VYOTE NDANI GONGA94
MR GENERAL : KUMBE ULINIPENDA EEE SEHEMU YA 16
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
“Sikuwa najua kama nilikuwa sikuridhi…kabla hajamaliza nikaanza kumkiss, akawa kama hataki, najuaga udhaifu wake, nikataja jina lake kwa ile sauti ya kutolea nyoka pangoni, aisee akanisogelea na kuanza mashambulizi yeye, siku hio sikutaka hata ahangaike, nikamfunga mikono na miguu..
Sijui alijua nataka kumteka, maana ni kama hakuwa ananiamin amin, maana mambo hayo yalikuwa mageni sana kwake, ila ni kweli nilikuwa nataka kumteka, ila nilikuwa nataka kumteka kwenye huba langu…
Kuanzia nimemjua mume wangu sikuwah kumuona anapiga kelele kiasi kile, alikuwa kama amepagawa kwa raha ambazo alikuwa anazipata, alikuwa analia kama mtoto mdogo kwa utamu, siku hio nilitaka mimi ndio nianzishe mapambano na niyamalize mwenyewe…
Shughuli ilikuwa pevu na kwa mara ya kwanza nikamuona amechoka akasema
“Msengerema yoyote Yule akikusogelea na ua, hata kama nina mashine kubwa kama mlingoti utaivumilia na hakuna mtu atakugusa wewe ni wangu pekee yangu kisha akaamka na kwenda zake kuoga, ametoka akaniambia
“Jiandae tunatoka…
Mimi tena kwanini nijivunge, yaan nilijua lazima naenda kutolewa lunch sehemu, sehemu flani hivi ya maana sana, kweli nikavaa nikapendeza, mume wangu akaniangalia kisha akasema “Nilitaman nikuvue nikuvalishe matambara maana wivu utaniua mimi…
“ Kwa hio nikabadilishe nguo, embu nambie nivae nini, si unajua mimi nipo hapa kwa ajili yako na nipo tayar kabisa kuishi chini ya amri zako…
Akatabasamu kisha akasema “Nataman mwanaume yoyote kwenye hii dunia asione uzuri wako zaidi yangu, nataman ukiwa na wanaume wengine usiongee kwa namna unavyoongea na mimi, na usivae vinavyonivutia maana naogopa wengine wanaweza wakavutiwa na mimi kama ambavyo wewe umevutiwa na mimi, ila nashindwa kabisa kukuambia ukapendeze maana naamin muonekano wako mzuri ndio dira na nuru yangu, na ndio uanaume wangu kuwa naweza kumtunza vizuri mke wangu, nikasogea na kumshika mkono kisha nikamuambia
“Nakupenda…
Akatabasamu ila hakunijibu kitu, basi hao tukapanda zetu gari na kwenda mpaka sehemu moja hivi , ilikuwa nin sehemu tulivu sana, yaan hakuna watu, na kulikuwa na chakula kizuri, akamuita muhudumu, na mara baada ya kumuita muhudumu tukaagiza pale tukawa tunakula polepole, na wakati wote huo alikuwa ananiangalia akiwa anatabasamu tu…
Nikaona kabisa hapa nimeshamshika pabaya mtu wangu, tumemaliza akanambia kuna sehemu tunaenda na tunaweza tukalala huko huko, nikamuuliza ni wapi, ila akanambia kuwa nitapajua tukifika, kweli nikaenda kupanda kwenye gari, na tukaanza kwenda sehemu moja hivi, ilikuwa ni nyumba ya kawaida kidogo, tukaingia mpaka ndani, kisha nikamkuta mwana mama mmoja, alikuwa anaonekana kama ana miaka 60 au karibu na hio, akanipokea vizuri sana, kisha tukaenda kukaa ukumbin na mume wangu alikuwa amekaa pemben yangu…
Akaja mdogo wake wa kiume, aisee hii familia imejaaliwa mahandsome boy, yaan wanavifua flani hivi, alafu ni warefu, na kingine wanakarangi flani hivi, yaan ukiwaona unawazia kuzaa watoto wazuri kama wakifanana na baba zao, maana mimi ni black mamba, yaan labda watoto wachukue sura yangu alafu rangi ya baba yao…
Mume wangu akaniangalia kisha akamuangalia mdogo wake, nikajua baba cha mawivu ameshaanza wivu wake..
Nikawa siangalii sehemu yoyote naangalia chini tu, basi baada ya muda akaja baba yao, kumuangalia vizuri ndio Yule mzee ambae alikuwa amekuja kunioa, na ndio alikuwa amekuja kunitolea mahari, nilipomuona nilishtuka, ila aliponiona akatabasamu na kusema
“Karibu sana nyumban kwetu bint yangu…
ITAENDELEA ….
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi mr-general-kumbe-ulinipenda-eee-sehemu-ya