MIMBA YA BESTMAN 15
Mulky alimuangalia Yasini usoni akagundua alikuwa anaongea kwa upendo wa hali ya juu na anamaanisha kile anachosema, alinyanyua mikono yake na kuushika uso wa Yasini ,akambusu na kusema
" Basi nakuahidi sitakunyima tena amani , nitakufa ya uwe na furaha kuanzia sasa kila litakalotokea nitakushirikisha mume wangu.
" Hilo ndilo ninalotaka na utakuwa imekamilisha ule msemo wa kuwa sisi ni mwili mmoja shida zangu ni zako na zako ni zangu.
Mulky akimkumbatia na kumwambia
" Nakupenda sana
"Mimi pia nakupenda zaidi.
Baada ya kuongea waliendelea kuogeshana waliomaliza walirudi chumbani .
Siku hiyo hawakukaa mbali walikuwa mithili ya kinda la ndege na mama yake .
Ilifika majira ya saa moja usiku Sameer akiwa kwenye chumba chake cha hotel alikuwa katoka bafuni kuoga mwili wake ulikuwa bado unamajimaji na kiunoni alifunga taulo , alisogea karibu na kitanda akachukua simu yake na kutafuta namba ya Mulky akajaribu kupiga lakini simu ya Mulky ilikuwa haipatikani.
" Pumbavu yani nimekuja hapa kwaajili yake kaamua kunifanyia uhuni kama huu kazima simu hivi hajui nimetumia gharama kiasi gani mpaka kufika hapa, chumba nimelipia hiyo ni pesa imetumika na muda wangu nimepoteza bure haiwezekani Mulky atalipia hili.
Aliongea Sameer kwa hasira huku akijaribu kupiga simu ya tena na tena wakati huo Mulky na mume wake walikuwa wakifurahia penzi .
Mwisho Sameer alianza tamaa akaacha kumtafuta.
Kesho yake kulipokucha Mulky aliamka wa kwanza akawa kakaa kitandani akimsubiri Yasini aamke. Baada ya Yasini kuamka wakijulikana hali
" Umeamkaje mume wangu kipenzi?
" Salama.
"Yasini mume wangu kuna jambo naomba unisikilize.
" Jambo gani malkia wangu?
" Naomba turudi nyumbani kwetu....
" Kama unataka hivyo basi hakuna shida unataka tuondoke lini?
" Leo , tujiandae muda huu tuondoke.
" Sawa.
Yasini hakupinga ombi la mke wake wala hakuhoji kwanini waondoke ghafla vile kabla siku waliopanga haijafika , walianza maandalizi baada ya hapo walichukua usafiri na kuelekea uwanja wa ndege .
Walipanda kwenye ndege na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao.
Walipofika nyumbani Mulky akawasha simu yake alikutana na messege nyingi za kumlaumu kutoka kwa Sameer.
" Mmmfyuuuuu kijiti mingine sijui ikoje yani anajilizaliza kwa mke wa mtu hata uwoga hana huyu nikimchekea atanifanya tambara la deki atanifutia kila anapohitaji kufanya hivyo. Sijui nafanyaje kumsomesha ili na mimi niwe na amani .
Akiwa bado anawaza nini cha kumfanya Sameer alipiga simu Mulky hakupokea ndio kwanza aliweka pembeni na kuendelea na mambo yake.
Kadri siku zilivyokuwa zinaenda Sameer hakukata tamaa aliendelea kumsumbua Mulky na kumpa vitisho kuwa ana ushahidi wa kumpatia Yasini kuwa ana msaliti. Mulky anaogopa akaamua kukutana na Sameer walipanga wakutane nyumbani kwa Sameer.
" Hivi una jielewa wewe unataka nije nyumbani kwako ili iweje, itakuwaje kama mume wangu akifika ghafla huko nyumbani kwako?
" Nina maana yangu kukwambia hivyo nimejioanga na kuhakikisha usalama upo.
Mulky alikubaliana na Sameer alikodi tax mpaka nyumbani kwa Sameer akiwa ndani ya taxi alimpigia simu na kumtaarifu kuwa kashafika.
" Nipo nje ya geti lako.
" Safi sana , fungua geti uingie.
Mulky alifanya malipo kwa dereva taxi kisha akashuka kwenye taxi na kuingia moja kwa moja ndani kwa Sameer . Akiwa anaelekea sebleni alisikia mziki laini wa mahaba. Alisimama mlangoni mara mlango ulifunguliwa na Sameer alisimama mbele yake akiwa mwenye bashasha na uso wa tabasamu. Alimuangalia Mulky juu mpaka chini na kumpa sifa zake.
" Wewe mtoto wa kike utakuja kuniuwa mwenzio....
" Sijafuata mambo hayo nataka tuongee mambo ya maana.
" Karibu ndani.
Mulky aliingia ndani huku Sameer alimfuata nyuma na kwenda kukaa kwenye sofa. Waliangaliana kwa muda bila kuongea neno, Mulky aliamua kuvunja ukimya kwa kusema
" Sameer nini unataka kutoka kwangu?
" Nataka kile tulichokuwa tumekianzisha.
" Nia yako ni kuvunja ndoa yangu?
" Hapana ila niangalie na mimi nipe kile moyo wangu unachotaka ili tuende sawa .
" Twende sawa wakati unafanya kusudi kunipigia simu usiku wa manane, messege kama vile ujanidai mpaka mume wangu akashituka alafu saizi unasema unataka twende sawa usawa upi unaotaka wewe?
" Tupange ratiba angalau mara mbili kwa wiki uwe na mimi.
" Aaaaah siwezi, siwezi kutumikia wanaume wawili kwa wakati mmoja mume wangu ananitosha Sameer.
Sameer hakueleza alichokiongea mulky ndio kwanza alimsogelea na kumshika na kuanza kumbusu kwa lazima huku akipapasa mwili wake .
" Acha ujinga.....
Aliongea mulky huku alijitahidi kunipambania lakini hakuweza Sameer aliweza kumdhibiti hatimae alimnyanyua juu juu na kumpeleka chumbani kwake
Itaendeleaaaaa
Full 1000
Whatsp 0784468229.