MIMBA YA BESTMAN 7
Mulky alikuwa kajiinamia anaangalia chini , Yasini alimshika begani huku akimuita jina lake.
" Mulky....
Mulky alinyanyua kichwa akamuangalia
" Mulky mke wangu hakuna mtu yoyote wa kuingilia maisha yetu naomba upuuzie kile ulicho tokea .
" Nawezaje kupuuzia wakati kilichoongelewa kina ukweli ? Familia yako inatamani kuona unaitwa baba wanatamani kuona watoto waliruka ruka ndani ya hili jumba hata mama yako nahisi anatamani sana ila hajawa na ujasiri wa kuniambia.
" Hata kama hawawezi kuingilia maisha yetu. Na kuhusu mama yangu hana Uswahili huo anaamini Mungu ndio mpangaji na mtoaji kwa yule ambae amepanga kumpa .Mulky mke wangu kuwa na amani baada ya muda fulani mambo yatakuwa sawa hata hiyo mtoto atapatikana.
" Kila siku umekuwa ikiniambia hivyo kwani hiyo siku haifiki mume wangu?
" Ipo siku itafika tunakotoka ni mbali na tunakoelekea ni karibu mke wangu kipenzi endelea kuwa na subira.
Safari hii mulky hakujibu alimuangalia tu .baada ya hapo alinyanyuka akaenda kuungana na wageni.
Wageni walipokuwa wanaondoka mama yake Yasini alisogea pembeni na mulky .
" Mwanangu msameje shangazi yako huwa anapenda kuongea sana.
" Usijali mama mimi nipo sawa.
" Sawa Mwenyezi Mungu atakujalia upate familia iliyo bora na kizazi chema.
" Ameeen mama.
Baada ya kuongea aliwasindikiza mpaka getini kisha akarudi ndani.
Siku zilienda huku mulky akiwa anavumilia alishindwa kuchukua maamuzi magumu sababu alikuwa anampenda sana mume wake .
Siku moja Yasini alimuaga mke wake alikuwa anaenda safari nchini Dubai kwaajili ya biashara zake.
Siku ya safari mulky akimsindikiza mume wake uwanja wa ndege.
" Nakutakiwa safari njema.
" Asante mke wangu na wewe ubaki salama pia kuwa muangalifu kuangaliwa sana.
" Usijali
" Sawa ubaki salama.
" Sawa.
Walimaliza kuagana Yasini aliingia ndani kusubiri kusubiri muda wa ndege kuondoka ili waanze safari na Mulki alielekea kwa rafiki yake Hamida.
Siku hiyo mulky aliamua kumueleza kila kitu Hamida.
" Hamida naomba nishauri nifanye nini sina amani kwenye ndoa yangu.
" Wewe unataka kuniambia Yasini anakutesa au anakunyanyasa?
" Hapana hajawahi kunifanyia hivyo ila.......
Alipofika hapo alitulia kwanza.
" Ana nini niambie basi.
Mulky aliendelea kukaa kimnya na Hamida alionekana kuwa na shauku kubwa ya kujua.
" Usiniambie Yasini ana mchepuo.
" Hapana hana mchepuo.
" Sasa nini?
" Tangia nimefunga ndoa sijawahi kukutana kimwili na mume wangu.
Hamida alishangaa
" Kheeeee wewe unaishijevsasa kwenye ndoa ya aina hiyo na kwanini anakufanyia hivyo?
" Nahisi kuna tatizo lakini haniambii tatizo lake .
" Sasa umeamuaje?
" kwa sasa sijaamua chochote ila mbaya zaidi shangazi yake alikuja anataka mtoto.
" Mmmmh ndugu wa mume wameanza mbona kama watakusumbua sana?
" Ni huyo tu lakini mama mkwe wangu hana shida kabisa.
" Kuna kitu nataka kukishauri kama utaweza basi kutachukua ushauri wangu.
" Nipe ushauri.
" Kuishi hivyo bila yake mambo yetu ya kikubwa ni uongo unaonaje kama utapata jamaa wa pembeni ukamaliza shida zako kwa siri?
Mulky alishituka
" Unamaanisha nimsaliti mume wangu? Vipi akijua?
" Kwani utamwambia?
" Hapana nishauri kingine hicho siwezi.
" Kama hutaki basi lakini tambua utakuwa kwenye ndoa iliyojaa maneno mengi na itakushinda.
Mulky aliona kama Hamida anazidi kumchanganya hakupata nafuu ambayo alihisi atapata baada ya kumwambia.
" Acha niende nitakuja wakati mwingine.
" Kwahiyo ndio ningekufukuza au?
" Hapana
Mulky alinyanyuka akaondoka.
Alifika nyumbani kwake akiwa hayupo sawa kabisa alijitupakwenye kochi akawa anafikiria ushauri wa Hamida.
" Sijawahi kuchepuka na wala sitamani hilo litokee.
Akiwa bado yupo kwenye mawazo mlango uligongwa .
" Karibu fungua mlango uko wazi.
Mlango ulifunguliwa Sameer akaingia huku akiwa Kawambwa na tabasamu mwanana usoni mwake na Mulki alimpokea kwa tabasamu.
" Karibu Sameer
" Asante shem, uko poa?
" Niko poa.
" Mbona kama umepooza hivi au sababu jamaa kaondoka?
" Inawezekana ikawa hivyo si unajua wawili ni wawili tu.
" Ni kweli lakini usijali nipo hapa nitakuliwaza japo kuwa sitamfikia jamaa.
Mulky alitabasamu tu
" Unaonaje tukicheza game kidogo
" Sawa.
Walicheza game kidogo mulky alichangamka na kusahau maneno ya Hamida.
Muda ulienda Sameer aliaga .
" Shem muda umeenda acha niondoke sasa
" Sitamani hata uondoke .
" Hahahaha nitakuja siku nyingine.
" Naomba iwe kesho tafadhali.
" Sawa nikitoka kazini nitapita.
" Nitafurahi sana kukuona doctor Sameer.
Siku zilizidi kwenda Mulk y na Sameer walikuwa wanaona kila siku na walikuwa kama marafiki na kila mmoja alijali mipaka yake.
Siku moja Sameer akiwa nyumbani kwa Mulky mvua kubwa sana ilinyesha na huko nje kulikuwa na ukungu sana kila Sameer alipotaka kuondoka Mulki alimzuia.
" Hali ya hewa ni mbaya sana bora ubaki tu .
" Nitabaki vipi nyumbani kwa mke wa mtu ikiwa mwenyewe hayupo?
" Mmmh unaanza kukuza mambo kwani tunalala chumba kimoja ? Vyumba vipo vingi sana hapa.
Mulky alimsihi sana mpaka Sameer akakubali kubaki.
Mulky alienda kuandaa chumba kwaajili ya Sameer kulala alipomaliza alienda kumuita na kumuonyesha.
" Shukran sana shemeji acha mimi nipumzike.
" Sawa uwe na usiku mwema
" Na kwako pia.
Mulky alitoka pale chumbani na kufunga mlango kisha akaenda chumbani kwake.
Baada ya nusu saa mulky alikumbuka hazina taa za jikoni ilimbidi atoke akiwa kavaa night dress yake fupi hakuwa na wasiwasi alijua Sameer hataweza kutoka . Alienda akiwa jioni kainama ghafla Sameer alifika akawa kasimama na kumuangalia Mulki kwa mshangao mkubwa , Mulky nae alipogeuka alimuona Sameer akiwa kasimama anamuangalia kifua kukiwa wazi na chini alivaa bukta fupi.
Full 1000
0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni