๐ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO ๐ 16 -- 17
SEHEMU YA 16
Denis hakujibu kitu alikata simu ๐ฑ hapo hapo nilishikwa na machungu ๐ sana nilifuta namba yake kwa hasira๐กnikaanza kulia ๐ญ kilichokuwa kinaniumiza zaidi ni kuachwa bila kutarajiwa halafu mtu anayemchumbia ni mtoto wa mama yangu wa kambo ada bado sijamaliza sijalipa na kodi inaisha mbona patamu wahenga walisema siku ya kufa nyani miti yote huteleza .
Niliwaza hadi nikapitiwa na usingizi nilikuja kuamka asubuhi muda wa kwenda chuoni uzuri sikupanga mbali sana nilijiandaa taratibu nikaenda chuo.
Nikiwa nawahi maana nilichelewa sikuliona gari ๐ lilikuwa linakuja nalo chuoni maisha bhana wengine wanakuja na magari basi bhana lilinigonga likanidondosha pembeni nikawa nimechubuka kidogo kwenye mguu alishuka mdada mmoja ambaye nasoma nae na sinaga mazoea naye hata siku moja anaitwa Gladness akaja hadi nilipoangukia huku na watu wengine wakisogea sogea.
Sorry umeumia sana nikupeleke hospitali ๐ฅ yule dada aliniuliza huku akinipa mkono nisimame . Hapana sijaumia nilitaka kusimama lakini nilishindwa . Ngoja tu nikupeleke tu hospitali๐ฅ , watu walinisaidia kuniingiza kwenye gari ๐ yake akanipeleka hospitali kutibiwa.
Tulifika hospitali nikapokelewa na wauguzi nikapelekwa kwenye chumba mara akaja mkaka ilionekana wanafahamiana na Glad , Ushafanya maafa gani tena umenitoa kikaoni sasa hivi. Kaka nimemgonga mwanafunzi mwenzangu bahati mbaya i need your help , Sawa yule kaka alinitibia mguu ulikuwa umeteguka . Utaendelea vizuri shida haikuwa kubwa apumzike tu na wewe G naomba siku nyingine uwe makini nitakupokonya hilo gari ๐ utaniletea kesi kwa baba wakati alinikataza nisikupe. Samahani kaka halitojirudia , Sawa mnakula nini niwaletee .
kaka chips na kuku tu Glad alijibu yule kaka aliondoka .
Tunasoma darasa moja ila sijawahi kuwa karibu na wewe mbona kama una stress maana nilipiga honi hujanisikia una shida gani ๐ค Glad aliniuliza , Asante kwa kujali naomba unisaidie nipate kazi ili niweze kumudu maisha yangu sina msaada wowote ule nadaiwa ada na kodi sijui hata natoa wapi ? Pole aliyekuwa anakulipia mwanzo imekuaje ๐ค amekataa kulipa tena ana majukumu mengi sasa hivi.
Aisee pole ngoja nijaribu kukutafutia kazi unaitwa nani mwenzangu . Naitwa Nelly , ooh jina zuri mimi ni Gladness aliyekuhudumia ni kaka yangu wa tatu kuzaliwa akitoka yeye ndio nafuatia mimi yeye ni daktari wa hapa imekuwa kama bahati anahusika na mifupa . Nimefurahi kumfahamu mara chakula kililetwa tu na mtu na hivi nilikuwa sijala toka asubuhi ๐ nilikula sana . Mida ya jioni niliruhusiwa Glad alinirudisha hadi ghetoni kwangu ile nimeshuka tu mwenyenyumba ๐ก alikuwa amekuja kudai kodi yake maana ilibidi nimpe toka jana muda huo Glad alikuwa hajaondoka bado.
MWISHO WA KIONJO
17
Nimekuja muda kweli sijakukuta na leo ndio ulinihaidi unanipa hela ya kodi . Dada ni kweli ila naomba unipe siku mbili nitakupa hela yako nilipatwa na matatizo nimetoka hospitali sasa hivi si unaona nina bandeji kwenye mguu.
Hilo mimi sijali mama yangu anaumwa anahitaji pesa ya matibabu halafu na wewe unanipa sound huna hela toka nipangishe mwingine . Mtoto wa mwenyenyumba ๐ก alikuwa mkali kama kalamba pilipili kichaa Glad alishuka kwenye gari ๐ , Dada samahani lakini si umemuona mwenzio ni mgonjwa . Sijakupangisha wewe kaa kimya, mhh Glad aliguna kwani, unamdai kiasi gani dadam? Glad aliuliza namdai kodi ya miezi minne laki mbili .Sawa nitajie namba yako nikurushie kwenye simu sina cash yule dada alitaja namba yake Glad akamtumia hiyo hela. Nadhani tumemalizana mpe mkataba wake , nilipewa mkataba mpya mbele ya Glad nilimshukuru sana nikamuhaidi nikipata kazi nitamrudishia hela yake. Usijali Nelly ugua pole Glad aliniaga kisha akaondoka zake nilikuwa siamini kama nimelipiwa kodi na mtu niliyezoeana nae kwa siku moja tena kwa majanga
.
Kesho yake asubuhi ๐ niliamka nikajiandaa kwenda chuo taratibu nilifika nikaenda darasani kukaa, Sikuwa na furaha nina mawazo kichwani namfikiria Denis mwanaume aliyenifungulia dunia ya mapenzi akanijali na kunipenda leo hii hila ya mama yangu wa kambo na mama yake mzazi imefanya tuachane na kwenda kumchumbia mtoto wa mama yangu wa kambo kwangu ilikuwa ngumu kulipokea hili nikiwa katikati ya mawazo mara akaja Glad mahali nilipokaa , naona unaendelea vizuri mgonjwa wangu hadi umepata nguvu ya kuja shule. Naendelea vizuri namshukuru ๐ Mungu nilimjibu , Jambo zuri mrembo wangu nina habari njema kwako nahisi utafurahia , niligeuka nikamuangalia vizuri Glad habari gani njema hiyo, Habari gani hiyo Glad ๐ค nilimuuliza niliongea jana na
kaka yangu kuhusu kazi nikamuelezea na hali halisi ya maisha yako ya sasa kanikubalia ukamfanyie usafi kwenye nyumba yake ili upate hela ya kujikimu kwahiyo leo tutaenda wote tukitoka chuo ukapaone then uanze kazi .Wow nimefurahi sana kusikia hivyo sijui nikupe nini Glad zaidi ya shukrani kwako, Usijali maisha ni kusaidiana leo kwako kesho kwangu. Nilitamani ningeonana na Glad toka muda mrefu ila kila kitu na makusudio yake .
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni