CHUO CHA MIHEMKO SEHEMU YA 12
SEHEMU YA 12
---
Siku iliyofuata ilianza kama kawaida, lakini ndani yangu haikuwa kawaida hata kidogo.
Ujumbe ule wa usiku bado ulikuwa unanifanya nione sura ya Teddy kwa jicho la pili.
Ile sauti ya kutokuwa na uhakika ilinibembeleza kichwani:
“Neema usiwe wa kuaminia mapenzi kirahisi… kumbuka ulichojiambia kabla hujaingia chuo…”
Nilijaribu kupotezea, nikajifanya niko sawa, lakini moyoni kuna kitu kilikuwa kinatamba hofu ya kuumizwa na mtu uliyeanza kumuamini kabla hata hujampa nafasi ya kukudanganya.
Siku hiyo tulikuwa na group discussion pale old library. Nilipofika, Teddy tayari alikuwa ameketi kwenye kona tuliyokubaliana.
Alinikaribisha kwa tabasamu ile ya kutuliza vita ya ndani.
Nikaketi naye, lakini tofauti na siku zingine, sikuwa na ile mood ya kumsogelea wala kumchekea.
Alinisoma fasta.
“Upo poa leo?” aliuliza kwa sauti ya taratibu.
“Poa tu,” nikamjibu huku nikiwa najiuliza kama ni kweli.
Tulimaliza discussion kwa utulivu, lakini kabla sijaondoka, akaniambia kwa sauti ya chini:
“Naomba dakika zako kumi tu. Sitaki kuondoka na maswali moyoni mwako.”
Nikasimama kimya. Niligundua ameanza kusoma dalili.
---
Tulijipenyeza mpaka maeneo ya garden ya faculty ya arts, pale ambapo watu hawafiki sana.
Akaanza kuongea.
“Neema, najua umepokea ujumbe. Nilitabiri hilo. Kuna watu hawataki kuniona na mtu yoyote mpya. Wanaona nikiwa na wewe ni kama najisahaulisha yaliyopita.”
Nikamtazama.
“Yaliyopita yapi Teddy?”
“Sitaki kukuficha. Niliwahi kuwa kwenye mahusiano na msichana aliyenifanya niamini mapenzi ni vita. Tulinuniana, tukagombana, tukajaribu kuokoa kilichovunjika... lakini mwisho wa siku, tulitoka kila mmoja na majeraha yake. Wengine waliona mimi ndiye chanzo cha machungu, wakaanza kuniandama kimya kimya.”
“Na huyo msichana yuko hapa chuo?”
“Ndiyo, mwaka wa tatu, anaitwa Amanda.”
“Amanda gani?”
“Amanda wa BBA.”
Nikameza mate. Amanda? Yule mrembo mwenye followers 15k Instagram?
---
Basi hapo moyo wangu ukachanganyikiwa zaidi.
Huyo Amanda nilikuwa namjua mwanadada anayejulikana chuoni kwa jina la “Fashion Killer.”
Sasa nikawa najiuliza:
“Iweje mtu kama Amanda akosee kuchagua mwanaume sahihi? Huyu Teddy ana nini cha kipekee au cha hatari?”
Lakini pia nikawa najitetea: “Kosa la mmoja si kosa la wote.”
Teddy alinishika mkono, kwa mara ya kwanza kwa ujasiri wa mtu anayejua hofu yangu.
“Sitaki ushindwe kuniamini kwa sababu ya mabaya ya nyuma. Siwezi kujisafisha kwa maneno, lakini naweza kukuthibitishia kwa vitendo kama utanipa nafasi.”
Nilimtazama. Nikamwona mtu aliyebeba mzigo wa hatia za zamani lakini bado ana tumaini la kesho.
---
Usiku ule, nikiwa kwenye room yangu, nilipokea message kutoka kwa Amanda.
Amanda:
“Neema, sikutegemea kama na wewe utakuwa wa aina hii. Kumchukua mtu ambaye hakuweza kunipenda ipasavyo siyo ushindi. Ni kama kubeba boksi la glass lililovunjika.”
Nikakaa kimya. Sikutaka drama, lakini sikutaka pia kusemwa kimyakimya.
Nikajibu:
“Sikuchukua kitu cha mtu. Huu si ushindani. Kila mmoja anapendwa kwa namna tofauti. Kama yeye hakukupenda ipasavyo, haimaanishi hata wengine atawafanyia hivyo.”
Amanda hakujibu. Ila hiyo message ilitosha kuniweka kwenye orodha ya ‘wasiohitajika’ katika ulimwengu wa fashionista huyo wa chuo.
---
Siku zikasonga.
Teddy aliendelea kuwa karibu nami.
Alikuwa ananipikia chai ya maziwa hostelini kwetu, akileta na maandazi aliyotengeneza mwenyewe.
Alinifundisha namna ya kutumia Excel vizuri na akanisaidia kuandika CV yangu ya kwanza.
Kila siku alinipa sababu mpya ya kumuamini, lakini sauti ile ya nyuma bado haikunyamaza.
Kila nikipata utamu, kuna kitu kilikuwa kinaniambia:
“Ukishazoea, ndio watakuharibu.”
---
Siku moja, nilipokuwa nikienda kununua vocha cafeteria, nikasikia wasichana wawili wakiongea nyuma yangu:
“We unajua Teddy alikuwa na scandal na lecturer mmoja wa kike mwaka jana?”
“Umeambiwa na nani?”
“Mbona ipo wazi. Yule lecturer wa media studies. Alimpa Teddy A halafu story zikasambaa. Ila walinyamaza kimya kimya.”
“Wanaume kama huyo sio wa kuamini, anajua kucheza akili za watu.”
Nikashtuka.
Nikajikuta nasimama ghafla, moyo ukidunda kama ngoma ya maombolezo.
Sasa tena scandal na lecturer?
---
CHUO CHA MIHEMKO - SEHEMU YA 13 inakuja hivi punde:
Neema anaanza kuchokonoa ukweli wa Teddy.
Ni kweli alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na lecturer?
Na je, Amanda alikuwa akisema ukweli kuhusu heartbreak?
Je, Neema ataendelea kusimama na Teddy au moyo utamkimbiza mbali na penzi lenye kivuli cha mashaka?
Tukutane kwenye sehemu inayofuata – "Ukweli wa Chumbani na Hadaa ya Maksi."
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi




Maoni