tina alitetemeka akaona sasa mwisho wake umefika ,akajua anaenda kutolewa kafara viungo vyake vitundikwe kama vile anavyoviona, akamuona Mery akivua nguo zote akibaki kama alivyozaliwa,. Nilsahau kukwambia uvue nguo 'unaona watu wote wanaoingia ukumbini wapo Kama walivyozaliwa, ni kweli kwenye ukumbi ule wa kutisha kila mtu hakua na nguo wala hakuna anaemshangaa mwenzake,si mwanamke la mwanaume ,wote walikua bize kukaa nafasi zao .baada ya ote kuketi kilipita kiza cha ghafla ukafatia mwanga mwekundu, kila mtu aliinama kuonesha heshima isipokua watu wachache sana walioonekana kushangaa. Kikapita kimya kifupi sauti ikasikika "nimekuja kupokea na kuwaapisha watumishi wapya ',nawakaribisha sana kwa moyo wao wa kufanya kazi na sisi, hakika maisha yako huku, ss ndio tumeishika dunia, bila ss hakuna chochote duniani, naomba wageni wote wapya waje hapa mbele. Mery akamwambia Tina nenda usiogope huyo ndio mkuu wetu, hofu ilimtawala Tina 'akanyanyuka kwa woga akiwa na watu kadhaa hadi mbele ,ghafla akajikuta yuko sehemu tofauti kwenye chumba akiwa amesimama, akiendelea kujishangaa akahisi joto kali, jasho lilianza kumtoka, pembeni aliona bomba la maji ndipo akaona afadhali ajimwagie maji kidogo kupoza hali ya joto ,alipofungulia bomba, badala ya kutiririka maji zikatiririka damu aliruka toka pale moyo ukipiga kwa kasi, sauti ikasikika kuwa hayo ndio maji yetu Tina 'usiogope we ingia uoge utatamani usitoke jinsi utakavyojisikia raha, sauti ikaendelea kumhimiza ikimwambia ingia, ingia, akahisi kusukumwa na kitu akajikuta yupo kwenye zile damu zikimloesha mwili wake, ajabu alijisikia raha sana tofauti na anavyooga maji ya kawaida, kidogo akaanza kujisikia kiu kadri muda ulivyokua unaenda kiu nacho kilizidi 'akaanza kusikia kizungu zungu "oh Mery uko wapi mwenzio kiu kinaniua huku. Akaona glasi iliyojaa damu, macho yalimtoka, sauti ikasikika kunywa ni tamu zaidi ya kinywaji chochote ulichowahi kunywa ukiacha unakufa shauri yako, alionja kwa kutumia ulimi akakutana na ladha nzuri tofauti alivyokua akifikiri, akaipeleka glasi yote kinywani, mh mbona tamu hivi,yani kule hospitali huwa tunaona kinyaa kumbe nilikua sijui ,ikatokea glasi nyingine tena, wala hakujishaua akaichangamkia fasta, akaanza kusikia nyama zilizobanikwa zikinukia harufu tamu, Tina udenda ukaanza kumtoka wa kula nyama, hakujua ni nyama gani hizo, akaanza kufatilia harufu inapotokea alifika akakuta nyama zimebanikwa vipande vipande, akachukua kipande cha kwanza akakila, utamu aliousikia acha tu akavishambulia tani yake mpaka akashiba ,aliposegea mbele akakuta mikono, vichwa, miguu navyo vimebanikwa .mamaaa ina maana nimekula nyama za watu??,kidogo akaona mtu akija kwa kasi ameshika fimbo wakati bado akimtafakari akashtukia anatandikwa fimbo mfululizo alitaka kupiga kelele sauti yake haikuotoka, zile fimbo zilimpeleka chini. Tina akaona asipojitetea atauwa kutazama pembeni akaona kisu, ukichanganya hasira na maumivu aliyokuwa nayo aliinuka na kile kisu moja kwa moja akakizamisha kifuani, alikitoa akamchoma zaidi ya mala moja ,yule mtu akaanguka chini na kufa papo hapo, hasira zake ziliisha akajikuta ameua, mikono ilimtetemeka akakitupa kisu akaanza kukimbia, akajikuta yuko tena pale ukumbini 'sauti ikasikika "nashukuru Sana kwa kupata watu majasiri ambao hawataogopa kwenda kutekeleza kile tutakachoitaji, kila mmoja atatumia nafasi aliyonayo duniani kututumikia, kabla ya kuja hapa mlikua hamjawai kuua ila Leo kila mtu ameua, sidhani kama mtaenda kuogopa kuua. Tina alitaka kumuona anaeongea hakumuona ,na ni kweli katika maisha yake hajawai kuua wala kusubutu lakini Leo ameua. Hawakujua kama ni moja ya somo tu la kuwafanya wawe majasiri zaidi. Waligawiwa Pete.,hizo Pete tutatumia kuwasiliana na nyinyi, pia zitawasaidia kufanya maajabu, ni imani yangu mtakua watiifu nawatakia majukumu mema. Ule mwanga mwekundu ulipotea ukarudi wa kawaida, Mery alimkimbilia Tina 'hongera jamani, hongera sana, akimkubatia na kumbusu, sasa umekua Tina, nimeshukuru pale hospitali sasa tutakua wawili, twende tukawaoneshe kua wapo chini yetu, Tina alifurahi kimoyo moyo kuona kuwa nae ana nguvu kama za mery.Tina alimwambia Mery 'tuondoke basi maana nina zamu ya kuingia asubuhi. We si mgeni tena wala si mtu wa kawaida, tangulia mi nitakuja shoga, iamuru iyo pete ikufikishe nyumbani. Na kweli alivyoiamuru tu Tina akawa kwake, ilikua saa moja kasoro, haraka ajavaa nguo zake za unesi kuwahi zamu, alipofika walikabidhiana na nesi anaemaliza zamu, alipita kukagua wagonjwa alipomaliza akarudi kwenye chumba chao kupumzika akiukumbuka usiku uliopita ulivyomwingiza kwenye ulimwengu wa ajabu usingizi ukampitia,. We nesi, nesi, nesiii "ilikua sauti ya mtu anaemuuguza mgonjwa wake ikimuamsha Nesi Tina, akiwa bado kwenye uchovu wa usingizi alifikicha macho yake "unasemaje??, siyo unasemaje!!!!?, nyie manesi wa siku hizi hamna huruma kabisa, mgonjwa wangu analalamika kwa maumivu makali badala uje umsaidie we unasinzia, kwani umekuja kulala hapa?, huko kwenu hujaacha kitanda. kaka kua mstaarabu basi. We ndio umekosa ustaarabu, mgonjwa analalamika muda mrefu unakoloma tu hapa. Nesi Tina hasira zilimshika mpaka mdomo wake wa chini ulicheza, alimtazama kwa jicho kali kisha akasema "naona unanifundisha kazi sawa nimekuelewa nenda, nakuja kumhudumia sasa hivi mgonjwa wako. Jamaa aliondoka akitabasamu kwamba amemkomesha " hawa manesi wa siku hizi ndio dawa yao ukijifanya kuwaogopa mgonjwa wako atateseka bure .Nesi Tina akiwa amefura hasira alichukua chupa yenye sumu akaelekea kwenye kitanda cha yule mgonjwa.Naomba unipe bomba lake la sindano na hiyo chupa ya dawa, alipopewa aliichanganya ile dawa na sumu aliyokuja nayo, akaivuta kwenye bomba la sindano, akamchoma begani. Haya kaka tayari nishamtibia mgonjwa wako una lingine?? , hapana nesi nashukuru sana
ITAENDELEA
FULL 1000
0699286085.