Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

SIMULIZI: LUCKY (SIHITAJI KURUDI NILIKOTOKA)  SEHEMU YA 01
Gonga94 Β· Stories

SIMULIZI: LUCKY (SIHITAJI KURUDI NILIKOTOKA) SEHEMU YA 01

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
SIMULIZI: LUCKY (SIHITAJI KURUDI NILIKOTOKA)

SEHEMU YA 01

Mwaka mmoja ukiwa umepita tokea binti mwenye umri wa miaka 24 Lucky ajiunge na chuo kikuu cha Dar es salam ( University of Dar es salam ) maarufu kama UDSM. Marafiki zake aliokuwa anakaa nao chumba kimoja katika vyumba vya kulala wanafunzi chuoni hapo, waliojulikana kwa majina ya Mariam, Tunu na Amina. Asubuhi na mapema ya siku ya wikiend ya jumamosi waliamua kumkalisha chini rafiki yao huyo kwa ajili ya kuongea naye mambo flani mawili matatu kutokana na jinsi walivyokuwa wanaishi naye katika hali ya unyonge na kuonekana hapendi kushirikiana na mtu yoyote kimasomo hadi starehe za hapa na pale.

Maisha waliyoishi naye yalikuwa yanawatatiza, yanawakosesha raha. Waliishi naye kama sio mwenzao, walipohitaji ushirikiano wake hakuhitaji kuwa nao, muda mwingine walimshuhudia akikaa kiupweke hadi kutoa machozi kwa muonekano wa kuwaza mambo mazito aliyonayo moyoni mwake, walimuonea huruma hasa kwa sababu wao ni watu waongeaji wacheshi wa muda wote. Walimkalia vikao vya kimya kimya walipopata nafasi ya kipeke yao, lakini namna siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo Lucky alizidi kutia huruma na kuishi katika mazingira ya kuusononesha uso wake, uvumilivu uliwashinda na kuamua kumkalisha chini ikiwezekana awaambie chochote kinachomsumbua moyoni mwake huenda wakawa na ushauri wa kumshauri au wakampatia msaada uliopo ndani ya uwezo wao.

"Lucky mpenzi kikao hichi ni kwa ajili yako, tumeacha shughuli zetu ili tuongee na wewe. Tumeishi hapa mwaka sasa, lakini mwenendo wako na wetu ni vitu viwili tofauti, kuna muda tumekushuhudia ukimwaga machozi bila sababu, mawazo yasiyoisha, huzuni wasiwasi na vyengine kama hivyo, vitu ambavyo vimetushinda kuvivumilia kiukweli, kwa sababu sisi wakati wote ni watu wa kufurahi, kucheka. Kununa na kukasirika sisi hatujui Lucky. Tunaumia sana tunapoona mwenzetu tunayeishi naye chumba kimoja haupo kama sisi, huoneshi furaha hata siku moja, tunaomba utueleze kitu gani hasa kinasumbua maishani mwako tafadhali huenda ikawa njia ya kuondokana na hiyo hali inayokutatiza muda mwingi bila shaka"

Tunu aliyekuwa pembeni yake alimuuliza akiwa amemuangalia kwa kushika mkono kwenye tama, Lucky mwenyewe alishikilia mto uliokuwa mapajani mwake machoni akionesha hayupo nao, Mariam na Amina walikuwa wamekaa katika kitanda cha pili wakimtizama kwa macho yasiyoisha huruma.

"Tunaomba utuambie kitu gani kinakusumbua maishani mwako sisi ni marafiki wema, au tokea uingie hapa kuna jambo lolote baya tumekufanyia linalokufanya uwe hivyo?" Aliuliza Tunu Lucky akatingisha kichwa kuashiria hamna. " Sasa kwa nini unatufanyia hivyo hatupendi sisi Lucky, tuambie nini kinakusumbua hatuhitaji uwe katika hali hiyo"

" Hapana Tunu mimi sina tatizo lolote" Alisema Lucky baada ya kupitisha mkono machoni kufuta machozi yaliyokuwa tayari yanamlenga.

"Lucky unajaribu kuficha ugonjwa usiofichika, hapo tu tayari machozi yanakutoka kisha unasema huna tatizo? Tupo wanne tu hapa, zaidi yetu hakuna mwengine anayetuona wala kutusikia tuambie tafadhali" Alisema Mariam ambaye walipendelea sana kumuita Baby Merry.

"Mtoto koma mwengine yupo anayetusikia" Amina Alidakia maneno ya Mariam.

"Ushaanza nani anatuona hapa?" Aliuliza Mariam kwa kushtuka, Amina kidogo alikuwa shambenga asiyetaka kitu kimpite.

"Sir God, anaona hadi uvunguni kama hujui"

"Nilijua tu utasema hivyo, usilete matani wakati tupo ndani ya serious issue bhana, unaichukulia baridi hali ya mwenzetu?"

"Hapana kazi na dawa, kucheka kidogo kununa kidogo maisha yanaenda, baby Lucky tunaomba utuambie basi kitu gani kinakusumbua mamy, ujue kukaa na tatizo moyono si kutatua tatizo ee." Alisema Amina.

"Sina tatizo mimi Amina nipo kawaida."

"Tatizo unalo, ujue hapa chuoni kuna kamchezo kabaya kanaendelea japo kwa upande mwengine kazuri, tukikuona hivyo hatukuelewi tutaenda kushtaki kwa kiongozi wa chuo, bora utuambie sisi mpenzi umbea utabaki humu humu ndani" Alisema Amina huku akiwa amewaangalia wenzake.

"Nawaomba hali yangu msimwambie mtu yoyote, sihitaji watu wajue ninavyoishi tafadhali, haya ndio maisha yangu tokea nipo nyumbani" Alisema Lucky akiwa ameangalia chini, waliendelea kumshawishi ili awaambie kile walichokuwa wanakihisi toka kwake lakini wapi, mwisho waliamua kuachana naye wakimsihi sana abadilike laa sivyo watashindwa kuishi naye, upweke anaoweka hawauwezi kutokana na jinsi walivyozoea kucheka na kila mmoja.

Siku zilisonga mbele maisha ya Lucky yakiwa hayo hayo ya ukimya, muonekano wa msongamano wa mawazo na kujipwekesha na wenzake, ilifika sehemu wenzie anaolala nao walichoka ikabidi wamfate tena kumuweka chini lakini hakuna kilichobadilika. Jinsi alivyokuwa anakaa alifanana na msaka tonge anayesaka tonge lake katika wakati mgumu, wakati anatoka moja ya familia za kitajiri mno jijini Dar es salam.

Alivyoishi chuoni hapo Lucky. Aliwachukiza tu wale anaoishi nao chumba kimoja ila walimu wengi walitokea kumpenda na kumjumuisha katika daftari la wanafunzi bora mfano wa kuigwa na kila mmoja. Kipindi chote cha mwaka mzima alibahatika kupokea tuzo ya mwanafunzi msafi na mwenye nidhamu kuliko wote, hakuna alichoambiwa na walimu afanye akakataa labda kiwe kibaya, alikuwa mtiifu kuliko watiifu, upole huruma kwa wanafunzi wenziwe pamoja na muonekano wa kudeal na masomo wakati wote hata alipokuwa chumbani.

Wengi walipendelea mambo ya michezo wanapokuwa hawana ratiba yoyote ya masomo, au kutumia muda huo kwenda kula bata sehemu mbali mbali maclub na kwengine, lakini yeye aliutumia muda huo kupitia vitabu mbali mbali, baadhi ya wanafunzi wakawa wanamuonea wivu.

Tabasam kwake ndio kilikuwa kicheko, tofauti na wengine. Hakuna alichokihitaji zaidi ya kusoma, pale alipochoka alipanda kitandani kulala, lakini moja ya kawaida yake ambayo anao lala nao waliizoea, hawezi kulala mpaka machozi ya mawazo yamtoke, kitu kilichopelekea waamini huenda alipitia kipindi kigumu cha maisha ndio maana analia kila wakati, na ana maisha magumu kupita maelezo. Jambo ambalo lilikuwa sio sahihi.

Hakuna aliyeweza kujua kama Lucky anatoka kwenye familia ya kitajiri sana huenda kuliko wanafunzi wote chuoni hapo, hakuwa akijionesha kuwa kwao uwezo upo tena mkubwa, alionekana mwanafunzi wa kawaida kuanzia mavazi, misuko ya nywele na vitu alivyokuwa anatumia.

Familia yake yote ilikuwa ikiishi pembezoni mwa jiji la Dar es salam msasani karibu kabisa na bahari ya hindi, Mama yake aliyejulikana kwa jina la Jenipha alikuwa mganga mkuu katika Hospitali ya Muhimbili, kaka yake anayemfata alikuwa mmiliki wa makampuni matatu ya usafirishaji madini kwenda nje, huku baba yake mzee Edward akiwa mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa aliyekuwa na jina kubwa mno Africa mashariki ya kati.

Utajiri wa familia yake ulikuwa mkubwa kuliko hata wa viongozi waliokuwa madarakani. Iliishi kwa upendo muda wote, majirani waliiangalia kwa jicho la tatu namna inavyoishi hiyo familia, waliyatamani maisha yao wanayooneshana wakiwa nje, kitu kilichokuwa tofauti kwa mama mwenye nyumba Jenipha aliyekuwa anaiona bora jana kuliko leo, ila haikuonekana hivyo kwa majirani kwa sababu waswahili walishasema " usilolijua ni sawa na usiku wa kiza"

Maisha ya chuo kwa Lucky yalisonga mbele, Mariam, Tunu na Amina waliamua kumuacha kama alivyo, wao wakaendelea na ya kwao, walimtoa thamani na kumuona mjinga asiyejua kitu na huenda ametoka shamba ( kijijini) ndio maana anakuwa hachangamki, ila lililokuwa moyoni mwake hakuna aliyeweza kulifahamu kwa haraka, na alikubali kuonekana mjinga mbele ya wanaojiona wajanja ili maisha yake yaweze kusonga mbele..

"Rafiki yangu namuonea huruma sana huyu mwenzetu, yani anaishi kama mtu wa kijijini mshamba mshamba kimandazi mandazi hivi tu sijui yukoojee, yani ni kajitu tu kapo kapo sio hata kajanja kananiboa kama nini msiiiiu"

Asubuhi ya Jumatatu moja Lucky akiwa bafuni anakoga kujiandaa kuingia kwenye kipindi ambapo wao walishajiandaa, Tunu alisema na wenzake namna anavyomchukulia Lucky kwa kipindi hicho mbali na nyuma alivyokuwa akimueshimu.

"Si bora mandazi hayachachi? Ila achana naye mshamba tu huyo shoga yangu, ukimuita haitiki, ukimsemesha anajibu shoti, ukimuomba hiki mpaka atake, ana nini kwani hadi tumbembeleze bhana, uzuri wa kutuzidi hana, akituzidi sehemu nyingine tu lakini sio sura, na shepu pia tumepewa ana nini cha mno? Akwendege uko tufanye yetu tumpotezee aishi kivyake" Alidakia Amina.

"Mimi nilidhani mnanikalisha chini kusema vitu vya maana kumbe ni huyu tahira, achaneni naye bhana. Kila mmoja mzuri humu ndani hana cha kuringia na kila mtu nyodo anaziweza, ametunyodoa tumnyodoe basi kila mmoja ashike hamsini zake, tena sasa hivi niwa kupewa visa mpaka chumba akihame hiki asilete mambo meusi. Twendeni darasani tusije kukuta professa ashaingia yakawa mengine kisa kumuongelea huyu taka taka" Alidakia Mariam.

"hhhhhmmmmm!" Aliguna tunu. " kumbe na wewe umo?"

Walinyanyuka na kicheko kila mmoja akabeba mkoba wake na kwenda darasani. Lucky alitoka bafuni akiwa na khanga moja mwilini akakaa kitandani na kujifuta futa maji bila ya kujali kama kile kilichoongelewa dhidi yake amekisikia au laa, hakukaa dakika akanyanyuka na kusogea kwenye kioo kujiangalia mwili wake wote ulivyo. Alivuta mafuta aina ya lotion akajipaka baadhi ya sehemu za mwili wake, alipomaliza aliitoa khanga mwili ukabaki tupu kisha akavaa nguo za ndani zilizokuwa kwenye henga.

Alimaliza kwa nguo za chuo akabeba mkoba na kutoka ndani, hadi anafika darasani hakuna aliyeweza kumpa habari ya hellow! kwa sababu ya kusikojulikana sana na watu, kwa alivyokuwa anajiweka hakuna aliyeweza kumzoea kwani hata mbinu ya kumuingia haikuwepo, wapo wanaume waliojifanya midomo mirefu kutaka kuingiza mistari ya kumtongoza kutokana na uzuri wa mvuto aliokuwa nao kuanzia sura hadi maumbile, lakini walijikuta wanashindwa na kujionea aibu tu namna ambavyo Lucky hakutaka upumbavu.

Masomo yalipoisha wanafunzi waliokuwa wanamaliza vipindi walitoka madarasani akiwemo mwenyewe Lucky, mkoba wake ulikuwa begani bila kuongea na yoyote akashika njia ya kwenda kwenye chumba anachokaa, alisimama ghafla baada ya kusikia sauti ya kiume inamuita nyuma yake, aligeuka akakutana na sura ya mmoja ya wanaume ambao huwa wanamsumbua sana chuoni hapo kumuhitaji kimapenzi. Aliitwa Deniss.

"Samahani Lucky kwa kukusimamisha" Alisema Deniss akimtazama vizuri Lucky usoni baada ya kuwa tayari wamesimama wote wawili.

"Bila samahani"

"Leo tumebahatika kutoka mapema darasani, vipi tunaweza kuwa pamoja mchana kwa ajili ya kupata launch?"

"Hapana haiwezekani"

"Kwanini Lucky?"

"Sina sababu ila wewe jua hivyo, haiwezekani"

"Hivi unajua kuwa wewe Lucky ni msichana mrembo ambaye kila mwanaume hapa chuoni anakumezea mate? Ila sijawahi kukuona ukiwa na mchanganyiko wa mtu yoyote Yule kuanzia wanawake wenzio mpaka wanaume kwa nini? Nimekuwa nikikufatilia muda mwingi natamani kuwa sehemu ya maisha yako. Natamani kukujua zaidi Lucky tafadhali nikubalie tuwe na urafiki wa karibu wenye kuendelea pengine hapo badaye yanaweza kutokea makubwa zaidi baina yangu na wewe. Tafadhali Lucky"

Alifinya sura Lucky alipoona mtu aliyesimama naye anataka kumletea mazoea ya kijinga asiyoyataka kabisa.

"Hiyo ni moja ya sehemu za maisha yangu Deniss, ndio staili yangu niliyopanga kuishi, halafu usiishi kwa kukariri kuwa kila mwanamke aliyepewa uzuri lazima awe na mchanganyiko wa watu, uzuri wangu haumaanishi kila mmoja anayeniita niitike, heshimu mawazo yangu ili uwe salama nakuomba"

"Una maanisha nini?"

"Nakuomba tu usinisumbue, sipendi usumbufu usiokuwa na maana"

"Unataka kuniambia nikikusumbua itakuwa sehemu ya kuhatarisha maisha yangu?"

"Hautakuwa salama kwa asilimia mia moja"

"Nipo tayari Lucky nisiwe salama kwa asilimia mia moja ila naomba tuwe marafiki wa karibu tafadhali"

" Nisamehe"

Ulipita ukimya kidogo ulio ondolewa na Deniss.

"Ok Lucky, mimi nikutakie siku njema ila ningeomba kupata japo namba yako ya simu basi kama hutojali, nadhani nitajiona mwenye bahati sana"

"Samahani Deniss pia haiwezekani kupata namba yangu"

"Dah! Okey poa"

Lucky aligeuka na kuondoka zake huku nyuma akimuachia lawama nzito kijana Deniss namna alivyokuwa anatingisha mauno yake aliyojaaliwa na Mwenye Ezi Mungu, ni kama alikuwa anafanya makusudi, kijana huyo hakuweza kugeuka kirahisi hadi alipoona Lucky ameishilizia ndio aliweza kugeuka na kuanza kutembea mate yakimtoka, moyoni alikuwa na maumivu makali ya kukosa bahati ya kupata walau namba ya Lucky msichana aliyevutiwa naye tokea anajiunga naye siku ya kwanza darasani.

Lucky alifika chumbani kwake akaweka begi kwenye kiti akajitupa kitandani kidogo, alilala chali macho yakawa juu na kuingia katika wingu zito la msongamano wa mawazo, dakika kumi mbele tayari alikuwa anabubujikwa na machozi ambayo hakufahamu yanatokea wapi, yalikuwa ni machozi yaliyozungukwa na maumivu makali kutokana na kumbu kumbu zake za maisha, yaliuteketeza uzuri wote alionao usoni, marafiki zake anao kaa nao waliingia kipindi hicho hicho bila yeye kusikia hata mlango ukifunguliwa, huenda kutokana na kuwa mbali kimawazo, Tunu, Mariam na Amina walisimama vizuri mlangoni kumwangalia kwa makini, walipoteza zaidi ya dakika nzima wakashuhudia jinsi anavyobubujikwa na machozi na anavyoteseka, huruma iliwaingia wakamsikitikia kisha kumsogelea taratibu, Mariam alifika karibu naye akakaa pembeni yake na kumshika pajani, Lucky alisisimka, alishtuka akawaangalia na kuanza kufuta machozi.

"Why Lucky why why, why my dear friend why!" Alisema Mariam kwa uchungu, aliendelea. "Kwanini unatufanya kama watoto lakini, kwa nini unatufanyia vimbwanga vya roho Lucky kwanini, kwanini jamanii! Kitu gani kinakusumbua moyoni mwako hadi sasa? Si utuambie jamani mbona unakuwa hivyo? Unatuchukuliaje sisi? Unahisi sisi ni wanyama hatustahili kushirikishwa katika shida? Unahisi sisi ni watu makatili kiasi icho hatutoweza kukusaidia?" Aliuliza Mariam kwa hasira zilizoambatana na uchungu. Lucky alinyanyuka akakaa, sura yake ilijaa huzuni, ilijaa maumivu, ilijaa kila aina ya mateso ya maisha anayopitia.

"Hamna kitu Mariam" Alisema kwa ufupi akivutia mafua kwa ndani na sura yake kuielekezea chini kama mtu mnyonge asiyekuwa na haki yoyote, akamuweka katika kipindi kigumu cha kumkatili moyo Mariam.

"Dah! mimi ni rafiki yako Lucky, nakuomba usinifanyie hivyo nakupenda, mimi nakupenda Lucky, naumia sana ninapokuona katika hali hii sema kama unaumwa tukupeleke hospitali mbona marafiki zako tunakupenda sana why wewe huoneshi upendo kwetu jamaniii?" Aliongea kwa uchungu Mariam lakini Lucky hakuwa tayari kuongea chochote, Mariam naye alianza kulia baada ya kuona ni kama vituko wanafanyiwa na binti huyo wanayeishi naye chumba kimoja bila ishara ya kuonesha kabisa kuwa nao, Tunu aliingilia kati akamzuia Mariam kulia, walichukuana wote watatu wakatoka nje wakamuacha Lucky peke yake, walipofika nje walisimama na kuanza kushauriana nini wafanye juu ya rafiki yao huyo japo walishaamua kumtoa thamani ikiwa yeye haoneshi ushirikiano nao, ila hali waliyomkuta nayo ilibidi wabadili mawazo yao na kutafuta mbinu ya kumsaidia kumwondoa katika janga alilonalo.

"Kiukweli hali ya Lucky mimi inanichanganya sana siwachifi, yani bora kuishi na nyoka ikawa inakudonyoa tu huenda maumivu yataisha kuliko kuishi na mtu wa aina hii Akyamungu" Alisema Mariam.

"Mariam unajiumiza kichwa tu my dear friend, hadi machozi yanakutoka kabisa kwa mtu kama huyo?" Alihoji Amina.

"Sijafundishwa hivyo Amina, roho yangu ni nyepesi sana ninapomuona mtu anateseka kwa kitu kisichojulikana"

"Mimi nina wasiwasi Lucky ametokea kwenye maisha ya shida sana ndio maana yupo vile, au hapa mjini ni mgeni maana kila kitu hajiwezi, story hawezi, kampani hakuna, kicheko kwake hakijawai kuonekana, kuongea na mwanaume hapana, kuvaa hajui anavaa tu visasampure vya ovyo ovyo hajui kudamshi jamani! Yani ni kajitu kapo kapo tuuuu sijui hata! Sasa sisi tumchukuliaje? Ujue anazingua sana huyu demu e au mwangaa!?" Alisema Tunu akashika kiuno.

"Yani Tunu wewe acha tu anazingua zaidi ya sana halafu umegusia pointi nzuri, anaweza kuwa mwanga kweli waswahili wanasema muogope mtu mkimya, isije kuwa anatutoa ujungu usiku maana kuna siku huwa naota ndoto sizielewi elewi, ila nina wazo" Alisema Amina.

"Wazo gani? Aliuliza Mariam.

"Twende tukapeleke malalamiko kwa msimamizi, kiongozi. Tusikae nalo hili jambo yakaja kutokea makubwa zaidi ikawa shida, twende kwa kiongozi tumueleze moja mbili tatu nne, kama ni mwanga siku akitugeuza misukule tukawa hatuonekani ghafla hapa chuoni wajue ni yeye"

"Yani leo umeongea kitu kizuri wewe mshenzi, aidia nzuri sana hiyo, twende huko huko tumueleze kuwa mwenzetu hatumuelewi kabisaaaa tumpe A to Z" Alisema Tunu.

Wazo hilo lilipita kwa wote wakatoka taratibu hadi sehemu alipokuwa msimamizi wa wanafunzi wote chuoni hapo, alikuwa mwanadada aitwaye Sophia wakakaa chini na kuanza kumpa moja mbili tatu kuhusu Lucky, Lucky mwenyewe hakuwa anajua chochote wanachofanya watu anaoishi nao chumbani, alijipozea tu kitandani wimbi la mawazo likizidi kumtafuna.

"Dada Sophia tumeishi na mwenzetu Lucky mwaka sasa, lakini kwake hatujawai kuona kicheko, tabasam, furaha zaidi ya huzuni, kilio kisichoisha na ukimya basi, tunahisi atakuwa ana kitu kikubwa sana akilini mwake kinachompelekea kuwa hivyo. Ila sasa hali yake inatutesa, kama kuna uwezekano mhamisheni hata chumba chengine au kaa naye chini umsomeshe umpike akueleze kinachomsumbua, abadilike sisi hatuwezi kuwa na mtu wa aina ile, wewe mtu hatujui kicheko chake, tabasam kwake ni kama sikukuu, aka! sisi hatuwezi dada Sophia, pia tunamuonea huruma maana si usiku si mchana yeye kilio, kilio na yeye ndio nini sasa?" Alisema Amina akitumia zaidi ya dakika tatu kuongea, kila kitu kilichokuwa kinaendelea kwa dada Lucky alikiropoka mbele ya Sophia ili kuangalia kama uwezekano wa kutatua tatizo lake utakuwepo au laa.

"Mmekaa naye mwaka sasa katika hali hiyo, kwa nini hamkufanya hivyo kipindi cha nyuma mfanye sasa?" Aliuliza Sophia baada ya kumsikiliza Amina kwa makini.

"Sasa sisi tulikuwa tukimuangalia tu labda atabadilika lakini wapi habadiliki, imefikia sehemu tumehisi kama hajaharibika kisaikolojia basi ni mwanga" Alisema Amina.

"Mmejaribu kumkalisha chini kumweleza?"

"Ndio tena sii mara moja wala mara mbili"

"Okey sawa nimewasikia nitalifanyia kazi"

"Tena ukikaa naye mwambie kabisa tumechoka, tumechoka tumechoka tumechoka, wewe jitu halijui hata kucheka bhana" Alidakia Tunu akaongea kwa hasira.

"Sawa nimewaelewa rudini chumbani kwenu" Alisema Sophia kwa muonekano wa kuwa mkali kidogo, ila hawakushtuka ilikuwa kawaida yake, waliinuka kurudi chumbani kwao kabla ya kufika popote Tunu aligeuka.

"Halafu bora umwite sasa hivi uongee naye maana yupo analia huko chumbani, kinachomliza hatukijui"

"Naomba mrudi kwenye chumba chenu tafadhali"

"Tunarudi ndio ila uliambie! Tumeshachoka. Hatuendani naye hata kidogo yani"

"Rudini chumbani kwenu" Alikuwa mkali Sophia akasimama.

Hawakumsemesha jengine walitoka wakatembea hatua kadhaa ambazo ziliwafikisha mlangoni wakafungua na kwenda moja kwa moja chumbani, Lucky tayari alikuwa ashamaliza kulia muda huo alikuwa amekaa kitandani anajisomea, pia hawakushangaa kwani ilikuwa moja ya kawaida zake, walipita kila mmoja akapanda kitandani kwake wakatoa simu zao na laptop kwa ajili ya kuanza kuchart na kuperuzi katika mitandao mbali mbali.

Lucky aliwaangalia akatingisha kichwa na kuendelea kujisomea huku wao wakiwa wanachart, masaa yalisonga mbele siku ikaisha na kuingia siku nyingine, ilikuwa jumamosi kulikuwa hakuna anayeingia darasani, kila mmoja alichelewa kuamka isipokuwa Lucky alieamka saa moja na kuingia katika dimbwi zito la mawazo, mlango uligongwa akashtuka na kujiuliza nani anawagongea mlango asubuhi yote hiyo wakati dada wa usafi huwa anaingia saa mbili na nusu. Uligongwa tena akaweka khanga yake vizuri aliyokuwa ameiegesha tu mwilini kisha kuinuka kitandani, alisogea hadi mlangoni akafungua na kuchungulia nani anagonga, macho yake yaligongana na macho ya Sophia kiongozi wa chuoni hapo, woga ulimuingia mapigo ya moyo yakaamka akamkaribisha huku moyoni akijiuliza mbona Sophia yupo hapo kwa muda huo.

"Karibu Sophia"

"Asante nishakaribia mambo?" Alisema Sophia baada ya kukaribishwa.

"Poa."

"Nimekuharibia usingizi wako ee? Nisamehe mwaya"

"Wala! Nilishaamka zamani usijali kuhusu hilo"

"Mapema yote hii?"

"Yeah kuna masomo jana yalinichanganya kidogo ndio nilikuwa nayapitia, si unajua asubuhi kunakuwa hakujachanganya hivyo masomo yanaingia?"

"Ni kweli nalijua hilo, na wenzio vipi hao tayari au bado wameuchapa?" Aliongea akiachia tabasam.

"Wao bado wamelala"

"Okey poa, basi tafadhali nakuomba ofisini kwangu mara moja nina maongezi na wewe, samahani sana lakini" Alisema Sophia, Lucky akashangaa na kupokea mshtuko mwilini mwake.

.........
Muendelezo sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005

Maoni

You're not logged in


Tangazo - Sasa nakupenda fully episode
Sasa nakupenda fully episode
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SIMULIZI: LUCKY (SIHITAJI KURUDI NILIKOTOKA) SEHEMU YA 01

SIMULIZI: LUCKY (SIHITAJI KURUDI NILIKOTOKA)

SEHEMU YA 01

Mwaka mmoja ukiwa umepita tokea binti mwenye umri wa miaka 24 Lucky ajiunge na chuo kikuu cha Dar es salam ( University of Dar es salam ) maarufu kama UDSM. Marafiki zake aliokuwa anakaa nao chumba kimoja katika vyumba vya kulala wanafunzi chuoni hapo, waliojulikana kwa majina ya Mariam, Tunu na Amina. Asubuhi na mapema ya siku ya wikiend ya jumamosi waliamua kumkalisha chini rafiki yao huyo kwa ajili ya kuongea naye mambo flani mawili matatu kutokana na jinsi walivyokuwa wanaishi naye katika hali ya unyonge na kuonekana hapendi kushirikiana na mtu yoyote kimasomo...

πŸ‘‰ Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/simulizi-lucky-sihitaji-kurudi-nilikotoka-sehemu-ya-01

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama #fblifestyle #BeautyBattle #AfricaVsWorld #Tanzania #Kenya #Congo #Rwanda #Burundi #SouthAfrica #USA #VoteNow #DebateTime #Trending <br>

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu Β· dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi simulizi-lucky-sihitaji-kurudi-nilikotoka-sehemu-ya
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

*MY HOT PILOT* (rubani wanguπŸ”₯) EP 15.

*MY HOT PILOT* (rubani wanguπŸ”₯) EP 15.

373
SHAMIRA 82 MPK  86

SHAMIRA 82 MPK 86

322
SHAMIRA 87 MPK. 91      (SEASON FOUR)

SHAMIRA 87 MPK. 91 (SEASON FOUR)

252
SHAMIRA 79  MPK. 81.    (SEASON 4)

SHAMIRA 79 MPK. 81. (SEASON 4)

213
MY HOT PILOT* (rubani wanguπŸ”₯) 17 to 18 final

MY HOT PILOT* (rubani wanguπŸ”₯) 17 to 18 final

192
JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 7

JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 7

165
JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 6

JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 6

163
ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY 1 ---- 5

ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY 1 ---- 5

154
NAKUPENDA BILA  13 - 25

NAKUPENDA BILA 13 - 25

149
SHAMIRA 92 kwa 93

SHAMIRA 92 kwa 93

128

ZIMESOMWA ZAIDI

β€ŽTUNDA LA  DADA β€Ž β€ŽSEHEMU YA KWANZA

β€ŽTUNDA LA DADA β€Ž β€ŽSEHEMU YA KWANZA

11.78K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.5K
πŸ™„ NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWAπŸ”₯  sehemu ya tisa.  πŸ‘‰ Akaanza kunipamp sasa...πŸ‘‡

πŸ™„ NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWAπŸ”₯ sehemu ya tisa. πŸ‘‰ Akaanza kunipamp sasa...πŸ‘‡

3.85K
πŸ”₯ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯  Sehemu ya sita.  πŸ‘‰ Aaaaaaaaa chomoa...πŸ‘‡  Shemeji inauma utanichana.

πŸ”₯ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯ Sehemu ya sita. πŸ‘‰ Aaaaaaaaa chomoa...πŸ‘‡ Shemeji inauma utanichana.

3.34K
MY WANGU❀️ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGU❀️ sehemu ya 119 na 120.

2.95K
MY WANGU❀️ sehemu ya 108

MY WANGU❀️ sehemu ya 108

2.93K
MY WANGU❀️ sehemu ya 116 na 117

MY WANGU❀️ sehemu ya 116 na 117

2.76K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯  Sehemu ya 20.  πŸ‘‰ Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...πŸ‘‡

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯ Sehemu ya 20. πŸ‘‰ Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...πŸ‘‡

2.73K
MY WANGU❀️ sehemu ya 106 na 107

MY WANGU❀️ sehemu ya 106 na 107

2.67K
πŸ”₯ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯  Sehemu ya 16.  πŸ‘‰ nakupenda pia...πŸ‘‡

πŸ”₯ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoaπŸ”₯ Sehemu ya 16. πŸ‘‰ nakupenda pia...πŸ‘‡

2.6K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
MY HOT PILOT* (rubani wanguπŸ”₯) 17 to 18 final Post Mpya
MY HOT PILOT* (rubani wanguπŸ”₯) 17 to 18 final
@majario LIVE

* * MTUNZI: SMILE SHINE EP 17. Mikononi mwake nilikuwa sarama, siku ya ndoa, ilifika na vicram tulimualika na familia yake, kama wao walivyofanya, ila hii ndoa nilijua kupendeza jamani, nilipaka na Hina yangu...

SHAMIRA 92 kwa 93 Post Mpya
SHAMIRA 92 kwa 93
@majario LIVE

SHAMIRA Mwandishi; lissa wa huru media Sehemu ya 92 Basi bwana siku zikapita kidogo nikawa nipo apa naendelea na kazi zangu ili iki kitoto hapana . Kina tabia mbaya jamani mh...

NAKUPENDA BILA MIPAKA 26 - 35 Post Mpya
NAKUPENDA BILA MIPAKA 26 - 35
@majario LIVE

:26 Nikacheka na kusema β€œMuanko ana muda sasa, hacheki na yeyote, yaani tabasamu lake tangu nifike pale sijaliona dada hivi unanielewa.” Alinitazama akisema β€œeenh chaupole wangu nipe nipe.” Nilimtazama na kusema β€œwewe tena...

NILIKUTANA NA MAREHEMU MKE WANGU AKIWA KWENYE GARI LA TAJIRI MKUBWA  ​Episode 1 Post Mpya
NILIKUTANA NA MAREHEMU MKE WANGU AKIWA KWENYE GARI LA TAJIRI MKUBWA ​Episode 1
@majario LIVE

​Mvua ya rasha rasha ilikuwa ikidondoka jijini Dar es Salaam, ikichanganyika na moshi wa magari na kelele za wapita njia. Nilikuwa nimesimama kando ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi, nikisubiri...

BILLIONS OF LOVEπŸ’“πŸ’“   SEHEMU YA "6"πŸ’“πŸ˜½ Post Mpya
BILLIONS OF LOVEπŸ’“πŸ’“ SEHEMU YA "6"πŸ’“πŸ˜½
@majario LIVE

"BY BABIE LOVE" Basi bwana kakabaki ka laki na nusu nikasema hatakama kesho sipiki lazima tu niende road nikatafute chakuniinguzia pesa Mnakuja nn πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ vitoto vya mskini sisi akili ni...

JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 7 Post Mpya
JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 7
@majario LIVE

πŸ“ Mwandishi:lissa mwalla Reyhan kwel ananifanyia mm hiv?niliumia sana huku nikimuangalia ivan anaonfoka zake.reyhan akasema imeisha hio huwez nifanyia mm umalaya ww,unanijua unaskia?sasa uneshakua malaya kweli washkaj malizaneni nae m najikataa.aliongea huku...

NAKUPENDA BILA  13 - 25 Post Mpya
NAKUPENDA BILA 13 - 25
@majario LIVE

MIPAKA:13 β€œKeti tafadhali.” Nilimtazama, yeye hapo hata hajainua uso wake. Nilimeza mate nikaketi hapo moyoni najisemesha β€œwenye hela wana ringa jamani kwani si anitazame hata.” Nilipoketi aliniinua uso wake na kunikabidhi karatasi akisema...

SHAMIRA 87 MPK. 91      (SEASON FOUR) Post Mpya
SHAMIRA 87 MPK. 91 (SEASON FOUR)
@majario LIVE

πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€ SHAMIRA Sehemu ya 87 Mwandishi; lissa wa huru media Siku iyo sasa nimeenda kazini. Ile nimefika tu asubuh love akainiita mh nikaogopa nikahisi au nimeharibu sehemu.mana kufika na kufika nimeitwa.nijaenda kisha ...

JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 6 Post Mpya
JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 6
@majario LIVE

πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“πŸ“ Mwandishi:lissa mwalla Sasa hapo ndio nimekwisha sasa,uwiii,niliogopa nikamsukuma ivan,akasema nani huyo?nikasema ni ticha,akasema ticha wako ndio anakufata mpaka huku?mm nikatoa tu macho,ivan akasema subir hapa,nikasema sawa,akanyanyuka akavaa nguo akatoka mm name...

SHAMIRA 82 MPK  86   Post Mpya
SHAMIRA 82 MPK 86
@majario LIVE

(SEASON FOUR) (HURU MEDIA) πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€ SHAMIRA Sehemu ya 82 Mwandishi; lissa wa huru media Basi shoga yenu maisha yakaanza dodoma sasa. Nikawa nipo na kiakiba changu ndo kinanisapoti naendesha maisha mdogo mdogo. Apo...

ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY 1 ---- 5 Post Mpya
ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY 1 ---- 5
@majario LIVE

SEHEMU YA KWANZA Ni majira ya jioni ikiwa ni muda mfupi tokea ametoka bafuni kuoga kwa ajiri ya kujiandaa aweze kurudi nyumbani mara baada muda wa kazi kuisha, Isabela akiwa...

SHAMIRA 79  MPK. 81.    (SEASON 4) Post Mpya
SHAMIRA 79 MPK. 81. (SEASON 4)
@majario LIVE

(HURU MEDIA wababe wa hili Game) πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€ SHAMIRA Sehemu ya 79 Mwandishi; lissa wa huru media Nimawa nagoma kutoka .uku nalia nikawa nasema mama usinizalilishe plsss .yule mama akasema nisikuzalilishe nini...

*MY HOT PILOT* (rubani wanguπŸ”₯) EP 15. Post Mpya
*MY HOT PILOT* (rubani wanguπŸ”₯) EP 15.
@majario LIVE

Nilikaa na kimimba changu kilimpenda, king Yani akikawia tu kuludi nyumbani najikuta naanza kulia, mpaka majilani nawapa Malala Miko napita Kwa majilani Yani mpaka king aje ndo naakubali kulejea nyumbani,...

*BILLIONS OF LOVEπŸ’“πŸ’“*  "1__5" Post Mpya
*BILLIONS OF LOVEπŸ’“πŸ’“* "1__5"
@majario LIVE

SEHEMU YA "1"πŸ’“πŸ˜½ BY BABIE LOVE "Alikuja kama muuza chai kumbe ni BillioneaπŸ’΅" Nyie njooni niwaambie kitu ……… mnazijua chapati? Sambusa je ? πŸ˜‚πŸ˜‚ nani hazijui halfkeki ? Wote mnazijua ? Ona sikilizeni...

Nargis and Sunil Dutt were not just legendary stars of Hindi cinema, but also one of the most respected and inspiring couples in Bollywood Post Mpya
Nargis and Sunil Dutt were not just legendary stars of Hindi cinema, but also one of the most respected and inspiring couples in Bollywood
@majario LIVE

. Nargis was known for her natural acting and powerful screen presence. Films like Mother India made her a timeless icon, and even today she is remembered as one of...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest