. Gari hilo lilijulikana kama Benz Patent-Motorwagen, na linatambuliwa rasmi kuwa gari la kwanza la kisasa linalotumia injini ya petroli.
Karl Benz alitengeneza gari hilo kwa kutumia injini ya silinda moja yenye uwezo wa 0.75 horsepower. Lilikuwa na magurudumu manne na liliendeshwa kwa kutumia petroli kama chanzo cha nishati.
Alipata hata hati miliki ya uvumbuzi huo tarehe 29 Januari, 1886, hatua iliyozindua enzi mpya ya usafiri wa barabarani.
Lakini pia, historia ya mafanikio haya haikamiliki bila kumtaja mkewe Bertha Benz, ambaye mwaka 1888
aliamua kuchukua gari hilo na kusafiri kilomita 106 bila kumwambia mumewe
Asubuhi tulivu mwaka 1888, Bertha Benz aliacha ujumbe mfupi, aliwaambia ataenda kuwatembelea bibi yao pamoja na watoto. Hakusema kuwa safari hiyo ya maili 66 ngefanyika kwa kutumia gari la kwanza duniani.
Lakini watu wengi hawakuamini kama lingeweza kufanya kazi. Wakati Carl akiwa amelala, Bertha alilivuta taratibu nje ya nyumba, akanyaga injini.
Bertha Benz akaondoka na gari nyumbani kwake m akiacha mumewe amelala.
Alipanda milima, akapitia barabara za matope, na kukutana na changamoto mbalimbali. Mafuta yalipopungua, Bertha alisimama katika kitio cha mafuta.
Alitoboa bomba la mafuta lililoziba kwa kutumia sindano ya kofia, na kurekebisha breki kwa kutumia kipini cha nywele.
Safari hiyo ya saa 12 haikuwa tu matembezi ya kifamilia, bali jaribio la kishujaa lililoonesha uwezo wa uvumbuzi huo. Aliporudi, dunia ilianza kuliona gari hilo ni bora sana.
Akawa mtu wa kwanza duniani kufanya safari ndefu kwa gari. Safari hiyo ilisaidia kuonyesha uwezo wa gari hilo kwa umma na kuongeza uaminifu wa watu kwenye uvumbuzi huo.
Leo tunavyoona magari ya kifahari, magari ya umeme na hata magari yanayojiendesha yenyewe, tusisahau kuwa ilianza na injini ndogo ya Karl Benz mwaka 1885..
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments