"Weee unaumwa kwani??" Mama Recho akamuuliza
Qassano aliwasalimia na wote wakabaki wanamshangaa midomo wazi Recho akam-bonyeza Vicky anamuuliza kwa ishara huyu nanii??
Vicky hakuwa anaweza kujibu mana Mr Qassano hakuwa mbali na yeye ,
Mr Qassano alifungua Gari akatoa vitu vya Vicky ni ule mfuko wa nguo
"Chukua mizigo yangu" Recho akachukua mizigo huku ana sintofahamu nyingii kichwani
Vicky akawaweka chini wote akawaaambia kila kilichomkuta,Mr Qassano akabaki kuomba msamaha kwa mama Recho akiamini ndie mama mzazi wa Vicky na ndio hivyo alitambulishwa
Vicky akasema usijali kila kitu kimeisha nashukuru kwa msaada wako
Qassano akamwambia sawa nashukuru nimepajua nyumbani lolote litakalo tokea nijuze
Ndio Qassano akakumbuka alimchukulia simu bila Laini ooh akasema nitajitahidi nikueletee laini ya simu
Vicky akamwambia hapana Nitasajiri tu usijali
Qassano akamwambia nafanya kwa ajili ya mtoto kwahiyo niache, Vicky akacheka kama kawaida, Qassano alikuwa ashapata cha kusingizia tayari .
Akamwambia umepata matatizo ukiwa upo kwenye majukumu yako , na Ujauzito wako ni mkubwa huu kwahyo kwa kipindi hichi naomba utulie mie nitajumuika na kila kitu mpaka utakapo jifungua usitoke nyumbani kama sio lazima utokee"
Vicky alishtuka akamtazama mama yake na Recho pamoja na Recho kwa zamu ,kisha akamtazama na Mr Qassano
"Hapana ,Acha basiii Mr Qassano please inatosha sio makosa yako jamani"
"Kaka anguu kama umeamua wewe kumsaidia msaidie huyu bint anateseka sanaa lakini muda wote anajifanya yupo sawa ,Madhali hujalazimishwa msaidie tu baba yangu"
Mama Recho alimuwahi Vicky baada ya kuona anakataa msaaada wake, Vicky alikataa sana lakini mama Recho akaweka ngumu
"Na ukikataa nitamwambia kila kitu kuhusu maisha yako hapaa ili akuonee huruma vizuri "
Vicky hakuwa tayari mambo yake kila mtu asikie akakubali tu kishingo upande
Mr Qassano kuna kitu kiliongea na akili yake haswa baada ya kauli ya mama Recho hakutaka kuonesha kama amejali sanaa lakini moyoni aliijali ile kauli ila akawaza huu sio muda sahihiii
Baada ya kukaa muda mrefu sana nyumbani kwa kina Vicky ndio akaaga kuondoka .....
Rahul alimpigia simu Mr Alberto baada ya kuona umekuwa muda mrefu mtu haji
"Boss muda wa kikao umefika bado lisaa moja tu unatakiwa kuwa hapa kiongozi " Rahul aliongea kwa kulalamika
Mana Boss wake Tangu amefika Ratiba zake hazieleweki kabisa
"Yeah naelewa nipo njiani ,sikupata nafasi ya kwenda kwa masha Sijui atanielewa??"
"Boss huyo mwanamke yupo hapa ofisini ,Kuwa makini na wanawake wa huku ujue"
"Hahah usijali Rahul I'm on my way"
Aliikata simu akanyoosha njia kuelekea Bagamoyo Sehemu ilipo Studio yake ...
*******
Masha alichoka kusubiri nyumbani alikua na hamu ya kumuona Mr Alberto mana hajawahi kumtia machoni zaidi ya kuona picha ama kuongea nae kwa video call WhatsApp
Sasa Tangu asikie amekuja Tanzania hajawahi hata kumtafuta kwenye simu ,wala kuja nyumbani kwake , leo akaona wacha amfate huko huko Ofisini kwake
Gari ya Mr Alberto inafikaa Masha alikua wa kwanza kuiona alikimbia mbio za haswa mpaka mlangoni akasimama kabla hata Gari haijasimama vizuri
"OMG!!!kumbe ni mzuri kiasi hichii kuliko hata kwenye picha. Asante munguu"
Wakati mr Alberto anashuka Masha akajisemea moyoni
Akamkumbatia huku analiaa
Mr Alberto nae alimkumbatia Masha
"Noo!! Usilie tafadhali"
"Kwanini hukunambia kama unakuja nije kukupokea??"
"Sikutaka kukusumbua that's why "
Rahul akafika muda huo huo , Mr Alberto alimtoa masha kifuani kwake
"Ni muda wa kikao Tafadhali nenda nyumbani nitakuja"
Masha alikasirikaa ujio wa Rahul alinuna lakini akajichekesha
"Nakusubiri,wahi nyumbani please "
"Okay, Mhuu Rahul nipe Ratiba"
Aliachana na masha akaanza kuongea na Rahul huku wanaondoka kuingia ndani ya ukumbi wa kikao chao walichoandaa na baadhi ya wawekezaji wengine kwenye kiwanda cha Sanaa Tanzania
Itaendelea.....
Muendelezo saa 10 kamili jion.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.