Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

CHUO CHA MIHEMKO SEHEMU YA 9

30th Nov, -0001 Views 53

CHUO CHA MIHEMKO

SEHEMU YA 9

Ronnie, ah! Huyu jamaa alikua kama bahasha yenye barua nzuri nje umependeza, ndani una ujumbe wa moyo.
Tangu alipojitokeza kwenye ile party, kila kitu kikawa kama kimetulia… angalau kwa nje.
Lakini moyoni, bado kulikuwa na mdundo wa maswali:

"Je, huyu si mwingine tu kama Adam aliyevaa ngozi ya fadhili?"

Lakini jamani, moyo wa mwanamke ni kama plastiki ya nailoni unayeyuka kwa moto wa maneno matamu.
Ronnie hakusema mengi, lakini kila alichokisema kilikuwa kina timing, kina uzito, na kina direction.

Siku moja alinipigia nikiwa darasani. Nika-text: “Nipo lecture, nikutafute baadae?”
Akanijibu fasta: “Sawa, focus baby girl… elimu kwanza, emotions zifuate.”
Nikacheka kimya kimya.
Huyu mtu alikuwa anaongea lugha ya mwili wangu kabla hata hajau

Siku ya Jumatano, alinialika kwenye picnic.
Mitaa ya Njiro, bustani ya kisasa, maua, muziki wa taratibu na vibes za starehe.
Alikuja na kikapu cha chakula, mistari ya kutosha na ile harufu ya kiume inayomfanya msichana ajisikie salama bila hata silaha.
Tulikula, tukacheka, tukazungumza mambo ya maisha, siasa, na ndoto.

“Neema,” aliniangalia machoni kama mtu anayepima kina cha roho,
“Najua haujapona kabisa. Na sitaki kuwa dawa, nataka kuwa hewa — kitu usichohitaji kupona ili uendelee kuishi.”

Mimi? Nikaishiwa maneno.
Nikatabasamu kama binti wa mjini anayejua penzi halali limemvizia.

Lakini chuo sio paradiso.
Na kila safari ya furaha huwa na kivuli chake.

Siku moja, nikiwa nimetulia hostel nikipiga Netflix, Mwanaisha akanigongea mlango kwa nguvu.

“Neema! Fungua haraka!”
Nikadhani labda moto umetokea. Kufungua mlango, akanirusha na simu:
“Tazama hii!”
Nikachukua simu, nikaiangalia video ya Ronnie yuko kwenye club, akimshika kiuno demu mrembo wa Law School, anayeitwa Debby, wakicheza kimahaba hadi watu wakaanza kupiga video kwa kisiri.
Caption ya mtu mmoja kwenye WhatsApp:
"Sema tena anampenda Neema, kumbe usiku ni DJ wa mioyo ya wengine."

Nilikaa kitako nikiwa kimya.
Si kwa sababu ya kushtuka, bali kwa sababu nilikua nimeanza kuzoea maumivu haya.
Ya kuwa na matumaini halafu yachomwe kama picha kwenye moto wa wivu.

Nilimpigia. Simu ikaita mara mbili, akaipokea.
Sauti yake ilikuwa tulivu kama kawaida:

“Hey baby.”
Nikamjibu, “Still unaniita baby hata baada ya video ile?”
Akakaa kimya kwa sekunde.
“Neema, hiyo video sio kama inavyoonekana…”
Nikamuuliza: “Sio wewe huyo unamshika kiuno?”
“Ni mimi, lakini”
Nikakata simu.

Mwanaisha akaniuliza, “Utafanya nini sasa?”
Nikamjibu, “Nitakaa kimya, nitajifunza.”

“Na moyo wako?”
Nikamuambia, “Moyo wangu hauna bima ya mapenzi… ila nitapambana.”

Siku ya Ijumaa, nilivaa suruali ya jeans iliyonikaza kama swali gumu, top nyembamba, nikajiremba, nikachukua kitabu changu cha Ethics nikasogea Library.
Kama kawaida, midomo ya watu haikosekani.

“Yule wa Adam.”
“Yule wa Ronnie.”
“Yule wa video.”
Lakini nilitembea kifua mbele, nikiwa najua kitu kimoja chuo ni darasa la kila aina ya somo: la mapenzi, la kuvunjwa, na la kuamka ukiwa mpya.

Na siku hiyo, nilianza kuandika ukurasa mpya.
Nilikaa, nikajibu maswali ya Ethics, huku nikijifunza Ethics ya moyo wangu.

Ni wakati wa kupenda tena, lakini kwa akili.
Kupenda kwa hisia, lakini na mipaka.
Na kujiweka mbele kabla ya yeyote.

Nachelewa kwasababu ham like, gonga like uone kama soketi mapema kabisa, haya sasa kimbiza like zifike 100....

Kama haupo kwenye page yangu basi jiunge, kama zikifika like 100 kwenye page mnaweka mwendelezo mapema sana, na kama tukienda mwendo wa haraka tutafika final chap..
Kama haupo kwenye page yangu Facebook basi fursa hapa kisha follow page yangu Facebook..
????????????
Layman Donsue Simulizi.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

CHUO CHA MIHEMKO SEHEMU YA 9   >>> https://gonga94.com/semajambo/chuo-cha-mihemko-sehemu-ya-9

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest