali tunajifungia ndani na wake zetu tunaenjoi maisha!Hatujazoea maisha ya mateso kabisa!Kwanza wanawake wetu ni kama wa kitanga,wanajua kutudekeza bwanaaa!Basii basi tuendelee na Mr Franklin!
Sasa yule mzungu bwana wakati ametia nanga pale,akaanza kuzunguka huku na kule kuangalia mazingira,ndiyo katika pitapita zake akamuona Binti mrembo Moza anaosha mwili wake!Franklin akapagawa!Kwa kutembea kwake ni wazi hakuona kabisa mrembo kama yule machoni mwake!
Haraka bila kupoteza muda,akachukua kamera yake na kumpiga picha kadhaa Moza bila kujua kama anapigwa picha,ghafla katika harakati za kupiga mbizi ndiyo anamuona mzungu!
Moza alishtuka sana,haraka akatoka kwenye maji,sasa wakati anamshangaa mzungu,akasahau kama hana nguo yuko uchi!Ni kama alikuwa anajiuliza huyu kiumbe wa aina gani huyu!Kosa alilolifanya Franklin ni kupiga hatua kumsogelea!
“Mamaaaaaaaaaa!Jiniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!”,hapo akatoka nduki nguo kashika mkononi,akaenda kuvalia mbele huko!
“Nooo!Wait!Please wait!”,alijarivu kumsimamisha Moza,lakini binti aliendelea kuchanja mbuga,na kijiji chetu kipo karibu na ufukwe sana,makelele ya Moza yakawafikia wanakijiji,wakatoka haraka kwenda kuangalia kuna nini?Wakakutana na Moza njiani yuko uchi wa mnyama!Wanawake wakamshika na kumvisha nguo kwanza!
“Jiniiii! Jini mama nimeona jiniiii!”,Moza aliendelea kupiga kelele!
“Moza ebhu tulia!”
“Nimeona jini mweupe mama ni jiniiiiiiiiii!”,mama yake alipoona binti hatulii,akamchapa vibao vitatu ndiyo akatulia na kutoa maelezo yaliyonyooka!
“Una uhakika umeona jini!?”
“Ndiyo nimeona!”
JE NINI KITAENDELEA?WANAKIJIJI9 WATACHUKUA HATUA GANI WAKIWAONA WATU WEUPE WAMEVAMIA KIJIJINI KWAO?
????SOMA VIPANDE YA MBELE VYA HADITHI HII KWA KULIPIA VIPANDE 10 KWA 1,000/= AU YOTE FULL KWA SH 4,000/=
NAMBA ZA MALIPO NI HIZI!
TIGOPESA ????0715919396
M PESA ????0760199396
Majina ???? JACKSON MAGOSHA
LIPA NAMBA M PESA 5892883
Jina???? MR MAMBO
????MTAG MWENZAKO...MWAMBIE TUMEWASHAAAAA!
????Bandika...Banduaaaaaa!
#LIKEEEEEEEEEEEEEEEEEE????
#KOMENTIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII????????????????
#SHAREEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE????????????????
#ProfesaMambo
#GOD over everything!
[28/04, 11:05] Mr Mambo:
[20/08, 18:47] Tabasamu na Mambo:.