*IN LOVE WITH ZURI* *SEHEMU YA 14*
Basi bwana siku hiyo chai ilishuka bila wasiwasi kabisa, maana zuri kila muda alikuwa ananijali sana, utasikia frank nikuletee maji?? Mara ohooo kaka Frank umepaliwa jamani pole
Yani alikuwa anaongea huyu binti, ndio nikajua kwamba Zuri ni mwanamke muongeaji mno binti anaongea huyu acheni kabisa
Zuri.."
Tukiwa jikoni siku hiyo namsaidia saidia kukatakata vitunguu nilimuita, zuri akageuka tu na kuniangalia akanikuta nalia jamani ni kwa sababu ya vitunguu
Ikabidi achukue mtandio wake na kunifuta futa pale huku akiniambia pole, haya mahaba me ndio nayaona saivi kwa kweli sijawahi fanyiwa hivi na mwanamke mimi
'Nenda kapumzike hii kazi niachie mimi.."
Zuri aliniambia, kwa kuwa nilikuwa nimekiona cha moto sikukataa
"Sawa lakini baadae naomba nitoke na wewe.."
"Tutoke twende wapi tena,?? Harafu unajua kabisa me siruhusiwi na madam kutoka hapa.."
"Usiwe na wasiwasi nitaongea na mama.."
"Sawa lakini tusichelewe kurudi tu, maana
natakiwa kupika.."
'Kwa leo atapika Anita..."
Nilisema na bila kusubiri chochote nikashika njia na kuondoka zangu nikimuacha Zuri ananitazama na asinielewe, basi bwana nilielekea zangu chumbani kwa rast born Ethan ili aende akanielekeze baadhi ya mambo
Si mnajua tena me na wanawake hola holatH
'Nakuona mwenyewe..."
Baada ya kuingia tu nikakutana na neno kutoka kwa Ethan, huyu kijana walah simuwezi mimi, ila nisiwe muongo ninaenjoy sana kuwa na huyu dogo
"Acha maneno mengi nipe maelekezo.."
Nilimwambia
"Mh."
"Unaguna nini we niambie basi haraka haraka.."
"Eeh amekubali??."
"We kufika hapa jua kuwa amekubali, sasa ndio naomba unifundishe vimaneno vya kumwambia
kule.."
"Dah basi sawa, sasa sikia kwani unataka kutoka nae kwenda nae wapi..??"
"Me nataka nimpeleke kule beach nimeagiza watu wanipambie, so ndio nampeleka kule.."
"Acha hizo bwana mpeleke hotelini.."
"Ethan.??"
"Ethan kitu gani, me nakufundisha hapa harafu unaleta ujuaji nitakuacha ohoo..."
Eeeh
"Basi basi Ethan, nakusikiza.."
'Fanya hivi, waambie wale watu wachane na
huko Beach we waambie wakuoambie kwenye hotel yani namaanisha uchulue chumba mazima
mazima usije kusumbuka baadas
Kisha waambie wakupambie huko ndani waweke kila kitu, sijui champagne bila kusahau wine yani we waambie waweke Malaga zaga chakula kama chote wapambe humo ndani kuwe na mauwa mekundu tu mpaka kitandani wapambe na kuandika kuwa unampenda zuri
Sasa nakwambia hapa uende ukaboronge huko, oky sasa baada ya hapo ndio unampeleka huyo
mtoto huko ukishamfikisha kumbuka unaenda na ua lako kabisa umeliandaa kwa ajiri ya kumpa na bila kusahau Pete
Umenielewa??"
"Yes broh.."
"Harafu baada hayo unapangiloa maneno ya kumwambia yani unaanza na kumuuliza uko tayari nikuoe?? Hakuna mate mgumu mbele ya chai lazima atakubali tu, sasa akishakubali
hakuna kupoteza muda unat..."
"Sasa Ethan yani ndio nimeanza jana tu hapa kumpa zawadi ndio unasema niende nae hoteleini kweli jamni..??"
"Oneni hili boya lenu huku.."
Eeeh me leo nimekuwa boya, hata hivyo fresh tu bana sema nipo najifunza hapa acha nikaze
fuvu
Itaendelea........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni