CHUO CHA MIHEMKO
SEHEMU YA 15
---
Siku ya safari ilifika. Mabasi mawili ya chuo yakajaa wanafunzi wa Debate Club, baadhi wakiwa wamevaa rasmi suti zao, wengine casual lakini na confidence usoni kama wanasiasa wa opposition.
Mimi nilikaa kiti cha nyuma karibu na dirisha, nikishikilia notebook yangu yenye nukuu za points kali. Nilivaa top nyeupe ya shingo-funga, sketi ya jeans na viatu vya sport. Nilionekana kama Neema mpya msomi, mrembo, lakini anayejua ku-balance akili na feelings.
Wakati bubu wa mawazo akinitembelea kwa mbali, nikasikia vibration ya simu yangu:
Teddy: “Najua unazidi kung’ara. Kumbuka you’re not just representing chuo, unaniwakilisha mimi pia. Nakupenda Neema.”
Nilikaa kimya sekunde kadhaa kabla sijamjibu. Mapenzi hayapimwi kwa ujumbe mmoja wa maneno matamu. Lakini maneno yake yalinisisimua kama ka-AC ka hostel kazima kwa bahati mbaya.
---
Tulifika Dodoma mida ya saa kumi na moja jioni. Tulipokelewa na wanafunzi wa chuo wenyeji kwa mbwembwe za kutosha. Nikakutana na Maimuna mwanafunzi wa sheria kutoka chuo cha wenyeji, ambaye alikuwa mshindani wangu wa debate.
“Nimekusikia Neema... wewe ndo Rising Star wa Mbaya University?”
“Naam, ila nyota zangu zikiwaka usije ukachomeka.”
“Haha! Basi tutawaka wote, bora kushindana kuliko kuogopana.”
Maimuna alikuwa mzuri, mrefu, na mwenye confidence kali kama vile anakula hoja kwa kifungua kinywa.
---
Usiku huo tulienda kulala katika hostel ya muda, ambapo wasichana tuligawanywa vyumba viwili. Nililala na Asha msichana wa mwaka wa pili, mwenye ndoto za kuwa mwanasiasa.
“Neema, usidanganywe. Debates ni siasa. Ukishinda leo, ushawahi kufungua milango ya connections. Tumia nafasi hii.”
“Sawa Asha, lakini moyo wangu bado uko nyumbani.”
“Kama ni wa mwanaume, tafadhali uache hostel. Hii ni safari ya mafanikio, siyo picnic ya feelings!”
Tulicheka, lakini nilijua maneno yake yana uzito. Nilielewa kuwa huu ulikuwa wakati wa kupambana si kupendapenda.
---
Kesho yake mjadala ulianza. Ukumbi ulijaa. Kamera zilikuwa zikiwaka, na waamuzi walisimama kwa ustadi.
Topic: “Social Media Does More Harm Than Good.”
Neema upande wa kupinga.
Maimuna upande wa kuunga mkono.
Saa ya kupambana ilifika. Niliposimama kutoa hoja zangu, moyo ulinitetemeka mwanzo, lakini baada ya sentensi ya pili, confidence ilirudi kama nishati ya jua mchana.
“Mitandao ya kijamii imewapa vijana sauti. Kama ingekuwa ni madhara tu, basi hata hii debate usingesikia kuhusu mimi kabla sijafika Dodoma.”
Watu wakapiga makofi. Nikaongeza pointi nyingine juu ya elimu, ajira, na ushawishi mzuri.
Maimuna naye alikuwa moto. Alitumia mifano ya visa vya kuharibika kwa ndoa, kupoteza muda na uongo mtandaoni. Ukweli ni kwamba, ilikuwa vita kali ya hoja.
Baada ya rounds tatu, majaji wakatangaza washindi…
“Timu ya Neema – Mbaya University, mmeshinda kwa hoja thabiti na uwasilishaji mzuri.”
Watu wakapiga makofi. Nilihisi nguvu mpya, heshima mpya. Lakini furaha hiyo haikudumu sana.
---
Usiku ulipofika, nikiwa napanga notebook yangu, Doreen alinipigia:
“Neema, kuna kitu nimeona... na sidhani kama utakitaka.”
“Sema tu Doreen.”
“Amanda ameweka picha kwenye status yake, yuko club na... Teddy wako.”
“Wewe unatania?”
“La hasha. Wamekaa karibu. Caption yake ni ‘Vitu vya zamani vikikumbusha kumbatio.’”
Simu yangu ilinishika butwaa. Nilitamani kusema siyo kweli, lakini moyo ulianza kubisha hodi ya hasira.
Nilifungua status ya Amanda kwa line ya WiFi niliyochukua kwa mdada wa reception.
Picha hiyo ilikuwa halisi. Teddy yupo, Amanda yupo. Meza ya vinywaji ipo. Ukaribu wao hauna ubishi.
---
Niliumia. Nilikaa kimya, nikiwa nimebanwa na maswali elfu kichwani:
Je, ni kweli Teddy anarudi kwa Amanda?
Ni kiki au ni kumbatio la ukweli?
Nilishinda debate, lakini naonekana kushindwa kwenye mapenzi.
Na je, huu ni mwisho wa safari yangu na Teddy, au ndio mwanzo wa kujua ukweli wote?
---
SEHEMU YA 16 INAKUJA HIVI PUNDE:
Neema akarudi chuoni akiwa na ushindi wa kitaaluma lakini majeraha moyoni...
Je, atakabiliana na Teddy?
Amanda ana mpango gani tena?
Na je, kuna sura mpya inayokuja kuibadilisha game?
Umejipanga? Nikupige Sehemu ya 16 sasa hivi?
Haya gonga like hapo na uniambie kwenye commentn chochote....