Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

MIMBA YA BESTMAN 10

7th Jun, 2025 Views

MIMBA YA BESTMAN 10

Mulky aliendelea kumuangalia moja kwa moja na Yasini alimkazia macho kisha akamuita
" Mulky naongea na wewe.
"Mume wangu Unajua nashangaa sana, umenishangaza mno siku zote huwa unasafiri unarudi na kila kitu kinakuwa sawa, haujawahi nauliza maswali kama hayo sasa leo hii umenijia na mapya. Mume wangu sijawahi kufanya ushenzi najitambua , najiheshimu mimi ni mke wa mtu hata kama kuna mambo hunitimiziii lakini najali sana heshima yangu na yako mume wangu.
Yasini alimuangalia jinsi alivyokuwa anakueleza kisha akaachia tabasamu alafu akasema
" Nilikuwa na kupima tu mke wangu najua huwezi kufanya hivyo.
Mulky alishusha pumzi
" Unajua umenifanya nijisikie vibaya sana ....
" Pole mke wangu nilikuwa nakujaribu tu .
" Nikajua ndio umeshaanza kusikiliza uzushi wa watu.
" Hapana tuendelee kula mke wangu baada ya kumaliza kula kuna jambo zuri nitakuinyesha.
" Na nilivyokuwa nina hamu na hizo zawadi.
" Unawaza hizo tu.
" Sasa unafikiri nitawaza nini zaidi ya hizo zawadi.
" Mmmh basi leo ni zaidi ya zawadi.
" Mbona kama unajiweka roho juu natamani bilionea hicho kitu sasa hivi.
" Kula kwanza ushibe baadaye utakiona tu.

Waliendelea kula walipomaliza kula mulky alifanya usafi pale mezani akaelekea jikoni akiweka vitu sawa mara Yasini alifika jikoni na kusimama nyuma ya mke wake akamkumba tia huku mikono yake ikiwa imezunguka vizuri kwenye kiuno cha mke wake.

Safari hii Yasini alionekana kuwa na mihemko flani tofauti na hapo mwanzo Mulky hajawahi kumuona akiwa hivyo.
" Yasini unanini?
" Nakuhitaji mke wangu.
Maneno ya Yasini yalizidi kumshangaza Mulky ilikuwa ni mara ya kwanza kulisikia hilo neno kutoka kinywani kwa Yasini.
Mulky alijitahidi kumgeuka na kumuangalia usoni macho ya Yasini yalikuwa yana maanisha kile alichokiongea.
" Umesemaje mume wangu?
Mulky aliuliza tena , safari hii Yasini hakujibu
alisogeza uso wake na kutaka kumbusu
"Hebu subiri kwanza unajua bado sijakuelewa kabisa.
Yasini aliachia tabasamu alafu akasema .
" Haujanielewa nini wife?
" Matendo yako...
" Twende ndani utanielewa tu.
Yasini alimshika mkono Mulky wakaelekea chumbani kwao. Yasini alimkalisha Mulky kitandani alafu akavua vest na kulitupia pembeni , alimlaza Mulky kitandani na vidole vyake vilianza kutembea mwilini kwa Mulky na kufanya kuamsha msisimko mkubwa sana.
Yasini alionekana kuwa fundi sana kwani hakumpa nafasi aliongoza jahazi na safari ilienda vizuri sana mpaka walipofika salama na meli ikatoa nanga Yasini alijipata pembeni na mulky nae alikuwa kajilaza upande wa pili alimuangalia sana Yasini bila kummaliza maana alikuwa na maswali mengi kichwani kwake.
" Hiki nilichokiona ni kweli au naota kwanini haya hakunionyesha tangia mwanzo? Mulky akiwa bado anatafakari Yasini , Yasini aligeuka kumuangalia alafu akasogea karibu yake zaidi na kumkumbatia akambusu kwenye paji la uso.
" Nakupenda sana mke wangu pia nashukuru sana kwa kunivumilia kipindi chote nilichokuwa na changamoto ya kushindwa kushiriki tendo na wewe.
Mulky alimuangalia alafu akauliza
" Ulikuwa na tatizo gani?
Yasini alitulia kwa muda wa dakika kama tatu alafu akaanza kumsimulia tatizo lilipoanzia.
" Mmmh miaka mitatu iliyopita hili tatizo la kushindwa kushiriki tendo lililojitokeza ghafla ile hali ilinikosesha sana amani nilihangaika sana kutibiwa , nilikumnywa dawa za kila aina, nilikutana na washauri wengi sana lakini ilikuwa bado .lakini sasa nimepona nina imani tutafurahia ndoa yetu mke wangu .
" Hii kwangu ni zaidi ya furaha kwanza siamini kama leo nime enjoy kiasi hiki.
Nashukuru sana kwa hiki ulichonionyesha.
" Asante pia mke wangu
Ilikuwa ni furaha kwa wote wawili yani ilikuwa kama ndio wamefunga ndoa siku hiyo.

Siku zilienda mulky na Yasini waliendelea kufurahia ndoa yao Sameer nae alikuwa akitoa lawama kwa Mulky kuwa anasahau sana yupo Bize na mume wake .
Siku moja ilikuwa siku ya jumamosi mulky aliamka asubuhi akiwa na furaha , sura iliyochangamka alinyanyuka kitandani akamuacha Yasini akiwa bado kapumzika akaingia bafuni akaoga baada ya hapo alienda jikoni akapanda kifungua kinywa safi na kuandaa mezani , akiwa anamalizia kuandaa mpango uligongwa.
" Ni nani tena asubuhi asubuhi ?
Aliongea huku akiwa anaelekea mlangoni kufungua .
Alipofungua mlango alikutana na sura ya Sameer. Mulky alishituka akageuka nyuma kuangalia kama mume wake anatoka chumbani.
" Wewe mbona asubuhi?
" Unajua unakusumbua sana akili yangu wewe mwanamke.....
" Eeeeeee..... Sameer kwani hujui mimi ni mke wa mtu?
" Kwani tulipoanza hukujia kuwa wewe ni mke wa mtu? Na makubaliano yetu yalikuwa ni yepi?
" Mume wangu anajibana siwezi kuhudumia wanaume wawili kwa wakati mmoja.
Sameer alicheka alafu akasema.
" Unafikiri sijui mume wako ana shida?
" Ilikuwa zamani baba lakini sasa yupo vizuri sana uwanjani anapiga mashuti kama yote na hodari wa kufunga Magori.
" Ahaaaa sasa nasema hivi ulichokianzisha utakiendeleza huwezi kunilambisha asali alafu unaniacha nameza mate.
" Hayo mambo sitaki tuachane.
" Hakuna cha kuachana hapa .
Wakizozana pale mlangoni mpaka waliposikia Yasini anashuka ngazi waliacha"
" baby unafanya nini hapo mlangoni?
" Kuna mgeni wako.
" Sasa mbona kumkaribisha ndani.
Sameer aliingia ndani wakasalimiana na Yasini .
" Umekuja wakati muafaka karibu huku.
Yasini alimkaribisha dinning wapate kifungua kinywa pamoja.
Mulky aliungana nao mezani wakawa wanakula pamoja huku Yasini na Sameer wakiongea mambo yao lakini Sameer hakuacha kumtupia Mulky jicho la kuibia.
" Vipi mke wangu mbona upo kimnya tunaongea sisi tu?
Aliuliza Yasini na Sameer akasalia
" Nashangaa na sio kawaida yake au kuna kitu umeuudhi?
" Sidhani au kuna kitu mama watoto?
" Hapana nipo sawa hayo maongezi yenu siyajui hivyo siwezi kuingilia nyie endeleeni kuongea tu.
Waliendelea kunywa chai walipomaliza Mulky akisafisha mezani akaenda jikoni kufanya majukumu yake mengine huku akiwaacha Sameer na Yasini wakiwa wamekaa sebleni.
Sameer alijikuta anakosa kabisa utulivu alitamani kumfuata Mulky alitafuta sababu ya kumpeleka jikoni.
" Aaaaah acha nikachukua maji ya kunywa.
" Sawa mwambie Mulky akupe korosho.
" Poa.
Sameer alinyanyuka haraka akaenda mpaka kwenye mlango wa jikoni alisimama kidogo akawa anamuangalia mulky ambae alikuwa kasimama anatosha viombo.
Sameer alinyata na kwenda kumkumbatia kwa nyuma huku alimbusu shingoni , mulky aliachia tabasamu akijua ni mume wake badae alishituka alipogundua marashi yanayoinukia sio ya mume wake alimsukuma Sameer na kumuangalia kwa hasira.
" Hivi unataka nini kwangu ? Unataka niharibikiwe ndio ufurahie , hujui kama mume wangu yupo karibu unafanya ujinga wako? Aliongea Mulky kwa ukali huku akiwa kakunja uso

Itaendeleaaaaa

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MSHANGAZI EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

YAMENIKUTA

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 9

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINSI YA KUTUNZA UKE

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

PART 5 MY HEART

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MY HEART 03--04

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

*MY HEART* *1---2 *

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

ANIPHA 6--7.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 05

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest