*NIMEKOMA MIMI ๐* Chapter 15 Baada ya Bishop kuondoka, nililala kwa sababu nilikuwa nimechoka sana na mwili wote
unauma. Nilipoamka ilikuwa jioni kabisa, njaa inauma. Wakati nikijifikiria niende jikoni kutafuta msosi au nisiende, Tobias akaingia akiwa amebeba trey lenye chakula.
"Nimekuletea chakula ule najua haupo vizuri kiafya
Nikamuambia "Asante kwa chakula"
"Sawa, kula tu kisha ulale tena"
"Kwani Tobias Nitakaa hapa kwa muda gani?"
Akanijibu "Sijuil Maybe Mpaka Bishop abadili mawazo yake. Kwa sasa kula, pumzika, na jaribu tu kutokujihusisha naye wala yeyote humu ndani"
"Asante Tobias. Wewe tu ndiye mtu pekee hapa.
ndani ninayemuamini
"Sawa" aligeuka kisha akaondoka.
Lakini alipokuwa anatoka chumbani kwangu, akakutana na Bishop pale koridoni. Bishop hakufurahia hata kidogo kumuona anatoka kwenye chumba changu. Akamtazama vibaya sana
"Ulikuwa unafanya nini huko ndani?"
"Nilikuwa nimpelekea chakula, hajala toka jana, nikadhani ni vyema ale"
Bishop akacheka kwa dharau kidogo "Najua, lakini sikukuambia upeleke chakula"
"Sorry....nilikuwa najali tu"
"Sawa, lakini hii ndiyo mara ya mwisho nisikuone upo chumbani kwake. Kama anataka chochote, aje mwenyewe anieleze mimi. Tumeelewana?"
"Ndio boss"
Bishop akaondoka, lakini ukweli ni kwamba alikuwa na wivu. Kwani ndo kashaanza kunipenda au ana lake rohoni linalo msumbua?...Ngoja tutaona.
Anyways Nilimaliza kula, nikapeleka trey jikoni kisha nikarudi ndani kulala. Toka siku hiyo maisha yangu pale yalikuwa ya bata. Nilikaa tu
kama malkia, Sifanyi kazi yoyote. Kazi zote alizifanya zmlinzi mpya waliomuajiri Yeye ndiye alikuwa anafagia, anapika, anafungua na kufunga geti
Mimi nilikuwa tu ndani, ninalala, nakula, na kuangalia TV. Ila nilikuwa bored sana kwa sababu sikuwa na simu. Tobias naye alianza kunikaushia sikujua kwa nini, pia sikua namuona Bishop maana mda huo alikua bize sana.
Sasa siku moja jioni, nilichoka kukaushiwa nikaamua kumfuata Tobias chumbani kwake. Siku gonga hata hodi, nilifungua mlango moja kwa moja nikaingia. Nilimkuta amekaa kitandani kajilaza! Ile kaniona tu, Akainuka haraka na kuuliza "Unafanya nini chumbani kwangu?"
"Unanikaushia na nataka kujua kwanini
"Kwa sababu hakuna kitu cha kuzungumza mimi na wewe"
"Najua lakini usinikwepe. Nilikuwa nakuja kwako kila nikiwa na shida. Kwanini unanikaushia sasa? Si vizuri
"Kama una tatizo lolote, nenda kwa Bishop. Yeye ndiye atakusaidia sio mimi. Please kaa mbali na mimi
Nikashangaa Kimekutokea nini?" nikamuuliza "Kwanini?
"Kwa sababu Bishop hapendi nikae karibu na
wewe"
"Kwanini hapendi?"
"Sijui ila please toka" Sauti yake ilikuwa serious kweli akitaka niondoke. Japokua hata mimi alinifanya nijisikie vibaya ila nilifata amri yake nikatoka nje.
Nilipotoka tu nikakutana uso kwa uso na Bishop. Tangu siku ile aliniletea pads hakua amenisogelea tena wala kuzungumza nami. Lakini alivyoniona nikitoka kwa Tobias, uso wake ukabadilika ghafla. Akanishika mkono kwa nguvu, akanivuta hadi chumbani kwake.
Akanibana ukutani akipumua kwa hasira "Ulikuwa unafanya nini chumbani kwa Tobias?"
"Unaniumiza.....unaniumiza nililalamika kwa sababu kweli alinishika vibaya sana, mkono wangu ulianza kuuma Lakini hakujali.
Akarudia tena kwa sauti ya juu "Nakuuliza,
ulikuwa unafanya nini chumbani kwa Tobias?"
"Nilitaka kumcheki tu kwa sababu nilikuwa nahitaji kitu"
"Kama unahitaji kitu, njoo kwangu! Usiende kwa Tobias"
Nikamwangalia nikamuuliza "kwanini?"
Hakusema kitu, na ivi tulikua tupo zero distance
hali ikaanza kuwa mbaya. Namna alivyokuwa ananiangalia, akili yangu ilihama kabisa. Macho yake yalikuwa na upendo ndani yake kitu ambacho sikuwahi kuona kwa muda mrefu. Hata Michael hakuwahi kunitazama vile.
Ghafla Nilianza kujisikia tofauti, Moyo ulikuwa unadunda kwa kasi. Sio kwangu tu hata Bishop naye alianza kuwa taabani. Macho yake yakatua kwenye lipsi zangu. Alikuwa anataka kunibusu, niliona kabisa.
Sio kwamba sikutaka, ila hisia zile zilikuwa ngeni kabisa. Nilijisikia raha lakini pia niliona ajabu. Nikamsukuma taratibu, nikatoka mbio kurudi chumbani kwangu.
Nilifunga mlango kwa funguo nikianza kupumua kwa nguvu nikijiuliza "Kuna nini kinanitokea? Kwa nini najisikia hivi? Hizi ni hisia gani?"
Embu subiri kwanza
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni