PENZI LA OMBA OMBA😍❤️😍❤️😍❤️ Sehemu ya 09
KIUKWELI nilishangaa sana, kwa maana sikujua ni kitu gani kilikuwa kimempa hasira shureymu kiasi chote kile, kuna muda nikawa nahisi labda simtendei anayoyataka vizuri, sijui hata nilikuwa na wasiwasi wa nini…
Kwenye majira ya kama saa nne usiku nikaona sms kutoka kwa shureymub inasema “ hivi kutengengeneza dimpos siinawezekana?...
“ kiukweli sijui ila naamin hakuna kitu kinachoshindikana chini ya jua, kwa maana kama kutengeneza shepu inawezena na kinaonekana ni kitu kikubwa sana, sasa sidhan kama kutengeneza dsimpos kitakuwa kitu kigumu sana, nikajibu na mimi kwa sms….
“ ila mwanaume kuwa na dimpos ni sawa kweli au ndio anageuka piss kali, akatuma sms nyingine shureym…
“ weee sio kweli, kuna wanaume wakiwa wanadimpos unajikuta unataman kuwaona wakiongea kila wakat, unataman uwaone wanacheka kila dakika, maana hizo dimpos zake zinamfanya anazidi kuwa handsome kama huyu shemeji yako muswaabu, yaan akicheka tu mimi hoi, nikajibu sms nyingine hivyo….
Nikashangaa shureym hajibu tena sms yoyote ile, alikuwa kama amekasirika, ila kwaakili zangu nikajua labda atakuwa kalala, hivyo nikaachana nae, kisha nikampigia my wangu kwaajili ya kumtakia usiku mwema, na kweli baada ya sekunde kadhaa akapokea, na badala ya kutakiana usikun mwema tukajikuta tunaanza kupiga sory, kwa maana ndjo penzi jipya tena, yaan mnataman kuongea kila wakat, yaan mkifanya mchezo mnaweza mkajikuta mnakesha kila siku kwa sababu ya kuongea na simu usiku….
Tukapiga story weee, mwisho mm nikaanza kusinzia, ikabidi nimaage muswaabu, ila kitendo cha kukata simu, nikashangaa sms zinaingia mfululizo kwenye simu yangu kutoka kwa shureymu, ya kwanza inasema, “ badala ulale unakaa kukesha kuongea na wanaume..
“ yaan sijui unataka mwanao awe mtoto wa aina gani kwa kukubali kuongea ujinga na huyo mpuuzi wako usiku kucha, sms nyingine ilikuwa inasema hivyo…
“ huyo my wako jaribu kumuambiaq unapotoka, ili akupende kama ulivyo, sms nyingine ikawa inasema hivyo,…
“ ila shemeji yangu anadimpos nzuri, atakuwa amefanana sana na mama yake, maana kwa ninavyojua mwanaume hasifiwi uhandsome anasifiwa pochi, sms nyinine ikawa inasema hivyo, ila hata sikutaka kuzijibu, mkwa maana sikujibu sms hata moja, kwa maana niliona kama nikijibu sms yoyote ile, nitaanza kusababisha ligi na shureymu, hivyo nikaamua kulala zangu…
Kulipopambazuka, nikaamka nikamuandaa mwanangu ilikuwa ni mapema sana, na kwenda nyumban kwa shureymu, kwa maana nilihisi huenda anakasirika kuona kama yeye anatoa kila kitua alafu mm nipikie kwangu, nikaona bora nikafanye kila kitu nyumban kwake, basi nikaingia ndani nikamkuta bado amelala, nikampigia na kumuambia kuwa nipo hapa ukumbin kwako, kwa maana nilifunguliwa na mlinzi, nikashangaa shureymu anatoka na kiboksa, nilishtuka kwa maana nilimuona kama yupo uchi vile…
“ habar za asubuh salha, akasema ..
“ habar za asubuh, nikajibu, mara katoto kakasema baba…
“ owww mama yako ndio hataki kuniita baba saidi ata kiutani, sijui atakuwa ameshakutafutia baba mwingine, akasema shureymu, kisha akamchukua mtoto na kwenda nae chumban, basi na mm nikaona bora nianze kupika, basi nikapika pale, na mara baada ya kumaliza kupika nikafanyab usaf kidogo kisha nikaenda kumuita shureymu aje kula kifungua kinywa,. Safar hii alitoka kifua wazi, na vile alivyojazia, alikuwa ni kama ananifanyia makusudi, ila hata sikujal kabisa, nikaenda kuchukua maji jikon, kwa maana nilipasha maji ya moto kwaajili ya kumnawisha mikono, kwa maana niliamin kuwa nikimuhudumia vzr zaidi huenda asiwe na kisirani, nikahisi labda anakisiran kwa sababu kuna baadhi ya vitu sikuwa navifanya, kumbe ndio nilikuw nazidi kulikoroga, alafu kulinywa siwezi….
Basi nikamchukua mtoto na kumuweka mgongoni, na kwenda mpaka alipo shureymu nikaanza kumnawsha mikono, ila sijui hata nani aliniambia nishike mikono yake nianza kumsaidia kuiosha, kumbe namsisimua jamaa na sijui, nikashangaa wakati naishika mikono yake kumsaidia kuiosha naona abdala kichwa wazi kama anataka kuleta shida, ila sikuwa hata nawaza, na kwaakili zangu nikahisi ni hali ya kawaida kwa mwanaume, kwa sababu kuna muda nikiwa nimekaa na muswaabu nilikuwa naona kichwa wazi wake analeta tabu, ila nikashangaa shureymu ameleea, akawa ananiangalia kwa macho malegevu, hapo mimi sina habari, ila sijui ndio ushamba wa mapenzi au nini, kwa maana nilihisi kama ninayoyafanya ni sawa, kumbe nilikuwa nazidi kumvuruga kijana wa watu, na baada ya hapo nikamiminia chai, nikamuwekea na vitafunwa kisha nikawa naondoka zangu, kwa sababu mimi nilikuwa nimeshakula…
Nikashangaa navutwa kisha shureymu akaniulia “ embu nambie unataka kwenda wapi?...
“ naenda kumaliza usafi jikoni, nikajibu, kaniangalia kisha akasema “ embu kaaa ule, nitaenda kusafisha hata mwenyewe, haso nikakaa nikawa nakula, ila wakat wote alikuwa ananitazama kwa macho flani hivi, ila sikumjali maana kila nikiwaza kumpenda nakumbuka maneno yake, ya kuwa anataka mm nay eye tuwe dada na kaka, sasa moyo wangu nilishauambia upunguze kiherehere, tukawa tukula pale, ila alikuwa ananiangalia sana mwisho akaniuliza…
“ eheee embu nambie kuhusu jana ilikuwaje na bwana shemu kwa maana nimesikia anamadimpose na ni mweupe kama mama yake, akasema shureymu nikaona kama anataka kuanza kumdhalilisha mwenzake kimtindo hivi…..
“ yaan unavyomuongelea kana kwamba unamuongelea mwanamke flani hivi, ila ka macho yangu namuona muswaabu ni bonge la handsome nikajibu, nikashangaa amepaliwa, akaanza kukohoa mfululizo….
Nikaenda kumchukulia glass ya maji kisha nikampatia, ila wakat naondoka nikashangaa navutwa, akamshusha mtoto chini taratibu kwa maana alikuwa ameshaanza kutembea na kunishushia kiss la maana, na kila nilipokuwa najaribu kujitioa, nashangaa mtu ananing’ang’ania anaendelea kunikiss, ikabidi nimuache anikiss kwa tani yake, amemaliza akaniambia ety, lile busu halina maana yoyote ile, alikuwa ananiambia kuwa chakula cha leo ni kitamu sana, asante…
Nikashangaa, yaan kuambia asante ndio mpaka mkiss, na anaonekana kabisa nakiss kwa hisia, alafu anakuja kuniambia sijui mambo gani, ety ni busu la asante…
“ usijal naelewa, nyie matajiri mkimkiss mtu ni kwasababu unataka kumuambia huypo mtu asante, na nashkuru sana kwa kushkuru, nikasema na shureymu akatabasamu, mara simu yangu ikaanza kuita na aliekuwa ananipigia alikuwa ni muswaabu, nikashangaa shureymu amezima simu kisha akasema “ leo ni zamu yangu….
JE NINI KITAENDELEAAA!! "
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni