YENYE KIRUNGU 💛 ❤️💚 SEHEMU YA 07
MR. AB
TULIPOISHIA
Piiiiiiiii, alipiga honi konda, nikasogea na kuchungulia vizuri, kweli ilikuwa kama nimetabiri hivi, nilimshuhudia Jerry anashuka kwenye pikipiki amevaa shati na suruali ya kitambaa akasogea
“Mke wangu Anita” Alisema Jerry huku akinifuata anikumbatie mimi nimebaki nimeganda kama sanamu sijui nifanyeje.
Alinikumbatia ila mimi sikuonyesha ushirikiano maana nilikuwa nina wasiwasi sana akiingia ndani itakuwaje maana atamkuta mwanaume mwenzake.
ENDELEA
“Mke wangu” Alisema Jerry huku akiwa amenikumbatia “Mbona hauna raha?” aliniuliza na kuniachia akaniangalia usoni mimi machozi yashaanza kunilenga lenga “Et baby” aliuliza na kunifuta machoni kidogo
“Why??? Why mume wangu why??” nilimuuliza kwa hasira huku nikiwa natafuta njia yoyote ya kumzuia asiingie ndani kwanza
“I’m sorry mke wangu.....najua kiasi gani unajisikia kwa kutokunipata hewani kwa muda wote huo.....nilipitia matatizo makubwa” aliniambia huju akinishika katika misuli yangu ya mikononi.
“No, sihitaji kusikia lolote kutoka kwako, naomba urudi huko kwa wanawake wako” Nilisema huku nikijitoa kwake na na kuwahi mlangoni ili nimzuie “haiwezekani ni karibia mwezi sasa sijui ulipo na haupatikani” nilisema lakini nia yangu ilikuwa kumzuia tu asije akaingia ndani akamkuta mwenzake
“Please mke wangu usifikie huko, I missed you, naomba niingie ndani tukae nikuelekeze” alisema
“Nooooo....nononono sihitaji wewe jiondokee tu” nilijaribu kumzuia, halafu nikaukamata mlango nataka nifunge niingie ndani halafu nikamtoe nje yule mwenzake kupitia mlango mwingine.
Jerry alinizuia kwa kutumia nguvu ili nisifunge mlango na alifanikiwa kuzuia, alikuwa na nguvu kuliko mimi, alipambana na mlango mi namzuia ila kwa bahati mbaya akaona raba za kiume sebuleni.
Zilikuwa za yule kijana mwingine ambaye yupo ndani.
“Wait....wait....wait...” Alisema kwa mshangao “Hizo...” alisema huku akinyoosha kidole kuzinyooshea zile raba “Hivyo viatu mbona.....ah” alisema kwa mshangao ameshahisi kitu tofauti.
“Uko na mwanaume ndani ndo maana unanizuia?” Alisema kwa hasira na kusukuma mlango kwa nguvu nami nikaishiwa nguvu akaingia ndani “Anitaaa” alinifokea huku akizivitazama vile vitabu
“Mume wangu” Nilisema huku nikiwa naogopa zaidi na zaidi mwili wote unanitetemeka.
Mume wangu alitoka pale kwa kasi ya ajabu anaenda chumbani kuangalia kama kuna mtu mwingine, ilibidi nimfuate nyuma.
“Jerry....please sio kwamb.....” Nilisema kwa huruma ninatamani ardhi ipasuke sijui la kufanya.
Nilishangaa Jerry aliingia chumbani na mimi nilimfuata nikiogopa atampiga kijana wa watu lakini tulipofika ndani nilikuta Mume wangu anachungulia kila mahali kutafuta mtu aliyeko ndani, wakati mimi namuona kabisa yule Jerry Feki ameketi kwenye kochi la chumbani anamtazama kwa tabasamu
Ghafla Jerry mume wangu alitoka ndani ya chumba na kuelekea bafuni na chooni akatazama, halafu akatoka na kucheki kila chumba huku akinitukana na kuniambia maneno mabovu sana ya kashfa
Alirudi tena chumbani akasimama mbele yangu, mi namuangalia, kisha namuangalia yule mwenzake anacheka, nikashindwa kuelewa
“Niambie ukweli” Alisema Jerry
“Ukweli gani mume wangu?” niliuliza
“Vile viatu vya nani?” alisema huku akikagua chumbani zaidi “Nambie” alinifokea mara tena akaona begi la kijana yule akalivamia “Na hili begi la nani?” aliniuliza lakini mimi kimya bado nashangaa na kujiuliza ina maana hamuoni?”
Jerry alilibeba lile begi akaenda kuketi nalo pale pale mwenzake alipo, kama vile alikuwa anamkalia lakini kijana yule alipotea paap na kutokea katika kitanda akaketi.
Mume wangu alifungua lile begi huku anajaribu kuangalia kilichopo ndani, alitoa nguo zilizokuwepo akazitupa chini
“Anitaaa!!!” alifoka “Niambie hivi vitu ni vya nani?” aliniuliza kwa hasira
“Mume wangu mimi sijui” Nilimjibu
“Hujui kivipi? Eeh huju....daah?” Nilishuhudia akitokwa na machozi ndipo akalipiga begi chini puuh
“Kwa hiyo limetokea lenyewe humu ndani?” Aliuliza Jerry kwa hasira
“Hata sielewi kweli Jerry sijawahi kukusaliti...”
“Usiongee ujinga” Alisimama anataka kunipiga mara akapiga teke kwenye zile nguo, puuh kwa hasira, nikashuhudia hirizi jekundu limeruka na kudondoka mbele yangu linawaka waka.
Jerry alilitazama huku akihema kwa hasira ila alipolitazama kwa muda niliona kama amelishangaa na kurukia hirizi ile.
Aliibeba na kutazama hirizi kweli inang’aa alipotazama hivi Jerry alishtuka sana na alianza kulia
“Hapana.......hiiiii hapana....this can’t be happened......hihihiiiii aii” alisema akilikumbatia hirizi lie
“Jerry....” Nilimuita kwa mshangao “Umepatwa na nini?” Niliuliza na kumshika, alilegea na kupiga magoti chini analia
“Aaah......Nooo daah” Alisema Mume
Niliinua macho nikamtazama yule kijana ambaye alikuwa yeye hamuoni. Kijana alinionyesha ishara kwamba nikae tu kimy. Sikuelewa kinachoendelea.
Nilisubiri kama dakika kadhaa Jerry aliinuka macho mekundu akanikumbatia
“Nisamehe mke wangu, sikujua....” Alisema Jerrt mume wangu
“Nini mume wangu?” niliuliza lakini Jerry aliukamata mdomo wangu tayari kwa Romance alionekana amenimiss sana. Lakini nilikuwa namuonea aibu yule mwenzake ambaye alikuwa pale ndani bila yeye kujua
“No, usifanye hivyo hapa” Nilisema
“Kwanini?” Jerry aliniuliza ila kabla sijajibu yule mwenzake alinionyesha ishara ambayo sikuelewa kitendo kilichofanya nikaropoka na kumuuliza
“Unamaanisha nini?. Nitumie meseji” Nilisema maneno yaliyomshtua Jerry
“ee? Meseji? Unaongea na nani?” Jerry aliniuliza
“Noo baby sorry” Nilisema na kumkumbatia tena
Jerry aliendelea kuninyonya ulimi ndipo ghafla yule mwenzake akaondoka kwa hasira kuelekea mlangoni
HAKIKA SIKUELEWA NIFANYE NINI
JE NINI KITAFUATA? KWANINI JERRY AMEONA HIRIZI AKASHTUKA?
MIMI NA WEWE HATUJUI SABABU, HUENDA TUKAIPATA KATIKA SEHEMU YA 08
USIKOSE
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni